Ushauri: Anasema nisubiri aolewe kisha afanye visa aachwe ndio tuwe pamoja

CHIMBULI WA CHIMBULI

JF-Expert Member
Jan 10, 2013
468
160
Wanajamvi! Awali ya yote ningependa niwatakie heri ya krismass.

Mimi ninatatizwa na jambo moja, nalo ni kwamba nimetokea kumpenda binti mmoja hivi lakini wakati najaribu kufuatilia nyendo zake ili nimfahamu na tabia zake vyema akatokea kijana akatoa barua ya kuchumbia bila mimi kufahamu.

Siku namfuata mimi tayari barua ishatoka lakini binti alinikubalia na kuniuliza kwanini nilichelewa? Mimi nikamweleza kuwa nilihtaj nimjue tabia zake japo kwa ufupi.

Niliendelea nae mahusiano na binti kuonesha kunikubali sana. Sasa shida ni kwamba, mahari nusu imetoka na binti aliniambia nimpe muda kidogo kwakuwa kukatiza process kwa sasa ni vigumu hivyo nimvumilie kdogo akaishi na jamaa then atafte kisirani waachane kisha aje kwangu nipige nae pingu za Maisha.

Sasa wadau binti nampenda naye ananipenda ila influence ilimpelekea akubali posa la hyo kijana. Naomba mawazo niendelee kumsubiri nivunje uhusiano wao ili binti nimpate ama nimpotezee?

Ushauri please sio kejeli.
 
Anakupenda wapi wewe!

Huyo kategea, yuko Mguu mmoja ndani Mguu mmoja nje.

Yaani huko mambo yakiharibika, ana uhakika anayo sehemu nyingine ya kuegemea, ambayo ni kwako.

Kingine,

Huyo Mwanamke hafai hata kidogo itakapotokea yuko na wewe, na kukawa na jamaa mwingine mwenye maslahi nae, kaa ukijua na wewe utafanyiwa vituko kama alivyofanyiwa mwenzio na kisha yeye kwenda kuegemea sehemu nyingine.

Kifupi achana nae.

Huyo Demu pasua kichwa
 
Hahaha....hii ndio JF bana.

Kwa akili ya kawaida tu...Kweli Mwanamke anakuambia hivyo na bado unaomba ushauri?

Aolewe na mtu mwingine kwa mahari halafu wewe umsubiri wagombane ndio aje kwako?

Umezoea makombo eeh
2016-08-13-16-02-42--397584204.jpeg
 
Wenyewe wanasemaga haina makombo wala ushemegi... dah ni matamanio tu hapo hakuna ndoa wala mapenzi
 
Umempigia dereva wako wa bodaboda usiku akufate anakokufata akupeleke nyumbani anakwambia napeleka abiria umbali wa km 20 ntakufata nawe unamsubir,labda kama huna haraka,ila kama una haraka unatafuta bodaboda nyingine
 
Nadhani suala hili niliwahi kukutana nalo nilipokuwa na miaka 21 hivi kwa vile niseme tu nilikuwa na akili kama zako za sasa sikuona,
Ukweli uko hivi huyo mwanamke Kwanza anakwambia yeye anaolewa kwa kulazimishwa wala hataki,
Subiri aolewe ili afanye visa aachwe, ukweli kuwa una create problem isiyo na maana,
Mchezo mzima anaucheza peke yake, tafuta watu wa karibu wa huyo jamaa anaetaka kumuowa jaribu kuyachimba utayajua mengi, toka nje ya box la kupenda utauona ukweli kwa upana,
 
Wewe endelea kula papuchi kisela huku ukitafuta mtu mwingine. Huyo dada hafai.
 
Na mm ameniambia akiachana na Wewe anakuja kwangu.

Acha upuuz ni ma GT wa ngono tu ndo wanaweza kufikiria upuuz kama huu.
 
Back
Top Bottom