Ushabiki wa vita vya nje kabla ya vya ndani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushabiki wa vita vya nje kabla ya vya ndani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by tutaweza, Aug 13, 2012.

 1. tutaweza

  tutaweza JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Jamani nadhani kuna watu wanataka kuzibadili fikra zetu za kupambana na maadui wa kweli waliojidhihirisha Tanzania (ufisadi, umaskini, siasa chafu, n.k both domestic) na kututaka tushabikie vita na Malawi.
  Yaani tunataka kupigana na nchi wakati vita na mtu mmoja mmoja inatushinda (simaanishi kwamba hatuwawezi Malawi kwa vita - wale tunachapa anytime, ila sio priority)?
  Tumeshindwa kuwashtaki mafisadi na kurudisha fedha zetu zilizoibiwa. Kumbuka tukishinda vita ya ufisadi na uongozi mbovu wa baadhi ya wanasiasa pato la nchi yetu litaimarika maradufu na kuachana na bajeti tegemezi ya ombaomba huku maisha bora kwa kila mtanzania yakiwa dhahiri (na sio midomoni mwa watu wachache kama ilvyo sasa).
  Kwanza vita na Malawi inatakiwa iwe solution ya mwisho kabisa baada ya kushindikana kwa njia nyingine zote. Hapa nimeshanganzwa na kauli za kibabe kutoka kwa wanasiasa wetu (mnawajua) mara tu baada ya kuibuka upya kwa mgogoro wa lake Nyasa. Sio kauli zilizotegemewa kutoka kwa wanasiasa wa nchi inayoonekana kwa nje eti ya kidiplomasia!
  Kwanza Malawi wenyewe hawajatamka kwamba watatetea ziwa lao kwa vita. Hapa inaonekana kama tunaogopa kupambana na Malawi kwa hoja!
  JAMANI EEEH! MAADUI ZETU WA NDANI NI WENGI NA WANAMADHARA MAKUBWA KULIKO YALE YA KUKOSA KASEHEMU KATIKA ZIWA NYASA!
   
 2. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Adui number moja kwa sasa ni CCM na tayari tumeishamuweka kwenye kilengeo, muda ukifika tunatandika manati ya kichwa na kumalizana nae. Kumbuka ni CCM ni waanzilishi wa hizi fyokofyoko za ugomvi ili kutuondoa kwenye mstari, bahati mbaya ni kwamba ni wao waliotufundisha kwamba mshika mbili moja umponyoka, hakuna kuwa na agenda nyingi sana. only one is enough. kuiondoa ccm.
   
Loading...