Mtaji wa Tsh. Milioni 1 hadi 5: Naweza kufanya Biashara gani Tanzania?

Habari za wakati huu manaJF!
Kama kichwa hapo juu kinavyojieleza, nina mtaji wa milioni 2 na ninataka kuanza biashara. Suala gumu kwangu linakuja ni kuamua aina ya biashara ya kuanza nayo kutokana na kutokuwa na uzoefu wa masoko ya biashara tofauti tofauti hapa jijini Dar es Salaam.

Naombeni ushauri wenu wanaJF juu ya biashara ambayo inalipa kwa kuanzia na huo mtaji.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu.
 
dream chaser, nunua vitabu usome
ukifanya wazo ambalo ni la kuambiwa litakuja kukusumbua baadae
tumia masaa matatu kwa siku soma vitabu
utapata mawazo mazuri mengi sana
anza na kitabu kimoja kinaitwa ''as a man thinketh'' David allen
 
Hivi biashara watu mnazichukuliaga poa sana eh..... faida milion 2 kwa mwezi kwa mtaji huo? Basi tungekua mamilionea wengi
 
Tafuta eneo lenye nyomi ya watu weka biashara ya miamala ya fedha unapata laki 5 uhakika kila mwezi.
 
Watu wanapenda kuvunjana moyo wanashangaa na wengi wao hawajawahi kujaribu hata kidogo.

Kwangu jaribu biashara ya chupi za kike na sidiria au pia waeza jaribu viatu vya kike vsendo vile vinavyojaa mitaani ila tu ujaribu kua na kila type kila vinapoingia, zingatia soko na ujitume.

Thank me later
 
Mkuu hii ni kama faida au mauzo?
Kwa mtaji wa 15m ukianzisha duka la spare za magari hio 3m kwa mwezi hata huumizi kichwa. Ila kuwa tofauti na wauzaji wengine,dont be just like everybody else. Kuwa tofauti. I'm talking from experience.
 
Back
Top Bottom