Elections 2010 USHAHIDI: Media za Tanzania zimenunuliwa na CCM kumhujumu SLAA

EL+RA=UFISADI

Member
Jul 4, 2010
56
6
Salaam,

Sote tumeona kuwa kumekuwa na unfair coverage (very biased) kwenye media ya Tanzania kuhusu kampeni za uchaguzi zinazoendelea. Coverage yenyewe imekuwa na lengo la kuibeba CCM na Kikwete na kumhujumu SLAA na CHADEMA.

Ufuatao ni ushahidi kuwa media za Tanzania karibu zote kubwa zimekuwa zikipendelea CCM kutokana na wamiliki wake kuwa karibu na chama tawala au kununuliwa. Huu ndiyo ushahidi wenyewe:

TELEVISION STATIONS

1. TBC1 (inamilikiwa na serikali, pro-CCM)
2. ITV, Radio One (inamilikiwa na Reginald Mengi, mwanachama hai wa CCM)
3. Star TV, Radio Free Africa (inamilikiwa na Anthony Diallo, kada wa CCM)
4. Channel Ten, Magic FM (inamilikiwa na Tanil Somaiya, kada na mfadhili wa CCM)
5. Clouds TV, Clouds FM (Joseph Kusaga na wengine, wanajipendekeza kwa CCM)

MAGAZETI YA CCM

6. New Habari Corporation - Mtanzania, Rai, etc (Rostam Aziz, huyu ni mmiliki wa CCM)
7. IPP Media - Nipashe, The Guardian, etc (Reginald Mengi)
8. Jambo Leo (Ridhwani Kikwete, Juma Pinto, Malegesi, etc)
9. Daily News, Habari Leo (Mhariri wake, Mkumbwa Ally amediriki kuandika: "Slaa will never be the 5th president of Tanzania)
10. Tazama (linafadhiliwa na Lowassa)
11. Changamoto (linafadhiliwa na Usalama wa Taifa)
12. Sauti Huru (linafadhiliwa na swahiba wa JK, Subhash Patel)
13. Taifa Tanzania (Prince Bagenda, Nazir Karamagi)
14. Tafakari (Salva Rweyemamu, Gideon Shoo)
15. Al-Huda (Waislamu feki walionunuliwa na CCM)
16. UHURU, MZALENDO (magazeti ya chama)

MAGAZETI HURU MACHACHE

1. MWANAHALISI (inamilikiwa na Kubenea)
2. MWANANCHI, THE CITIZEN (inamilikiwa na Nation Media Group)
3. TANZANIA DAIMA (inamilikiwa na Freeman Mbowe)
4. RAIA MWEMA (Jenerali Ulimwengu and others)

5. MAJIRA (wafanyabiashara binafsi)
  • HAKUNA HATA TV AU RADIO MOJA ILIYO KWENYE MAINSTREAM MEDIA AMBAYO NI HURU. ELECTRONIC MEDIA YOTE NCHINI IKO PRO CCM.
  • MLIMANI TV YA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDSM) SO FAR IMEKUWA VERY PROFESSIONAL NA INATOA FAIR COVERAGE KWA WAGOMBEA WOTE. LAKINI TV HII BADO NI CHANGA NA HAIJAENEA NCHINI KOTE. KUNA JITIHADA ZA CCM KUITEKA TV HII.
Kazi ya kuwaweka sawa wamiliki wa Media za Tanzania watoe upendeleo kwa CCM na Kikwete na kumkandamiza SLAA na CHADEMA inafanywa na Abdulrahman Kinana, January Makamba na Ridhwani Kikwete. Je, tutafika?
 
watu wanajua kupima ...ccm haina chake sasa....hata wakinunua tv na redio watu wamechoka nao.
 
EATV channel 5 & EA radio Je? unawaweka upande gani? sababu nimeona campaign yao ya kuhamasisha vijana kupiga kura
 
MAGAZETI HURU MACHACHE

1. MWANAHALISI (inamilikiwa na Kubenea)
2. MWANANCHI, THE CITIZEN (inamilikiwa na Nation Media Group)
3. TANZANIA DAIMA (inamilikiwa na Freeman Mbowe)
4. RAIA MWEMA (Jenerali Ulimwengu and others)

5. MAJIRA (wafanyabiashara binafsi)
  • HAKUNA HATA TV AU RADIO MOJA ILIYO KWENYE MAINSTREAM MEDIA AMBAYO NI HURU. ELECTRONIC MEDIA YOTE NCHINI IKO PRO CCM.
  • MLIMANI TV YA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDSM) SO FAR IMEKUWA VERY PROFESSIONAL NA INATOA FAIR COVERAGE KWA WAGOMBEA WOTE. LAKINI TV HII BADO NI CHANGA NA HAIJAENEA NCHINI KOTE. KUNA JITIHADA ZA CCM KUITEKA TV HII.
Kazi ya kuwaweka sawa wamiliki wa Media za Tanzania watoe upendeleo kwa CCM na Kikwete na kumkandamiza SLAA na CHADEMA inafanywa na Abdulrahman Kinana, January Makamba na Ridhwani Kikwete. Je, tutafika?
Lakini wananchi wamegundua kuwa wakitaka habari zilizo fair wananunua magazeti ya hapo juu, na kuna taaarifa iliyoonyesha kuanguka kabisa kwa mapato ya magazeti ya chama ya pale juu kutokana na kupunguza copies zinazozalishwa baada ya kuona hayana walaji!..kwahiyo wananchi wanayakataa indirectly, na mwisho wasiku watagundua kosa lao na kujirekebisha...Ni process ndefu kama evolution, lakini inafanya kazi kubwa ajabu!
 
Na bado Vodacom mtandao wa simu.................... But People power is around the corner. Wakijua kwamba tasilimali zao zinamegwa hovyo...
 
Wasome magazeti wasisome ,waangalie TV wasiangalie wananchi wameamua kufanya kazi moja tu ambayo ni kuitosa CCM chama cha Mafisadi tarehe 31/10/2010
 
Pamoja na kueteka vyombo vya habari umoja ndani ya CCM ni history na umehamia kwa familia No 1. Haya ni matokeao ya kutaka Urais for fun.
 
nashauri wana-JF au wenye uwezo wa hili kuanzisha kituo cha television, inahitaji kujipanga with a vision and focus. sio tu kwa habari ya uchaguzi tu, kwa sababu hata station tulizo nazo hazina vipindi vya maana sana!

nilihuzunika sana jana usiku ITV walipoamua kutorusha mdahalo wa dkt. Slaa, na hii imenipa hamasa ya kuangalia mbali zaidi kwani tusipokuwa na vituo mbadala basi hakutakuwa na fair coverage kwa chaguzi zijazo.

Nawakilisha,
 
mbona siku zimeisha!!!!?
na tulishaawagundua toka kitambo sana

nina kazi moja tu hiyo octoba 31 nayo ni kumwondoa mtu dhalimu
 
woga Tu. Kama mengi angestahili kuhama CCM zamani.
Kama sio woga wa kufilisiwa nina uhakika 100% huyu jamaa asingekua mwana CCM.
Mnakumbuka ile ya ''by 2015'' Hairuhusiwa mtu kumiliki zaidi ya Kituo kimoja Cha habari.
Hii ilikua ya kumpa kashkash Mengi. alipoanza kujiita mpambanaji wa mafisadi papa.
Mzee wa watu alipoona maji yamefika kumshingo akatulia mpaka leo hii sijamsikia akitaja neno fisadi.

Tujiulize Tanzania ina kina Mengi wangapi?
 
Taarifa ya habari ya itv is very predictable these days. Wataonyesha kampeni ya "Dk" kikwete kwanza kwa muda mrefu, dk Shein na kampeni yake muda mrefu then dk Bilal na kampeni yake ya upupu.baada ya hapo wanatuzuga kidogo na Dk Slaa kwa sekunde chache then Maalim Seif kiduchu hapo wamemaliza habari za kitaifa.
 
Hiyo ni bongo zaidi uijuavyo,ila nadhani sasa watanzania wamechoka,hata ununue vyombo vya habari vyote wakiamua kufanya maamuzi mazito wanafanya
 
honestly ingawa Tanzania daima ni ya mbowe,haipendelei kama magazeti mengine,ina chambua vyama vyote ingawa inaweza isiwe saana lakini inaonesha kuwa mbowe hatumii magazeti yake kujitangaza,then kuna Kulikoni i like it sijui la nani?
 
woga Tu. Kama mengi angestahili kuhama CCM zamani.
Kama sio woga wa kufilisiwa nina uhakika 100% huyu jamaa asingekua mwana CCM.
Mnakumbuka ile ya ''by 2015'' Hairuhusiwa mtu kumiliki zaidi ya Kituo kimoja Cha habari.
Hii ilikua ya kumpa kashkash Mengi. alipoanza kujiita mpambanaji wa mafisadi papa.
Mzee wa watu alipoona maji yamefika kumshingo akatulia mpaka leo hii sijamsikia akitaja neno fisadi.

Tujiulize Tanzania ina kina Mengi wangapi?
[/QUOTE

1. Philip Marmo
2.Njelu Kassaka
3.Samwel Sitta
4.Judge Werema.....
 
Back
Top Bottom