Ushauri: Biashara inakaribia kufilisika, pesa ya biashara inatumika zaidi kwenye mambo binafsi

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,028
Ipo hivi wakuu, kuna biashara ya rafiki yangu ambayo ni ya familia ambayo ilikuwa inaenda vizuri tu inaingiza milioni 8 kila mwezi na ndiyo inayolisha familia

Sasa ile ni biashara ya familia na mkurugenzi ni baba yao, Pesa ikaanza kuchotwa dukani ili mzee afanyie mambo yake kwenye kesi ya kulipwa fidia ya ardhi huko kwao ambapo endapo atalipwa fidia basi atapata milioni 250.

Sasa gharama za kusimamia hii kesi zote zinahudumiwa na duka.

Duka lao kwa sasa lina madeni sana maana hata wanaowakopesha hizo bidhaa wamekosa imani nao.

Mzee kakazia bado ishu za kesi.

Je hapa nini kifanyike?
 
....wamevunja sheria ya biashara apo watarajie anguko tuu.

Biashara ni artificial person na circulation ya damu yake ni ile pesa inayoingia na kutoka,Sasa kama kinachotoka ni kingi kuliko kinachoingia apo tutarajie mauti tuu..

Yaani ni sawa na mgonjwa wa kipndupndu...anachoharisha ni kingi kuliko anachokula.
 
....wamevunja sheria ya biashara apo watarajie anguko tuu.

Biashara ni artificial person na circulation ya damu yake ni ile pesa inayoingia na kutoka,Sasa kama kinachotoka ni kingi kuliko kinachoingia apo tutarajie mauti tuu..

Yaani ni sawa na mgonjwa wa kipndupndu...anachoharisha ni kingi kuliko anachokula.
Ushauri je??
 
Hapo cha Kufanya.. ni Kuzuia KUTOA hela nyingine

Pili
Kupunguza Matumizi ya pesa ktk Familia ili pesa izunguke kufidia pesa inayopotea

Tatu.
Kufanya Uchunguz yakinifu je ni kwel pesa zinaend ktk KESI? zinatumikaje? Uchunguz ufanywe na Familia mmoja wao. Ili Kujua Njia mbadala na kusaidia Kushinda kesi kwa gharama nafuu bil kuharibu BIASHARA.

Nne.
Kuomba Mkopo wa kuimarisha Duka (Ukizingatia BIASHARA imekuwa DAMAGED) Mkopo huo uwe nafuu na Kuwe na masharti ya kutoa hela kwa kugawanya kwa Asilimia na ku rekod kila hela inayotoka na kuingia.
 
Hio biashara ya Million 8 kwa mwezi faida si ni biashara ya hela ndefu sana 😂😂😂 pengine kuzidi hata hicho ambacho huyo mzee anadai
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Back
Top Bottom