Ushauri; Ana mtoto wa jicho-haoni vizuri na anataka kupata tiba

Kichwa Ngumu

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
1,726
312
Habari JF; Baba yangu mzazi mwenye umri wa miaka 81 anayeishi katika wilaya ya ludewa mkoani njombe anatatizo la mtoto wa jicho kwenye kila jicho lake na kwa sasa haoni vizuri na alipokwenda hospitali ya wilaya ya Ludewa walimwambia hawawezi kumtibu na baada ya miezi mitatu hata ona kabisa. nataka nimpeleke hospitali ambayo anaweza kutibiwa macho yake na akapona. hospitali yenye historia nzuri na hasa kwa wazee. Wana JF naomba kwa anayejua hospital nzuri aniambie na yenye gharama ambazo mwananchi wa kawaida anaweza kuzimudu. Natanguliza shukrani

Habari JF
 
Kama uko ludewa pia waeza fika Mbeya referral nadhani gharama za kawaida sana, sina hakika kama CCBRT wako karibu huko ludewa.
 
Tatizo lake linatibika kwa kufanyiwa opareshen yaani surgery ambayo inaitwa (Cataract Surgery)Hii inafanywa kwenye hospitali nyingi za mkoa si opareshen kubwa sana na within a week atakuwa poa kabisa wala haina gharama
 
Chief - Mpeleke CCBRT .

Nenda CCBRT.

Kama uko ludewa pia waeza fika Mbeya referral nadhani gharama za kawaida sana, sina hakika kama CCBRT wako karibu huko ludewa.

Tatizo lake linatibika kwa kufanyiwa opareshen yaani surgery ambayo inaitwa (Cataract Surgery)Hii inafanywa kwenye hospitali nyingi za mkoa si opareshen kubwa sana na within a week atakuwa poa kabisa wala haina gharama

Ushauri wa m2flani name Balaki uzingatie, btw nyamatarekwetu acha utani, hayajakukuta

Asanteni sana kwa wote mlionishauri; nilimpeleka babangu CCBRT ametibiwa kapona kabisa hata yeye (baba) hakuamini km anaona.
CCBRT wame mhudumia vizuri tena kwa kutumia bima ya afya kwenye kila kitu hadi chakula; gharama yetu ilikuwa kumsafirisha tu.
Nichukue nafasi hii pia kuwashukuru CCBRT kwa huduma yao nzuri na nawaomba wa endelee hivyo hivyo na hospitali nyingine waige mfano wa CCBRT.

Vituko baada ya kuona.
Baunsa alikuwa anapita km mita 15 toka alipobaba; baba akasema mwoneni yule anatembea km anataka kupigana kuweni makini.
Mdada alivaa kimini; baba aliuliza hawa ni watoto wa mtaani?
Sharobaro alipita kwa style ya kudunda dunda; baba huyu akitembea kwa kuruka ruka hivi hadi jioni si atakuwa amechoka sana.

Kifupi nawashuru sana kwa ushauri wenu.
 
Hiyo CCBRT iko mkoa gani mkuu?maana hata mimi nasumbuliwa na huu ugonjwa kwa muda mrefu!NAOMBA UNIPM UNIPE NAMBA YAKO
 
CCBRT ipo DAR ES SALAAM,
ukifika/kama upo Dar panda daladala zinazokwenda Msasani, Shuka kituo kinaitwa Macho au CCBRT.
Hapo kituoni muulize yeyote hosp ccbrt iilipo utaonyeshwa ni mwendo wa dk 3 au 5 kutoka hapo kituoni.
 
Asanteni sana kwa wote mlionishauri; nilimpeleka babangu CCBRT ametibiwa kapona kabisa hata yeye (baba) hakuamini km anaona.
CCBRT wame mhudumia vizuri tena kwa kutumia bima ya afya kwenye kila kitu hadi chakula; gharama yetu ilikuwa kumsafirisha tu.
Nichukue nafasi hii pia kuwashukuru CCBRT kwa huduma yao nzuri na nawaomba wa endelee hivyo hivyo na hospitali nyingine waige mfano wa CCBRT.

Vituko baada ya kuona.
Baunsa alikuwa anapita km mita 15 toka alipobaba; baba akasema mwoneni yule anatembea km anataka kupigana kuweni makini.
Mdada alivaa kimini; baba aliuliza hawa ni watoto wa mtaani?
Sharobaro alipita kwa style ya kudunda dunda; baba huyu akitembea kwa kuruka ruka hivi hadi jioni si atakuwa amechoka sana.

Kifupi nawashuru sana kwa ushauri wenu.

hahahaha, mkuu umenifurahisha sana! kumbe sio mchezo mtu kutokuona kwa muda mrefu, hahaha
haya msalimie baba au tupe nyingine mpya baba aliyosema
 
Thanks mkuu!
 
Salamu zimefika ila anataka akuone

Kingine baba alikuwa na presha kipindi haoni ila chakushangaza baada ya kuona tatizo la presha halipo tena nadhani ilisababishwa na msongo wa mawazo wa kutoona
 
Mkuu naomba msaada wako,niPM then nikuulize baadhi ya maswali juu ya hii huduma
 
Asanteni sana kwa wote mlionishauri; nilimpeleka babangu CCBRT ametibiwa kapona kabisa hata yeye (baba) hakuamini km anaona.
CCBRT wame mhudumia vizuri tena kwa kutumia bima ya afya kwenye kila kitu hadi chakula; gharama yetu ilikuwa kumsafirisha tu.
Nichukue nafasi hii pia kuwashukuru CCBRT kwa huduma yao nzuri na nawaomba wa endelee hivyo hivyo na hospitali nyingine waige mfano wa CCBRT.

Vituko baada ya kuona.
Baunsa alikuwa anapita km mita 15 toka alipobaba; baba akasema mwoneni yule anatembea km anataka kupigana kuweni makini.
Mdada alivaa kimini; baba aliuliza hawa ni watoto wa mtaani?
Sharobaro alipita kwa style ya kudunda dunda; baba huyu akitembea kwa kuruka ruka hivi hadi jioni si atakuwa amechoka sana.

Kifupi nawashuru sana kwa ushauri wenu.
Kwa kukadiria ulitumia kama kiasi gani cha pesa?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom