Ushahuri wa bure kwa wamiliki wa Clouds na Mh. Sugu

kabindi

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
333
120
Kwanza Clouds!
Hakuna ubishi kwamba mnasikika kwa wengi na hasa katika vijana. Mmejipatia umaarufu kutokana na ubunifu wenu wa kutoa burudani na kutangaza. Bado kwa kiasi kikubwa mnaheshimika katika tathnia ya Muziki na Habari! kwa bahati mbaya sana ni kama mnaanza kupoteza mwelekeo wa mlichokusudia au mnachokusudia katika jamii ya Watanzania kwa kutaka kuwa na malumbano au kwa kujitetea katika misingi ya kuwakandamiza wapinzani wenu! Msifanye kosa hilo kwani litawaghalimu sana! mnaweza kutoweka kabisa katika akili za watanzania mkajikuta mnaharibu business zenu! kwani mkikosana na mtu katika jambo lolote hamuwezi kukaa chini na kumaliza tofauti zenu?! hivyo arrange na Mh. Sugu ili mmalize tofauti zenu la sivyo Sugu atawamaliza maana kajipanga na anakubalika!. Kingine pia, inaonekana kama mko kwa karibu sana na Sysytem kwa maana ya Serikali au kuna watu wanaonufaika na System kiasi cha baadhi ya watangazaji kushindwa kuficha hisia zao!. Si vibaya kushirikiana na System ila katika tathnia ya habari na hasa Radio jitahidini kuwa neutral maana mnawatangazia walio wengi. Hisia zako za moyoni zisitawale matangazo ila mwongozo na ethics mlizojiwekea ndizo zitangulie kama wanavyofanya Radio nyingine!. Jaribuni kusoma nyakati, pimeni mwelekeo wa kisiasa maana kuna watu wanazama hata ikipita miaka 10 dalili hazionyeshi kwamba watapona na wakati huo mtajiweka katika mizani gani?.

Mh. Sugu!
Hongera zake maana hakuna ubishi kwamba mh Sugu nyota yake inazidi kung'ara! ana supporters wengi kwelikweli na hii ni tangu nilipomfahamu tukiwa tunasoma wote pale Mbeya Day, maana shughuli ya Muziki kaianza mapema wakati ule akiwa ana-rap na kudanc na wakati huo akivalia suruali kifuani! checkbob kwelikweli wakati huo na chunusi kwa wingi BUT really Smart!. BIG UP MEN umetoka mbali!. Namshauri yafuatayo; Achana na malumbano yatakupunguzia sifa! ili uendelee kukubalika na watu wa kaliba zote fanya jitihada zote na wakati wote kujitengenezea heshima!. najua ni mpiganaji na wakati mwingine huwa hukubali jambo kirahisi na pale unapoonewa! badilika kwa sasa maana unao supporters wa kutosha likiharibika jambo wambie supporters nao watahukumu!. Tumia muda wako kuleta na kutafuta mbinu za kuleta maendeleo jimboni kwako maana 2015 si mbali hata kama hutapenda kuendelea wewe lakini usikiangushe chama chako! Bila shaka umeishajitengenezea kamati ya kuleta maendeleo na pengine kutokana na muongozo wa Chama chako!. Achana na upuuzi wa kulumbana maana unaweza kukasilishwa ukajikuta unazungumza mambo yatakayokuondolea heshima. Mwisho burudani yako tunaitaka, ukiwa unapata nafasi kama ilivyojitokeza juzi, tuite tutakuja!
 
mkuu kwa mtazamo wako kajikita zaidi kwenye burudani kuliko maendeleo ya jimbo lake mbona huko atujasikia malalamiko jambo la msingi ni ruge kuachana na mambo binafsi kuchanganya na radio hiyo ndio pointi kubwa kama vipi yeye ruge akomae na juhudi za kuibadilisha clouds kuwa radio ya taifa kama inavojionesha sasa.

sugu komaa na kazi yako ya uwaziri kivuli kupigania sanaa iwe inalipa pamoja na hip hop ya kibongo na yenyewe ilipe.

jm
 
S6302667.JPG
Salaam kutoka kwa mashabiki
S6302650.JPG

S6302585.JPG

S6302673.JPG

S6302642.JPG

S6302730.JPG

S6302598.JPG
Sehmu kubwa ya Maeelfu ya watu waliojitokeza kwenye tamasha la kihistoria la Vinenga
S6302736.JPG
Wadau Mbalimbali
S6302633.JPG
Mheshimiwa Mbunge wa Mbeya Mjini- Chadema Joseph Mbilinyi ‘Sugu'(Kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na Mdau Hajji Muki na Kulia ni Mheshimiwa Mbunge wa Ubungo -CHADEMA)John Mnyika ndani ya Tamasha la Vinega Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook


Older Posts Home
 
You have handed them a very constructive advice but I am afraid neither Sugu nor Cluods will bother buy it. Two parties' minds are rife with a sense of blood feud to an extent of being ready to take life of each other. At this stage of strife nothing can really be done to reconcile them but should rather be ignored and watched from afar because the fact that people keep on talking and exaggerate the contention give them a reason to perpetuate the situation.
 
  • Thanks
Reactions: Obe
Hapa ule mwimbo wa Sugu kolabo na hayati Justin kalikawe unaingia akilini - "Haki"

Sugu was way ahead of his time! To date he is still championing haki kwa wasanii wote wa bongo flava! You go, boyyyyyy!!!
 
kukaa chini na kumaliza tofauti kwa majadiliano ni njia bora kabisa iwapo pande zote husika zitakua na dhamira ya dhati kufikia muafaka,huku pande zote zikiheshimiana kama wadau walio na haki sawa.Tatizo upande wa Clouds Fm unaamini ni superior zaidi na unaweza kuathiri maamuzi ya kimfumo na kwa kutumia Radio yao wanadhani wataendelea kudanganya watu milele.SUGU ana historia ndefu ktk harakati hiz za hiphop,anapigania alichokiamini kabla hajawa mbunge na amedhihirisha hilo hadi sasa.pambana kaka mkubwa mpaka kieleweke,najua hata wasanii waliokusaliti wanakuunga mkono tatizo ni njaa,kutokutambua thamani yao na kukosa ujasiri.SUGU MOTO CHINI eehhhh
 
Kwanza Ruge amlipe fidia kwa kuchukua idea yake ya malaria halafu aache kuwaibia wasanii kisha aendelea na idhaa yake ya taifa ya radio kilauds fm baasiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii! ugomvi utakwisha.
 
Yani huyu Ruge alivyo ovyo alikuwa na ugomvi pia na Afande sele sasa kwa kuona Mh.Sugu anaanza kuwarushia makombora heavy amekwenda kumlamba masaburi ili eti wasanii kwa wasanii wapambane huu ni uchonganishi huu yani anaonyesha wazi ubaya wake juu wasanii!
 
Umetoa ushauri mzuri sana mkuu..

Kwa clouds..

Huo ushauri uliowapa we sio wa kwanza kuna watu wameishawaketisha nakuwapa somo lakini wapi,kiburi cha mafanikio kimewapofusha na sasa hawatazami tena hali halisi ilivyo wamejigeuza sikio la kufa..lile tukio la jumamosi la vinega lilivyoshona watu ilikuwa ni ujumbe tosha walikuwa wanapelekewa kwamba kuna vitu wanafanya haviko sawa,na watu wamewachoka na ujanja ujanja wao uliopitiliza.

Tatizo wanaamini wao ndio wajanja kuliko watu wote hapa mjini,wamesahau tabia ya wabongo wakishaamua kumpotezea mtu kuwarudisha tena ni ishu.

Kuhusu Sugu..

Umempa ushauri mzuri kiasi chake,lakini hamna kitu sifagilii kama kumwogepesha kiongozi asifanye jambo nyeti eti kisa litamnyima kura uchaguzi ujao.mabadiliko tunayaitaji sasa, sio tujenge mfumo wa kuishi kwa kuvizia kura.
 
Hivi hamjui zilipo ofisi za Clouds?
Watu tunagonga cheers tu kunywa champagne kusherehekea kuumbuka kwa redio ya wafu juzi jumamosi, usifanye mchezo na maamuzi ya umma.

Leo wenzako wanaongea mpaka mipovu inawatoka kudadakeki, yaani hapa JF umebakia peke yako tu wenzakop wanauguria hasara walioipata jana, na watu wana mpango wakuifikisha redio ya wafu mahakamani kwa kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu, maana walidanganya show ya juzi angekuwepo DMX.
 
Sugu ni zaidi ya mwanamziki.
Sugu ni zaidi ya Mbunge.
Sugu ni zaidi ya mwanaharakati.

Usimdefine Sugu, Sugu ni chata ingine.


Il Gambino.
 
Clopuds, angalieni matumizi mabaya ya chombo chenu cha habari. Ngoma ikivuma sana uju inakaribia kupasuka
 
Basi fungeni masufuria yenu. Hakuna aliyewaomba ushauri.

Lol!! ha! ha! ha!

Thats over reacting buddy!! chochote kinachopanda hushuka!!Hii ni time yenu ya kushuka! shikilia vizuri kwani mshuko huo waweza kuwa si mwema kwenu!!! ha! ha!ha!
 
ushauri wako umetulia mkuu,ila nadhani ili yote yaishe ruge amlipe fidia suggu na wasanii wote aliowanyima haki zao za msingi then aite media na kuomba msamaha,ni vigumu sana kwake kuuzima moto wa suggu na asipoangalia itamgharimu mno.
 
Back
Top Bottom