Ushahidi Kagoda waitikisa Serikali

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,975
9,566
SAKATA la Kampuni ya Kagoda iliyokwapua sh bilioni 33 kutoka kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), mali ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), limechukua sura mpyaa baada ya ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP)na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kuunda kikosi kazi kuchunguza sakata hili.

Habari ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata, zilisema kuwa ofisi hizo zimeteua maafisa wake kuunda kikosi kazi kuchunguza sakata hilo lililoibuka upya wiki iliyopita baada ya mwanaharakati maarufu nchini, Kainerugaba Erick Msemakweli, kuja na ushahidi mpya.
Msemakweli ambaye pia ni mwanasheria, alimtaja mfanyabiashara maarufu nchini Yusuph Manji and Rostam Aziz kwamba ndio wamiliki wa kampuni hiyo tata ya Kagoda Agriculture Ltd.

Kwa mujibu wa Msemakweli, wengine katika sakata hilo ni Tabu Omari, John Kato, Barati Goda, Gulam Abdurasul Chakaar na Bahram Abdurasul Chakaar.

Majina ya walioteuliwa kuunda kikosi kazi hicho na taasisi wanazotoka kwenye mabano ni pamoja na Benn Lincoln (TAKUKURU) na askari aliyejulikana kwa jina moja la Mswano, pia kutoka TAKUKURU. Wamo pia Fadhili Mdemu toka ofisi ya DCI na Biswalo Makanga kutoka ofisi ya DPP. Vyanzo vyetu vya habari kutoka ndani ya taasisi hizo, zilisema kuwa serikali imeamua kuchunguza upya sakata la Kagoda kutokana na ushahidi huo ambao ni wa kwanza kwa uzito kutolewa nchini.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari hivi karibuni, Msemakweli amewasilisha ushahidi unaonyesha jinsi Rostam na Manji na washirika wao walivyohusika kuchota fedha hizo.

Moja ya ushahidi huo unaonyesha jinsi fedha hizo kutoka Kagoda, zilivyokuwa zikihamishwa kupelekwa Uarabuni. Kwa mujibu wa ushahidi huo, inaonyesha kuwa kati ya Oktoba 28 na Desemba 27, 2005, kiasi cha sh bilioni 3,081,648,500, kilitolewa kutoka katika akaunti ya Agriculture Company Limited. Kiambatanisho KM-15 cha kivuli cha moja ya maombi yaliyofanywa na kampuni hiyo kwa Meneja wa Tawi la Holland House Novemba 24, 2005 kwa vielelezo namba KAL/CRDB/09/05.

Desemba, 2005 fedha yote katika matawi mbalimbali ya CRDB ilikuwa tayari imebadilishwa kuwa dola za Marekani na kuhamishiwa katika akaunti ya dola ambayo Kagoda Agriculture Company Limited waliifungua kwa msaada wa Yusuf Manji na Rakesh Mehta katika CRDB Holland House. Desemba 2005 na mwanzoni mwa mwaka 2006, fedha yote ya Kagoda Agriculture Company Limited kwenye akaunti yake katika tawi la Holland House yenye jumla ya dola za Marekani 28,960,000, ilihamishiwa katika akaunti ya mhusika wa kwanza kwenye tawi hilo kupitia cheki nne za benki kama ifuatavyo: cheki hizo ni dola 7,600,000 ya Desemba 27, 2005, cheki ya dola 7,400,000 ya Desemba 29, 2005, cheki ya dola 7,060,000 ya Januari 2, 2006 na cheki ya dola 6,900,000 ya Januari 2, 2006.

Kwa mujibu wa ushahidi huo ambao nakala tunayo, zaidi ya miezi kadhaa taratibu zilifanywa na Rakesh Mehta kwa maelekezo ya Yusuf Manji, kuhamisha dola za Marekani 28,960,000 nje ya nchi na kuzipeleka Dubai. Fedha hiyo ilihamishwa kwa wingi wa dola 1,000,000 au jumla pungufu kiasi; kwamba Machi 31, 2006 kulikuwa na salio la dola 9,084,762.64 ambazo zilikuwa hazijahamishwa.

Katika tarifa yake, Msemakweli alikanusha kuwepo uhusiano wowote wa fedha hizo na uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, uliomwingiza Rais Jakaya Kikwete madarakani. Badala yake, Msemakweli alisema uchunguzi ulionyesha waliohusika na Kagoda ni wafanyabiashara maarufu wawili nchini kwa kushirikiana na jamaa zao wa karibu, "Watu hawa wamekuwa wakieneza uvumi kwamba fedha ziliibwa na kutumika kwa madhumuni ya kampeni ya CCM mwaka 2005, jambo ambalo si kweli."

