Ushabiki ni mkubwa kuliko uhalisia, Vijijini kuna Umasikini wa kutisha

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,482
8,698
Weekend iko poa.
Wakuu nilikuwa na safari za kikazi kwenye mikoa ya Kigoma na Tabora na ilinipeleka hadi vijijini ndani ndani kabisa, Aisee huwezi amini kuna umasikini wa kutisha, hizo Shule za Misingi nilipita Kaliua ni shida tupu.Zahanati yaani haho Mashuka unaweza omba hata ulale bila kufunikwa.

Kufika Kigoma nilianzia Uvinza huko kwa kweli vijijini hali ni mbaya mno, Watoto wanaenda shule peku peku na sale ni zimechakaa hasa.

Kasulu kote huko na Kibondo kote huko hali ni mbaya sana.

Vinavyo itwa vituo vya Afya ni Majengo tu yako pale hizo huma unaweza lia kabisa.

Kibondo nilifika pale hakuna Maji, watu walisha zoea yale Maisha.

Shida kubwa Ushabiki umekuwa mkubwa kuliko uhalisia.
 
Njia pekee ya kuondoa umasikini Tanzania pamoja na mengine ni kuifungua mikoa wilaya vijiji na vitongoji kwa Barbara umeme maji ili miradi ya maendeleo na kufikika kirahisi kuwezekane jambo ambalo rais JPM anafanya kwa kasi kubwa. Tumuunge mkono rais wetu! Maeneo mengi ya nchi hii yalikuwa yamesahaulika na AWAMU zoote ni JPM tu ndo kawakumbuka
 
Mimi naona Magufuli hajaifanyia kigoma chochote mpaka sasa,
Kigoma kwa niijuayo mimi, ingepewa barabara tu za uhakika (lami) kutoka na kuingia,
Aise kigoma ingekuwa mbali sana.
Kinachoiweka kigoma nyuma ni barabara tu, haya mengine ni kama ziada.
 
Kwahiyo watoto kuvaa peku,uniform chafu na mashuka machafu ya zahanati hapo napo analaumiwa Magufuli?
Enyi watu weusi ni nani aliyewaroga?
 
Kigoma inafunguka kwa barabara ambazo zimejengwa na zinaziendelea kujengwa. Nchi hii ni kubwa ni kama tone bahalini? Huwa najiuliza tukiondoa Nyerere aliyejenga misingi ya nchi. Mwinyi Mkapa Kikwete walifanya nini? Nchi ilikuwa inaibiwa hawaoni!
 
Hebu tuwekee hizo picha zenye kuogofya mkuu...kama zipo asante.
 
Kwahiyo watoto kuvaa peku,uniform chafu na mashuka machafu ya zahanati hapo napo analaumiwa Magufuli?
Enyi watu weusi ni nani aliyewaroga?
Maana yake maendeleo ya kiuchumi hayajafika kwa watu wa chini, hakuna mipango ya muda mrefu au mfupi ya kiuchumi. Mfano tungewekeza kwenye kilimo kwa nguvu kubwa kama tunavyofanya kwenye ununuzi wa ndege na umeme wananchi wengi kipato chao kingeongezeka.
 
Kigoma inafunguka kwa barabara ambazo zimejengwa na zinaziendelea kujengwa. Nchi hii ni kubwa ni kama tone bahalini? Huwa najiuliza tukiondoa Nyerere aliyejenga misingi ya nchi. Mwinyi Mkapa Kikwete walifanya nini? Nchi ilikuwa inaibiwa hawaoni!
Nyie watu mnadharau sana. Kikwete kajenga daraja la malagarasi lakini bado mnamuona hana lolote. Sasa niambie Tangu Magufuli aingie madarakani amejenga miundimbinu gani huko kigoma?

Barabara ya Kidahwe-Nyakanazi hamna kitu tangu aondoke. Ameshindwa hata kumalizia hiyo Kidahwe hadi Malagarasi
 
Njia pekee ya kuondoa umasikini Tanzania pamoja na mengine ni kuifungua mikoa wilaya vijiji na vitongoji kwa Barbara umeme maji ili miradi ya maendeleo na kufikika kirahisi kuwezekane jambo ambalo rais JPM anafanya kwa kasi kubwa. Tumuunge mkono rais wetu! Maeneo mengi ya nchi hii yalikuwa yamesahaulika na AWAMU zoote ni JPM tu ndo kawakumbuka
Fact
 
Kigoma inafunguka kwa barabara ambazo zimejengwa na zinaziendelea kujengwa. Nchi hii ni kubwa ni kama tone bahalini? Huwa najiuliza tukiondoa Nyerere aliyejenga misingi ya nchi. Mwinyi Mkapa Kikwete walifanya nini? Nchi ilikuwa inaibiwa hawaoni!

Nyerere pekee ndio alijitahidi akaja kuharibu kwa misimamo yake isiyo na tija. Hawa wengine wote akiwemo Magufuli kila mmoja alijikita kwenye eneo moja. Nyerere pekee ndio aliyejenga viwanda, miundombinu mbalimbali, alitoa huduma nyingi bure kama elimu, afya nk na kwenye uongozi alikuwa muungwana na sio mnyanyasaji.
 
Weekend iko poa.
Wakuu nilikuwa na safari za kikazi kwenye mikoa ya Kigoma na Tabora na ilinipeleka hadi vijijini ndani ndani kabisa, Aisee huwezi amini kuna umasikini wa kutisha, hizo Shule za Misingi nilipita Kaliua ni shida tupu.Zahanati yaani haho Mashuka unaweza omba hata ulale bila kufunikwa.

Kufika Kigoma nilianzia Uvinza huko kwa kweli vijijini hali ni mbaya mno, Watoto wanaenda shule peku peku na sale ni zimechakaa hasa.

Kasulu kote huko na Kibondo kote huko hali ni mbaya sana.

Vinavyo itwa vituo vya Afya ni Majengo tu yako pale hizo huma unaweza lia kabisa.

Kibondo nilifika pale hakuna Maji, watu walisha zoea yale Maisha.

Shida kubwa Ushabiki umekuwa mkubwa kuliko uhalisia.
Vijijini hiyo hali wameshaizoea! Kwenda hospital na kurudi na Panadol tu kwao kawaida na vile uelewa ni mdogo hata hawahoji Mungu tu ndo mlinzi wao

Shule kuchakaa hiyo si vijijini tu hadi mijini hali ni mbaya!

Kuna siku nilitembelea Morogoro maeneo ya Mwembesongo na mafisa pale kuna shule za msingi tatu unaweza usiamini kama ziko manispaa.

Moja inaitwa Mtawala iko barabarani kabisa kama kilomita tatu au nne kabla ya kufika mjini! Wakati huo (July 2019) ile shule madarasa yake nadhani hadi walimu wanaogopa wakiwa wanafundisha muda wowote yanaweza kudondoka!

Kuta zimepasuka pasuka, zimechakaa kiasi kwamba wanafunzi wakiegemea zinadondoka!

Vyoo vimetitia kabisa hadi unajiuliza wanavitumiaje

Shule zote hizo ziko mjini na nadhani tangu zijengwe (sijui enzi za ukoloni) hazijawahi kufanyiwa ukarabati! Zimechoka hadi huruma.

Tembelea shule za kata uone walimu wanavyonyang'anyana madawati ya kukalia na wanafunzi hadi huruma!

Nenda zahanati na vituo vya afya ushuhudie foleni za wagonjwa zinazosubiri huduma ya daktari mmoja au pengine nesi tu anayehudumia zaidi ya vijijini vinne

Watu wanaishi mjini hasa Dsm wanapoona hayo madaraja ya ubungo, terminal 3 za Airport, muhimbili na Amana zilivyopambwa kwa tiles, watoto wanavyo-shine na uniform zao kwenye school bus, wanadhani Tanzania yote ni hivyo hivyo!
 
Kumbukumbu la Torati 15:11
Kwa maana maskini hawatakoma katika nchi milele; ndipo ninakuamuru na kukuambia, Mfumbulie kwa kweli mkono wako nduguyo, mhitaji wako, maskini wako, katika nchi yako.

JPM afanye linalowezekana , tatizo lililolimbikizwa Kwa miaka maelf Hawezi kuliondoa with in 5 yrs
rs or 10, I will stand with JPM ..
 
Back
Top Bottom