Ushauri: Biashara ya Apartments Dar es salaam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri: Biashara ya Apartments Dar es salaam

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by S. S. Phares, Aug 28, 2009.

 1. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wadau,

  Nafikiria kuingia kwenye biashara ya kujenga na kuzikodisha apartments jijini Dar es salaam.

  Nina kiwanja cha 500 sqm maeneo ya katikati ya Morocco na Victoria (upande wa Petrol Station na Knight Support) kama unaelekea Mwenge kupitia New Bagamoyo Road.

  Sina uhakika wa soko likoje (scary, I know) ila naona kuna pengo kwenye soko. Walengwa wangi ni vijana wanaopata kazi professional jijini Dar es salaam na wanaotaka kuondoka kuishi na wazazi wao au walitokea mikoani wanaohitaji apartments za kukodisha. Pia nafikiria kulenga wageni wachache wanaokuja Tanzania kwenye kazi za mkataba wa miaka kadhaa.

  Lengo langu ni kuwekeza Shs 100 Mil katika kipindi cha miaka 3 ijayo (2012 ujenzi uwe umekamilika). Jengo liwe na apartments 3 au 4 (kutgemea na ushauri wa wachora ramani) kila moja iwe na vyumba 2 vya kulala (1 kiwe ensuite), sebule, jiko, dining, stoo na veranda.

  Ili mtaji wangu urudi nategemea nikodishe kila apartment kwa kati 500 – 600 USD kwa mwezi.

  Naombeni ushauri wadau, hasa wale ambao pengine tayari wana nyumba za kukodisha Tanzania au wameshajihusisha na mradi kama huu.

  Natanguliza shukrani.

   
 2. K

  Korosho Senior Member

  #2
  Aug 28, 2009
  Joined: Nov 30, 2007
  Messages: 132
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Yebo Yebo, wazo zuri lakini kuna angalizo: bei ya 500-600 USD kwa mwezi inaweza kuwa kubwa kwa walengwa unaowafikiria...Ni vizuri ufanye utafiti zaidi katika hili.

  Ila kwa kiwanja hicho hicho unaweza kuweka ofisi ambazo zitakupa return nzuri kuliko residential apartments...
   
 3. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Naona kama shs 100 milioni hazitoshi kutoa kitu quality cha ukubwa huo.
   
 4. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2009
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Mil 100 ni hela ndogo sana kama alivyosema Bluray kufanya kitu ambacho unatarajia.

  Sina hakika kama upo Bongo au nje. Kama upo nje au hujawahi kujishughulisha na shughuli za ujenzi hivi karibuni ukweli ni kwamba life hapa town imebadilika sana na vitu vingi, hasa vya ujenzi viko juu.

  Mil 100 inatosha kujenga kitu kizuri, lakini katika quality ya $500 - $600 monthly inaweza ikawa ni ngumu. Ila chini ya hapo unaweza kufanikiwa.

  Kuna ramani fulani kwa ajili ya vyumba vidogo, inakuwa na vyumba viwili, bafu, jiko na choo ... ila sio self contained na watu hulipa on average 150K hadi 250K... inategemea ipo wapi, security, barabara (usafiri), upatikanaji wa maji n.k.

  Ila kama kiwanja chako kipo maeneo ya moroko, I believe ni sehemu iliyotulia na uwaweza ukapata zaidi ya hiyo hela niliyosema hapo juu.
   
 5. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #5
  Aug 28, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Wazo lako zuri ila niko mweupe kwenye majengo ya ofisi. Naomba masaada kidogo wa bei za kukodisha ofisi kwa sasa Dar es salaam hasa katika maeneo Kinondoni Morocco, Mwananyamala na Victoria.

  Ahsante
   
 6. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #6
  Aug 28, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Niko nje kwa muda (10+ Yrs) na ndiyo sababu wazo la kuwekeza kwenye apartments yamenivutia kwa sababu nitakuwa sina ulazima wa kuwepo kila siku kufuatilia kipindi ujenzi ukishakamilika.

  Mambo mawili Ramthods na Blueray mmeyagusia yameniweka kwenye utata sana na pengine mfanya biashara yoyote ataogopa: kuongeza mtaji na wakati huo huo kupunguza matarajio ya mapato. Huo ni mtihani mkubwa...

