OllaChuga Oc
JF-Expert Member
- Jul 4, 2016
- 21,127
- 24,063
Niaje Mabroo na Masista. Maisha yanaendelea poa, mimi niko Kahama hapa kuna mishe nilikuja kufanya ila mda siyo mrefu nageuza kurudi A Town, aka A City, Geneva of Africa, City of God ..ni hivi wakuu tuachane na mbwe mbwe za majina.
Ni Kwamba katika muda niliokaa hapa kahama nimetamani kufanya hii biashara ya mchele ..yani nichukue kutoka huku na kupeleka pale Arusha mjini na kuuza kwa jumla na reja reja. Bei ya huku siyo mbaya inaonesha bado uko chini sana ..kwa mfano supa waweza kupata hadi kwa tzs 1200 hadi 1100. Grade two ni hadi 1000 mpaka 900.
Tofauti na Shinyanga mjini ambapo bei iko juu kidgo. Nikacheki na bei ya mpunga ili ukoboe upate mchele bei yake ni kama tzs 45000/= hadi tzs 50000, changamoto kubwa iliyopo ni kujua upi ni mpunga mzuri ili ukikoboa usije pata mchele ule wanaita "biriani" ni balaa. Kitu ambacho nimegundua ukiwa na uzoefu unapata mchele mzuri ila ukija kichwa kichwa utapigwa tu.
Hivyo wakuu naombeni uzoefu wenu hasa kama kuna wadau wanaofanya hii biz, je inalipa? Mimi kwa sasa nauza chakula pale sakina na matunda pale kilombero. Ila kwakua kuna mishe nilipata huku ivyo vijana wangu wa kazi bado wanaendesha mapambano. Hivyo nikiwa narudi Arusha nirudi na hata tani mbili kwanza za kuanzia ila sijajua nitaanza vip kwa maan ya bei iliyopo sasa ni tzs ngap?
Mfano nikinunua mchele huku kwa 1100/= kuna gharama zingine ndogo zitajitokeza hapo kwa maana hiyo
nitanunua kwa kilo kwa bei ya JUMLA ni tzs 1,250 per kg ina maana 1,100 ni kwa bei ya kununua na hiyo 150 itaingia kweny gharama zingine kama usafiri, ushuru, kununua mifuko, na gharama za ku grade. Hivyo basi kwa Tani moja nitanunua kwa tzs 1,250,000.
Je nikifikisha Arusha nikauza kwa 1600per kg, hadi 1500 per kg nitakuwa nmepoteza Muda tu na nguvu huku faida ikiwa kidogo? Ukiisha wote kwa bei ya 1600/kg nitakuwa na tzs1,600,000. Hivyo faida itakuwa ni sawa na 1600-1250=350, ina maana faida itakuwa ni 350,000. Hapo bado sijaweka Muda ambao nitatumia kuuza mchele huo.
Ni bado sijaanza kuifanya ndo natathmini kwanza, hivyo naombeni ushauri wenu wadau ili nijue moja nifanye au niendelee zangu na matunda tu na chakula kwanza. Asanteni