Ushauri bure kwa Kesi yoyote ya Madai au Jinai

Mkuu, 666 chata "HAPO HAKUNA UKOMO"

Wakati wa kuomba Mirathi hutegemea na marehemu alikufa kwa kuacha wosia (testacy) ama bila wosia (intestacy). Sasa wakt wa kufungua MIRATHI huwa kuna nyaraka zinaambatanishwa, ambazo pamoja na mambo mengine ni:-

1. Mhutasari wa wanaukoo au wosia
2. Cheti cha kifo kutoka RITA
3. fomu za mirathi ikiwa imejazwa sahihi
4. Ada ya mahakama n.k

Vitu hv vinatakiwa ndani ya miezi 3. Sasa kanuni ya 31 inaweka mazingira kuwa endapo mtu hataleta hv vitu ndan ya miaka 3 basi aongezee (i.e 5. hapo juu) maelezo ya kwa nn amechelewa zaidi ya miaka 3. Akiambatanisha tu maelezo basi kesi inafunguliwa. Na maelezo hayo sio extension of time kama ilivyo kwny torts (3yrs), contract (6yrs) , land (12yrs), Fatal accident 6 months) n.k

So naungana na PTER kuwa hakuna ukomo ili kuna kuongeza nyaraka baada ya miaka 3 kupita.

NB: Sheria hupendeza sana kutoa hoja na supporting authority (section of law or precedence)View attachment 1029965

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu nimeona hata na wewe hapa nisikuache hivi hivi, naomba nikueleweshe kuhusu hio kanuni uliyo i quite na hayo maelezo yako, hahahaha, ni kwamba kanuni ya 31 inatumika kwenye kufanya application upya kabisa endapo mtu atakua kachelewa kufanya application baada ya miaka mitatu, na sio et akichelewa kuleta izo barua sijui vyeti rita hahaha, soma ata marginal note hapo, alaf rule hio iko ndani ya sehemu ya sita ambayo ina husu taratibu za mtu kua granted letter/probate, lakini sijui ata unaitafsiri vipi rule 31(1) mbona iko very clear, ivi ukiisoma hii rule inaendana na iki ulichokiandika hapa? really?.... anyway its hard to point a finger to a lawyer if your one among of them,,, lakini interpretation of law hua ni tatizo kubwa sanaa kwa wanasheria wengi. hivi mkuu ni petition gani itapokelewa mahakamani endapo ikiwa haina ivyo vitu vinne ulivyovitaja? so unataka kuniambia wewe mwanasheria unaweza kufanya application ya probate ikiwa na will na zile forms tu labda alaf mahakama ikapokea ikawa inakusubiri wewe ndani ya miaka mitatu uvilete ivyo vitu then ndio iendelee? really? mahakama gani hio?
 
Mkuu samahan kwa hili swali juu ya mjadala mzito unaoendelea kuhusiana na kesi ya hawa jamaa waliochoma moto kituo na hukum yao ilvotoka..
Wengi wanadai yule aliyekuwa mwanafunz kipind iko ameonewa kutokana na ishu nzima ya umri wake wakat anakamatwa
Nifungue macho....
Kisheria hii imekaaje na je kuna sintofaham yoyote kweny hiyo hukum???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hii hua tunaiita kikaza hukumu, kikawaida hua inafanyika baada ya muda kutajwa ambao mdaiwa anapaswa kua amelipa umeisha, sasa execution/kikaza hukumu kwa mahakama za wilaya kwenda mbele hua zinaendeshwa kama kesi kabisaa, ila mahakama ya mwanzo ukirudi unapeleka malalamiko yako pale kwa maandishi au kwa njia ya mdomo, alaf yule mdaiwa atapelekewa samansi aje ajibu ni kwanini mpaka muda huo hajatelekeza hukumu hio, asipotolewa sababu za msingi na analipaje ilo deni basi wewe unaweza iomba mahakama itoe oda ya kuuza mali zake ili deni lifidishiwe.
Naomba kujua nini hatma ya hili ikiwa aliehukumiwa kulipa hana mali yoyote ambao mahakama inaweza toa order ya kukamata au ana mali zenye thamani ya chini kulinganisha na deni analopaswa kulipa. Je mahakama inaweza mpeleka gerezank ikitokea hali hiyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba kujua nini hatma ya hili ikiwa aliehukumiwa kulipa hana mali yoyote ambao mahakama inaweza toa order ya kukamata au ana mali zenye thamani ya chini kulinganisha na deni analopaswa kulipa. Je mahakama inaweza mpeleka gerezank ikitokea hali hiyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
miaka ya nyuma tatizo hili lilikua linaumiza sanaa vichwa watu, lakini baadae zikawa zinatoka decisions mbali mbali toka mahakamani zikiwasihi watu wakopeshe watu kwa kuangalia na mali wanazo miliki, mfano hauwezi kumkopesha mtu milion 50 wakati mali zake anazomiliki hazina hata thamani ya milion 20.

madai pia yanafunga, mtu akishindwa kabisaa kulipa ndugu mdai unaweza kukazia hukumu mtu huyo afungwe jela mpaka pale atakapo kua tayari kulipa 'civil prisoner' ila atafungwa kwa gharama zako mdai kwa maana utakua unamlipia gharama za kukaa jela.

lakini vile unaweza kuomba ziuzwe hata zilizopo na aende na jela pia endapo utakua tayari kumlipia kukaa jela.
 
Mkuu samahan kwa hili swali juu ya mjadala mzito unaoendelea kuhusiana na kesi ya hawa jamaa waliochoma moto kituo na hukum yao ilvotoka..
Wengi wanadai yule aliyekuwa mwanafunz kipind iko ameonewa kutokana na ishu nzima ya umri wake wakat anakamatwa
Nifungue macho....
Kisheria hii imekaaje na je kuna sintofaham yoyote kweny hiyo hukum???

Sent using Jamii Forums mobile app
ni kweli wakati anakamatwa alikua ana miaka 14 na umri huo huo ndio ulio hesabiwa ktk mashtaka yake na hukumu na sio huu ambao anao leo.

sheria ya mtoto ya mwaka 2009 inasema mtoto ni yule mwenye umri wa miaka 18 kushuka chini. na bwana mdogo yule kweli ni mtoto.

tatizo kosa alilolifanya ni jinai na sheria ya jinai tunayoongozwa nayo ndio hio inaitwa Sheria ya Kanuni za adhabu/penal code sura ya 16, ambayo kimsingi sheria hii chini ya kifungu cha 15 kinasema wazi juu ya makosa yatakayo fanywa na watoto na kusamehewa kua ni yale ya chini ya miaka 12, yaan kumi 12 kushuka mpaka 0, kwaio mtoto wa miaka 13 kwenda mbele atahesabika kafanya jinai akiwa anaelewa anachokifanya.

kitu cha kusikitisha kabisa ni kwamba dogo alifanya kosa kinyume na kifungu cha 319 ambacho kinahusu arson/uchomwaji wa nyumba/jengo nk. ambayo adhabu yake moja kwa moja ni kifungo cha maisha.

kwaio hua hatu tumii sheria nyingine endapo kutakua na sheria husika iliyotoa ufafanuzi jambo husika, utaona hapo msala wa dogo umeangulia penyewe kabisaaa mule mule.
 
Aisee
ni kweli wakati anakamatwa alikua ana miaka 14 na umri huo huo ndio ulio hesabiwa ktk mashtaka yake na hukumu na sio huu ambao anao leo.

sheria ya mtoto ya mwaka 2009 inasema mtoto ni yule mwenye umri wa miaka 18 kushuka chini. na bwana mdogo yule kweli ni mtoto.

tatizo kosa alilolifanya ni jinai na sheria ya jinai tunayoongozwa nayo ndio hio inaitwa Sheria ya Kanuni za adhabu/penal code sura ya 16, ambayo kimsingi sheria hii chini ya kifungu cha 15 kinasema wazi juu ya makosa yatakayo fanywa na watoto na kusamehewa kua ni yale ya chini ya miaka 12, yaan kumi 12 kushuka mpaka 0, kwaio mtoto wa miaka 13 kwenda mbele atahesabika kafanya jinai akiwa anaelewa anachokifanya.

kitu cha kusikitisha kabisa ni kwamba dogo alifanya kosa kinyume na kifungu cha 319 ambacho kinahusu arson/uchomwaji wa nyumba/jengo nk. ambayo adhabu yake moja kwa moja ni kifungo cha maisha.

kwaio hua hatu tumii sheria nyingine endapo kutakua na sheria husika iliyotoa ufafanuzi jambo husika, utaona hapo msala wa dogo umeangulia penyewe kabisaaa mule mule.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
miaka ya nyuma tatizo hili lilikua linaumiza sanaa vichwa watu, lakini baadae zikawa zinatoka decisions mbali mbali toka mahakamani zikiwasihi watu wakopeshe watu kwa kuangalia na mali wanazo miliki, mfano hauwezi kumkopesha mtu milion 50 wakati mali zake anazomiliki hazina hata thamani ya milion 20.

madai pia yanafunga, mtu akishindwa kabisaa kulipa ndugu mdai unaweza kukazia hukumu mtu huyo afungwe jela mpaka pale atakapo kua tayari kulipa 'civil prisoner' ila atafungwa kwa gharama zako mdai kwa maana utakua unamlipia gharama za kukaa jela.

lakini vile unaweza kuomba ziuzwe hata zilizopo na aende na jela pia endapo utakua tayari kumlipia kukaa jela.
Mungu akubaliki na usichoke.

Jana nilikupa mfano wa kesi ya wizi, pamoja na kifungo mahakama imetaka mkosaji alipe fedha alizoiba na sio madai. Ndipo sasa nataka kujua ikiwa kamaliza kifungo au kalipiwa ya kifungo ila hajalipa fedha alizoiba. Je hili uhesabiwa kama deni na lapaswa kudaiwa sawa na kesi ya madai?. Na akishindwa kulipa anaweza kufungwa tena!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ni kweli wakati anakamatwa alikua ana miaka 14 na umri huo huo ndio ulio hesabiwa ktk mashtaka yake na hukumu na sio huu ambao anao leo.

sheria ya mtoto ya mwaka 2009 inasema mtoto ni yule mwenye umri wa miaka 18 kushuka chini. na bwana mdogo yule kweli ni mtoto.

tatizo kosa alilolifanya ni jinai na sheria ya jinai tunayoongozwa nayo ndio hio inaitwa Sheria ya Kanuni za adhabu/penal code sura ya 16, ambayo kimsingi sheria hii chini ya kifungu cha 15 kinasema wazi juu ya makosa yatakayo fanywa na watoto na kusamehewa kua ni yale ya chini ya miaka 12, yaan kumi 12 kushuka mpaka 0, kwaio mtoto wa miaka 13 kwenda mbele atahesabika kafanya jinai akiwa anaelewa anachokifanya.

kitu cha kusikitisha kabisa ni kwamba dogo alifanya kosa kinyume na kifungu cha 319 ambacho kinahusu arson/uchomwaji wa nyumba/jengo nk. ambayo adhabu yake moja kwa moja ni kifungo cha maisha.

kwaio hua hatu tumii sheria nyingine endapo kutakua na sheria husika iliyotoa ufafanuzi jambo husika, utaona hapo msala wa dogo umeangulia penyewe kabisaaa mule mule.

Habar mkuu,
kaka kuna ndugu yetu Ana kesi mahakama ya mkoa, Ipo ivi,
Ana rafiki yake anafanya biashara Ya bidhaa za vyakula km mafuta ya kupikia, súkari ña vinginevyo,
Sasa huyo rafiki yake polisi walienda kupekua kwake wakamkuta ña bidhaa ambazo hazina docoment halali,
Sasa bwana ajabu ya polisi wamemuunganisha na ndugu yetu kuwa nae alikamatwa nyumbani kwa huyo rafiki yake wakiwa na hizo bidhaa, wakati ndugu yetu hapajui kabisa anapoishi huyó rafiki yake baada ya kuhama alipokuwa anaishi mwanzo, wala hakuwepo alipokamatiwa huyó rafiki yake hapo nyumbani kwake, lakini kwenye hati Ya mashtaka eti wameandika kuwa wamekamatwa wote nyumbani kwa Jamaa ña hizo bidhaa,

Ña kosa la Pili eti Kuna watu waliwauzia hizo bidhaa mnamo mwaka juzi, wakati yeye aelewi lolote,
Sasa hapo Mkuu awabane vipi mashahidi upande wa mashtaka siku Ya kuanza kutoa ushahidi wAo,
 
Nahitaji kujua mkuu sheria inasemaje kwa MTU aliyekutwa na kosa LA kura njama ya wizi na kufanya he sheria inatoa adhabu gani

Sent using Jamii Forums mobile app
kosa la kula njama kisheria hua ni makosa ambayo hayajakamilika kwa maana hua ni nia hovu tu na kitaalam huitwa inchoate offences, sasa kwa sheria yetu ya makosa ya jinai yanajulikana kama conspirancy au kula njama, hii ipo chini ya vifungu vya 384 na 385 ambazo kifungo chake ni miaka isiyozidi mitatu.
 
Mungu akubaliki na usichoke.

Jana nilikupa mfano wa kesi ya wizi, pamoja na kifungo mahakama imetaka mkosaji alipe fedha alizoiba na sio madai. Ndipo sasa nataka kujua ikiwa kamaliza kifungo au kalipiwa ya kifungo ila hajalipa fedha alizoiba. Je hili uhesabiwa kama deni na lapaswa kudaiwa sawa na kesi ya madai?. Na akishindwa kulipa anaweza kufungwa tena!

Sent using Jamii Forums mobile app
bila shaka hio itakua ni mahakama ya mwanzo,huko wanaruhusu watu binafsi wajiendeshee kesi zao, so utaratibu utakua ni ule ule wa kukazia hukumu, lakini ingekua ni mahakama ya wilaya kwenda juu hua ni fine au kifungo au vyote kwa pamoja kwenye makosa ya jinai, ambapo victim au alieibiwa anaweza kuichukua hio judgement kama reference na kwenda kufungulia kesi ya madai, na wilaya kwenda mbele jinai haina kukazia hukumu.
 
Habar mkuu,
kaka kuna ndugu yetu Ana kesi mahakama ya mkoa, Ipo ivi,
Ana rafiki yake anafanya biashara Ya bidhaa za vyakula km mafuta ya kupikia, súkari ña vinginevyo,
Sasa huyo rafiki yake polisi walienda kupekua kwake wakamkuta ña bidhaa ambazo hazina docoment halali,
Sasa bwana ajabu ya polisi wamemuunganisha na ndugu yetu kuwa nae alikamatwa nyumbani kwa huyo rafiki yake wakiwa na hizo bidhaa, wakati ndugu yetu hapajui kabisa anapoishi huyó rafiki yake baada ya kuhama alipokuwa anaishi mwanzo, wala hakuwepo alipokamatiwa huyó rafiki yake hapo nyumbani kwake, lakini kwenye hati Ya mashtaka eti wameandika kuwa wamekamatwa wote nyumbani kwa Jamaa ña hizo bidhaa,

Ña kosa la Pili eti Kuna watu waliwauzia hizo bidhaa mnamo mwaka juzi, wakati yeye aelewi lolote,
Sasa hapo Mkuu awabane vipi mashahidi upande wa mashtaka siku Ya kuanza kutoa ushahidi wAo,
hua nawashauri watu sanaa juu ya umuhimu wa wao kupata mawakili au msaada wa kisheria pindi wanapo pata makosa ya jinai, ktk jinai ni hatari sanaa mtuhumiwa kujiendea endea bila kupata huduma hizi.

imekua ni kawaida kwa askari wetu kujiandikia tu makosa kwa kadri wanavyojisikia na kuwaweka watu bila kufikiria, sasa hii kesi yako ni nyepesi sanaa, hawa wamejitungia tu hayo makosa basi sehemu nzuri ni kuwakamatia wakati wa kesi ikiwa inaendelea na wakati wa kuleta ushaidi, haya ni kwa kua kesi iko mahakamani tayari, nafikiri tunaweza wasiliana inbox ntajaribu kukutumia baadhi ya mbinu na maswali ambayo anaweza kuyatumia.
 
asnte kaka
 
Hivi we ni practioner kweli?? Like seriously? Kabisa someone anakutrust umtetee? Unapanic fasta? Unatoa mapovu? Sasa sijui we ni practitioner gani. See now? We ndo unajiita msomi? Unajua fika unaongea na mwanaume yet unaniita dada sasa inaonesha mm na ww nani kilaza.

Mi nafanya street fighting kind of practice, uliza sehemu nilizopita...nimeacha alama.

Much to your dismay, nashindwa kudisclose hapa maana I chose to be anonymous on here.

Ila Ask Them and they Will Tell You!

Sikuaribii uzi ila kama unalisha wadau matango pori, For God's Sake I have the ULTIMATE DUTY to intervene in order to save the PROFESSION from gang rape If I may call it!

N.B Reg. 103(1) ya Professional Conduct and Ettiqutte Regulations, 2018 inasema kua myie mnaojiita "mawakili wasomi" mnaotoa legal services to the public muwe mnaitoa iyo services kwenye namna ambayo itacommand RESPECT ma CONFIDENCE ya wadau dhidi ya PROFFESION yenu...

Sasa kitendo cha kulisha wadau matango pori ni uvunjivu wa kanuni (GN 118 ya 2018) tena una bahati sijajua Bar # yako ningekuripoti kwenye Kamati Yenu nyie Mawakili Wasomi!

Garbage!

Aisee!
 
Anaonekana kasoma law, ila kashindwa kuwa Wakili kwa sababu aidha kafeli Law School au kafaulu ila akanyimwa uwakili kwa sababu ya misconduct, au hajaenda law school kabisa kwa kuwa n masikini na hana hela. Kati ya hayo ni majibu.

Kimaadili, Wakili hawezi Ku behave kama huyu na kimsingi, kuna kupingana kwa hoja ila kuna namna bora sana ya kupinga na siyo kama anavyofanya Hutu.

Ana stress fulani
yeah, very true, siku ya kwanza nilijua huyu hata sio bure ndio wale walienda law school waka disco kabisaa, ajabu akawa anasema hapa sio namwambia kosoa alaf useme yako tuone, hawezi kusema. so ni stress tu na ugumu wa maisha.
 
Back
Top Bottom