  Nikiongeza kiwango cha mtaji kufikia Shs 200 Mil nitahitaji muda ziadi angalau miaka 5, ujenzi ukamilike 2014. Kwa mtaji huo iwapo nitashusha matarajio ya kodi kufikia 300 USD kwa mwezi kwa kila apartment ina maana mtaji utajilipa baada ya takriban miaka 15 (iwapo nyumba zitakuwa full booked wakati wote..!!). Sio tu kwamba hilo sio jambo rahisi, lakini pia huo ni muda mrefu sana. Itakuwa si busara kuingia kwenye biashara kwa namna hii.

  Naombeni ushauri mbadala; kama upo.!!
   
 7. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #7
  Aug 28, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  regardless of the details, kama hesabu zako ziko sawa, kurudisha hela yako kwa investment ya nyumba katika miaka 15 si deal baya.Think about it, baada ya miaka 15 unakula faida tu na nyumba hii ni bonge la investment itakayosaidia hata vizazi.

  Ukitaka return ya miaka 5- 10 kukodisha si biashara nzuri, unaweza kufanya vizuri zaidi kwa ku flip (go slow please, usiturushie bei kiajabu kama madalali wa DSM).
   
 8. K

  Koba JF-Expert Member

  #8
  Aug 29, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  wewe yeboyebo acha utani na hizo change zako za 100m sijui kama unaweza kutoa kitu quality ya 500$ per month,nafikiri kwa hicho kiwanja kilipo na hiyo size kinazidi hizo 100m...anyway tafuta $$$ zaidi au fikiria kitu kingine cha kufanya na hizo 100m,hi pesa ndogo sana kwa project kama hiyo!
   
 9. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #9
  Aug 29, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Kama walivyoshauri wakuu hapo juu, pesa ni ndogo sana. Utakuwa nayo nafasi ya ku-minimize gharama kama wewe mwenyewe ni mjenzi na utaweza kusimamia still seems you need to tripple that amount. Mahali kiwanja kipo unatakiwa ujenge kitu kizima na tena una option ya kuziuza hizo apartment badala ya kukusanya kusanya miaka 20. Ila hapo unahitaji mahesabu ya mbali sana kwamba utakuwa na uwezo na nia ya kupata sehemu nyingine na kuendelea hivyo.
  By the way kwa habari nilizopata hivi karibuni Tanzania ilikuwa hatuna sheria ya kuuza (au haitoi) subtitles za apartments, ndiyo sasa inafanyiwa kazi.
   
 10. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #10
  Aug 29, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kwa kuongezea majibu ya Bluray, investment ya majengo hairudi katika muda mfupi sana na benefit inayopatikana katika investment kama hiyo ni kulitumia hilo jengo kama collateral ya kukuwezesha kukopa pesa ambazo pia utainvest katika project zinazolipa kwa muda mfupi au kuongeza mtaji wa biashara ya majengo yako.
  (assumption ya ushauri huu: fedha ya awali uliyowekeza katika mradi huo ni pesa yako mwenyewe)
   
 11. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #11
  Aug 29, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Koba,

  Thanks mkuu ila umenitisha sana; plan haikuwa kukopa ila kama Shs 100 Mil ni chenji kwa kiwango cha huu mradi ni itanilazimu niangalie uwezekano wa kukopa...sitaki kukopa kabisa kwa ajili ya mradi huu.
   
 12. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #12
  Aug 29, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0


  Wakuu, nakubaliana na nyie kabisa kuwa miaka 15 sio mingi kwa mradi wa majengo. Ila kauli yangu ya mwanzo ililenga sana ufahamu wa Tanzania ya leo ambayo ukiwekeza "vizuri" Shilingi 1 basi inazaa Shilingi 2 katika kipindi kifupi 2 years au chini ya hapo...nikadhani hili nalo pia lipo kwenye majengo ya kukodisha (kwa miaka 5-10); kasoro ya maarifa yangu ni kuweka matarajio ya kodi juu sana $500-600.


  Nimewasikia, Ahsanteni.
   
 13. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #13
  Aug 29, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wadau,

  Mawazo ya wengi hapa ni kuwa Shs 100 Mil hazitoshi kabisa kwa mradi wa 4 apartments. Nimekubali ushauri wenu....

  Naomba kwa wale wanaojua, wanisaidie tena mawazo. Kwa mtaji wa Shs 100 Mil ni jengo la aina gani nitakaloweza kupata kwa maeneo ya kati ya Morocco na Victoria?


  Lengo ni kupangisha na kurudisha mtaji na faida kidogo kwa njia hiyo na si vinginevyo.

  Nilivyoona; ni vigumu sana kufanya utafiti wa soko na kupata majibu ya uhakika Tanzania; hivyo naogopa sana kukopa hela au kuwekeza zaidi ya kiwango hicho.


  Shukhrani.
   
 14. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #14
  Aug 29, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  kwa mradi kama huo na kwa hiyo fedha ndugu yangu ni kuja kutafuta ugonvi na nduguzo au contractor,
  kama wewe mwenyewe utasimamia hiyo project (ujenzi) katika kila process unaweza kujenga Nzumba nzuri (family house) na kutokana na hilo eneo unaweza kupata 1m kwa mwezi. kwa maaana hiyo fwedha yako inaweza kurudi baada ya miaka 10 na faida itafata baadae, na lazima ujue ndani ya hiyo miaka kumi lazima kutakuwa na renovations za hapa na pale,
  kuinvest kuzuri katika hizi project ni bora kutafuta mkopo, tumia hiyo 100m, kupatia mkopo,
   
 15. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #15
  Aug 29, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Ahsante kwa mawazo yako Kituko,

  Naomba ufafanue kidogo hapo kwenye maandishi ya red. Sijakuelewa unamaanisha nini. Nitawezaje kutumia helo iliyo benki kuombea mkopo?
   
 16. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #16
  Aug 29, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  usiifanye hii biashara kienyeji, fungua company (estate developer) au kitu kama hicho, na hiyo 100 inakuwa kama ndio capital yako pamoja na hicho kiwanja chako, anza hiyo project na andaa mchanganuo wako mzuri wa biashara, kisha unaenda banki kuomba boost ya project yako, kwa hiyo bac kwa hiyo project yako ya 100m inaweza kukupa mkopo mkubwa ambao utaweza kukamilisha hiyo project yako kwa kiwango unachokitaka.
   
 17. Ether

  Ether Senior Member

  #17
  Aug 31, 2009
  Joined: Mar 16, 2008
  Messages: 137
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  yebo yebo ...... i think you shouldn't go after any loans (construction, mezzanine loans) since you have approx. $100K. yu could first start by building 2 apartments then use the profits generated from it after 3- 5 yrs to start the other 2 apartments. ritenow banks don't lend out money on fair interest rates and if you go for the loans yu will end up paying interest (not including the principal) for the lifetime of your apartments. also, yu could build these apartments yourself and not hire a construction company. i know itz time consuming but $100K is no joke to waste.

  anotha option is to build 2 apartments then use them to secure a construction loan (if available) to build the other 2 apartments. by doing this after renting 4 apartments in 5 years you should be able to pay back your loan, but again this economy is jus unpredictable. real estate development is a high risk game!
   
 18. O

  Ogah JF-Expert Member

  #18
  Sep 1, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
 19. Ulate

  Ulate Member

  #19
  Sep 1, 2009
  Joined: Dec 20, 2007
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  babu ni mjengo wa aina gani huo utakaochukuwa miaka mitano hadi kukamilika,pindi pesa unayo na vifaa vya ujenzi vimejaa madukani?.wewe cha muhimu jikusanye ukiwa tayari kifedha wala haitachukuwa muda huo uliosema kwani pesa unayo,mafundi wapo na vifaa vinapatikana aaaah kama unalia,bongo mambo mswano ukiwa na pesa unafanya kila kitu tena fasta
   
 20. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #20
  Sep 1, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Sehemu aliyotaja kwa investiment si nzuiri ki-ofisi labda residential. Na mtaji wake wa 100m ni mdogo sana. Kodi yake hiyo nafikiri alenge hao wazungu wanaotoka nje ingawaje nao wakija huku wanaishia magomeni kusaka za bei rahisi.

  All in all tafuta business nyingine au ongeza mtaji.
   
Loading...