Ushauri: Baba hataki nimuoe binti kisa baba yake mkubwa alikuwa mwizi!

Ototo

JF-Expert Member
Jun 26, 2016
1,120
2,000
Mods mnashobo sana, mimi mbona sijaomba mnirekebishie heading? Mmeweka heading isiyovutiwa wachangiaji
 

lenyu

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
449
500
Ayo maneno ya kiutu uzima

Wazee wa siku izi wamoto atakua kashamla uyo so anatafuta sababu usimuoe Ila anashindwa kukuchna ukwel

Msikilize dingi yako anamaanisha
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
121,516
2,000
Mwambie Dingi aache utoto 😂😂😂😂😂 kaza buti uoe haraka kabla wahuni hawajakuzidi speed na kumuoa mrembo au kumpa mimba.
Habarini za wakati huu mabibi na bwana wa JF.......!

Mimi ni kijana wa kwanza kuzaliwa kwa wazazi wangu.

Kwa sasa nina umri wa miaka 27, kama mjuavyo huo ni umri sahihi kabisa wa mimi kuwa na mwenza wa kusaidiana nae kulisongesha gurudumu la maisha...!

Na mzee wangu amekua mastari wa mbele katika kunisisitiza nioe haraka iwezekanavyo....!

Sasa mchumba niliyempata kwa upande wake yuko vizuri kuanzia tabia yake, matendo yake...! Kiukweli ni binti aliyejitunza na kujiheshimu sana, vijana wa kileo tunaita "wife material" na halikadhalika mama yake ni mama anayejishemu na kuheshimu ndoa yake sana....!

Tatizo ni pale nilipomjulisha baba yangu juu ya kutaka kumuoa huyo binti....! Baba mwanzoni alikubali na kumsifia sana yule binti maana anamfahamu,....! Tunaishi jirani tu

Ila mzee hakuishia hapo akafanya uchunguzi akagundua baba yake mkubwa na huyo binti alikua mwizi...! Na aliuwawa kwa ajili ya wizi, kwa mantiki hiyo baba yangu kasema siwezi kumuoa sababu ya baba ake mkubwa kuwahi kuuwawa kwa ajili ya wizi....!

Akiwa na maana ya kwamba hata kizazi changu kinaweza kuwa cha wizi....!

Sasa ndugu zangu hiyo sababu inatosha kweli kumuacha binti wa watu, kwa kuhofia kuja kupata kizazi cha wizi? Hivi wizi huwa nia tabia ya kimalezi au kurithi?

Ushauri wako kwangu ni muhimu sana....! Maana jf kuna ma great thinker wengi
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
52,553
2,000
Mahusiano siku zote ni watu wawili ukiingiza mtu wa tatu tiyali mahusiano yameshaingia dosari

Kosa kubwa mleta mada nikumwingiza baba yako katika mahusiano yako kama mtu wa tatu katika mahusiano yenu .
Jirani yangu ni Engineer Davis, mke wake mrembo alimuoa baada ya kumsomesha mwenyewe mpaka Form Four. Mashemeji wa Engineer Davis wote ni madereva wa yale ma truck yanayokwenda nje ya nchi. Watoto wake wote wameshapata leseni baada ya kuwa makonda wa ma uncle zao.
 

Mpatuka

JF-Expert Member
Nov 15, 2015
725
1,000
Jirani yangu ni Engineer Davis, mke wake mrembo alimuoa baada ya kumsomesha mwenyewe mpaka Form Four. Mashemeji wa Engineer Davis wote ni madereva wa yale ma truck yanayokwenda nje ya nchi. Watoto wake wote wameshapata leseni baada ya kuwa makonda wa ma uncle zao.
😂😂😂una maanisha nini hapa?
 

Niwaheri

JF-Expert Member
May 2, 2020
970
1,000
Huwa inasemekana, mtoto hufata Sana tabia za kutoka kwa mzazi wa kike na uzao wao hasa maankoli, iyo ndio sababu baba kagoma na hakuna lingine.

Ikumbukwe hakuna mzazi anaeweza kuona tatizo na asimwepushe mwanae, unless hakupendi, ila ongea nae athamini hisia zako pia na ufanye uchunguzi baada ya kusikiliza sababu za mzee, tafuta wazee wengine pia ujiridhishe ili unapomjibu uwe well informed
Sina cha kuongezea watu wazima wakati mwingine wanaona mbali na ndo maana zamani wazeee walitahadharisha watoto wao kwamba usioe kwa fulani,pole sana ila tafuta suluhu kwani mama yeye anasemaje
 

Muuza simu used

JF-Expert Member
Aug 23, 2017
3,820
2,000
Mimi mwenyewe kuna totozi nzuri tu nilitaka kuweka ndani dada yangu mwenyewe alimpitisha anafaa kuwa wifi,nikamshirikisha bibi maana tunaelewana sana ananiambia endelea kutafuta mjukuu wangu maana mama wa yule binti ni mchoyo sana aliwahi kumnyima mama yake mkwe chakula akiwa mgonjwa hadi akaaga Dunia kumaanisha na huyu totozi alikuwepo ikabidi nikubali kushingo upande nisepe
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom