Ushairi: Karibu mabadiliko

SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,616
7,863
KARIBU MABADILIKO
Nawasalimu kwa hamu, wabara na visiwani
Mimi malenga adimu, najitosa shehereni
Sherehe hii adhimu, nikikosa nitafuteni
Karibu mabadiliko, hongera watanzania

Yalianza mafuriko, wakayabeza Lumumba
Ufipani kwa muamko, wakageuza ndio mwamba
Wakajenga mitiririko, sisiemu wakaita kamba
Karibu mabadiliko, hongera watanzania

Vijana wa kila rika, mabadiliko waliyadai
Na wazee pasina rika, wakaimba kwa kujidai
Kina mama wakafurika, kwa hiyari bila madai
Karibu mabadiliko, hongera watanzania

Mabadiliko ya sera, si sura tulizozoea
Elimu isiyo kera, ni msingi wa kuzozea
Ombaomba inakera, mali zetu tumepotezea
Karibu mabadiliko, hongera watanzania

Tunaianza safari, mabadiliko ndio sera
Tumejaliwa mandhari, mali na wanasera
Tuzikatae mahari, ufisadi usiwe sera
Karibu mabadiliko, hongera watanzania

Sisiemu baibai, asante kwa utumishi
Kwa miongo ulilaghai, ufisadi tuliuishi
Maendeleo hayajai, nusu karne hatujilishi
Karibu mabadiliko, hongera watanzania

Amani tunda la haki, tuitunze bila visasi
Mabadiliko ni haki, maneno bila risasi
Tubadilike kwa haki, dhahabu na almasi
Karibu mabadiliko, hongera watanzania

Mabadiliko ni Lowassa, hayaji bila ya wewe
Kwanza tuache siasa, ni kazi bila kiwewe
Kagame mfano hasa, wanyarwanda ni kama wewe
Karibu mabadiliko, hongera watanzania

Mimi malenga adimu, namekuja kwa msimu
Mabadiliko ya hamu, yanakuja kwa msimu
Usijeyatia ndimu, yakachacha bila msimu
Karibu mabadiliko, hongera watanzania
------------​

RAI YANGU: Ndugu zangu wa JF, nawatakieni upigaji kura wa amani. Tujitokeze kwa wingi kupiga kura ili tulete mabadiliko tunayoyataka - kupitia kwa Lowassa (UKAWA) au kupitia kwa Magufuli (CCM).

Tunayo maisha baada ya uchaguzi. Maendeleo yataletwa na sisi wenyewe mmoja mmoja na katika ujumla wetu bila kujali itikadi zetu za kisiasa. Vyama vya siasa na wanasiasa kazi yao kubwa ni kuweka mifumo rafiki na shirikishi ili sisi wenyewe tuweze kuleta mabadiliko katika maisha yetu binafsi, jamii zetu na taifa kwa ujumla.

Mabadiliko yataanza na wewe na mimi kwanza kwa kufanya uamuzi sahihi lakini pili kwa kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa letu kwa kutumia vema mali na vipawa tulivyonavyo.

Asanteni sana, nawatakieni afya njema na kila la heri siku ya tarehe 25 Oktoba 2015 na baada ya hapo.
 
Team lowasa takamstake ikulu mtaisikia radioni magazetini hatapia kwenye TV mtaisoma namba
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Wameifanya jeuri, wananchi kubeua,
Sera zao za hatari, za raia kuwaua,
Linawangoja kaburi, ndivyo tulivyoamua,
FISIEMU baibai, karibu mabadiliko.
 
Team lowasa takamstake ikulu mtaisikia radioni magazetini hatapia kwenye TV mtaisoma namba
Tanzania iwe mbele, vyama vyetu namba mbili
Usilete kimbele mbele, wa moja havai mbili
WanaUkawa wapo tele, sisiemu namba mbili
Karibu mabadiliko, hongera watanzania
 
Back
Top Bottom