Ushahidi wa Tundu Lissu na dereva wake wameshautoa kwa hiyo kazi kwenu Polisi kuufanyia kazi

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,480
30,152
Viongozi wa serikali ya awamu ya tano wamekuwa wakidai kuwa wanamsubiri Tundu Lissu na dereva wake wapone ili wakamilishe uchunguzi wa tukio lile ambalo Tundu Lissu alishambukiwa na risasi zaidi ya 30 pale mjini Dodoma, hapo tarehe 7/09/2017 kwa lengo la kumwua

Sababu kuu inayotolewa na Jeshi la Polisi nchini ni madai kuwa eti kwa kuwa hawajampata Tundu Lissu na dereva wake kwa hiyo uchunguzi umeshindikana kukamilishwa!

Hata hivyo katika mahojiano ya hivi karibuni kwa vyombo vya habari vya kimataifa pamoja na kuongea na watanzania waishio ughaibuni, Tundu Lissu na dereva wake wametoa Maelezo ya ushahidi ambao endapo Jeshi la Polisi utauifanyia kazi wanaweza wakawapata "watu wale wasiojulikana"/waliofanya shambulio lile kwa nia ya kumwua Tundu Lissu

Tundu Lissu na dereva wake wametoa ushahidi wao kama ifuatavyo:-

1. Kwa kawaida huwa panakuwepo ulinzi wa Massa 24/7 wa askari wenye silaha pale kwenye geti la kuingilia kwenye makazi yao. Lakini cha kushangaza siku ya tukio lile hapakuwepo na ulinzi wowote. Kwa hiyo Tundu Lissu na dereva wake wanawataka Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi ni nani aliamuru kusiwepo ulinzi siku hiyo??

2. Palikuwepo CCTV camera kwenye majengo hayo ya viongozi wa ngazi za juu wa Taifa hili, lakini camera hizo za CCTV zilinyofolewea na kupelekwa mahali kusikojulilama, kwa hiyo wameliomba Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi ni nani aliyehusika na kuzinyofoa camera hizo??

3. Tundu Lissu amedai kuwa kuna Mkuu wa Mkoa mmoja ambaye alionekana mkoani Dodoma, siku hiyo ya tukio hilo mjini Dodoma. Wakati ambapo siku hiyo hiyo kulikuwa na tukio la kukabidhi ripoti ya makinikia, kwa Mheshimiwa Rais, tukio ambalo siyo kawaida kwa Mkuu huyo wa Mkoa kukosekana kuhudhuria tukio hilo, kwa hiyo ingekuwa vyema Mkuu huyo wa Mkoa akahojiwa alikuwepo Dodoma kwa shughuli gani kwa kuwa kuna kitu kinachoitwa "suspicious characters" kwa lugha ya kisheria, ambazo inabidi zifanyiwe uchunguzi

Polisi huwa wanaomba ushrikiano kutoka kwa raia wema ili watoe ushahidi wa matuio kama hayo yanapotokea, kwa hiyo Tundu Lissu na dereva wake wameshatoa ushirikiamo kwa tukio zima hilo, kwa hiyo ni kazi ya Jeshi la Polisi kumalizia kazi ya kuwabaini wahalifu hao

Kama Polisi wasipofanyia uchunguzi wa ushahidi huo na wanaendelea kusisitiza tu wanamtaka Tundu Lissu na dereva wake warejee nyumbani ili wake watoe ushahidi wao, ndipo hapo tunapijiuliza iwapo Tundu Lissu na dereva wake wameshatoa ushahidi wao ni kwanini Jeshi la Polisi liendelee kisisitiza kuwa ni lazima Tundu Lissu na dereva wake warejee nchini ili watoe "physically" ushahidi huo, je dhamira yao ni nini??

Je wanajilaumiu kwa kutoweza "ku-accomplish" jukumu hilo zito la "kutoa" uhai wa Mheshimiwa Tundu Lissu kwa hiyo kumtaka arejee nyumbani ili wajje wakamilishe zoezi lile "lililofeli" mwaka 2017 kwa second chance??

Kama Jeshi la Polisi litakanusha kuwa hilo siyo lengo lao basi wakubali wachunguzi wa nje waje nchini kulichiunguza kwa undani tukio hilo ili kila kitu kiwekwe hadharani!

Kwa kukataa wachunguzi kutoka nchi za nje waje kuchunguza tukio lile, ambalo ni zaidi ya mwaka mmoja unusu hawajamkamata hata mtuhimiwa mmoja kumuhoji ni "indirectly" wanakiri kuwa ni "wao" ndiyo waliohusika na shambulio lile!
 
Dah we jamaa sijui una mtindio wa ubongo???... Unasubiriaga vitu vijadiliwe wiki nzima,unakusanya uliyoyasoma koteeee unaanzisha Uzi mwingine upya.Nadhani bado huamini kuwa ishu ya Lissu ndo imetoka hivyo.Mjadala ulishafungwa hata hiyo ya dereva ni zuga tu.Huwezi kufanya uchunguzi wa ishu ambayo tayari muathirika wake ameshatuhumu nani wanahusika.Kubali kataa ishu ya Lissu ndo inaishia hivyo, ziara zake zimeisha.Na nakuhakikishia hakuna litakalobadilika.Jifunze kukubaliana na uhalisia.Mmebaki kupoteza muda wenu tu Jamii Forums, hakuna atayechangia lolote jipya thread hii maana haina tofauti na thread zaidi ya 50 zilizoanzishwa ndani ya hizi wiki 2.
 
Mkuu jmc06 mbona unweweseka sana??

Kama siyo nyinyi mmehusika katika tukio lile ni kwanini basi mnakataa wachunguzi wa nje waje wawasaidie kuwatia mbaroni wahalifu hao??

Hivi kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu bila kumkamata mtuhumiwa yeyote na kumuhoji, bado mnatutaka watanzania tuwaamiini kuwa mpo "serious" kuwatafiita hao wauaji??
 
sera za chama chao ni matukio na uzushi..... Na hii inawafanya wajione ma genius and not masaikoz
 
Wauaji wa Lissu wamebaki kuwa na laana itakayowatafuna maishani. Watatangulia kufa kabla ya Lissu. Tena ni kifo chenye mateso makali mno. Mungu siyo Juma.
 
Mkuu jmc06 mbona unweweseka sana??

Kama siyo nyinyi mmehusika katika tukio lile ni kwanini basi mnakataa wachunguzi wa nje waje wawasaidie kuwatia mbaroni wahalifu hao??

Hivi kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu bila kumkamata mtuhumiwa yeyote na kumuhoji, bado mnatutaka watanzania tuwaamiini kuwa mpo "serious" kuwatafiita hao wauaji??
Mkuu panua wigo wa akili yako, mnachosahau dunia haiendeshwi kama mnavyodhani.Kilichosababishwa Lissu kupigwa risasi ni kujiona special na nyie mkamfanya special mitandaoni, mnadai waliuawa watu 300 kibiti mbona hampigi kelele waje wachunguzi wa kimataifa?,walipigwa risasi kibao Askari Polisi nane wenye familia na watoto umeona wakipiga kelele eti serikali haifai sababu wamepigwa risasi?,Lissu ni mbinafsi anajiona Very Special ndo maana wazungu wamemsikiliza weeeeee wakaona tatizo lake lilipo.Nchi zote alikopita zina wawakilishi Tanzania(mabalozi) unadhani hazijui yanayoendelea Tanzania??,Kuna jamaa aliuawa uturuki tena ubalozini kwa kuchinjwa na ushahidi upo umeona dunia ikisimama?,waingereza na wamarekani wamefanya nini?,kuna misingi na kanuni za kidunia usipozifuata utapata tabu maisha yako yote.Nakuhakikishia mwisho wa Lissu kisiasa ni 2020.
 
Wauwaji wa Lissu wamebaki kuwa na laana itakayowatafuna maishani. Watatangulia kufa kabla ya Lissu. Tena ni kifo chenye mateso makali mno. Mungu siyo Juma.
Je wauaji wa Kasshogi,Mwangosi,Aquillina,Askari wetu kule kibiti,viongozi wa CCM kibiti,watoto waliouwawa kule njombe last week,albino walio uwawa miaka kadhaa iliyopita!!??????,.. the list goes on. Hawa wengine niliowataja sio binadamu wanaohitaji attention kama Lissu au zaidi yake?? Mnapokosea ni kujaribu kuonyesha Lissu ni mtu special na tofauti, hujiulizi kwanini wazungu wamempuuzia wamemuona fala?,anajieleza vyombo vya kimataifa as if ni wa kwanza duniani kupigwa risasi, sitetei mauaji ila yapo duniani kote.Dunia haiwezi simama sababu ya Lissu. Kazunguka weeeeee kapata nini?,tii mamlaka iliyopo,fata kanuni za maisha na maisha yatasonga.Ukijifanya much know unapewa ngumi za uso unabaki kutoa laana as if Mungu yupo upande wako tuu.
 
Maneno kama haya ndio yalimtia uwenda wazimu dereva baadala ya kwenda kituo cha polisi kwa usalama yeye akakimbilia nyumbani!
 
Je wauaji wa Kasshogi,Mwangosi,Aquillina,Askari wetu kule kibiti,viongozi wa CCM kibiti,watoto waliouwawa kule njombe last week,albino walio uwawa miaka kadhaa iliyopita!!??????,.. the list goes on. Hawa wengine niliowataja sio binadamu wanaohitaji attention kama Lissu au zaidi yake?? Mnapokosea ni kujaribu kuonyesha Lissu ni mtu special na tofauti, hujiulizi kwanini wazungu wamempuuzia wamemuona fala?,anajieleza vyombo vya kimataifa as if ni wa kwanza duniani kupigwa risasi, sitetei mauaji ila yapo duniani kote.Dunia haiwezi simama sababu ya Lissu. Kazunguka weeeeee kapata nini?,tii mamlaka iliyopo,fata kanuni za maisha na maisha yatasonga.Ukijifanya much know unapewa ngumi za uso unabaki kutoa laana as if Mungu yupo upande wako tuu.

Off point.
 
Kama jamaa kila mmoja kwa wakati wake watapitia post hii basi watachota busara na hekima wala hawatompotosha tena mgonjwa!
 
Mkuu panua wigo wa akili yako, mnachosahau dunia haiendeshwi kama mnavyodhani.Kilichosababishwa Lissu kupigwa risasi ni kujiona special na nyie mkamfanya special mitandaoni, mnadai waliuawa watu 300 kibiti mbona hampigi kelele waje wachunguzi wa kimataifa?,walipigwa risasi kibao Askari Polisi nane wenye familia na watoto umeona wakipiga kelele eti serikali haifai sababu wamepigwa risasi?,Lissu ni mbinafsi anajiona Very Special ndo maana wazungu wamemsikiliza weeeeee wakaona tatizo lake lilipo.Nchi zote alikopita zina wawakilishi Tanzania(mabalozi) unadhani hazijui yanayoendelea Tanzania??,Kuna jamaa aliuawa uturuki tena ubalozini kwa kuchinjwa na ushahidi upo umeona dunia ikisimama?,waingereza na wamarekani wamefanya nini?,kuna misingi na kanuni za kidunia usipozifuata utapata tabu maisha yako yote.Nakuhakikishia mwisho wa Lissu kisiasa ni 2020.
Kumbe kilichosababisha Tundu Lissu apigwe risasi ni kujiona so special??

Hayo maneno umeyatamka wewe mwenyewe jmc06

Unaweza kuniambia ni ibara ipi ya Katiba ya nchi inayompa mwananchi yeyote kibali cha kutoa adhabu ya kuua kwa mwananchi yeyote??

Tunajua ni mahakama pekee yenye uwezo wa kutoa hukumu kwa mashitaka yoyote ya jinai....

Hivi nyinyi maccm mmefikia kiwango hicho cha ulevi wa madaraka hadi kufikia kufikiria mna uwezo wa kuua??
 
Back
Top Bottom