USANII WA WIZARA YA MIUNDO MBINU;TRL, ATCL zakwama kujadiliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

USANII WA WIZARA YA MIUNDO MBINU;TRL, ATCL zakwama kujadiliwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Jan 23, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,216
  Likes Received: 5,615
  Trophy Points: 280
  na Deogratius Temba


  KIKAO cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika jana Ikulu jijini Dar es Salaam, kimeikwamisha Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu kujadili utendaji hafifu wa Kampuni ya Reli (TRL) na Shirika la Ndege (ATCL).
  Jana asubuhi Waziri wa Miundombinu pamoja na Menejimenti ya TRL na ATCL walitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo, iliyokuwa ikiendelea na vikao vyake katika Ofisi Ndogo ya Bunge jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa taarifa na msimamo wa serikali juu ya mkataba wa kampuni hizo.
  Hatua ya kukwama huko ilitangazwa mbele ya waandishi wa habari jana na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mohamed Misanga baada ya wabunge kukusanyika ukumbini kwa ajili ya kupokea taarifa hizo.
  Misanga alisema jana asubuhi kamati ilipanga kukutana na waziri husika na viongozi wengine ili kutoa msimamo wa serikali juu ya mkataba wa kampuni hizo.
  “Tulipanga leo tupokee taarifa hizo mbili na kujua msimamo wa serikali, lakini nimepokea barua ya waziri iliyoandikwa na msaidizi wake akiiomba kamati ihairishe kikao hiki hadi atakapopata nafasi,” alisema Misanga.
  Barua hiyo yenye kumbukumbu namba WMI/Gen/2009 kwenda kwa mwenyekiti wa kamati na kusainiwa na msaidizi wa waziri, Alphonce Mwingira, ilisema Waziri Kawambwa atakuwa kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri kilichokuwa kikifanyika Ikulu.
  Kamati hiyo iliridhia maombi hayo na kudai kuwa itapokea taarifa hiyo mjini Dodoma wiki ijayo kwenye mkutano wa 17.
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Dr Kawambwa huyu sio yule aliyekuwa pale IPI enzi zile. Amebadilika bwana. Ndio siasa zinavyowabadilisha watu?
   
 3. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Kuna jambo hapa, ATC walisema wanawapa wachina na kama itakumbukwa wachina walipokuja hapa kutiliana saini walikuwa wanalalamika saana kuhusu ukiritimba wa viongozi wa serekali, tukasubiria kw ahamu tukajua watakabidhiwa shirika, hakikufanyika kitu muda si muda tunasikia serekali inatafuta mbia wa kuendesha ATC, mbona nyie watawala mnakuwa wasanii????
   
Loading...