Ushauri - Biashara ya Kufua nguo na kufanya usafi majumbani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri - Biashara ya Kufua nguo na kufanya usafi majumbani

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Ashangedere, Oct 8, 2010.

 1. A

  Ashangedere Senior Member

  #1
  Oct 8, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari wana jamvi, mimi ni mwanamke mjasiriamali, bado niko kwenye utafiti, maandalizi na huku nikiendelea kutafuta wateja naomba mnishauri pale mnapoona muhimu.
  Ninaanzisha biashara ya kufua nguo(lakini ofisi yangu iko nyumbani na nitakuwa nafulia kwa mashine hapa nyumbani) na pia kufanya usafi majumbani kwa wateja.

  1.Kufua nguo - Najua kuna baadhi ya watu wanapata challenge kutokana na mahousegirl kutokufua nguo vizuri hasa zile nguo muhimu kama za kazini, mashuka n.k hivyo nimepanga kuwa nawafulia na kupiga pasi nguo za wateja, ambapo mteja akijiandikisha atakuwa akilipa mwisho wa mwezi kwa bill, mimi nitakuwa nafuata hizo nguo kwake naenda kuzifua na kupiga pasi kisha narudisha nitafanya hivyo mara nne kwa mwezi yani kila wiki kwa wateja wacontract na gharama haitakuwa kubwa itarange kutoka 65,000Tshs+ kwa mwezi kutokana na ukubwa wa kazi yake. pia nitakuwa nachukua na wasiokuwa kwenye contract hao tutakubalina bei.

  2. Kufanya usafi majumbani, ninafahamu kuna watu nyumba zao zinafanyiwa usafi usioridhisha na mahousegirl, pia nitakuwa na contract ambapo nitakuwa ninafanya usafi kila wiki mara 4 kwa mwezi kwa wateja wangu wa mkataba na cost itaanzia 120,000+ kwa mwezi pia nitachukua wateja wa maramoja bei tutakubaliana na huduma itainclude
  a) kusugua tiles/sakafu/sahani ya choo/ masink
  b)kuosha kuta madirisha n.k
  c)kuosha vyombo vyote kabatini na kupanga
  d) kupanga sitting,dining room na kusafisha vyumba vyote vya ndani mteja akipenda
  e) kwa ujumla usafi wote wa nyumba kama nitakavyokubaliana na mteja.

  Nimeanza kununua vifaa na kutrain kikundi changu lakini ninawateja wachache sana ambao wameconfirm wanahitaji mpaka sasa na bado ninawasiwasi na jinsi ya kupata wateja na nimeona hapa jamii forum mwaweza kunishauri kuanzia jinsi ya kutoa huduma hadi jinsi nitakavyopata wateja zaidi. Nitaanza rasmi January 2011 hapo naamini team yangu itakuwa imejipanga vizuri. tafadhali ushauri na maoni yenu ni muhimu sana kwa hii biashara yangu mpya.
   
 2. S

  Superstar Member

  #2
  Oct 8, 2010
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera sana dada keep up the good job hujatupa contact zako
   
 3. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Hii post wameisoma wengi lakini naona hakuna hata mmoja aliyetoa maoni, lakini nina imani utapokea maoni ya utosha tu watu wakitoka kwenye jukwaa la siasa! Kwanza nikupongeze kwa KUTHUBUTU! Biashara kama hii sijaisikia hapa Bogo (Ni jambo la ubunifu lenye matumaini makubwa sana hapo mbele). Naomba nikushauri mambo kadhaa!

  1. Bei: binafsi naona kama umeanza na bei ya juu kidogo, ungeanza na hesabu ambayo iko chini, kisha bei kupanda kulingana na ukubwa wa familia na Nyumba! Biashara ikishaenda vizuri unapandisha bei taratibu.
  2. Nashauri usiwe na mabinti kibaao, watu wataona ni heri house girl! Kuwa na staff ndogo ya vijana wanaojiheshimu.
  3. Kwa bei hiyohiyo pia unaweza kuweka huduma ya dry cleaning.
  4. Tangaza biashara yako: Pita katika majumba na maofisi eleza faida ya kutumia huduma zako, toa bizcards na brochures.
  Amini nakwambia, utafanikisha, KEEP IT UP!
  Wakati bado naishi mjini niliwahi kuwaza kuanzisha huduma ya glass washing kwa maghorofa marefu ya vioo! Wadau wakanishauri majengo
   
 4. M

  Malila JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,413
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Kwa mfumo wa maisha tunaokwenda nao sasa hivi,hii ni biashara nzuri na itakulipa sana,isiwe majumbani tu,nadhani hata maofisi mengi siku hizi wanatumia mtindo huu. Mi si mtalaam wa biashara,mchango wangu utakuwa ktk manpower yako,hasa usafi wa vijana wako kimwili na kiroho. Ukifaulu hapo,utashangaa itakavyo panuka( usisahau kuwa na gardener japo mmoja ktk team yako)
   
 5. B

  Bunsen Burner Member

  #5
  Oct 8, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 95
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Yaap!! Ashangedere many congrats for comin out with something! Additional advice is "Please make sure you have VETTED PROPERLY "those workers manake uaminifu wa hali ya juu unatakiwa for such bussiness , otherwise wizi na udokoaji wa mali kwenye maeneo ya kazi unapokwenda fanya hizo services or upotevu wa nguo ulizochukua za wateja unaweza haribu biashara yako hiyo kabisaa!!
   
 6. A

  Ashangedere Senior Member

  #6
  Oct 8, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thanks Superstar usijali utazipata, nitaanza rasmi January sasa hivi tunajifua january nitaadvertise,

  Bei: binafsi naona kama umeanza na bei ya juu kidogo, ungeanza na hesabu ambayo iko chini, kisha bei kupanda kulingana na ukubwa wa familia na Nyumba! Biashara ikishaenda vizuri unapandisha bei taratibu. - Thanks Nafanyia kazi suala la bei, wadau wengine mnasemaje kuhusu bei??
  1. Nashauri usiwe na mabinti kibaao, watu wataona ni heri house girl! Kuwa na staff n
  2. dogo ya vijana wanaojiheshimu. Nina 1 girl 2 Boys so far lakini ni kweli itakuwa haimeki sense
  3. Kwa bei hiyohiyo pia unaweza kuweka huduma ya dry cleaning. good idea, Nafikiri nahitaji kujua zaidi kuhusu Dry cleaning
  Malila na bunsen burner nashukuru kwa ushauri wenu. Napata moyo sana.
   
 7. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  kwakeli ni ubunifu mzuri mtaani kwetu yupo kijana anafanya kazi kama yako yy anafanya kufua na kupiga pasi jioni anakuletea japo yupo kiloko ila kwa jinsi yako naamin una maono makubwa na utafanikiwa zaidi kwani wengi awtakuwa na haja ya mausigeli tena
   
 8. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hongera sana ndugu kwa ubunifu wa huduma inayohitajiwa na wengi.Ila kama alivyosema Amoeba hapo juu, anza kidogo kidogo kwa maana ya bei.Kumbuka kwa wale wenye kuzoea kupeleka nguo dry cleaners hutumia karibia kiasi hicho hicho na wengi wenye kuweza kukulipa kiwango hicho wanazo machine zao za kufulia nyumbani. Watakaopenda huduma yako ninavyoona ni wale wasiokuwa na mbadala na wengine wanao dobi wanaowafanyia kazi hiyo ama majumbani au kuchukua nguo kwenda kuzifua na kuzirudisha.
  Bei za dobi nadhani siyo ghali sana kama bei uliyopanga.

  Kuhusu usafi wa majumbani pia wapo wanaofanya na kwa mwezi kutegemeana na uzito wa kazi ikiwemo ukubwa wa nyumba huanzia 50,000/= hadi 500,000/=
  Ila usiache kuifuatilia biashara hii maana inalipa.
   
 9. C

  CLAY KITUMBOY Senior Member

  #9
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 8, 2009
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Very good idea nakushauri ujikite katika kazi moja tu kwanza,hasa jaribu ya kufua nguo tu kwanza.
   
Loading...