Wadau napenda kupata ushauri bishara ya kukamua na kuuza mafuta ya alizeti kwa Dar inalipa? Nimefunga mashine kwa hapa dar lakini material kwa maana ya mbegu itanilazimu nikanunue Singida au Dodoma. Nimeamua kufunga hiyo mashine hapa Dar kwa ajili ya urahisi wa kusimamia maana mimi ni mwajiriwa pia.