USHAURI: Achana na kutembea na CVs andika Application Letter (Barua ya kuomba kazi) kwa mwenendo huu

FAHAD KING

JF-Expert Member
Sep 14, 2017
301
373
Wanabodi

Habari za mchana kwa member wote wa humu JF.Wengi ni walezi wa watoto ambao bado wanasoma (Advance) ningependa kutoa pole kutoka kwa moyo wangu mkunjufu kwa mihangaiko ya hapa na pale maana Sanitizer, Barakoa,Kilo za Tangawizi na Malimao sio poa.Uchumi umeyumba sana pia niweke Hongera kwa wote. Mungu awatilie uwepesi kwenye utafutaji wenu wa halali.

Kwa wale Wazee wa kuunga unga nanyi sitawasahau.Mungu awaone kwa jicho lake la neema.Awape rizki za kutosha mpaka ushangae.Yaani kama wewe dalali basi uweze kua na uwezo wa kununua nyumba kabisa sio tu kuunga unga kwa kutafuta wapangaji wanachuo wa IFM,UDSM,CBE au Kilimanjaro College. Amen!!

Nisiwachoshe, nafahamu mihangaiko ni michosho tosha kwa siku.Hebu soma tena kichwa cha habari.Kimeandikwa:Achana tena na CV andika Application Letter kwa mtindo huu huenda ukawa wa kipekee sana na kuweza kukusaidia kupata kazi kwa haraka sababu ya ubunifu ndani yake.

Tufahamu tu kwamba tunapata wasomi wahitimu zaidi ya 300,000 kwa mwaka ngazi za vyuo.Nadhani takwimu ziko na ukweli ndani yake.Niko tayari kurekebishwa kama bado hatufikii idadi hii ya wahitimu kwa mwaka Tanzania. Ni idadi ya wahitimu wengi sana kulinganisha na miaka ya nyuma.Hapa naongelea kuanzia mwaka 2015-2020 and counting.Idadi inaweza ikawa kubwa sana kwa miaka michache ijayo.

Bila kusahau ajira ambazo zinatolewa kwa mwaka na serikali pamoja na mashirika ambayo si ya kiserikali haizizidi 150,000 kwa mwaka mzima.Plus umri wa kustaafu miaka 60+ ko ni nadra sana kupata ajira ndani ya serikali. Kwa hesabu ambayo haihitaji hata kikokotozi (Calculator) au hata formula za kihesabu (Mathematics Formula) ni kwamba, idadi ambayo wahitimu watakua ajira kwa mwaka ni 150,000 hawa watakua mitaani tu wakizunguka.Wengi hawatakua na chakufanya sababu Elimu si Guarantee ya Maisha Bora Mtaani.

Kuna Thread nyingi tu humu JF zinaelezea Ushauri hasa kwa wasomi wetu.Namna ya kujiajiri nk.Lakini mi leo nitaelezea namna ya kipekee ya kuandika Application Letter (Barua za kuomba kazi) ambazo hazijazoeleka sana kwenye makampuni tofauti. Sina uhakika wa moja kwa moja ila nina imani huenda kuna mtu kama sio watu watanufaika na Thread hii kwa namna moja ama nyingine.

Twende kwenye Mada.

Mtindo wa kuandika barua za kuomba kazi huambatanishwa na CVs mara nyingi wengi hufanya hivi.Mtu ataandika kazi ambayo angependa kufanya blah! blah! Nyingi kisha anaambatanisha CVs zake za Elimu. Sio mbaya kuambatanisha CVs ila muenendo huu umezoeleka sana na ushapitwa na wakati.Haustahili tena kuwepo kwa dunia ya sasa.Kuwa kitofauti kuna ka asilimia kakubwa sana la kufikiriwa.

Mitaa mingi ya Posta, Dar Es Salaam utaona wasomi wakizunguka kutafuta huku wamebeba vyeti vyao ajira si mchana si asubuhi wala si jioni.Muda wote wapo.Na mara nyingi hua kazi wanakosa. Sababu kubwa ukiacha na ile ya Technical Know Who pia ubunifu wa kuandika barua unachangia kwa kiasi chake. Imagine watu 150,000 wanaandika kwa mtindo mmoja tena wengine wana Grade nzuri sana pamoja ya GPA hapo kuna nafasi kweli?..Ipo sema ndogo sana nikama tembo kupita kwenye tundu la sindano.

