Ushauri: Bomoa bomoa ifanyike nchi nzima

Mimi kuna kitu najiuliza sipati jibu. Hivi hawa maafisa mipango miji huwa wanafanya kazi gani? Kila siku wako maofisini na mishahara wanalipwa. Tena huenda minono. Sasa inakuwaje kuwe na bomoabomoa kama wanapanga miji?

Jiji kama dar ina maana hakuna master plan inayoelekeza nini kijengwe wapi? Hizi bomoabomoa zinahusika either na uzembe wa watu flani ambao hawakifanya kazi zao au rushwa au labda mipango yetu ya miji ni ya miezi sita sita.

Inastaajabisha mji unaokua kama Iringa majengo marefu yanasimamishwa katikati ya mji na wakati barabara ni nyembamba sana. Hakuna hata parking. Halafu baadae tunaambiwa hayo majengo yanayoota kama uyoga yavunjwe kupisha upanuzi wa barabara. Kama manyumbu hivi. Inaudhi na inatia gasara sana.

Naunga mkono hoja mkuu. Bomoabomoa ifanyike nchi nzima, once and for all na ofisi ya mipango miji ifikiriwe upya.
Ni kweli Maafisa mipango miji wapo ofisn ila kuna upande wa ukweli haupo sawa na wengi hawaujui!

Kupanga miji sio kutengeneza streets tuu.. Ni pamoja na kuandaa development control codes.. Kuwafundisha wananchi nakuwaelewesha dhana nzima ya mpango na kuwafanya primary management team.

Huu ni mchakato unaohitaji pesa nyingi.. Kuna survey kujua terrain ..isaidie kabiliana na surface flow ta maji..pia storm water drains..kuna planning ambayo ni participatory.. Vikao vingi na wananchi maana sehemu kubwa ya miradi serikali haina pesa za kulipa fidia hivyo inabidi ipange maeneo ya watu ambao kutwa na objections..

Kuna changamoto za ongezeko watu katika rate ambayo haiendani na uwezo wa serikali kuandaa viwanja vilivyopimwa kuweza kulikidhi soko. Hii automatically inapelekea kuwepo na makazi holela

Pia kuna dhana kupanga sio muhimu Tanzania budget ya mipango miji utacheka... Mnaweza mkawa wilayani mkaletewa laki mbili... Sasa kinachobakia afisa anakaa ofisini anasubiria kero tu.. Huyu anatiririsha maji kwangu huyu anaziba njia huyu lile na yakiwa meengi anafanya moja mengine basi.

Kama utamaduni wa kuheshimu kupanga hautakuja toka serikali kuu msahau kuwa na maeneo bora ..kamwe. Kutakuwa na visegment tu hapa Mara pale basi.
 
Back
Top Bottom