Ushauri bure kwa Kesi yoyote ya Madai au Jinai

Sasa watendaji wana nguvu gani ya sheria nikitaka kuuza kiwanja changu? Role yao ipi kisheria?
Kikubwa tu atakuwa kama shahidi tu na atatoa ushahidi kama mtu mwingine lkn hakimu na wakili wao ndio wanatambulika kisheria katika hati za viapo
 
Sasa watendaji wana nguvu gani ya sheria nikitaka kuuza kiwanja changu? Role yao ipi kisheria?
Ila ushauri ukitaka kuuza kiwanja tafuta mwanasheria kwa sababu ndio wenye nguvu za kisheria lkn ndio wanaojua kutengeza mikataba ambayo ni legal
 
Kwenye kesi ya madai,Mfano Mahakama imesema natakiwa kumlipa Mr X milioni 10,Sina hiyo pesa wala sina mali yoyote inayoweza pigwa mnada kufidia.
1.Mdai anatakiwa kufanya nn ili ipate hiyo haki yake?
2.Mdaiwa atapata athari gani kisheria?
 
Mdai anaweza kuomba maombi mahakamani ukakamatwa na kufungwa kama civil prisoner mpaka utakapolipa deni la watu au ndugu zako walipe

Upande wa mdai hakuna madhara zaidi tu ya gharama ya uendeshaji kesi na kucheleweshwa
 
Tukio lilitokea mwaka 2018, kesi nilifungua 2021 baada ya kuona juhudi zangu za kufuatilia zikigonga mwamba. Hivi sasa ni miaka minne toka walipoahidi kulipa deni hilo. Je madai hayo bado yana mashiko kwa kuzingatia huo muda?

Nilitembelea taasis hiyo na kuambiwa ipo chini ya uangalizi wa mahakama (Receivership) hivyo ninasubiri uamuzi wa mahakama. Bado nakala ya hukumu niliyoshinda ninayo endapo mambo yakaenda ndivyo sivyo.
Mahakama inategemea na kiasi cha damage unachotaka ikiwa zaidi ya mil 200 ni Hc ikiwa less happo ni Dc au Rmc na ikiwa less 50 Pc ila zingatia muda toka tukio lilipotokea.
 
Naomba kujua kwa mtu aliyechelewa kufungua shauri la Madai na Redundancy kimakosa then akapata nafasi ya kufungua kwa njia ya Condonation.
Then akashinda hukumu zote mbili kwa ajili ya kusikilizwa Kesi za msingi.

Baada muda kwenda kuendana na changamoto akaziondoa na sio kufuta.
Je huyu mtu anayo nafasi tena ya kuendelea na hizi kesi?
 
Msaada kuna mtu nina mdai pesa 1mil na tuliandikishiana kuwa atalipa kwa hawamu mbili ya kwanza 22 August na ya pili ni 22 September na mashahidi wa pande mbili walikuwepo na kusaini yale makubaliano ila hadi sasa jamaa hajalipa ata sh kumi, mdaiwa ana car wash pia sasa nawaza niende kuchukua moja ya vifaa vyake ili akipata pesa yangu nimrudishie vifaa vyake maana nimeona hawezi tena kunilipa na deni ni la miezi zaidi ya 9 sasa, ushauri wenu wadau ninaumia sn coz ni haki yangu jamaa ananipiga kalenda tu
 
Mwandikie barua ya kisheria ya kumtaka alipe kwa muda kazaa akikataa mpeleke mahakani usichukie kitu cha mtu mambo yatakugeuka sheria haitaki hivyo
 
Msaada kuna mtu nina mdai pesa 1mil na tuliandikishiana kuwa atalipa kwa hawamu mbili ya kwanza 22 August na ya pili ni 22 September na mashahidi wa pande mbili walikuwepo na kusaini yale makubaliano ila hadi sasa jamaa hajalipa ata sh kumi, mdaiwa ana car wash pia sasa nawaza niende kuchukua moja ya vifaa vyake ili akipata pesa yangu nimrudishie vifaa vyake maana nimeona hawezi tena kunilipa na deni ni la miezi zaidi ya 9 sasa, ushauri wenu wadau ninaumia sn coz ni haki yangu jamaa ananipiga kalenda tu
jiulize hicho unachotaka kuchukua kilikuwa sehemu ya makubaliano yenu ya mkataba?

kama sio muandikie taarifa ya lengo la kumshtaki (DEMAND NOTICE) akigoma kukubaliana na takwa lako nenda mahakamani.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom