Usanii wa CCM kuelekea 2010 waanza rasmi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usanii wa CCM kuelekea 2010 waanza rasmi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Sep 17, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,745
  Trophy Points: 280
  Date::9/16/2009Makamba amfuata Spika Sitta Urambo, ampigia magoti
  ASEMA HANA UGOMVI NAYE, ASEMA ALIKUWA MLEZI WA NDOA ZA WANAYE

  Na John Dotto, Tabora
  Mwananchi


  KATIKA kile kilichoelezwa kwamba, ni kujisafisha mbele ya Spika wa Bunge, Samuel Sitta, CCM imesema ipo pamoja naye katika kutekeleza majukumu yake kama Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Mkuu wa CCM, Yusufu Makamba; ikiwa ni siku chache baada ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuondoa utata uliotokana na maazimio ya Halmashauri Kuu ya chama hicho ulioonyesha kuwa wabunge wanaopiga kelele dhidi ya ufisadi, wanakichafua chama na serikali yake.

  Akizungumza na viongozi wa CCM wilaya ya Urambo kwenye mkutano wa ndani uliohudhuriwa na Spika Sitta, Makamba, alitumia muda mwingi kumsifia Sitta kwamba ni mtu muelewa, asiyetetereka na wala kuyumbishwa na mtu yeyote na kwamba anachokifanya ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho.

  Makamba aliwaambia wanaCCM hao kwamba, hana chuki na Sitta, kwani hata alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alimkaribisha katika ndoa za wanawe na akapewa nafasi ya kuzungumza kama baba mlezi, heshima ambayo alisema hataisahau katika maisha yake.

  Alisema wana CCM wanatakiwa kupuuza maneno ya watu wanaodai chama kina mgogoro na Spika, kwasababu hakuna kitu kama hicho na yote anayoyatekeleza kwenye Bunge ni kwa niaba ya chama chake.

  Hata hivyo, baada ya kikao cha NEC, Makamba alikuwa mstari wa mbele kudai kuwa kikao kile kina uwezo wa kumuhoji mbunge yoyote hata Sitta kama anakwenda tofauti na chama.

  Makamba alinukuliwa akisema NEC ni mama na akina Spika ni watoto hivyo ina mamlaka ya kuhoji mienendo yao.

  Mara baada ya kikao cha NEC, Sitta alifanya ziara mkoani Tabora na kulalamika kwamba, CCM makao makuu wamewakataza viongozi wa chama hicho mkoani kumpokea.

  Hatua ya Makamba kwenda Urambo kuhutubia na Sitta, inatafsiriwa kama njia ya kuweka mambo sawa na kufuta makovu ya huko nyuma baina yake na Spika.

  Kwa upande wake, Sitta alimshukuru Makamba kwa kutembelea jimboni kwake na mkoa wa Tabora kwa ujumla.

  Katika mkutano wa hadhara uliofanyika baada ya kikao cha ndani kumalizika, Makamba aliwahakikishia wananchi wa Urambo kwamba CCM kipo pamoja na mbunge wao Sitta, ndiyo maana wanatekeleza ahadi zote ikiwemo ujenzi wa barabara ya Urambo Kaliua mpaka Tabora Mjini.

  Akizungumzia suala la ufisadi, Makamba alisema kuwa wanaCCM wote kuanzia ngazi ya matawi wanapaswa kuungana na wabunge wanaopiga vita ufisadi, kwani vita dhidi ya rushwa ni ya wanaCCM wote.

  Alisema anakerwa na watu wanaosema CCM ni chama cha mafisadi kwani ufisadi wa mtu mmoja si wa CCM na akatoa mfano kuwa dhambi ya Mkatoliki mmoja si dhambi ya Askofu Kilaini wala kanisa lote.

  Makamba alimaliza ziara yake jana mkoani Tabora na juzi alipokuwa akizungumza na viongozi wa CCM wakiwemo makatibu wote wa wilaya za Tabora kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM mkoa, aliwalaumu viongozi hao kukaa kimya wakati wapinzani wanakishambulia chama hicho kwa kukipakazia maneno machafu.

  Aliwataka waamke na kukipigania chama na kuacha kukaa kimya na kusubiri makao makuu ama Makamba kujibu mashambulizi.

  Baada ya kikao cha Nec kilichofanyika Dodoma mwezi uliopita, Makamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chilligati kwa nyakati tofauti walisema CCM imeunda kamati ya watu watatu, inayoongozwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi kuwachunguza wabunge wenye tabia ya kuishambulia serikali nje ya vikao vya chama.

  Habari za ndani ya kikao hicho ambazo baadaye zilivuja kwa vyombo vya habari, zilieleza kuwa Nec ilimweka kitimoto Spika Sitta kwa madai kuwa anaruhusu mijadala inayokichafua chama na serikali, huku baadhi ya wajumbe wakishinikiza anyang'anywe kadi ya CCM kwa madai kuwa anawapa uhuru bungeni watu wanaoishambulia serikali kwa ufisadi.

  Hata hivyo, mwanzoni mwa wiki hii baada ya hotuba ya Rais, Chilligati alisema chama hicho hakina ugomvi wala uadui na wabunge wake wanaoongoza vita dhidi ya mafisadi nchini.

  Kabla ya hapo, Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita ambaye alisemekana kumwandama Spika Sitta katika kikao cha NEC na akamwita faru aliyejeruhiwa anayetakiwa kumalizwa kabla hajasababisha madhara zaidi, naye alibadili msimamo na kuwaunga mkono wapiganaji wa ufisadi pamoja na Spika Sitta kwamba, wanatekeleza ilani ya CCM, hivyo wanastahili kuungwa mkono. Mabadiliko haya ya siasa ndani ya chama hiki tawala na mfululizo wa matukio ya aina hiyo likiwemo la Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile ambaye amekaririwa katika vyombo vya habari akisema hana ugomvi na Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe, anayesemekana kuwa ni hasimu wake kisiasa.
   
 2. Ndanda to Lomwe

  Ndanda to Lomwe Member

  #2
  Sep 17, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uuuuuuwiiii,kweli sisi ni wadanganyika,hawa wana sisiemu wa tabora kwanini hawakumzomea huyu makamba?kwa kweli hainiingi akilini.

  Ni huyu huyu makamba alieamrisha ccm mkoa wasimpokee sitta alipotoka nec leo bila aibu anakwenda kujiosha.ningemuona mtu wa maana kama angemuomba sitta msamaha alafu ndo akaendeleza hizo sanaa zake baadae.
   
 3. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hakika huu ni usanii!
   
 4. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Naona hii bado ni part 1 ya hizo series zao za Comedy. Ngoja tusubiri part 2. Hivi Watanzania watadanganyika hadi lini?
   
 5. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu BaK

  Hii ndio kazi mahsusi aliyonayo Makamba ndani ya CCM. Kama unavyoona anaitekeleza kwa juhudi na umakini mkubwa...
   
 6. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Naaam kumekucha! Na burudani iendelee..
   
 7. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,668
  Likes Received: 21,901
  Trophy Points: 280
  Bado Chama chenye viongozi kama hawa watu wanakiruhusu kurudi madarakani kwa kura zao wanategemea kupata nini kutoka kwao? SIO RAHISI KUDANGANYA WATU WOTE SIKU ZOTE, Mwishowe utaumbuka tuu. Ndivyo inavyotokea sasa
   
 8. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #8
  Sep 17, 2009
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Politics is a game of lies, but Politicians are damn liers
   
 9. C

  CreativeThinker Member

  #9
  Sep 17, 2009
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM ikitaka kurudisha heshima yake (kama ipo/ilikuwepo) mbele ya jamii ya WaTz, lazima kiachane na hawa vikongwe wao. Waruhusu vijana wenye akili timamu na elimu ya kutosha ili kukiongoza chama. Hawa wazee hata siamini kama baadhi yao wamewahi kuingia hata form one, wanachotumia ni uzoefu tu wa uanachama wa muda mrefu na kufikiri ndo tiketi ya kuongoza chama hata nchi. Bahati mbaya kwa uelewa wao mdogo wanafikiri ni waTz wote wako sawa na wao. Mbaya zaidi ndo wanaotuchagulia mtu wa kugombea urais na hatimaye kuiongoza nchi.

  Wazee hawa wamechoka, kiasi kwamba hawakumbuki hata wamesema nini dakika chache zilizopita sembuse wiki moja? Chiligati ni mfano mwingine Bubu ataka kusema alitupa mifano miwili ya statement zake zinazokingana kuhusu mafisadi na CCM. Ukiangalia vizuri ni kuwa aidha hakujua alikuwa anasema nini au uwezo wake wakuchambua maneno, hoja na kufuatilia mjadala ni mdogo, kiasi ambacho hajui tofauti ya mjadala na maamuzi ya kikao husika ama yote mawili.

  Sisi vijana na hasa waandishi wa habari kwa nini mnapoitwa na mtu kumcover (kutoa plantform ya) maongezi yake hamumulizi au hata kumkumbushia statement yake ya nyuma kuhusu jambo husika? au ndo na nyie ni wale wale hamkumbuki mliandika nini kuhusu mtu fulani juu ya jambo husika? Mie sio mwandishi wa habari, pia sijui ethics zenu zikoje hasa kuhusu kuuliza maswali yanayoibua hoja iliyopita lakini yenye mwendelezo wake kwenye coverage na mtu huyo huyo. Naomba tusaidiane. Manake inahudhunisha kuona hata wandishi wa habari wameitwa leo na mtu fulani wanaandika habari hiyo, kisha baada ya siku moja au mbili mtu yule yule anawaita anasema tofauti juu ya jambo husika/kukanusha alichosema/kutuhumu waandishi kuwa mlimwekea maneno/hamkuelewa alichosema, na nyie mnaondoka mnaenda mnaandika tena upya bila hata kuuliza swali just for clarification.

  Humu JF kuna waandishi wa habari wengi hebu tuelezeni hii michezo ya kuigiza mnayoshiriki na kuyumbisha waTZ katika decission making, share yenu ni ipi/nini? Lazima muwe critic (professionally analyse and interpretate) hoja husika. Vinginevyo tutaendelea kuona comedy hizi na comedian hawa milele.

  Heshima Mbele wazee.
   
 10. C

  CreativeThinker Member

  #10
  Sep 17, 2009
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukitaka kuelewa nilichosema hapo juu hebu chukua mifano hii miwili iliyowekwa na Bubu ataka kusema kuhusu Chiligati:

  Kutoka Gazeti la MwanaHALISI la August 26, 2009  Quote:
  [​IMG]

  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati aliwaambia waandishi wa habari baada ya kikao cha NEC, "Tumesema inatosha. Hapa tulipofika tusiendelee mbele. Wanaoropoka ovyo ni walevi na tumeona kuna kundi dogo ambalo linajiona kama ni wateule wa kuzungumzia ufisadi."

  Kauli hii ya CCM ililenga wabunge jasiri ambao wamekuwa wakiikosoa serikali, miswada yake na kutaka watuhumiwa wa ufisadi kuchukuliwa hatua.  Kutoka Gazeti la Mwananchi la Sept 15, 2009


  Quote:
  [​IMG]

  Jana, Chiligati alikuwa ni mtu mwenye kuunga mkono kikundi hicho wakati Mwananchi ilipotaka maoni yake kuhusu wabunge hao ambao wanaonekana kukaidi maazimio ya Nec, huku wakitamba kuwa hakuna anayeweza kuwafunga mdomo.

  "CCM haina ugomvi na wabunge wake wala mtu yeyote anayejitoa mhanga kupinga ama kupambana na mafisadi," alisema Chiligati ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

  "Msimamo wa chama chetu ni kwamba rushwa ni adui wa haki, usichukue, kuomba wala kutoa rushwa, huo ndio wimbo wa kila mwana-CCM.

  "Hatuna ugomvi wala uadui na mtu yeyote anayepambana na rushwa, ufisadi, uporaji, wizi na ujambazi. Huo ndio msimamo wa CCM."

  Hapa nategemea kuona swali la mwandishi wa habari makini akiuliza kulikoni mzee tarehe 26/8 ulisema hivi na leo 15/9 unasema hivi (tarehe hizo mifano tu), msimamo wako ni upi? nini kina/kilikusukuma kusema hivi/vile? n.k . Ukitoka hapo unahabari makini ambayo italeta mapinduzi katika jamii, utakuwa umesaidia waTz kufanya maamuzi sasa katika nani anafaa kuwa kiongozi na kwanini.

  Haya ni mawazo yangu, I may be wrong and am standing to be educated.
   
 11. C

  CreativeThinker Member

  #11
  Sep 17, 2009
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukitaka kuelewa nilichosema hapo juu hebu chukua mifano hii miwili iliyowekwa na Bubu ataka kusema kuhusu Chiligati:

  Kutoka Gazeti la MwanaHALISI la August 26, 2009  Quote:
  [​IMG]

  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati aliwaambia waandishi wa habari baada ya kikao cha NEC, “Tumesema inatosha. Hapa tulipofika tusiendelee mbele. Wanaoropoka ovyo ni walevi na tumeona kuna kundi dogo ambalo linajiona kama ni wateule wa kuzungumzia ufisadi.”

  Kauli hii ya CCM ililenga wabunge jasiri ambao wamekuwa wakiikosoa serikali, miswada yake na kutaka watuhumiwa wa ufisadi kuchukuliwa hatua.  Kutoka Gazeti la Mwananchi la Sept 15, 2009


  Quote:
  [​IMG]

  Jana, Chiligati alikuwa ni mtu mwenye kuunga mkono kikundi hicho wakati Mwananchi ilipotaka maoni yake kuhusu wabunge hao ambao wanaonekana kukaidi maazimio ya Nec, huku wakitamba kuwa hakuna anayeweza kuwafunga mdomo.

  “CCM haina ugomvi na wabunge wake wala mtu yeyote anayejitoa mhanga kupinga ama kupambana na mafisadi,” alisema Chiligati ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

  “Msimamo wa chama chetu ni kwamba rushwa ni adui wa haki, usichukue, kuomba wala kutoa rushwa, huo ndio wimbo wa kila mwana-CCM.

  “Hatuna ugomvi wala uadui na mtu yeyote anayepambana na rushwa, ufisadi, uporaji, wizi na ujambazi. Huo ndio msimamo wa CCM.”

  Hapa nategemea kuona swali la mwandishi wa habari makini akiuliza kulikoni mzee tarehe 26/8 ulisema hivi na leo 15/9 unasema hivi (tarehe hizo mifano tu), msimamo wako ni upi? nini kina/kilikusukuma kusema hivi/vile? n.k . Ukitoka hapo unahabari makini ambayo italeta mapinduzi katika jamii, utakuwa umesaidia waTz kufanya maamuzi sasa katika nani anafaa kuwa kiongozi na kwanini.

  Haya ni mawazo yangu, I may be wrong and am standing to be educated.
   
 12. M

  Magarinza Senior Member

  #12
  Sep 17, 2009
  Joined: May 9, 2008
  Messages: 122
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Na bado na bado na bado. (..........)
  Na bado na bado na bado. (..........)

  Jambo ambalo ninauhakika nalo ni kwamba TZ bila CCM inawezekana.
  Hawa machifu/wafalme wanajiaminisha hakuna mtu nje ya CCM anaweza tawala nchi hii ndo mana wanafanya haya madudu.
  Chadema lazima tuwasaidie ndugu zetu na nchi yetu.
   
 13. M

  M-bongo JF-Expert Member

  #13
  Sep 17, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 338
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Taarifa nyingine si sahihi! hivi ninavyoandika makamba ndio kwanza kaanza kikao na watendaji wote wa CCM wa mkoa Tabora sio jana na kikao kina fanyika uwanja wa Ally Hassan mwinyi si ofisi ya CCM mkoa kama mwandishi alivyoandika kwa maana ya leo tarehe 17/09/09.
   
 14. M

  Mchili JF-Expert Member

  #14
  Sep 17, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  ngoja tuone akina Gugunita na Kingunge watasema nini nao. Walikua hawajamwelewa Kikwete yuko upande gani sasa wanahisi wameachwa - aibu tupu.

  Sita anatakiwa awakaushie na kuwachanilia mbali kisiasa.
   
 15. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #15
  Sep 17, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wacha tuone ngoma inavyoendelea...
   
 16. M

  Magezi JF-Expert Member

  #16
  Sep 17, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mimi nilivyo soma hiyo habari kwenye gazeti sikuamini. Kweli Makamba alivyokuwa anatamba kwamba amemnyoosha sitta, leo hii hana hata aibu anakwenda Urambo kuomba radhi?? Najua katumwa na JK sawa lakini wananchi kama wana akili ni kuitupiliambali CCM ktk uchaguzi ujao.

  Halafu usanii wa CCM ulivyo, hebu angalia Guninita nae eti anasema anawaunga mkono akina six na timu yake? Hebu angalia John Mwakipesile naye anansema anaomba wazee wawapatanishe yeye na Mwakyembe??

  Wote hawa ni kwamba JK kama mwenyekiti ameagiza kuwa na mapatano ndani ya chama haraka kabla ya kikao kijacho cha bunge. Lakini mimi wasiwasi wangu ni kama kweli wanayo yasema yanatoka rohoni au ni kuona waking'ang'ana na misimamo yao JK atawamwaga.
   
 17. M

  Magezi JF-Expert Member

  #17
  Sep 17, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Si kweli, kikao kilifanyika urambo wilayani na siyo Tabora hiyo jana na ushahidi tunao. Leo makamba ndo anazungumza na viongozi na wananchi mkoani Tabora mjini lakini ni kweli jana alikuwa urambo.

  Msianze kuleta ushabiki wa ki-chama, ukweli muuache uwe ukweli.
   
Loading...