Mbwa wa Polisi kitengo maalum cha kupambana na madawa ya kulevya jana "aliwatia aibu" wachezaji wa Simba huko Mwanza.
Mbwa huyo ambaye amefunzwa kubainisha watu waliotumia/waliobeba madawa ya kulevya walitoa kali hiyo jana wakati wa mchezo kati ya Simba na Toto African, mchezo ambao ulifanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini humo.
Mbwa huyo ambaye alikuwa ameshikwa na master wake alianza kukukuruka kana kwamba amehisi kitu, ana alipofanikiwa kumtoroka master wake moja kwa moja alianza kumfukuza mshambuliaji wa timu hiyo Felix Sunzu.
Baada ya Sunzu kufanikiwa kumzidi mbio mbwa huyo ndipo mbwa akamgeuzia kibao kiungo wa timu hiyo Haruna Moshi "Boban". Mbwa huyo aliendelea kumtia msukosuko Boban hadi alipokamatwa na kutulizwa na master wake.
Watu wengi wamekuwa na maoni tofauti kuhusiana na sakata hilo.