Chakufanya ni hiki

Ukiwa unaandika barua ya kutafuta kazi labda kwenye makampuni binafsi usiishie kuandika blah! blah! za kila siku tena mwishoni unamalizia "Wako Mtiifu katika Ujenzi Wa Taifa" hapana. You need a little change

1:Jifunze historia ya kampuni
Ni muhimu sana kujua historia ya kampuni vizuri kwasababu hata kwenye Interview unaweza ukashuka nondo mpaka ma meneja wakashangaa.

Mfano kwenye Application Letter ukaandika
....Naifahamu kampuni ya CCTV FOOTAGE kwa miaka 10 sasa.Imekua ikifanya vizuri kwenye soko suala ambalo limekua likileta wateja ndani ya nje ya nchi.Toka ianzishwe mwaka 1960s CCTV FOOTAGE imekua ikiboresha bidhaa zake za Camera, TV na Kompyuta mpakato (Laptops).

Endelea kidogo afu tuliza

2:Fahamu Lengo la Kampuni
Kwenye uandishi suala la Malengo ya kampuni yafanye kipaumbele chako.Mfano

...Nikiwa kama mwajiriwa wa kampuni nitahakikisha kuna ushirikiano haina ya watu watatu.Wamiliki na Wafanyakazi wa kampuni.Wamiliki pamoja ya Wateja wa kampuni pia wafanyakazi pamoja na Wateja wa kampuni.Suala la Ushirikiano wa Wamiliki na Wateja ni kwenye eneo la kuwasilisha maoni ya moja kwa moja kuhusu ubora na ubovu wa bidhaa kwa lengo la kuboresha zaidi. Ushirikiano baina ya Wamiliki na Wafanyakazi ni pamoja na kuleta Ushindani baina ya Wafanyakazi kwa kufanya juhudi zaidi pamoja na motisha za hapa na pale hali itakayofanya kampuni kua na ubunifu wa hali ya juu kabisa.Pia ushirikiano haina ya Wateja na Wafanyakazi ni urafiki wa karibu wa wafanyakazi kutunza wateja ikiwa sambamba na lugha za kishawishi baina ya mteja na mfanyakazi.

Hayo hapo huwezi ukakuta kwenye Barua za wasomi wengi.Ni kitu muhimu sana kwenye kampani yoyote ile

3:Fahamu mashirika pinzani kwa kampuni

Kwenye biashara hiki kitu ni cha kawaida mno.Mfano Mo Energy Driver na Azam Energy Drink,Juice za maembe pia na nk

Weka banana mashirika ambayo ni shindani kwa shirika ambalo unaona kazi kisha weka mikakati jinsi ambavyo unaweza kuasaidia kuweka Status ya kampuni endapo ukipata chance ya kuajiriwa.Strategies sio lazima za muda mfupi, hata 5-10 years ina matter.Mfano

...Tukifanya haya na haya (orodhesha) tunaweza tukapata solo ndani la uhakika pia kupanua soko la nje na kufanya bidhaa kuzunguka kwa kiwango kikubwa kuliko hapo mwanzo.Mfano,tukijenga kiwanda cha Ngano DRC CONGO tutapata solo ndani ya nchi za Afrika ya kati kwa urahisi zaidi kuliko kusafirisha kutoka Dar Es Salaam.

Hapo ni vyema ujue sera za nchi husika kwenye suala zima kujenga viwanda nk.

4: Ambatanisha CVs
Ni suala muhimu sana.Ikumbukwe sijapinga hili isipokua nimepinga mwenendo wa kuandika barua za kuomba kazi ambazo zimeoleka kila siku, kila miaka, kila mhitimu lazima aandike hivyo hivyo kama wanavyo-google.

NB: SIMAANISHI ukiandika hivi basi ajira nje nje hapana.Ila nachotaka kusema ni kwamba ukiandika hivi basi una asilimia fulani ya kufikiriwa sababu ya Contents zilizomo kwenye barua.

Weekend njema

Ignore Typing Errors
 
Applications 200 POST moja nani ana muda wa kusoma barua, lakini anachosema mkuu ni sahihi kama application yako ikipitiwa they need SOMEONE like that sio kukariri mabarua
Nafahamu ni ngumu sana kusoma Application Letter zote hizo..Lakini ni vyema kidogo ili kua una uhakika walau kwa asilimia ndogo
 
Nimecheka sana, niwie radhi kwa cheko langu.
Sir hayo yote manne uliyoyaandika yapo kwenye tovuti mbalimbali you just Google utaona yani hivyo hivyo kwamba sijui soma historia ya kampuni yako waaaaaay back and people do that.

.
Kupata kazi ni nyota, kujuana na bahati, na ujuzi extra hakuna kingine.
.
Umeenda kuomba kazi NSSF unakutana na wenzio 500 na nafasi ni 20 tu wenye sifa zinazofanana mko 499!😝 utapenyaje hapa kama hujuani, huna bahati na huna vigezo vya ziada ambavyo hata wao hawavifikirii?
 
Nimecheka sana, niwie radhi kwa cheko langu.
Sir hayo yote manne uliyoyaandika yapo kwenye tovuti mbalimbali you just Google utaona yani hivyo hivyo kwamba sijui soma historia ya kampuni yako waaaaaay back and people do that.

.
Kupata kazi ni nyota, kujuana na bahati, na ujuzi extra hakuna kingine.
.
Umeenda kuomba kazi NSSF unakutana na wenzio 500 na nafasi ni 20 tu wenye sifa zinazofanana mko 499!😝 utapenyaje hapa kama hujuani, huna bahati na huna vigezo vya ziada ambavyo hata wao hawavifikirii?
Wala usicheke mwenzangu...Ni kwl lkn
 
Uko sahihi kabisa hii ni applicable endapo usahili unafanyika kwa uwazi mkubwa sana.

Shida kazi nyingi ni watu wanaajiriwa kwa vimemo, au unajuana na nani pale?

Ila kwenye private company kidogo ina sound endapo Director anakuwa mkari hasa kwenye kuajiri
 
Uko sahihi kabisa hii ni applicable endapo usahili unafanyika kwa uwazi mkubwa sana.

Shida kazi nyingi ni watu wanaajiriwa kwa vimemo, au unajuana na nani pale?

Ila kwenye private company kidogo ina sound endapo Director anakuwa mkari hasa kwenye kuajiri
Vimemo mmhh!!! Nimekuelewa Chief
 
Mkuu hii style ya uandishi nzuri, Nina jamaa angu RDC aliandika kwa style hii ,baadae akapewa kitengo / ofc km sehemu afanye wazo lake ilikua ni mambo ya IT ,kampuni ya madini
 
Najiuliza wakiamua kutumia wazo lako bila kukuita uletekeleze inakuaje
Kuna mambo mengi sana katika hili chief.Kuna wadau wengi sana nimewahi kuwasikia hasa wakiongelea kuhusu baadhi ya vipindi Clouds..Wanasema Nyumba ni Choo, Malikia wa Nguvu nk ni idea za watu ambazo wametuma kama hivi sema wanakataa kisha baada ya muda wanaanza kuzitumia pasipo ridhaa yako.

Hapo huwezi ukafanya kitu kisheria sababu wakati unaandika hapakua na masharti yako.Sasa unachotakiwa kufanya ni hivi...Ukiandika Idea yako ambatanisha na Mkataba unaojulikana kwa mwanasheria wako.

Mfano:Kabla ya Idea yako kuipeleka kwenye kampuni hakikisha Luna mkataba kwanza kabla ya kuona idea yako.Mkatana unaweza kuandika Simply and Clear kwamba;

Endapo hutapendezeshwa na Idea hii basi ni wajibu wako kutoitumia sehemu yoyote ile na kama ukiitumia basi ni uvunjifu wa sheria kisha asaini Ndio au hapana kabla ya hata kuona Idea yako

Kuna wengi sana wamepigwa za macho katika hili.Idea zao nyeti zinakataliwa afu baada ya muda zinaanza kutumika pasipo ridhaa yao.Mambo kama hayo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom