Ushahidi wa Mazingira na Kunyongwa - sheria zetu Tanzania

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,336
1,500
Nafikiri kuna kitu kimenipita. Kuuwa ni kosa baya na kubwa sana, ila hukumu ya kunyongwa lazima kosa lithibitishwe kwa ushahidi usio na mawaa wala chenga chenga, sasa jaji kuhukumu kunyonga kwa ushahidi wa mazingira inatisha sana. Kwa wale mnaojua sheria hasa sheria zetu za Tanzania hivi ndivyo sheria zinavyosema au ??
 
Barubaru

JF-Expert Member
Apr 6, 2009
7,161
0
Nafikiri tutatenda haki sana kama tutaona mwenendo wa kesi na kupata hukumu yake kisha kuweza kuchangia. Kwani hawa waandishi wengi wao hawana taaluma za kuandika mwenendo wa kesi na shughuli za kimahakama hivyo mara nyingi wanapotosha umma.

Lakin vile vile kila upande una haki kamili ya kukata rufaa kama hawakuridhika na hukumu iliyotolewa.

Huo ndio mchango wangu kwako.
 
TUKUTUKU

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
11,785
2,000
Nafikiri kuna kitu kimenipita. Kuuwa ni kosa baya na kubwa sana, ila hukumu ya kunyongwa lazima kosa lithibitishwe kwa ushahidi usio na mawaa wala chenga chenga, sasa jaji kuhukumu kunyonga kwa ushahidi wa mazingira inatisha sana. Kwa wale mnaojua sheria hasa sheria zetu za Tanzania hivi ndivyo sheria zinavyosema au ??
Unachokisema ni sahihi,lakini sijui unaongelea hukumu ya kesi gani?tafadhari nifahamishe!!
 
Mkirua

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
5,658
1,225
Nafikiri kuna kitu kimenipita. Kuuwa ni kosa baya na kubwa sana, ila hukumu ya kunyongwa lazima kosa lithibitishwe kwa ushahidi usio na mawaa wala chenga chenga, sasa jaji kuhukumu kunyonga kwa ushahidi wa mazingira inatisha sana. Kwa wale mnaojua sheria hasa sheria zetu za Tanzania hivi ndivyo sheria zinavyosema au ??
Nijuavyo kama ushahidi huo hauachi shaka basi mahakama haina budi kuukubali na kutoa hukumu kadiri ya matakwa ya kisheria...
 
mhandokajiru

Member
Oct 14, 2012
9
0
hata mimi nimepata shaka sana. wale wanajeshi kama wameonew. kisheria huwezi kutumia ushaidi wamzingira kumtia hatian mtuhumiwa na kutoa adhabu ya kunyongwa hadi kufa. kuna walakin hapo.
 
Top Bottom