Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,136
- 4,298
Kwa muda sasa wa siku chache mitandao mingi ya kijamii watu wamekua wakitoa maoni yao kuhusu mgogoro unaoendelea katika ya nchi ya Marekani na Iran huku baadhi ya watu wakionekana kuishabikia Marekani kwa kile walichokifanya huku upande wa pili ukionekana kuilUamu Marekani na kuunga mkono Irani kuwa imefanyiwa vitendo visivyo vya halali kwa kiongozi wao wa kijeshi kuuliwa.
Ushabiki mkubwa ulipo hapo siyo wa siasa na sera za kiamerika na kiirani,bali ni misukumo ya dini ambayo inapelekea watu wengi kuwa upande fulani wa mgogoro huo.
Siyo mara ya kwanza kwa Marekani kufanya shambulio kama hilo, miaka ya 1989, jeshi la Marekani lilitungua ndege ya shirika la Irani na kuua abiria wote 290 waliokuwepo ndani ya ndege hiyo.
JE, SABABU NI NINI MAREKANI WAMEFANYA HAYA LEO?
Ukitazama mgogoro huu haujaanza leo, taifa la Marekani limeonekana kwa muda mrefu likinyemelea mataifa ya kiarabu na mwisho kuyatafutia sababu za vita kwa ajili ya maslahi yao binafsi huku wanajeshi wao wengi na maelfu ya raia wakipoteza maisha yao na mwisho wa siku kuziacha nchi za watu zikiwa chakavu na uharibufu mkubwa.
Alichofanya Marekani ni kutafuta sababu ya kuingia na kuivamia Iran kwa sababu zake anazozijua yeye za kwanini ukanda huo wa Arab. Na kwa kuwa lengo lake ni kutaka vita,
JE KISASI KITALIPIZWA?
Kwa kifupi tusitegemee kuona kisasi kikilipizwa ndani ya Marekani, kisasi kitalipizwa nje ya Marekani kwa yeyote yule aliemmarekani kugeuzwa mbuzi wa tambiko ili Mmarekani apate sababu ya kuivamia Iran, atakua radhi atume pandikizi lolote ambalo litakamilisha kazi ya kisasi,atakabidhiwa dola zake za kutosha na kazi itakua imeisha kwa upande wa kwanza,hapo kisasi kitalipwa na Mmarekani mwenyewe,kwa sababu lengo la Marekani nyuma ya ukanda wa waarabu ni kutengeneza vita na siyo amani.
Yaliyotokea katika mataifa ya Afghanistani,Iraq na Libya,yalikuwa ni maandalizi ya kuivamia Irani,kwa sababu,wao waamerika waliamini wakiweza kuzipiga nchi hizo basi itakuwa rahjisi kuingia Irani kwa sababu tayari uwezo wa kupitisha silaha utakuwa mrahisi zaidi na uwezo wa kutengeneza viabaraka mapandikizi utakua wa kiwango cha juu.
Wakati waafrika tunashabikia hili,tusidhani hatupo kwenye shabaha ya taifa hilo,Afrika ipo katika shabaha hiyo,shabaha ambayo itafuata baada ya Irani kuharibiwa,baadae watamalizia na mataifa ya India,Korea na China,Kisha safari ya mwisho ya Marekani kuwa super power itakamilika ndani ya Afrika kwa muda mfupi kabisa kutokana na nguvu ndogo iliyopo ndani ya bara hili.
KISASI KITALIPWA NJE YA MAREKANI, Irani itavamiwa, vita kubwa itapiganwa, dunia itaathirika na mwisho Marekani wataondoka bila ya sababu ya msingi ya kuishambulia Irani, Uingereza itaomba raia wake msamaha kuwa ilikosea kuwa mshiriki wa vita hivyo, umasikini utarudi nchini Irani, soko la bidhaa la kidunia litapanda, hela itakua ndogo, Marekani atakula bata.
TUJIONGEZE.