Mtaji wa Tsh. Milioni 1 hadi 5: Naweza kufanya Biashara gani Tanzania?

maguu

Member
Aug 12, 2011
12
34
Wakubwa nina mtaji wa shilingi milioni mbili na nataka nifanye biashara.

Je, biashara gani ninaweza kufanya kulingana na pesa hiyo?

Nimetafakari sana ila nakosa kujua kwa usahihi biashara gani inanifaa.

===========
SIMILAR CASES:
===========

May 18, 2012:
Msaada jamani nataka kufanya biashara nina 1m. Sijui nifanye biashara gani?
May 10, 2014:
Ushauri wa kibiashara! nina mtaji wa milioni nne mkononi...

Nafikiri nianzishe biashara! ushauri wenu tafadhali ni biashara gani itakayoweza kunilipa kirahisi! m

Mhauri mmoja kaniambia nifungue mpesa-airtel money na pia niuze vifaa vya simu! Mwingine kanishauri niuze yebo yebo niwe naagiza kutoka kiwandani na kuuza huku kwa jumla jumla!

Bado sijafikia maamuzi nipeni ushauri kati ya hizo mbili au biashara nyingine!

Ahsanteniwajasiria mali wenzangu
May 16, 2014:
Habari zenu wadau na wakuu wa jamiiforums,

Mimi ni kijana wa elimu ya chuo kikuu, nimejizatiti hasa baada ya miezi miwili hivi kupita, nisaifiri kwenda Kaskazini kwa ajili ya kuanza biashara ndogo ndogo ya ununuaji wa madini aina ya dhahabu kutoka kwa wauzaji wadogo wadogo.

Wakuu, nimekuja hapa mbele yenu kuomba mwongozo juu ya ufanikishaji bora wa biashara hii, isitoshe mimi ndiyo mara yangu ya kwanza naingia katika soko.

Kwa kiasi fulani nilishaona dhahabu ikiwa inauzwa katika vipimo tofauti tofauti vyenye madaraja tofauti tofauti ya bei kama kuanzia shs elfu 30 na kuendelea.

Naombeni mwongozo kwa mnaoifahamu vizuri biashara hii,changamoto zake ni zipi?

NB; Pia kama kuna wazo lingine la biashara linaloendana na hili, tafadhali usisite kuninong'oneza!

Oktoba 09, 2014:
Wadau nimekuja kwenu nina vijicent kidogo tu mil 2. million mbili.

Nahitaji kuanza biashara mi nipo Dar; nahitaji biashara ambao ntaendelea kuikuza kadri iwezekanavyo.

Naomba mnisaidie kwa huo uwezo wangu naweza fanya nini. Naamini kuwa wajasiriamali wengi ambao wanaweza kunishauri nini cha kufanya.

Oktoba 22, 2014:
Wakuu mimi ni kijana wa Umri wa Miaka kama 30 hivi, Najua nimechelewa kutoka, Ila ni kutokana na kutokea kwenye familia ya kawaida sana. Sasa wakuu nimejichanga changa nimesave kama ka-milioni na taka kufanya jambo niongeze kipato.

Mnanishauri nifanye nini?
Novemba 10, 2014:
Nisaidieni jamani wapendwa nifanye biashara gani ili niweze kijipatia kipato angalau niweze kujikimu kimaisha.

Nina mtaji wa sh 1,500,000.00/= [milioni moja na nusu]

TUSAIDIANE JAMANI. MWENYE MSAADA ANI PM BASI.
Feb 18, 2015:
Habari wakuu,

Hivi wanabodi ukiwa na mtaji wa Tsh 5 million unaweza fanya mradi gani ukatoka?

Naombeni mawazo yenu wakuu

Aprili 13, 2015:
Ndg,

Bila shaka muwazima, mungu azidi kuwatia pumzi pamoja na upeo wa kufikiri.

Mimi nina milioni 1(1,000,000/=) Tsh.kama kianzia. Ninapenda nami siku niitwe tajili ktk kundi la watu ! Naomba msaada wa mawazo nifanye nn ili niweze kufanikiwa? Hii Pesa nimeipata kwa kufanya kazi za watu hivyo nimechoka kuajiliwa nami napenda nijiajili.

Nitafurahi sana kama mtakao npe ushauri mtanitajia na namna ya kukabiliana na changamoto nitakazo kutatana nazo katika kuendesha hiyo shughuli nitakayo ianzisha.Nipo tiari kuishi sehemu yeyote si mjini wala kijijini tu!

Nitashukuru sana kama nitasaidiwa

-----------

Biashara

Mtaji wako waweza kuwa mdogo au ni mkubwa, hii inategemea na aina ya biashara utakayo taka kuwekeza, ningependa kukupa angalizo kidogo, bila shaka litakupa mwangaza kidogo kabla ya kuwekeza ktk biashara yoyote.


  • Kwanza tafuta biashara ambayo itakujenga kiakili, ambayo haitakufanya kuwa mtumwa wayo, ambayo itakupa fursa ya kuwekeza kichwa pia, OJT au OBT (ON JOB/BUSINESS TRAINING), Hii inamaana wafanya biashara huku ukijifunza kuwa mweredi zaidi. Wekeza kichwani kwanza. Benjamin Frankilin aliwahi kusema:- "if a man empties his purse into his head, no man can take it away from him. An investment in knowledge always pays the best interest."
  • Biashara nzuri ni ile inayogusa jamii, kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii, hii yahitaji muda kidogo kufanya kautafiti, yaani ni kutafuta pengo na kulijaza ama kuwa suluhisho la changamoto.
  • Biashara nzuri ni ile ambayo itakupa passive income au Residual Income, itakayo kupa Inner Freedom, Location Freedom, Time Freedom na zaidi baada ya miaka mitatu au mitano yaweza kukupa financial freedom pia, tena ambayo yeyote aki – copy na ku-paste (kwani ni kawaida) biashara hiyo bado kwako itakuwa faida, yaani ambayo hautakuwa na choyo kumwelekeza mingine jinsi ya kufanya.
  • Tafuta Biashara ama fursa itakayokupa changamoto na kukupa ubunifu wa kupambana na changamoto hizo, kumbuka tunakua kutokana na changamoto tunazo kutana nazo kila siku, kubweteka ama kufanya kwa mazoea hakuletelezi kukua.
  • Pia ambayo itaenenda na mtaji wako, kwa kuwekeza kwanza kidogo, labda kama laki 4 kwanza na elimu (kwa gharama ndogo au bure) la namna ya kufanikiwa katika biashara hiyo la namna ya kuweka malengo na kufanikiwa. Tumia muda wa kutosha kujifunza kabla ya kutumbukiza pesa, jiridhishe kuwa hii biashara itakutoa. Abraham Lincolin alisemaga zamani – "Give me six hours to chop a tree and I will spend the first four sharpening the axe."
  • Katika karne hii ya sayansi na teknologia, fursa za biashara ziko za aina nyingi sana, ni juu yako kutafuta biashara sahihi na kuwekeza, usiangalie iliyorahisi sana au mazoea, au ambazo kila mtu anakimbilia, tafuta iliyohalali hata kama watu watakwambia ni ngumu, kumbuka wengi wanaosema biashara Fulani ni ngumu, asilimia kubwa hawajawai kuifanya, ama walisikia kuna mtu kajaribu kashindwa pasipo kujua kashindwaje, wao wanabeba bango kuwa ni ngumu, wanakuwa wanachagizwa na woga zaidi kuliko uhalisia.
  • Kila la kheri, ni PM ukiwa na swali lolote.

12 Aprili 2016

Habari ya muda huu wadau wenzangu. Nilikuwa na wazo la kufanya biashara kwa kuanza na mtaji wa milioni mbili, sasa bado sijajua uhakika kamili kwamba ni biashara gani naweza kuanzisha na ikanipa faida nzuri kwa kiasi hicho cha mtaji. Ahsanteni...
 
Sijawahi kufanya hata biashara ya kuuza pipi wapendwa, naomba mnishauri kwa hili.

Nina mtaji wa Sh. Milioni moja, naomba mnishauri nifanye biashara gani?

Mwanzo nilipanga kununulia simu kali, subwoofer, friji, na vitu vingine vya ndani, ila nimeona sio issue bora nifanyie biashara lakini ndio hivyo sijajua nifanyie biashara gani.

Wakubwa nina mtaji wa shilingi milioni mbili na nataka nifanye biashara.

Je, biashara gani ninaweza kufanya kulingana na pesa hiyo?

Nimetafakari sana ila nakosa kujua kwa usahihi biashara gani inanifaa.
 
Usikonde ndugu yangu. Hauhitaji kuzitumia zote. Wasiliana nami ili nikupeleke sehemu mwendo wa masaa matatu. Utakodi ekari 2 kila ekari moja utatumia laki 3 zikiwa ni gharama za kukodi shamba, kununua mbegu, kupandikiza mpunga, kulinda na kuvuna magunia 40 ya mpunga baada ya miezi mitatu na yatakupatia shilingi milioni 2.

Utaendelea na shule kwani unaweza kwenda shamba mara moja kila mwezi. Utasimamiwe kwa gharama hiyo hiyo ya laki sita kwa ekari mbili.

Ni kilimo cha umwagiliaji. Kwa uhakika utavuna na umetajirika kwani utaendelea kulima maishani.
 
Mdogo wangu kwanza nikupe hongera kwa kuwa na akili ya kazi. Kuona kwamba expenses sio sawa na asset.

