Ushauri: Biashara ipi bora ya usafirishaji kati ya gari la scania au faw?

Mtini

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
1,491
2,355
Wanajukwaa habari zenu!

Mimi ni mjasiriamali sasa nataka kuingia kwenye biashara ya magari (usafirishaji), nina plan ya kuanza na semi moja. Nauliza kwa mnaojua ni vyema nikaanza na gari aina gani kati ya hizi mbili Scania au FAW?
 
Nunuwa bajaj kwa huo mtaji ulionao utapata faida, sumu haijaribiwi kwa kuionja.
 
Maintanance cost gari za kichina zipo chini...unanunua gari mpya au used?
 
hadi dangote anatumia faw.. matajiri wote wa usafirishaji kina asas siku hizi ni faw tu na gari za kichina...

sasa wewe mpya na mtaji wa gari moja inakuaje ununue scania??

kwenye biashara usiangalie sifa za majiran bali angalia wapi hela yako itarudi haraka na kupata faida???
 
Scania ni gari aiseeh ila hii biashara na jinsi ulivouliza sikushauri uingie uku kwa sas utalia,tafuta biashara nyingne mkuu ambayo una uzoefu nayo kidogo
 
Kama ni mpya...Kwa mtu anayeanza ..nunua FAW au HOWO ..ukiacha low maintenance cost ...bei ya scania mpya unapata mchina na chenchi!......ila kama mtaji unao, hela za service zipo za uhakika scania, volvo, benz trucks ni mkataba!

NB: una uhakika wa kazi mahali? Au unategema upate kazi kwa madalali? Kama unategemea kazi kutafuta kwa madalali au ma agent, mimi binafsi siku shauri kuingia katika hii biashara sasa, weka hela yako bank usubiri kwanza au utafute biashara nyingine kwa sasa. Kwa watu wenye truck moja au mawili ....biashara ni pasua kichwa labda kama una mkataba wa uhakika sehemu au truck linahusika na biashara unazofanya.
 
Kwa bei ya Scania unaweza kupata Faw au Howo mbili au moja na chenchi. Anza na Mchina biashara ikikua hamia kwenye scania au brand nyingine nzuri.
 
Kama ni mpya...Kwa mtu anayeanza ..nunua FAW au HOWO ..ukiacha low maintenance cost ...bei ya scania mpya unapata mchina na chenchi!......ila kama mtaji unao, hela za service zipo za uhakika scania, volvo, benz trucks ni mkataba!

NB: una uhakika wa kazi mahali? Au unategema upate kazi kwa madalali? Kama unategemea kazi kutafuta kwa madalali au ma agent, mimi binafsi siku shauri kuingia katika hii biashara sasa, weka hela yako bank usubiri kwanza au utafute biashara nyingine kwa sasa. Kwa watu wenye truck moja au mawili ....biashara ni pasua kichwa labda kama una mkataba wa uhakika sehemu au truck linahusika na biashara unazofanya.
Asante kwa ushauri mkuu ila nitaufanyia kazi
 
Back
Top Bottom