USD 300 Million, Pro-Govt, Barrick Gold na Tundu Lissu

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
13,497
29,832
Kwanza niseme jambo moja! Barrick wamekubali kulipa USD 300 Million. Hili si jambo la kubeza lakini pia si la kushangilia! Si la kubeza kwa sababu, kama isingekuwa vurugu za JPM basi hata hizo USD 300 Million tusingepata!!!

Aidha, si jambo la kufurahia sana kwa sababu, mosi, Acacia wameshinda lakini pili, ni jambo lililotuvua nguo !! Wameshinda na tumevuliwa nguo kwa sababu hiyo USD 300 million ni less than 1% ya kile tulichoitangazia dunia kwamba tunawadai Acacia!!

Endapo tunachotaka kupata na tumekubali ni less than 1% ina maana mahesabu ya Acacia yapo sahii kwa angalau 99%!! Vinginevyo, ikiwa kweli serikali iliamini tunawadai Acacia zaidi ya Trillion 400, sijui logic ya kukubali Billion 660 inatoka wapi kama si kwamba serikali nayo imekubaliana na mahesabu ya Acacia kwa kiasi kikubwa!!!

Ngoja tukumbushane jambo dogo sana kutoka Ripoti ya Profesa Mruma. Ripoti ile inasema kwamba:
4. Kwa ujumla thamani ya metali/madini yote katika makinikia kwenye makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini, ni TZS bilioni 829.4 kwa kutumia viwango vya wastani na TZS bilioni 1,438.8 kwa kutumia viwango vya juu.
Hiyo ni Ripoti ya Profesa Mruma ambayo ilituambia kwa yale makontena yaliyokamatwa bandarini awamu ya kwanza peke yake yalikuwa na madini yenye thamani ya angalau Sh. 829.4 Billion!!!

Kwa maana nyingine, pesa tunayolipwa ni pungufu ya angalau TZS 170 Billion kwa kulinganisha na mapato ya makinikia peke yake, tena makinikia yaliyopo kwenye makontena 277 huku, according to JPM, ile siku ya kupokea ripoti alisema kwamba:
Kuna kamati inayotaka kujua makontena yanasafirishwa mangapi, haraka haraka ni makontena 250 na 300 kwa mwezi, kwa mwaka zaidi ya makontena 3600.
Sasa ikiwa madini kutoka kwenye makontena 277 tu yana thamani ya zaidi ya Billion 800; what about makontena yote 3600 yanayosafirishwa kwa mwaka mzima?!!

Swali; ina maana Profesa Mruma na wenzake walidanganya figures ambazo walizitoa?! Kama hawakudanganya, how come tushindwe kupata angalau 25% ya haki yetu?!

Kutokana na ukweli huo, ndio maana nina kila sababu ya kusema Acacia wameshinda tena 5-1!! Hapa ndipo inapokuja hoja dhidi ya wakosoaji wa Tundu Lissu! Wakosoaji hawa wanamkejeli Tundu Lissu kwamba mbona Acacia hawajaenda basi mahakamani!!!

Guys, wekeni siasa pembeni kisha tumieni vichwa vyenu kufikiri!! Kwa mujibu wa ripoti ya kwanza na ya pili Acacia wametufanyia umafia kwa miaka 17. Kodi ambayo tulikuwa tunawadai bila fani ni Sh. Trillion 108 na ukichanganya na faini inafikia zaidi ya Trilioni 400.

Kutoka kwenye Trillion 108 hadi Sh. 660 Billion; hivi hata ungekuwa wewe ungeenda mahakamani wakati unafahamu kabisa kwamba hata kama Trillion 108 sio sahihi basi angalau Trilioni 50 zitakuwa sahihi!!!!

Hivi hapo utaenda mahakamani kufanya nini wakati unafahamu consequences zake?!

Binafsi nimeshawahi kufuatilia kesi kadhaa zinazoendelea kwenye hizi mahakama! Hizi kesi zinachukua hata miaka 10 kabla ya kutolewa maamuzi!!!

Hivi hapo mlitarajia Acacia wangeendelea kurundika makontena kwa muda mrefu zaidi bila kufanya biashara yoyote huku wanaweza kuendelea kufanya biashara at the expense of only $ 300 Million?!

Mlishawahi kujiuliza ni kiasi gani Acacia wangepoteza compared to hizo USD 300 Million endapo wangeenda mahakamani?!

To sum up above argument; kumkejeli Tundu Lissu kwamba mbona Acacia hawajaenda mahakamani inaonesha ni namna gani tunavyoshindwa kuangalia mambo kwa mapana yake!!!

Kwa tozo ya USD 300 Million, Acacia hana sababu ya kwenda mahakamani kwa sababu wameshinda manake endapo wanaenda mahakamani hivi sasa, watakachopteza ni zaidi ya hiyo 300 million hata kama watashinda kesi!!!

Watakuwa wamepoteza zaidi ya 300 million kwa sababu, mosi ingechukua muda mrefu zaidi kurudi kweney biashara huku na pili, hisa zao zingeendelea kushuka!!

Je, Tundu Lissu ameshindwa?! Aliyoongea ni kwa sababu hajielewi?
Text version ya aambacho alisema Tundu Lissu ni hiki hapa:

Sisi Tanzania ni wanachama wa kitu kinaitwa the MIGA Convention. MIGA ni the Multilateral Investment Guarantee Agency ya Benki ya Dunia. Ukiwa mwanachama, Wawekezaji wakileta mali zao kwako, ukiwa-expropriate, ukichukua mali zao kama alivyochukua namna hii, utapelekwa kwenye mahakama za kimataifa... unaenda kushughulikiwa huko. Unaenda kushughulikiwa... huko!
....................................................

Kwahiyo tafadhali sana... na sisi tumezungumza, haya mambo tumeyapigia kelele for years... for years. Hatujaanza jana. Kama unataka kufanya hayo unayoyafanya, elewa hali halisi ilivyo. Tatizo liko wapi! Kama tatizo ni kwamba tunapata mapato madogo... na ni kweli wanatupiga kweli kweli. Wanatupiga kweli kweli. Kama unataka kufanya mambo... kweli kweli, kajiondoe kwanza MIGA ili hawa wawekezaji wasikushitaki kwenye hizo mahakama za huko.
Mosi, kwanini serikali imekubali kulipwa TZS 660 billion out of TZS 108 Trillion (bila faini) au TZS 425 Trillion (with faini)?

Kimsingi serikali wamekubali kwa sababu Acacia walikomaa na kubisha kulipa hayo matrilioni!!! Acacia walikomaa kwa sababu walifahamu endapo serikali wangekomalia hayo matrioni basi wao wangeenda mahakamani !!!

Tutake tusitake, kule mahakamani tungeshindwa tu!!! Kwa wanaofuatilia masuala ya nchi hii wanafahamu ni kesi ngapi tumeangukia pua kwenye hizi mahakama!!! Ukitaka kufahamu ushenzi wa hizi mahakama nendeni pale TANESCO muwaulize ni mara ngapi wamepigwa za uso kupitia issue ya IPTL!!!

Ni kutokana na ukweli kwamba hizi mahakama ni pumbafu, ndio maana Tundu Lissu akasema:
Kama unataka kufanya mambo... kweli kweli, kajiondoe kwanza MIGA ili hawa wawekezaji wasikushitaki kwenye hizo mahakama za huko.
Watu wanaojiita eti ni wazalendo wanakejeli kauli kama hiyo kwa sababu tu imetolewa na Tundu Lissu!!! Au ni uelewa?! Hivi ni uzalendo au ubutu wa kuelewa mambo?!

Alichosema Tundu Lissu ndicho hasa huwa kinafanywa na nchi ambazo zimeamua kuingia vitani kiukweli n hizi multinational companies! Unajiondoa kwanza ili kuwakatia pumzi wawekezaji!!!

Tumeona Acacia walikomaa kwa sababu walifahamu ni wapi wangekimbilia endapo serikali ingekomalia matrioni! Lakini endapo Tanzania wangejiondoa kwanza jeuri ya Acacia ingeishia hapo!!! Wasingekomaa kivile kwa sababu wangefahamu hatimae wanapambana na nchi isiyozitambua the so called sheria za kimataifa zinazolinda wawekezaji!!!

Kutokana na hilo, Acacia ingewabidi ama kukubali kulipa trilioni kadhaa (hata kama sio zote) au kufungasha virago na kuondoka!!

But again, ngoja tugusie kidogo hilo suala la USD 300 Million!!!

Kwenye posts zangu za nyuma nilizungumzia sana suala smelters!!! Kama kawaida, wapo ambao walikuwa wanakejeli na kudai eti unaweza kupata smelters kwa dola elfu kadhaa!!!

Nikatoa changamoto hapa kwamba, kama hizo smelters ni bei ndogo kiasi hicho, ni kwanini basi serikali isiwekeze ili kuwakomoa Acacia wanaotuibia kupitia mwanya wa kusafirisha makontena!

Wiki kadhaa baadae, kupitia ripoti nyingine serikali ikashauriwa kushirikiana na Acacia kujenga smelters!!! Wakati suala la smelters linakuja kwa mara ya kwanza, taarifa zilisema copper smelters zinazotakiwa zinafika hadi USD 500 Million!!!

Hivi sasa moja ya makubaliano ya serikali na Acacia ni kuanzisha kampuni ya pamoja itakayoendesha biashara ya madini kati yao!!! Sasa basi, wakati tunafurahia hizo USD 300 Million, serikali msisahau tumeshauriwa kushirikiana na Acacia kujenga hizo smelters ili makinikia yasisafirishwe!!!

What a genius move from Acacia?!

Yaani Acacia wanataka kutulipa USD 300 Million huku wakifahamu kabisa serikal watatakiwa kuzirudisha ili kujengea copper smelters na bado tunapiga makofi kwamba tumewakomesha!!!!!!

Mbaya zaidi, hivi sasa tutakuwa tunashirikiana na Acacia wakati kimsingi, kwa kiaisi kikubwa tumekubaliana na mahesabu yao na ndio maana tumekubali less than 1% ya kile tunachodai!!
 
Barrick hawajakubali kulipa hiyo $300m, hizo pesa wamezitoa kulinda urafiki tu na sio malipo yoyote. Hiyo ni sawa na rushwa.
Bhana eh, ndo nimeona habari sasa hivi! But you know what?! Hata wakikubali bado wao ni washindi!!! Sidhani kama wanaweza ku-opt kwenda mahakamani wakati wanafahamu paying 300 Million is too cheap kulinganisha na kwenda mahakamani hasa ukizingatia kwenda mahakamani ita-slow sana biashara yao!!
 
Bhana eh, ndo nimeona habari sasa hivi! But you know what?! Hata wakikubali bado wao ni washindi!!! Sidhani kama wanaweza ku-opt kwenda mahakamani wakati wanafahamu paying 300 Million is too cheap kulinganisha na kwenda mahakamani hasa ukizingatia kwenda mahakamani ita-slow sana biashara yao!!

Hawalipi pesa wanazitoa kwasababu ya kulinda urafiki. Inaonyesha yale mahesabu ya TRA yalikua ni ya kupika.
 
Unajua watanzania tuu mahodari wa kukurupuka. Umeambiwa the 300m is just a goodwill gesture but discussions on the tax issues a small committee will formed. Jambo halijamalizika sisi tushalikosoa.

Je, what is the value ya 16% na 50% ya profit value, tena ukichanganya na makubaliano yote , value that Tanzania has achieved is much higher than 190b , kueni nakini na hivi viji Lissu mchwara wanaopinga kila kitu JPM analofanya, kwenye hili nadhani hata Lissu angesema alilizungumzia Hilo bungeni ama angesema Wao kama Chadema ndio ulikuwa ushauri wao bungeni.

Wacheni siasa za kuharisha
 
BARICK hawajasema wanalipa,..So far wamesema hawana deni lolote
Hio Bil 600-700 wanasema wanatoa tu kwa nia njema..Ni kama tashtiti..yaani ni kwa vile tu kama mpiga debe anavyopiga kelele inambidi tu konda amtoe hata jero..ndio hivo yani
Alafu ujue nini Barick wanasema hata hiyo rushwa ya kimtindo inabidi bodi yao ikubali kwanza
 
Watanzania wachache wenye mrengo wa kupindisha ukweli na mema Yanayofanywa na Nchi Yetu mna matatizo sana.

Nilisikiliza jana yale Maelezo. Ile 300 million dollars ni pesa za awali kwa kuonyesha nia njema ya Barric katka majadiliano ya kiasi halisi cha kodi itakayolipwa. Kuna kikosi kazi kidogo kitakachoundwa kupitia nyaraka. Na risiti zote ili kukokotoa kiasi halisi cha kodi hiyo.

Hata kama mnapinga mafanjkio haya na kuupindisha ukweli, JPM ni kidume na anafanya. Kazi kwa ajili ya watanzania wanyonge.

Viva JPM. VIVA 2020.
 
value that Tanzania has achieved is much higher than 190b , kueni nakini na hivi viji Lissu mchwara wanaopinga kila kitu JPM analofanya, kwenye hili nadhani hata Lissu angesema alilizungumzia Hilo bungeni ama angesema Wao kama Chadema ndio ulikuwa ushauri wao bungeni.
hahahahaha..na hapo mnajidanganya big time kana kwamba hamjui ACACIA wanaondoka by 2020...ACACIA walikuwa wana wa cool down tu..walikuwa wanapambana kuhusu reputational damage tu ..nothing

hahahah..Ujue wabongo hasa wa CCM akili maji sana
 
Hiyo hela usd300 imetolewa ili kuficha aibu kwa serikali....na ukitaka kujua Hilo angalia hizo hela zitapelekwa wapi....mnakumbuka za radar ziliendaga wapi? Fuatilia mtakuja kuniambia
 
Huu mchezo wazungu wametuvua nguo mchana kweupee muda unavyokwenda tunavyozid kulitafakar tutajua ni namna gani hawa jamaa wametuacha kwenye mataa jana hii kauli ilinitisha

makubaliano kutekelezwa mpaka Approval ya bodi ya London

nashangaa watu wanashangilia ni sawa na mtu kutaka kuazima gar kwa mtoto wakat baba mwenye nyumba hayupo atakwambia msubir baba arudi akirud bado anaweza kukupa au kukunyima inategemeana na huruma yake.
 
Mimi naomba kueleweshwa sijaelewa wanaposema wamekubali sheria yetu mpya hivyo tutapewa hisa ya 16% lakini pia tutagawana faida Kwa 50% kwa 50%.
 
Umendka vzur ila ni
Wapi wamesema hzo 700bn ni malipo ya dai la kodi alilopeleka TRA?
 
Mkuu ungeuliza watu wanaojua uzalishaji wa hii kitu ndo ukaja hapa. Makontena 250 kwa mwezi ni ya makinikia ya wapi?

Tatizo letu watz kila mmoja anajua. Umekaa na kuamua kufanya hesabu zako ili wasiojua uwapotoshe.

Sasa naamini maneno ya msigwa kuhusu kazi ya upinzani.....

Watz tungetumia sehemu ya muda wetu kutembelea hii migodi tukkaona kinachoendelea, ukifuata taratibu unarusiwa bila shida kuliko kuuaminisha umma mambo yasiyokuwepo.
 
Nakumbuka neno moja tu!!! "Professional rubbish" Muungu amemponya Tundu Antipas Mgwai Lissu ili ashuhudie alichokisema kinatimia.Kwa mtu mvivu wa kusoma na kuweka kumbukumbu ni ngumu kumuelewa sana Lissu ila kwa mtu msomaji basi utamwelewa na kumpenda. Lissu ni mpango wa mungu.
 
Back
Top Bottom