Pili nikwambie kwamba usiwasikilize wanaokupa adisi za kwenda kuspend 60% ya capital yako kwenye expense moja katika business operational yako.

Ushauri wangu sababu bado upo shule, zunguka kwenye mabank mbali mbali angalia interest rate kwenye fixed deposit accounts. Kisha tulushie hizo rate hapa nitakuchambulia wapi ni bora.

Weka hiyo pesa kwenye fixed deposit kwa muda wote ambao upo shule, maliza shule hiyo fedha itakuwa imepata atleast 15% return. Then baada ya hapo twende kazi unaweza kuangalia wapi uwekeze.

Mwisho kumbuka unaweza 100% debt (sababu ni mkopo) na debt to equity ratio ni kwamba kwenye kila shilingi unayotaka kuwekeza umekopa shillingi nzima.
 
Mtanganyika, banks zina interest ndogo sana, CRDB ndo kabisaa

Niliwahi kuzunguka kipindi fulani.

Nafikiri hata akisema aweke fixed deposit hadi akija kuchukua ile pesa yote atakayopata itakuwa ndio thamani ya pesa kwa kipindi hicho.

Binafsi nafikiri interest rate ipo ili imcopasate mtu kutokana na thamani ya pesa inavyoshuka na sio imbenefit otherwise kama unaweka mahela mengi. (mnaweza kunisahihisha).
 
ila kwa mikopo ya chuo ina muda mrefu sana wa kuilipa pole pole sn so cjawaza kuusu kulipa, kuusu suala la kufungua fixed account nililifikilia pia, ila me nilivyo mh!!! nitaenda kuzitoa tuu hizo nitumie vitu vya kijinga
Ni ngumu kumanage biashara na masomo kwa wakati mmoja.

Biashara nayo inahitaji uangalizi wa makini.

Mimi niliwahi kuwa na duka la nguo nikamwachia ndugu yangu ambaye nilimuamini.

Sasahivi imebaki historia. Nakushauri uende maeneo ya chanika au kibamba ndani ndani ukanunue ardhi.

Hadi ukija kumaliza chuo hata ukitaka kuiuza utaiuza kwa faida maana ardhi value yake inapanda kila siku.

Au unaweza ukanunua printer na computer ukawa unatype kazi za watu hapo chuo.
 
Ni ngumu kumanage biashara na masomo kwa wakati mmoja.

Biashara nayo inahitaji uangalizi wa makini.

Mimi niliwahi kuwa na duka la nguo nikamwachia ndugu yangu ambaye nilimuamini.

Sasahivi imebaki historia. Nakushauri uende maeneo ya chanika au kibamba ndani ndani ukanunue ardhi.

Hadi ukija kumaliza chuo hata ukitaka kuiuza utaiuza kwa faida maana ardhi value yake inapanda kila siku.

Au unaweza ukanunua printer na computer ukawa unatype kazi za watu hapo chuo.
Kwa stationary hapana coz kila mahali zimejazana, hilo la ardhi cjui nimshirikishe mama? coz cjamuambia mtu
 
Ni ngumu kumanage biashara na masomo kwa wakati mmoja.

Biashara nayo inahitaji uangalizi wa makini.

Mimi niliwahi kuwa na duka la nguo nikamwachia ndugu yangu ambaye nilimuamini.

Sasahivi imebaki historia. Nakushauri uende maeneo ya chanika au kibamba ndani ndani ukanunue ardhi.

Hadi ukija kumaliza chuo hata ukitaka kuiuza utaiuza kwa faida maana ardhi value yake inapanda kila siku.

Au unaweza ukanunua printer na computer ukawa unatype kazi za watu hapo chuo.

Ni wazo zuri. Ikiwa utapata ardhi yenye thamani hiyo changamkia haraka. Kitu hupaswi kufanya kwa sasa ni kuanzisha biashara ambayo itakubidi ugawe wakati wako baina ya masomo na biashara. Na sula la kumwamini mtu asimamie ni sawa na kutia mkono gizani.

Ikiwa huna kabisa la kufanya weka kwenye Fixed Account deposit, huko hutaweza kutoa hata senti mpaka muda ufike.
Uamuzi wowote utaochukua, ninakutakia kila la heri.
 
kibananhukhu,

Kama uko serious, naomba pia ushauri. Mie hobby yangu ni kilimo, ila sipendi kilimo cha kutegemea mvua. ni wapi mashamba hayo yanapatikana?
 
To run a business na kwenda shule sio mchezo. Unless unataka kurun biashara ya hapo hapo chuo, weka copy machine au kitu chochote ambacho kipo maeneo ya chuoni.
 
cjawahi kufanya hata biashara ya kuuza pipi wapendwa, naomba mnishauri kwa hili , nina mtaji wa milion moja, naomba mnishauri nifanye biashara gani? mwanzo nilipanga kununulia cm kali, subufa, friji, na vitu vingine vya ndani, ila nimeona cio issue bora nifanyie biashara bt ndio hvyo cjajua nifanyie biashara gani?
NB: me bado ni dependent kwa wazazi wangu, am 22yrs old, niko chuo, hizi ela ni za mkopo, niliombaga bodi wakanizingingua ckupata ndio nimezifatilia bodi kwenyewe mpk zimekuja za awamu za mwaka huu zote kwa pamoja

Usishangae hapa kuna wenye mawazo dinamic na kuna wenye mawazo static.

Nakupongeza kwa kufunguka akili maana kutumia hiyo pesa bila kutumia akili ni ufinyu wa kufikiria. Kununua kiwanja ni mpango wa muda mrefu, na kumbe kwa sasa unataka pesa yako izalishe ili faida ndio uitumie.

Nakushauri angalia biashara ambayo haitakupa taabu ya kufuatilia wakati uko chuoni. Nakushauri jaribu kufikiria kati na ya chache zifuatazo;

Tafuta chumba na ajiri vijana kama wawili hivi ambao watafanya kazi ya barbar shop, au beauty.

Gharama ya vifaa ni ndogo tu, na baadhi ya pesa itabaki kuendeshea shughuli. Kwa biashara hiyo hutatumia mtaji mkubwa na mtaji ni vifaa ulivyo navyo na waajiriwa ndio mtaji mkubwa zaidi. Fanya mapatano kwa waajiriwa wako kila siku wakuletee pesa ngapi.

Biashara hiyo itakusaidia kuweka msingi wa kufikiria biashara nyingine itakayo kufaa siku za usoni ukiona ina tija. Utashangaa kila siku unaingiza zaidi ya 50,000 kitu ambacho bank huwezi kupata hata kwa mwaka mzima.
 
Kama huna uzoefu wa biashara yoyote mmh pagumu ni bora hizo fedha ukaziweka au kopesha watu kwa riba . tafuta biashara unayopenda kuifanya kisha jifunze namna inavyofanywa ndipo uingize pesa zako.
 
Duh! safi sana, kweli wewe ni Puuuuu!

nimecheka mbavu sina,hadi machozi yamenitoka, i wish ungekuwa Advisor wa Mh. Jay Kay.

Hapa dogo anataka to eat his cake and still have it,ninamaanisha Dogo anataka achukue bumu,libaki palepale pia apate faida ya kupoke hilo boom

wakati enzi zenu kina Puuu ukilipata tu boom, inakuwa Boom kweli miezi miwili ya mwanzo lazima baa za jirani na chuo zikuone wewe kweli umepata li boom la mapesa

Kama vp nenda hapo Salmacone agiza pizza na mabaga ule mpaka meno yaote kutu. Halafu wkend tuonane Stone au Villa Park pale kwenye vt vrefu tufanye kufuru ya maj matakatfu na hako ka m1.
 
Mkuu malila, Mahala Pazuri wapi? Mfafanulie akuelewe,mimi nahisi nimekuelewa na pia nina imani una nia njema ya kumsaidia kumanage boom lake ila kwa dunia ya leo imani imekuwa so Scarce commodity
Nipe nikuwekee mahali pazuri,ukimaliza chuo nitakupa milioni tatu.
 
Mkuu malila,Mahala Pazuri wapi?mfafanulie akuelewe,mimi nahisi nimekuelewa na pia nina imani una nia njema ya kumsaidia kumanage boom lake ila kwa dunia ya leo imani imekuwa so Scarce commodity
Ni kweli kabisa akinipa namuwekea na siku akimaliza chuo nampa haki yake na watoto juu,tatizo imani yake basi. Akikubali kwamba nimuwekee mahali pazuri basi nitamwambia hapa hapa jamvini ni wapi pazuri.
 
Kama lengo ni kutunza hiyo hela yako, naungana na waliokushauri ununue shamba/kiwanja kwani thamani ya viwanja inapanda thamani kila siku. Kama unataka fedha yako izalishe kwa sasa maana yake ufungue biashara ambayo utaweza kuisimamia/kufanya monitoring. Kitu ambacho nahisi kinaweza kuwa kigumu kwako unless uifungue hapo hapo chuoni.

Usiogope stationeries kuwa nyingi chuoni ukafikiri kuwa huwezi kupata wateja, inategemea strategy utakayotumia. Unaweza kunua printer kubwa ambayo watu kuwachapia na kuprint ukacharge bei ndogo ukilinganisha na bei zilizopo.

Kama una heavy printer hata kama ukicharge bei ndogo ya printing bado utapata faida kwani toner/catridge moja itakuwa na uwezo wa kutoa karatasi nyingi.
 
24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom