Ushabiki wa vyama vya upinzani unatufanya tuunge mkono mgomo wa madaktari? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushabiki wa vyama vya upinzani unatufanya tuunge mkono mgomo wa madaktari?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Vijisenti, Jun 30, 2012.

 1. Vijisenti

  Vijisenti JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 476
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Wengi mnaopita hapa jamii Forum bila shaka hamjawahi kuishi
  vijijini mkajionea wenyewe jinsi maisha ya WALIMU yalivyo. Pia
  hamjawahi kufanya uchunguzi juu ya ugumu wa Maisha katika
  Kada nyingine.

  Pia hamjawahi kutafakari jinsi madaktari hawahawa wanavyokuwa
  MIUNGU WATU katika sehemu zao za kazi, pengine hamjawahi kufikiri
  jinsi walivyokuwa wala Rushwa wakubwa hususani MOI.

  Kabla ya mgomo madaktari utendaji wao ni mauaji Tosha kwa watu
  wengi, Tatizo linalojitokeza kwenye mgomo ni ushabiki mkubwa wa vyombo
  vya habari na kutia chumvi kubwa ikiwa ni mtaji wa kisiasa kwa vyama
  vyetu vya upinzani.

  Mimi sio mwana CCM lakini hapa tusidanganyane MADAKTARI WANA MAISHA MAZURI
  sana kwa hali zetu za kitanzania, madaktari ni zaidi ya walimu,maendeleo ya jamii,
  watu wa kilimo n.k.

  Mwisho nimalize kwa kusema madaktari wa Kitanzania ni Wauaji kabla hata
  ya mgomo, wengi wao ni wajeuri hata sehemu za kazi, nimewahi kushuhudia
  daktari pale AMANA HOSPITAL akiondoka na Mwanamke, hawara yake (Demu wake)
  na kuwaacha wagonjwa kwenye foleni.

  Hapa ninachokiona MADAKTARI wanatutesa, serikali pia inatutesa wote
  ni watesaji na walio nyuma ya mgomo pia ni WATESAJI.
   
 2. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  madaktari wanatutesa,wapinzani na wanaowapinga wanatutesa sisi tusio na mielekeo ya kisiasa
   
 3. yaser

  yaser JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 1,373
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  kaka umeongea vzuri sana kias kwamba asiye na maskio pia ataskia hata kwa kunusa.ila ishu kwa cc wapinzani tukishaamka na ndoto zetu nyevu za 2015 itakua utata sana hasa kwa uliposema ww ni ccm.ila ukweli mgomo wa madktali umekuwa ukipewa support sana na wanasiasa wetu ambao kwa sasa wamesahau kabisa kuna watu wanapoteza maisha yao.ngoja tuone maoni ya wengine
   
 4. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Umenena vyema sana mkuu, hapa ndipo ule usemi kuwa adui yako muombee njaa, wengi wetu tunaunga mkono kwa vile madhira haya yapo chini ccm ila wamesahau kuwa ni binadamu wenzao ndio wanakufa. Mfano mzuri ni watu wapo bize kutafuta habari za DR U limboka na sio athari za mgomo.
   
 5. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  ili kutusaidia sisi wengine tulio na muda mchache wa kupata media, tufafanulie ni kwa namna gani wanasiasa wako involved katika mgomo. Mpaka sasa malaika wa Mungu wa kweli wametufunulia kuwa Dk Uli aliteswa akilazimishwa akiri kuwa chama cha CHADEMA kinawasaidia, pamoja na kungolewa meno na kucha hakukiri hivyo. Kama hutonifafanulia juu ya hilo, niache neindelee kukuaminisha kuwa JF nayo imeingiliwa na watu wanaotaka kupotosha jamii juu ya mgomo wa madaktari.
   
 6. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli sijapenda mgomo wa madr lakini huumgomo unasababishwa na serikali dhaifu na hawa wapinzani tunawapa sifa tu, jk ajitahidi kulishughulikia haya hakuna mambo yanayoisha bila kufanya kazi! Tatizo jk anataka nature iongoze ndo maana hata umeme alisema yeye hana nguvu za kufanya mvua inyeshe!
   
 7. yaser

  yaser JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 1,373
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  kaka support hapa zipo kwa namna tofauti.ile ya direct na ya indirect.wanasiasa wetu wanatoa support ya indirect na ndio maana wao muda wote wanajadili mgomo na hakuna hata mwanasiasa mmoja hasa wa upinzani uliyemsikia akiwasihi madaktali warudi kuokoa wananchi wanaopoteza maisha yao.ina maana hili hawalioni?hapo ndipo tunaoona mbali tunajua kua wansiasa wamepata ''loophole'' na kwa maelezo haya cdhani km napotosha jamii labda ambaye hataki kuelewa
   
 8. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  sasa nataka nikuunge mkono na kama ukiona yafaa ukiri kuwa nimekuunga mkono: wanasiasa ( wa chama tawala nawa upinzani) wote wameoneshwa kukerwa na ubadhirifu wa fedha uma huku wana nchi wakikosa huduma muhimu kama afya. Je; sasa tusme kuwa huu mgomo wa madaktari umelenga kutia nguvu kauli hizi za wanasiasa?!, kama ndivyo; basi hawa wanasiasa wanaolalamikia huduma duni nao wapelekwe mambwepande wkangolewe meno na kucha na kuvunjwa mikono na viungo vyao vya kiume kwa kuwa wao ndiyo chanzo cha mgomo?!!!!!!!. Tafakari vizuri chanzo cha mgomo hasa baada ya kupitia orodha ya malalamiko ya madaktari.
   
 9. F

  Froida JF-Expert Member

  #9
  Jun 30, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Si hitaji siasa kujua haki ya msingi haki ya kuishi ni pamoja na kupata tiba bora
   
 10. m

  mamajack JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  ndiyo maana nimesema tuache kufikilia kwa mtazamo huu.sio kila anayepaza sauti kuikemea serikali badhilifu ni mwanasiasa,watanzania inabidi tuwe na ptazamo mpana.lweli tunateseka,lakini wa kumlaumu sio dactari maana sie wananchi hatuna mkataba na dactari ila serikali ndiye anamkataba na madaktari.hata wlimu polisi etc ndiyo wentemkataba na serikali,lakini sie muhusika mkuu katika hili tunayeweza kumhoji ni serikali maana ndiyo tuliyoiamini tukawachagua kwa kura nyingi na wakaingia madarakani ili watutumikie.lakini hilo wamelisahau,wnajitumikia wenyewe kwanza,wakishiba watatukumbuka.hivyo basi kiliochetu tukielekeze kwa serikali ili wafikie muafaka na hao watu wao.kama wameshindwa wautangazue uma kuwa imeshindikana.
   
 11. kussy

  kussy JF-Expert Member

  #11
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 15, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  You are so right!!!!

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 12. H1N1

  H1N1 JF-Expert Member

  #12
  Jun 30, 2012
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 4,201
  Likes Received: 528
  Trophy Points: 280
  Umejitahidi sana kuandika,lakini umepungukiwa na kitu kimoja,UKWELI KUHUSU HOSPITAL ZA SERIKAL,kwa kadri ya uelewa wangu kitu Hospitali kukamilika ina maana ya Kuwepo na Majengo kwa anjili ya tiba kwa wagonjwa,kuwepo na wagonjwa wa kutibiwa hapo,kuwepo na vifaa vya TIBA pia pawepo na wahudumu wa TIBA Wauguzi na Madaktari. sina hakika kama umewahi kujiuliza kabla ya kuandika hapa kama hospital zetu zina sifa ya kuitwa hospital kweli na ukatathmini bila hila madai ya madaktari.Madai yao na mgawanyiko wake,ambapo kuna madai ya maslahi na madai ya mazingira ya kazi na vitendea kazi.
  Ukiacha ukweli kwamba wengi wa members wa JF ni watu wanaotibiwa kwa waajiri wao au kwa kujitegemea wenyewe ambapo kwa kutumia kadi za ajira za TIBA au pesa zao, mara nyingi sana huenda kutibiwa kwenye Hospital za binafsi na mashirika ya dini ambazo kwa ukweli zina sifa kiasi kikubwa kuitwa Hospitali,si kwa majengo tu bali hata kwa kuwepo kwa vitendea kazi.
  Ukweli wa kinachoitwa hospital za serikali sio hospital 'labda tuite sehemu za kupata ushauri wa kimatibabu' ambapo daktari anauwezo wa kumhoji mgonjwa juu ya ugonjwa wake,kumshauri akatafute vipimo popote,na mwisho kumwandikia dawa,either ni dawa ambayo ipo hospital hata kama si sahihi sana kwa ugonjwa wa mhusika au amwandikie dawa na amshauri akanunue duka la madawa.
  Kwa kipindi kirefu sana madaktari wamekuwa wanaangamiza wananchi kimya kimya kwa kukaa kimya huku wakijua hawawezi kutumia taaluma yao kuokoa maisha ya watz masikini waliotapakaa nchi nzima,kwa kukaa kimya na kufumbia macho ukweli wa kuwa wao hawafanyi kazi ya udaktari kwa kadri ya taaluma kutokana na miundo mbinu mibovu ya hospital za umma.
  Ni wakati sasa baada ya miaka 50 ya uhuru waTZ tuamke ili kodi yetu itumiike kwa manufaa yetu kwa kuimarisha huduma za elimu na afya,madaktari wameonyesha njia sisi wananchi tuungane kuhakikisha mabillion yaliyotengwa kwa anasa yatumike kununua vitendea kazi vya mahospital yetu yote kuanzia wilayani,mikoani hadi rufaa. Haiwezekani wakimbilie india kwa madaktari walio na uwezo sawa na wa kwetu ila wao wana vifaa TIBA vya kutosha,ni wakati wa kulazimisha viongozi wa serikali watibiwe kwenye hospitali wanazotibiwa wapigaa kura wao.TUACHE UNAFIKI TUNAANGAMIZA TAIFA
   
 13. yaser

  yaser JF-Expert Member

  #13
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 1,373
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  ndugu ulietangulia umeongea mengi sana na nmekuelewa nilivyopaswa.ila nina doubt kidogo na haya madai ya madktari.sidhani km kweli suala la vitendea kazi ni mkipaumbele cha mgomo ndani ya mioyo yao kwa sababu hili swala halikuanza leo,toka mwanzo wa hii nchi mamb o yalikua hivyo iweje,ina maana cku zote hizo hawakuona kua vifaa na mazingira ya kutendea kaz hakuna.ukitazama kwa mbali zaidi unajua kabisa wanachodai hapa ni pesa ambazo wanadhani zitwafaa kulingana na kupanda kwa maisha ya kileo.tunaishi nao kaka mitaani hawa jamaa,ni watu wanaopenda haya mambo ya "fweza".so mi nawasihi tu ndugu zangu warudishe moyo waendelee kutibu watanzania wenzao.by the way wengi nadhani walichagua udakitari kua "carrier" yao na sio tu "job" so km ndio hvyo basi wafanane na hiyo carrier.
   
 14. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #14
  Jun 30, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  No, ushabiki wa hospitali zenye dawa na vifaa vya tiba, na wataalam wa ukweli (wasiolazimika kukimbia nchi yao) ndio sababu. Nauli ya India siiwezi.
   
 15. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Si sawa kwa mtoto wa mbunge kusoma shule bora sababu tu eti mzazi wake ni mbunge, huku mtoto wa daktari (PROFESSIONAL) akisoma shule za ovyo kwa sababu mzazi wake ni daktari au mwalimu. Mafao yawe EQUITABLE.
  And we must start somewhere.
   
 16. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #16
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ukiona watoto wa CHADEMA JF wanashikia bango kitu ujue nyuma yake kuna UDINI! Same old consipiracy, if you know what I mean!
   
 17. m

  mkupuo JF-Expert Member

  #17
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Mimi jamani ni gamba nilikuwa napita tu wakuu!
   
 18. R

  Rebel volcano JF-Expert Member

  #18
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kilichobaki ni wananchi wanapokuwa hospitali na wakakutana na madoctor majeuri kama hao ni kuchukua hatua mkononi kwa kuwapa kichapo kama cha ulimboka,litakuwa funzo tosha,wananchi kuwanyanyasa muwanyanyase!vurugu mufanye!
  wale munaolilia uongozi 2015!jiekeni sawa uraisi ni kiti cha moto yoyote atakaekikalia lazma makalio yapate umoto wake!
  nimefikisha hoja!yatarudi yale ya mwembe chai ila mara hii tutajua kujitangaza kimataifa zaidi(lengo ni kuchafuana mwanzo mwisho)
   
Loading...