Ushauri: Amekuwa ni mtu mwenye hasira na kubadilika badilika

ladyc

Member
Feb 10, 2017
29
30
Habari za jumapili,

Nipo hapa ndugu zangu naomba msaada wenu wa mawazo katika hili...

Mimi ni ke na nina mpenzi wangu na ukweli I love him so much lkn ni week ya pili sasa uhusiano wetu umekua na matatizo ambayo binafsi nmeshindwa kupata solution ya tatizo. Kiufupi mm na huyu mpenzi wangu tangu tumeanza uhusiano wetu tulikua tukiishi mbali mbali lkn kwa kipindi chote cha nyuma tulikua ni couple yenye furaha, amani yani hadi mwenyewe nakiri kusema namshukuru Mungu kwa kunipa huyu mwanaume he is so loving na sijawahi kumeet na mwanaume mwenye tabia yake kiufupi nampenda sana kutokana na kuona tunaishi mbali mbali na is not good kwa afya ya uhusiano wetu ikabidi mimi nifanye maamuzi ya kuhamia ile sehemu tuliyokubaliana maisha yetu tutaishi hapo namshukuru Mungu nililifanikisha ingawa kwa ugumu kidogo sababu mimi ni mwajiriwa wa serikalini.

Huyu mwenzangu yeye anafanya kazi nje ya nchi na bahati mbaya alipata matatizo fulani huko kazini kwake na hapo ndio ikawa chanzo cha sisi kutoelewana. Ni week ya pili sasa amekua ni mtu mwenye hasira, mnaweza mkaongea baada ya dakika anabadilika, nikimtumia message anaitafsiri tofauti nikisema nikae kimya ananiambia simpendi yani hadi nashindwa kumuelewa, yani hakuna sasa hivi ninalofanya kwake likampendeza.

Nikisema nimshauri ananiambia hapendi kuona message zangu na nikikaa kimya analalamika simjali, muda mwingine hadi ananiblock yani vituko vimezidi, kinachoniumiza zaidi hupenda kuniambia mimi sina nia ya kuishi na yeye na hapo hapo amesahau mimi nimetransfer nilipokua mwanzoni kwa ajili yake na hii ndio point yake asubuhi mchana na jioni.

Naombeni ndugu zangu nisaidieni nifanye nini ili niweze kumsaidia arudi katika hali yake ya mwanzoni maana kila kitu nmefanya ila bado hali ni ile ile. Yeye pia ni member humu, ushauri wenu pia nahisi unaweza msaidia kulichukulia tatizo alilonalo kama ni hali ya kawaida maana nahisi kuchanganyikiwa at the axtent.
Am sorry baby ukiona post hii usikasirike nimefanya hivi ili na wewe upate msaada uweze kuondokana katika msongo wa mawazo unaokusumbua. And I do it for the sake of our love, nakupenda my 'L'
 
Ingawa hujatuambia tatizo lililompata kazini, nitaanzia ulipoishia..!

Kwanza,nakupa hongera kwa uwasilishaji wako mzuri,unatakiwa uelewe hizo ni frustrations za matatizo ya kazini ndio zilizopelekea hayo mabadiliko (kulingana na maelezo yako).

Pili, shukuru Mungu kuwa bado ana mapenzi na wewe(maana bado anaonesha wivu na kujali sometimes) licha ya vurugu zake za hapa na pale. Hiyo ni kama mama mjamzito anavyokuwa msumbufu kwa mumewe, na asipomuelewa, anaweza kuhisi mke wake anamchukia, kuwa na amani, he is still in Love.

Tatu, huo ndio wakati wako muhimu sasa wa kumuonesha mapenzi ambayo hata yeye na watu wenu wengine wa karibu watashangaa, (usitetereke na vurugu zake hata kidogo). Trust me, ukisikia kwenye safari ya mafanikio kuna mabonde na milima, ndiyo haya sasa, muoneshe kumthamini na kumjali hata kuliko zamani, mapenzi sio mchezo.
 
Asante bby nmeona ujumbe wako
Hahaha natania tu mm cyo mlengwa ingawa nakushaur tu. jitahid kuwa mbali nae cz mapnz yanakuwaga matamu kama mkiw mbali plus kumisiana bt mkiw karibu na mmoja wapo akaharbikiwa na mambo yake bas anakosa aman cz alishakuzoesha maisha flan hv mazur so mambo yakiw mabaya kwake anakosa aman na kuona kama hautarizika nae kwa hali hii igawa ww unajtahd kuonesha kila uwezalo kumsuport but upande wake hayuko hivo na hewz kuw hvo cz tial anajihis inferior.
 
So namsaidiaje sasa
 
Hata mm nna tatizo kama lako yani demu wangu ana nongwa simu hanipigii msg hatumi Sasa dawa yake tuwe pamoja ili tuwakomeshe au unasema
 
Pole sana kwa dhara hili linalokupata!

Una maana gani kusema " Yy pia ni member humu ushauri wenu pia nahisi unaweza msaidia kulichukulia tatizo alilonalo kama ni hali ya kawaida maana nahisi kuchanganyikiwa at the axtent.

Am sorry baby ukiona post hii usikasirike nmefanya hivi ili na wewe upate msaada uweze kuondokana ktk msongo wa mawazo unaokusumbua..... And I do it for the sake of our love, Nakupenda my 'L'"

Umekosea kuileta thread humu wakati naye anatumia JF,Nadhani hatolipenda hili endapo ataiona thread yako.Kwakuwa ushai-post humu,Nikushauri jambo fulani...

Kama wewe ni Mkristo kaisome biblia na Mungu atakufunulia Majibu ya matatizo yako,Kama siyo Muombe Mungu pia kwa imani yako naye atafanya njia.
 
Labda my L wako ana frustration si unesema kapata matatizo kazini

Mvumilie

Ila my L wa mleta uzi ukipita...jua hasira zako za.kibarua zitakusababishia ukose mwana na maju ya moto...unapitia kipindi kigumu ndio ila tuliza hasira.....
Naomba Mungu anisaidie nisichoke mapema maana hali ni tete
 
Time heals.....mambo ya pesa haya hususani kipindi hiki cha hapa kazi tuu sometimes yaanasababisha frustration saaana.

Kuwa kawaida kabisaa....kama ulivyokuwa...

Don't show any changes
 
"L" popote unapoona msg yangu hii you are very lucky guy, na nakushauri usiteme big G kwa karanga za kuonjeshwa. Hakuna mwanamke karne hii tena nchi hii anayeweza kwenda umbali alioenda mwenzio kwa ajil ya LOVE kwa mwenzie , ni wachache sana na katika hao wachache mwanamke wako ni mmoja wao.
Nataman kuendelea kuongea lakini nashindwa.
 
Ingawa hujatuambia tatizo lililompata kazini, nitaanzia ulipoishia..!

Kwanza,nakupa hongera kwa uwasilishaji wako mzuri,unatakiwa uelewe hizo ni frustrations za matatizo ya kazini ndio zilizopelekea hayo mabadiliko (kulingana na maelezo yako).

Pili, shukuru Mungu kuwa bado ana mapenzi na wewe(maana bado anaonesha wivu na kujali sometimes) licha ya vurugu zake za hapa na pale. Hiyo ni kama mama mjamzito anavyokuwa msumbufu kwa mumewe, na asipomuelewa, anaweza kuhisi mke wake anamchukia, kuwa na amani, he is still in Love.

Tatu, huo ndio wakati wako muhimu sasa wa kumuonesha mapenzi ambayo hata yeye na watu wenu wengine wa karibu watashangaa, (usitetereke na vurugu zake hata kidogo). Trust me, ukisikia kwenye safari ya mafanikio kuna mabonde na milima, ndiyo haya sasa, muoneshe kumthamini na kumjali hata kuliko zamani, mapenzi sio mchezo.
Sikuona kama ni busara kuweka wazi tatizo lililompata....... Lkn nashukuru sana kwa ushauri wako nitaufanyia kazi
 
Pole sana kwa dhara hili linalokupata!

Una maana gani kusema " Yy pia ni member humu ushauri wenu pia nahisi unaweza msaidia kulichukulia tatizo alilonalo kama ni hali ya kawaida maana nahisi kuchanganyikiwa at the axtent.

Am sorry baby ukiona post hii usikasirike nmefanya hivi ili na wewe upate msaada uweze kuondokana ktk msongo wa mawazo unaokusumbua..... And I do it for the sake of our love, Nakupenda my 'L'"

Umekosea kuileta thread humu wakati naye anatumia JF,Nadhani hatolipenda hili endapo ataiona thread yako.Kwakuwa ushai-post humu,Nikushauri jambo fulani...

Kama wewe ni Mkristo kaisome biblia na Mungu atakufunulia Majibu ya matatizo yako,Kama siyo Muombe Mungu pia kwa imani yako naye atafanya njia.
Asante ila sikua na maana mbaya kuileta huku nia yangu ilikua ushauri utakaotolewa unaweza ukampa ahueni asijione ni yy peke mwenye matatizo..... Nasali sana pia na nnaamini Mungu atafanya njia
 
Jitahidi uwe naye usiku mmoja umliwaze, watafute makungwi wakupe uzoefu ni kwa namna gani unatakiwa umliwaze mwanaume mwenye frustrations
 
Back
Top Bottom