Akasema kati ya Desemba 30, 2005 na Januari 2, 2006 fedha hizo zilikuwa hazijatumika na uchaguzi ulikuwa umemalizika.
Alisema waliohusika katika kusajili Kagoda BRELA ni watu wawili chini ya udhamini wa mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam kwa kutumia kampuni zake na watu hao walitumia majina ya uongo ya Francis William na John Kyomuhendo, tofauti na majina yao halisi.
Alisema Kamati ya Johnson Mwanyika iliyoundwa na serikali kuchunguza sakata la wizi wa fedha za EPA, ilibaini kuhusika kwa wafanyabiashara hao, hivyo iliamua kumnyang'anya mmoja wao hati ya kusafiria, kufunga akaunti zote za kampuni zake na kumuamuru kurejesha fedha hizo.

Msemakweli alisema uzushi unaenezwa kwamba mwizi wa Kagoda hajulikani, wakati Kamati ya Mwanyika ilimwita na kumpa muda wa kurejesha na akafanya hivyo.
 
Twende taratibuuuuu
&lt;br /&gt;<br />
&lt;br /&gt;<br />
wasiwasi wangu ni kwamba tume iliyoundwa/itakayoundwa haitakuwa huru kusema ukweli. Issue ya kagoda Jk hakosekani, kwani ndiyo pesa zilizotumika kumwingiza JK ikulu. Vilevile nina wasiwasi wakurugenzi waliounda hii tume walishakwapua sehemu ya pesa hizo.
 
hakuna kitu hapo maana jambo kama hilo lilishafanyika wakafunga majalada kwamba hakuna kitu zaidi ya kuibuka na majibu kwamba ni unknown sasa vp tena? ni maigizo tu
 
Kunakitu kina nichanganya hapa.

Kwani wamiliki wa Kagoda hawakukamatwa kwasababu walirudisha fedha au kwasababu hawajulikani? Maana mimi ninavyokumbuka na nilivyohifadhi taarifa zangu ni kuwa Mhe. Kikwete alisema wanaorudisha fedha hawata kamatwa! Hivyo nilijuwa kuwa hicho ndio kilichofanya hawaku kamatwa! au sasa watakamatwa kwasababu imebainika kuwa fedha hazikuingia katika kampeni za Kikwete!
 
Hakuna lolote la maana hapo. Tume inaundwa na watu toka ofisi ambazo zote hazina crdibility ya kusema ukweli sasa tutarajie nini cha maana? Another "funika kombe mwanaharamu apite"!
 
Kuna siku huu usanii tunaoufanya tutakosa pa kukimbilia.Tumuulizie Ghadafi ameishia wapi? we do not have immune for life
 
fedha za Kagoda zinahusiana moja kwa moja na CCM na baadhi ya wafadhili wake wakubwa Rostam na Manji. Lakini kinyume inavyoaminiwa na watu wengi fedha zile ni kiasi kidogo sana kiliingia kwenye uchaguzi huku kiasi kikubwa kikitoroshwa nje ya nchi. Manji na wenzake wamevunja sheria nyingi tu ambazo kama DPP angekuwa na uwezo japo kidogo angehakikisha wanafungwa siku nyingi sana. Baadhhi ya sheria ambazo naamini wamezivunja ni:

a. Proceeds of Crime Act ya 1991
b. Sheria ya Uhujumu Uchumi na Mitandao ya Kihalifu
c. Sheria ya masuala ya Benki

Na nyingine nyingi tu. Bahati mbaya sana DPP wetu hana uwezo na nia ya kupambana na watu hawa ndio maana alikubali "kuteuliwa" kuunda kamaati isiyo na nguvu ya kisheria wala madaraka ya kisheria kuchunguza uhalifu zaidi ya kuwa an advisory panel.
 
Ah.! Tz tabu 2pu. Nasikia semakweli ana2miwa na sisiemuu. Amejaribu kuinasua ktk hii tuuma ya kagoda. Mwanaharisi limeeleza.
 
CCM wanamtishia nyau Rostam ili asiwaharibie uchaguzi Igunga ,ila wajua siku ambayo Rostam atajibu
mapigo , ndo itakuwa anguko kubwa la JK
 












Mwandishi Wetu
7 Sep 2011
Toleo na 202












SERIKALI imezinduka kutoka usingizini na kuanza upya kuchunguza sakata la wizi wa shilingi bilioni 30 katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) iliyopo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupitia kampuni ya Kagoda Agricultural Limited, siku chache baada ya mwanaharakati Kainerugaba Msemakweli, kuwasilisha ushahidi wake serikalini.
Msemakweli aliwasilisha ushahidi wake Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), akiambatanisha vielelezo kadhaa kuhusiana na sakata hilo kabla ya kuitwa na kutakiwa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola vilivyoanza rasmi uchunguzi.
Raia Mwema imethibitisha kuwapo kwa mawasiliano rasmi kati ya DPP, polisi kupitia Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai (DCI) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuhusiana na kuanza upya kwa uchunguzi wa Kagoda, uchunguzi unaoratibiwa kwa karibu na uongozi wa juu kabisa wa taasisi hizo za dola.
Nakala ya barua ya Septemba 2, 2011 kwenda kwa Msemakweli inaonyesha kuwa DPP amelikabidhi suala hilo kwa DCI, ambaye atachunguza kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola, uchunguzi ambao tayari umekwisha kuanza baada ya mapumziko ya Sikukuu ya Iddi El Fitri.
Habari za uhakika zimethibitisha kuwapo kwa kikosi kazi kinachojumuisha ofisa mwandamizi kitengo cha sheria cha Takukuru, maofisa wawili wa polisi kutoka ofisi ya DCI, mmoja akitajwa kuhusika kikamilifu katika kesi kadhaa za EPA na anayeaminika sana serikalini na ofisa mmoja wa ngazi ya juu kutoka ofisi ya DPP.
Taarifa zinasema Msemakweli alikuwa afanye mahojiano na kikosi kazi hicho katika ofisi zake Mikocheni, Dar es Salaam mwanzoni mwa wiki hii lakini hilo likashindikana kutokana na hali ya afya yake kuwa dhaifu na hivyo mahojiano hayo kuahirishwa hadi leo Jumatano.
Msemakweli ameliambia Raia Mwema jana Jumanne kwamba amekuwa akitumia dawa zinazomchosha na kwamba amelazimika kupumzika kwa siku mbili nyumbani na ameomba kwenda kufanya mahojiano akiwa na nguvu za kutosha kuainisha ushahidi alionao kuhusiana na suala hilo.
Katika nyaraka alizowasilisha kwa DPP na baadae katika mkutano wake na waandishi wa habari wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, Msemakweli amewataja baadhi ya watu ambao anaamini wanahusika moja kwa moja katika wizi wa fedha kupitia kampuni ya Kagoda huku akionyesha jinsi fedha zilivyohamishwa kati ya Desemba 2005 na Machi 2006.
Tayari watuhumiwa kadhaa wamekwisha kufikishwa mahakamani kuhusiana na wizi wa fedha za EPA baadhi wakiwa wamehukumiwa kifungo, lakini wale wa Kagoda walikuwa bado hawajashitakiwa ikielezwa kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha.
Kiasi cha Sh. 33,956,442,875.99 (sawa na dola za Marekani 30,732,658.82 ) zililipwa kwa Kagoda kutoka BoT kupitia akaunti za kampuni hiyo zilizofunguliwa kwa siku moja katika matawi sita tofauti ya benki ya CRDB Limited ya

Holand akaunti namba 01J1021795700,
Azikiwe 01J1021795701,
Tower 01J1021795702,
Kijitonyama 01J1021795703,
Lumumba 01J1021795704 na Vijana.
Kwa mujibu wa nyaraka hizo, ni kiasi cha Sh 3,081,648,500 pekee ndizo zilizotolewa taslimu Novemba 2005, fedha ambazo zilitolewa kwa dola za Marekani kabla ya fedha hizo kufanyiwa ubadilishwaji kutoka dola kwenda shilingi za Tanzania na baadaye tena kwenda dola za Marekani kabla ya kuhamishwa kwenda Dubai kati ya Desemba 27, 2005 na Machi 2006.
Nyaraka hizo zinaonyesha kwamba kiasi cha dola za Marekani 28,960,000 zilikusanywa kutoka kwenye matawi mengine ya DRDB kwenda tawi la Kagoda la Holand na baadaye kuhamishiwa kwenye akaunti ya kampuni ya Quality Finance Corporation Limited (QFC) 02J1121066500 kwa mafungu kwa kutumia hawala ya benki (Bankers Cheques).
Nyaraka zinaonyesha kwamba dola 7,600,000 zilihamishwa Desemba 27, 2005, dola 7,400,000, Desemba 29, 2005, dola 7,060,000 Januari 2, 2006 na dola 6,900,000 Januari 2, 2006, fedha ambazo zilihamishwa kwenda Dubai, Falme za Kiarabu kupitia dula moja maarufu la kubadilisha fedha za kigeni kwa mafungu ya chini ya Dola za Marekani 1,000,000 katika kipindi cha miezi mitano.
Hadi Machi 2006, Akaunti ya Quality Finance ilikuwa na kiasi cha dola za Marekani 11,084,762.64 kutoka kampuni ya Kagoda zilizoingizwa kupitia akaunti ya tawi la CRDB Holand.
Kwa mujibu wa Msemakweli na nyaraka ambazo Raia Mwema imeziona baada ya Serikali kuunda tume ya kuchunguza sakata la EPA na kuamriwa wahusika kurudisha fedha hizo, mwaka 2008 miaka miwili baada ya kuchota fedha hizo (dola milioni 28.9) zikiwa katika fedha za kigeni, wahusika wa Kagoda walilipa fedha hizo kwa shilingi za Tanzania bila kuzingatia viwango vya kubadilisha fedha vya wakati huo kwa kulipa Sh 31,710,000,000 kati ya Januari na Juni 2008.
Wakati kampuni ya Quality Group Limited ikilipa Sh bilioni 31.7, kampuni ya Afritainer Limited ililipa Sh 3,081,648,500 kwa serikali kupitia akaunti yao iliyopo benki ya Exim, fedha walizoziingiza kama fedha taslimu benki na kuzilipa kwa Serikali kupitia bankers cheque.
Kwa mujibu wa Msemakweli, wamiliki halisi wa Kagoda wanaoonekana kwenye nyaraka za kampuni hiyo iliyosajiliwa Septemba 29, 2005 John Kyomuhendo na Francis William walitumia majina bandia na kwamba wamiliki halisi ni John Kato na Barati ambao nao amewaeleza kuwa walifanya kazi hiyo kwa maelekezo ya wafanyabiashara wakubwa.
Nyaraka zilizowasilishwa zinaonyesha kwamba wamiliki wa Kagoda walidhaminiwa kufungua akaunti benki na kampuni za Caravan Roadways Limited na Peak Traders Limited, ambazo ni kampuni zilizoko chini ya kampuni ya Quality Group Limited, inayomilikiwa na familia ya mfanyabiashara Yussuf Manji.
 
"serikali imeamua kuchunguza upya sakata la Kagoda kutokana na ushahidi huo ambao ni wa kwanza kwa uzito kutolewa nchini."

Is this statement serious??????
 
Brella ni ya serikali, inachekesha na kuhuzunisha serikali inaposema kuwa haiwafahamu wamiliki wa Kagoda. Hiki ni kielelezo kimoja wapo kati ya vingi kuwa wajanja wachache wameiweka serikali yetu mifukoni mwao.
 
Pamoja na kuusifu ujasiri wa Msemakweli na kumpongeza sponsor wake, ni mahali pamoja tu panaponikatisha tamaa juu yao, hili la kujikomba kwa CCM, sioni kwa nini msemakweli na sponsor wake wanahangaika sana kuonyesha kwamba fedha hiyo haina uhusiano na urais wa Kikwete, hapa nao wanakua kama hao hao wezi, wanabaka demokrasia, ni vizuri kama wanajikomba sana kwa JK, waache watanzania waamue kama hizo hela zilitumika wapi, kama msemakweli ni mkweli na msomi kama ninavyoamini, aache kabisa kukubali kuwa mpumbavu kwa kujiingiza kwenye unafiki wa sponsor wake, tunamjua na huyo sponsor pamoja na kufanyakazi nzuri tunamjua mnafiki kwa kuwa anajikomba kwa CCM tu kwa sababu ya maslahi yake binafsi. Huwezi kuwa popo kwenye ukweli na hiki ndio kina water down arguments nzuri na evidence nzuri za msemakweli. Hivi utasemaje eti hela hazikutumika kwa kuwa tarehe ya kuzihamisha ilikua baada ya uchaguzi? crap stop this rubbish, what is the relationship between tarehe ya uchaguzi na ya kuhamisha hela? hapa mngekazana na nani mwizi na yoyote aliyeshiriki ni culprit, mtatetea lakini tanzania ni ya watanzania wote siku ya siku bila kujali vyeo wala nini watafungwa tu jela watu hawa, hata mkiwauma na kupuliza, kumbuka hamuwezi kupambana na wakina Rostam na Manji mkitegemea eti kumwokoa JK, fanyeni maamuzi magumu kama mnajikomba sana kwa JK waacheni wakina Manji na Rostam wapumzike, hamuwezi kuwagusa hawa na kumponya JK wakati huo huo. neno linasema, mafuta na maji havichanganyiki, giza na mwanga vile vile, poleni sana
 
Jamani kutokana na wingi wa hizi skendo za serikali yetu kuna wakati nachangayikiwa kujua ipi inahusiana na wapi. Nisaidieni kwa hili tafadhali.
1.Hivi EPA na Kagoda si ndugu hawa!!!
2. Ile tume ya IGP, DCI, PCCB aliyounda Luhanjo ishughulikie EPA, iliwahi kutoa taarifa mahali popote duniani
3. Hii tume iliyoundwa baada ya Msemakweli kusema, ina nguvu gani kisheria na inawajibika kwa nani
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom