Ushahidi wa mikutano ya hadhara ya siasa Zanzibar huu hapa. Je, marufuku iliyoko Tanganyika ni halali?

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,441
55,017
Mkutano wa hadhara wa Act Wazalendo huo hapo chini.

Tena wanatishia kuvunja muungano na kurudisha kiti cha Zanzibar Umoja wa Mataifa.

Wakati huohuo huku Tanganyika vyama mbadala vinazuiwa kufanya mikutano ya hadhara.

Je, zuio hili la upande mmoja wa muungano kutokufanya mikutano, huku upande wa pili wakiruhusiwa ni halali?

Je, huu sio UBAGUZI?

Kwani Tanganyika ipo kwenye ramani?

IMG_0508.jpg

Bendera ya Tanganyika hiyo hapo bado ipo mioyoni mwa watanganyika
 
Siyo ubaguzi. Hsta wewe ukiruhusiwa kumfunga mpinzani wako mikono bila repercussion yoyote utaacha?
 
..Mkutano wa hadhara wa Act Wazalendo huo hapo chini.

..Tena wanatishia kuvunja muungano na kurudisha kiti cha Zanzibar Umoja wa Mataifa.

..Wakati huohuo huku Tanganyika vyama mbadala vinazuiwa kufanya mikutano ya hadhara.

..Je, zuio hili la upande mmoja wa muungano kutokufanya mikutano, huku upande wa pili wakiruhusiwa ni halali?

..Je, huu sio UBAGUZI?

Mada kama hizi nadhani inafaa tufike mahali tukubali yafuatayo:

Zanzibar ni nchi, iliyo na serikali yake, serikali inayosimamia mambo yanayofanyika huko.
Tanzania inaye rais, anayetambua mamlaka ya nchi nyingine inayosemekana ni sehamu ya nchi anayoitawala. Huyu rais, hata kama angekuwa ni yeye kwenye mamlaka ya serikali ya Zanzibar angefanya yale yale yanayofanywa na serikali iliyopo huko sasa hivi.

Kwa hali hiyo, utaanzia wapi kuhoji yanayofanyika sasa!

Jambo linalosikitisha sana kwa nchi yetu hii ya Tanzania ni kuona kwamba mtu anapokuwa rais wa nchi, inakuwa kama amechukuwa madaraka yote anayoyataka. Anaweza kufanya chochote kile bila ya kuhojiwa na mtu wala taasisi yoyote. Nchi inakuwa ni mali yake.

Hili nilidhani ni kwa sababu ya hulka tu ya kiongozi aliyonayo, kama ile iliyoonyeshwa na Jiwe. Kumbe, waTanzania na taasisi zote zilikwishajiweka tayari kwa yeyote anayeshikilia cheo hicho, hata kama hulka yake siyo ya kutumia mabavu.

Ajabu kubwa inayonishangaza, hasa kuhusu maudhui ya mada iliyopo ukumbini ni vyama vya upinzani, kama CHADEMA. Imekuwaje hata wao wakakubali marufuku hii ya kufanya mikutano? Hili ndilo linalonitatiza kwa sasa.
 
..Mkutano wa hadhara wa Act Wazalendo huo hapo chini.

..Tena wanatishia kuvunja muungano na kurudisha kiti cha Zanzibar Umoja wa Mataifa.

..Wakati huohuo huku Tanganyika vyama mbadala vinazuiwa kufanya mikutano ya hadhara.

..Je, zuio hili la upande mmoja wa muungano kutokufanya mikutano, huku upande wa pili wakiruhusiwa ni halali?

..Je, huu sio UBAGUZI?

Aiseeee !!
 
Kalamu,

..Juzi jeshi la Polisi Mwanza liliwakamata viongozi na wanachama wa Chadema waliokuwa wakifanya maandalizi ya mkutano wa hadhara.

..Na Chadema walifuata taratibu za kupeleka taarifa Polisi lakini majibu waliyoyapata ni hayo ya kutiwa nguvuni.

..Kwa upande mwingine hatuwezi kusema kwamba Zanzibar ni tofauti na Tanganyika tunapozungumzia masuala ya vyama vya siasa na haki zao.

..Masuala ya vyama vya siasa ni ya MUUNGANO. Msajili wa vyama vya siasa ni mmoja kwa Tanganyika na Zanzibar.

..Zaidi, jeshi la Polisi linalokamata Watanganyika kwa kuandaa mikutano ya hadhara ndilo hilohilo linaloruhusu Wazanzibari kutumia haki hiyo ya kikatiba.

..UBAGUZI huu unapaswa kukemewa na kila mpenda demokrasia wa Tanzania.
 
View attachment 2349206
Bendera ya Tanganyika hiyo hapo bado ipo mioyoni mwa watanganyika
Mkuu 'Arovera', hili wazo limeniijia kichwani baada ya kuiona hiyo bendera.

Bendera ni nzuri, na bila shaka hata nchi yenyewe Tanganyika ni nzuri na itakuwa nzuri ikirudi!

Lakini najiuliza: Hivi kweli li nchi hili linashindwa kuhimiri hivi vijimaneno ya hawa wapuuzi kiasi kwamba linatafuta urahisi wa kutaka kujiondoa?
Huu sio uzembe na udhaifu usiofaa kabisa?

Kweli nchi hii inakosa viongozi imara wa kukabiriana na hawa, kiasi kwamba njia pekee iliyo rahisi kwao ni kuhimiza kuvunja, au kurudisha Tanganyika?

Inawezekana sikuweka maneno yangu vizuri ili yaeleweke kirahisi, lakini msingi wa hoja yangu ni kwamba itakuwa ni uzembe kutokabiliana na hawa watu kwa hoja na kwa kila njia zingine zote zikiwemo za hoja kwa wenye nchi wenyewe waone maana halisi ya muungano wetu, zinazofaa kisheria kuimarisha muungano huu.
 
Kalamu,

..Juzi jeshi la Polisi Mwanza liliwakamata viongozi na wanachama wa Chadema waliokuwa wakifanya maandalizi ya mkutano wa hadhara.

..Na Chadema walifuata taratibu za kupeleka taarifa Polisi lakini majibu waliyoyapata ni hayo ya kutiwa nguvuni.

..Kwa upande mwingine hatuwezi kusema kwamba Zanzibar ni tofauti na Tanganyika tunapozungumzia masuala ya vyama vya siasa na haki zao.

..Masuala ya vyama vya siasa ni ya MUUNGANO. Msajili wa vyama vya siasa ni mmoja kwa Tanganyika na Zanzibar.

..Zaidi, jeshi la Polisi linalokamata Watanganyika kwa kuandaa mikutano ya hadhara ndilo hilohilo linaloruhusu Wazanzibari kutumia haki hiyo ya kikatiba.

..UBAGUZI huu unapaswa kukemewa na kila mpenda demokrasia wa Tanzania.
Mimi ni mmoja wa hao "wanaopaswa kukemea...", lakini pamoja na kukemea huko ni lazima vyama vya siasa vyenyewe viwe tayari kupigania haki zao.

Huku Tanganyika Kinana amezunguka nchi nzima kwa kwa mgongo wa kukagua uhai wa CCM. Mimi sioni tofauti yoyote na hao ACT huko Zanzibar na hawa CCM huku Tanganyika.

Kwa hiyo ninarudi kulekule kwa vyama kama CHADEMA. Hayo waliyofanyiwa Mwanza ndiyo yangepaswa kuwa kichocheo cha kukataa kabisa kunyanyaswa huko.
Haya mazungumzo ya "maridhiano" naona yameleta madhara makubwa sana kwa hiki chama. Mbona huko siku za nyuma wakati wakisurubiwa na Jiwe, lakini waliweza kusikika kila kona ya nchi?
Ni kipi kilichotokea sasa kinachowafanya kama wamedungwa sindano ya ghanzi? Kurudishiwa mali kwa viongozi wao; jambo ambalo ni haki yao?
 
..mimi nimewasikia Cdm sehemu mbalimbali wakifanya makongamano ya ndani ya katiba.

..tatizo ni marufuku inayowazuia kupeleka ujumbe wa katiba mpya kwa wananchi kupitia mikutano ya hadhara.
 
..Juzi jeshi la Polisi Mwanza liliwakamata viongozi na wanachama wa Chadema waliokuwa wakifanya maandalizi ya mkutano wa hadhara.

..Na Chadema walifuata taratibu za kupeleka taarifa Polisi lakini majibu waliyoyapata ni hayo ya kutiwa nguvuni.
Inabidi sasa watu wahoji mabadiliko haya ndani ya CHADEMA yametokana na nini. CHADEMA imepoa mno, wakati ambao wanatakiwa kuwa moto hasa.

Kumbuka, Samia amefanya juhudi zote aonekane yeye ni tofauti na Magufuli.
Amejitahidi aonekane ni mtu anyependa haki, mtu asiyependa kuonea watu wengine.

Sasa huku kuzuiwa kwa CHADEMA huko Mwanza inaonekana wazi kabisa kuwa ni kinyume cha anayoyataka yeye Samia.

Kwa nini CHADEMA wasitumie nafasi hiyo kuhoji dhamira ya kiongozi huyu?
 
..Ninavyoelewa mimi Cdm wamekuwa wakihoji kwa muda mrefu zuio la mikutano ya hadhara.

..Pia njia mojawapo ya kuwaonyesha wananchi na dunia unafiki wa Ssh ni hiyo waliyotumia Cdm ya kutoa taarifa za mkutano Mwanza na polisi kuwazuia.
 
Naomba sana sasa wasiishie hapo.

Ni wakati mwafaka sasa wa kusonga mbele zaidi, na kwa kasi zaidi.
 
..Na sisi wananchi tusonge mbele zaidi, na kwa kasi zaidi.

..Tukionyesha kwamba suala hili linatugusa tutawatia moyo Cdm kulipigania.
Wananchi wapo wa kutosha kabisa, kama madai ya CHADEMA ya kuwa na wanachama zaidi ya milioni (?)ngapi; na wapenzi wengi zaidi wa chama hicho.

Kazi ikifanyika ipasavyo, ndiyo njia ya kuongeza wananchi upande wao.
 
Back
Top Bottom