Ushahidi kuwa IPTL/PAP ililipa ushuru TRA

rebeccamrema

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
334
0
Imefahamika kuwa IPTL ililipa ushuru wa stamp Duty kwa TRA kama ilivyotakiwa kufanya kutokana na Mauzo ya Hisa kutoka Mechmar kwenda PIPERLINK INVESTMENTS LTD na Kutoka Piperlink Kwenda PAN AFRICA POWER SOLUTIONS (PAP), PAP Ililipa malipo ya Ushuru TRA wakati wa mauzo hayo ya hisa
Malipo hayo ilikuwa kama ifuatavyo:
1.Kutoka Kampuni ya Mechmar kwenda PIPER LINK INVESTMENT ltd IPTL ililipa kiasi cha Tsh 95,940,000/= kama malipo ya ushuru wa Stamp kwenda TRA.
2. Kutoka kampuni ya PIPERLINK INVESTMENT ltd kwenda PAN AFRICA POWER SOLUTION (PAP),IPTL/PAP ililipa kiasi cha Tsh. 315,200,000 kama malipo ya ushuru wa Stempu yaani Stamp Duty
Hivyo basi kufanya jumla ya Malipo ya Stamp Duty kwa kampuni hizo kuwa jumla ya Tsh 411,140,000.(Tazama Viambatanisho)
Kwa Ushahidi huu nachelea kujiuliza maswali mawili
1. Je CAG alipotoshwa au aliamua kupotosha Umma kwa makusudi kuwa mauzo ya Hisa kati ya kampuni Mechmar kwenda PIPER LINK na mauzo ya hisa kati ya Piperlink kwenda PAP hayakulipiwa ushuru wa stempu (Stamp Duty)
2. Je Ripoti ya PAC ilipotoshwa au iliamua kwa makusudi kupotosha umma juu ya suala hili?
Imefika wakati sasa viongozi wetu hasa wa kisiasa kuacha kutumia uongo na kupotosha umma ili kujitafutia umaarufu wa kisiasa katika mambo yenye maslahi mazito kwa Taifa letu hasa sekta ya Nishati.
Napenda kuwasilisha.

Capture.PNG

Capture 2.PNG

Capture3.PNG

Capture4.PNG

Capture5.PNG

Capture6.PNG

Capture7.PNG

PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,005
2,000
Hayo Malipo ni Kwa mkataba wa kughushi walitakiwa kulipa kwa bei halisi waliyonunua matapeli kabisa hao
 
MeinKempf

JF-Expert Member
Jun 11, 2013
11,108
2,000
Wewe wacha kutuletea makaratasi ya kugushi mihuri ya pale kariakoo .Ningeamini malipo hayo kama hayo makbrasha yangekuwa verified na ripoti ya ukaguzi ya cag.
 
Last edited by a moderator:

Enzymes

JF-Expert Member
Feb 14, 2013
4,341
2,000
Badala ya kulipa ushuru kwa dola za kimaekani million 500; mnalipa kodi ya Tsh million 500. Hapa hamchomoki leo
 
kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,727
2,000
MAJI YAKIISHA MWAGIKA hayazoleki, yaani mmeanza kuleta doc. za kuforge kama hizo Document zingekuwepo mbona mtetezi wa serikali jana Sospeter MUONGO hakuzitaja wala kuwanazo?
 
Gagnija

JF-Expert Member
Apr 28, 2006
8,171
2,000
Hayo Malipo ni Kwa mkataba wa kughushi walitakiwa kulipa kwa bei halisi waliyonunua matapeli kabisa hao
Mkuu usidanganywe. Hakuna mauziano yaliyofanyika baina ya Mechmar na hao Piperlink. Mechmar wamiliki wa 70% ya hisa za IPTL walifilisiwa tangu 2005 na mali zao ikiwemo hiyo mitambo ya Tegeta kuchukuliwa na wadai Danaharta ambao nao baadaye waliwauzia Standard Chartered ya Hongkong.

Huyo mwizi Singa akibanwa tutajua mhusika mkuu hasa ni nani.
 
King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
34,422

Singasinga ni misheni town,kapewa mchongo kaja kuipiga hela kawagawia washirika then anatambaa kama alivyowaliza wakenya.
 
ZIRO

JF-Expert Member
Nov 10, 2014
899
1,000
mbona documents zina muhuri wa bank tu? mbona muhuri wa tra haupo?
 
storage

JF-Expert Member
Jul 27, 2014
520
0
rebeccamrema tumia akili acha kutumia ujinga kuleta ujinga hapa.
Hizi taarifa CAG anazo au ziko kwenye ripoti ya PAC?
 
Last edited by a moderator:

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
7,094
2,000
Imefahamika kuwa IPTL ililipa ushuru wa stamp Duty kwa TRA kama ilivyotakiwa kufanya kutokana na Mauzo ya Hisa kutoka Mechmar kwenda PIPERLINK INVESTMENTS LTD na Kutoka Piperlink Kwenda PAN AFRICA POWER SOLUTIONS (PAP), PAP Ililipa malipo ya Ushuru TRA wakati wa mauzo hayo ya hisa
Malipo hayo ilikuwa kama ifuatavyo:
1.Kutoka Kampuni ya Mechmar kwenda PIPER LINK INVESTMENT ltd IPTL ililipa kiasi cha Tsh 95,940,000/= kama malipo ya ushuru wa Stamp kwenda TRA.
2. Kutoka kampuni ya PIPERLINK INVESTMENT ltd kwenda PAN AFRICA POWER SOLUTION (PAP),IPTL/PAP ililipa kiasi cha Tsh. 315,200,000 kama malipo ya ushuru wa Stempu yaani Stamp Duty
Hivyo basi kufanya jumla ya Malipo ya Stamp Duty kwa kampuni hizo kuwa jumla ya Tsh 411,140,000.(Tazama Viambatanisho)
Kwa Ushahidi huu nachelea kujiuliza maswali mawili
1. Je CAG alipotoshwa au aliamua kupotosha Umma kwa makusudi kuwa mauzo ya Hisa kati ya kampuni Mechmar kwenda PIPER LINK na mauzo ya hisa kati ya Piperlink kwenda PAP hayakulipiwa ushuru wa stempu (Stamp Duty)
2. Je Ripoti ya PAC ilipotoshwa au iliamua kwa makusudi kupotosha umma juu ya suala hili?
Imefika wakati sasa viongozi wetu hasa wa kisiasa kuacha kutumia uongo na kupotosha umma ili kujitafutia umaarufu wa kisiasa katika mambo yenye maslahi mazito kwa Taifa letu hasa sekta ya Nishati.
Napenda kuwasilisha.

View attachment 206418

View attachment 206419

View attachment 206420

View attachment 206421

View attachment 206422

View attachment 206423

View attachment 206424

kwenda zenu matapeli wakubwa. ducuments zote hizo za kugushi. tuna imani kubwa na cag,...wezi wakubwa.
 
rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,840
2,000
wewe unawashwa au nini?kwenda huko kamuombee audustino mrema anataka kufa kwa presha
 
  • Thanks
Reactions: BAK

afwe

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
4,085
2,000
Tumesha wajua nyie kwa uwezo wa pesa mlizo kwapua mnauwezo wa kununua chochote kutoka kwa watumishi wetu wenye njaa. Mihuri ya serikali inagongwa hata na mhudumu wa ofisi. Ondoa upuuzi wako
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom