Usanii wa serikali na uchakachuaji mitihani, kurudi f2. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usanii wa serikali na uchakachuaji mitihani, kurudi f2.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Paul Kijoka, Jan 16, 2012.

 1. Paul Kijoka

  Paul Kijoka JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Tumewahi kusema sana kuwa Serikali ya kisanii ni hatari katika
  kuendeleza mfumo wa elimu hapa nchi.

  Ni takribani miaka mitatu prof. Maghembe alisimama kwa mbwembwe na kulitangazia taifa kuwa
  mtihani wa f2 hautachuja wanafunzi tena. Akaendelea kuwa pia utakuwa ni bure kwa shule za serikali.

  Alisema kuwa kila mwanafunzi ana haki ya kumaliza f4.

  Huu haukuwa uchizi tu bali ilikuwa ni hakili ya kiprof. uchwara iliyochanganyika na uchu mambo yafuatayo:
  1. kuzuga wananchi ili washinde uchaguzi 2010
  2. kudhani kuwa mbinu hiyo ingeziokoa shule zao za kata ambazo zina utitiri wa matatizo zaidi ya 80%
  sasa kwanini wamerudisha mtihani huu kuwa na makali na kurudisha ada? sababu ni nyingi ila chache ni hizi:
  1. wameshindwa kulipa washihishaji wa mitihani ya kidato cha pili kwani malipo yamekaa kuwa 200/ kwa karatasi na wamekumbana na upinzani kutoka kwa wasahihishaji
  2. wameshashinda uchaguzi uliopita na wataondoa tena ikikaribia uchaguzi ujao
  3. shule zao zimeshindwa sana ( hii si sababu ya msingi)
  4. wanatafuta chanzo cha pesa kipya baadala ya kuishiwa
  Matokeo yake yatakuwa nini sasa?
  1. kuna uwezekano mkubwa shule za kata zikakosa wanafunzi wa kupanda kidato cha 3 na hivyo kuwahamishia shule jirani (tusubiri tuone)
  2. kuna uwezekano mwingine wa kutunga mtihani mwepesi ili wapitishe shule za kata
  Mhimu:

  1. serikali iwalipe wale waliofanya vibaya kidato cha 4 kwa kuwa imekiri kuwa kuondoka kwa kwa mtihani kumefelisha watu wengi
  2. Prof. Maghembe afukuzwe serikalini kwakuwa hafai na hana ubunifu wa kuisaidia serikali
  3. tuondoe ccm madarakani kwakuwa inachezea maisha ya watanzania kila idara
   
 2. Msafiri Kasian

  Msafiri Kasian JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Naona kuna ukweli hapo ulipo andika,maghembe ana mambo ya kisanii.
   
 3. L

  Lyahanda New Member

  #3
  Jan 27, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuhusu kufeli ka kwa wanafunzi sababu ni nyingi kama walivyoziainisha walio wengi, Ila serikali isijidanganye kuwa kuongeza idadi ya walimu tu mashulen ndio kutawafanya vijana wafaulu. Kwakweli ukweli ni kwamba walimu wengi wa shule za serikali hasa za sekondari wapo katika mgomo uliotangazwa mioyoni mwao pasipo posipo jamii kujua kwasabu ya maslahi duni wanayoyapata , yasiyoendana na mfumuko wa bei uliopo.
   
Loading...