Geza Ulole
JF-Expert Member
- Oct 31, 2009
- 59,185
- 79,366
16th October 10
Utafiti mpya wajibu Redet na Synovate
Elizabeth Zaya
Baada ya Taasisi ya Utafiti na Demokrasia (Redet) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Kampuni ya Synovate kutoa matokeo ya tafiti zao kuhusu wagombea urais mwaka 2010 na kuonyesha kuwa Mgombea wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, anaongoza, jana ulitolewa utafiti mwingine na kumweka nafasi ya pili.
Utafiti mpya uliotolewa jana ulifanywa na Shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Citizens' Information Bureau (TCIB) mbele ya vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri wa Idara ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliyefanya utafiti huo, Dk. Vincent Leyaro, alisema utafiti huo uliofanyika kati ya Septemba 27 na Oktoba 10, mwaka huu, ambapo jumla ya wananchi 3,047 walihojiwa.
Alisema katika matokeo hayo, mgombea urais kupitia Chadema, Dk. Willibrod Slaa, ameongoza kwa kupata asilimia 45, Rais Kikwete asilimia 41 na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF asilimia 10.
Wengine ni mgombea wa NCCR-Mageuzi, Hashim Rungwe aliyepata asilimia 2, Kuga Mziray wa APPT- Maendeleo asilimia 1 na Muttamwega Mugahywa wa TLP asilimia 1.
Dk. Leyaro alisema matokeo hayo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa katika mikoa 15 iliyochaguliwa kwa njia ya kinasibu na kwenye jimbo moja katika kila mkoa ambapo wananchi kati ya 60 na 100 walihojiwa.
Alisema wagombea hao wangepata matokeo hayo kama uchaguzi ungefanyika siku ambayo washiriki walihojiwa.
Pia, Dk. Leyaro alisema Dk. Slaa aliongoza pia katika swali lililouliza kuhusu mgombea ambaye anaaminika atashinda kama uchaguzi ungefanyika siku ya kupiga kura ya maoni hayo.
Alisema Dk. Slaa aliongoza kwa asilimia 48 akifuatiwa na Rais Kikwete (38), Profesa Lipumba (9), Rungwe (4), Mziray (1) na Mugahywa (1).
Dk. Leyaro alisema katika washiriki waliohojiwa, asilimia 18.3 walijitambulisha kuwa wanachama ama washabiki wa CCM, wakati Chadema walikuwa asilimia 15.6, CUF asilimia 12, TLP (6.8), NCCR-Mageuzi (6.6) na UPDP (6.1).
Pia alisema asilimia 31.6 ya waliohojiwa walisema si wanachama ama washabiki wa vyama vya siasa.
Hata hivyo, matokeo ya takwimu ndani ya vyama vya siasa yalionyesha kuwa asilimia 81 ya wana-CCM, mbili ya wana-Chadema na 48 ya wana-CUF watamchagua Rais Kikwete.
Matokeo hayo yalionyesha kuwa asilimia 90 ya wanachama ama washabiki wa Chadema, 15 ya wana-CCM na tano ya wana-CUF, walisema watamchagua Dk. Slaa wakati asilimia 38 ya wanachama ama washabiki wa CUF, mbili ya wana-CCM na moja ya wana-Chadema, walisema watamchagua Profesa Lipumba.
Dk. Leyaro alisema uchambuzi wa matokeo kimkoa, yalionyesha kuwa Dk. Slaa na Rais Kikwete wamechuana vikali katika baadhi ya mikoa kwa kufanya vizuri au vibaya.
Dk. Slaa ameonekana kukubalika zaidi katika mikoa ya Arusha, Kilimanjario na Manyara huku akifanya vibaya katika mikoa ya Lindi, Morogoro, Ruvuma na Tabora.
Kwa upande wake, matokeo ya utafiti huo yameonyesha kuwa Rais Kikwete anaongoza zaidi katika mikoa ya Dodoma, Morogoro, Tabora na Ruvuma huku akifanya vibaya katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.
Pia, alimtaja Profesa Lipumba kufanya vizuri katika mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Tabora.
Utafiti huo ulionyesha kuwa Dk. Slaa anaungwa sana mkono na watu wa rika ya kuanzia miaka 25 hadi 35 (asilimia 55) wakati Rais Kikwete anaungwa zaidi na wenye umri wa kati ya miaka 46 hadi 50 (asilimia 50).
Utatiti wa Redet ulibainisha kuwa Rais Kikwete aliongoza kwa kupata asilimia 71.2 akifuatiwa na Dk. Slaa asilimia 12.3 huku Profesa Lipumba akishika nafasi ya tatu kwa kupata asilimia 10.1 kwa mujibu wa utafiti wa Septemba mwaka huu.
Kwa mujibu wa utafiti wa Synovate, Kikwete alishika nafasi ya kwanza kwa kupata asilimia 61, Dk. Slaa (16) na Profesa Lipumba (5).
NIPASHE
Utafiti mpya wajibu Redet na Synovate
NB: naona mawaidha ya ma-Sheik yanatimia! that's a looser spirit for sure huyu Prof. Mapumba tuliyempigia kura kwa vipindi viwili vilivyopita ndo malipo yake haya! kamwe CUF hawatashinda Urais nchi hii kwa unafiki huu! Ndo maaana CHADEMA waliliona hili mapemaaa! Muungano kwao hawa jamaa ni lazma wao wawe mbele yaani Prof. Mapumba awe mgombea Urais na sio makamu au waziri Mkuu! cha ajabu wanadiriki hata kumsaliti mgombea wao Prof. Mapumba kisa itikadi za kidini kama baadhi ma-sheik wao wanavyojitahidi kuhubiri ati Kikwete ni Muislam mwenzetu!
Hivi hamuwezi kuwa kama Mh Zitto au Mh Said Afri? nani asiyejua Mh Zitto ni rais mtarajiwa akiwa ndani ya CHADEMA akiwa na umri wa miaka 45-46 kama Obama? au Udini tu unawasumbua watu nyie? nani asiyejua mchango wa Mh Said Arfi hawa ni watu waliofunguka macho na hawababaishwi na siasa chafu za kidini!