Usanii na Uhuni wa CCM Butiama

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,048
CUF yailaani CCM

na Asha Bani na George Maziku
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimeeleza kushtushwa, kusikitishwa na kukatishwa tamaa na tamko la Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi la kukataa mapendekezo ya Kamati ya muafaka ya vyama hivyo viwili.

Mwelekeo huo wa CUF umebainishwa katika tamko rasmi la kwanza la chama hicho lililosomwa jijini Dar es Salaam jana mbele ya waandishi wa habari na Katibu Mkuu wa chama hicho kikuu cha upinzani visiwani, Seif Sharif Hamad.

Katika tamko hilo ambalo Tanzania Daima imelichapisha katika ukurasa wa nne wa gazeti hili, CUF imeuelezea uamuzi huo wa CCM kuwa ni usanii wa kisiasa na ambao chama hicho cha upinzani hakitakuwa tayari kushirikiana nao.

Akisoma tamko hilo, Maalim Seif alisema uamuzi uliofikiwa na CCM huko Butiama mbali ya kwenda kinyume na ahadi nyingi za matumaini zilizopata kutolewa na Rais Jakaya Kikwete siku zilizopita, zinaonyesha dhahiri dhamira ya chama hicho kurefusha muda wa mazungumzo ya kutafuta suluhu ya mpasuko kati yao hadi mwaka 2010 au kuyakataa mapendekezo yaliyotolewa.

“CCM imeamua kufanya usanii wa kisiasa kwa kutumia lugha ya mzunguko, ya ubabaishaji na ya upotoshaji, kwa lengo la kuendelea kurefusha muda hadi mwaka 2010 au kuyakataa makubaliano ambayo wajumbe wake wameshiriki kuyaandaa katika miezi 14 ya mazungumzo kati ya vyama vyetu viwili.

“Chama cha Wananchi (CUF), hakiko tayari kushirikiana na CCM kuwafanyia Watanzania usanii wa kisiasa. Huu si utaratibu wa CUF katika uendeshaji wa siasa; siasa si propaganda zilizopitwa na wakati, bali ni utumishi wa dhati na uliotukuka kwa umma, uliowaamini viongozi wake, kwa msingi huo CUF haitakubali kurejea katika mazungumzo kwa utaratibu wanaoutaka CCM,” alisema Maalim Seif wakati akisoma tamko hilo.

CUF katika tamko lake hilo iliitaka CCM kurejea nyuma na kuheshimu makubaliano waliyofikia katika mazungumzo yao, na kikahimiza haja ya utekelezaji wake kuanza mara moja.

Maalim Seif katika tamko hilo aliuelezea uamuzi wa CCM wa kutamka kwamba suala la muafaka linarejeshwa kwa wananchi kwa sababu ya kupigiwa kura ya maoni, unaonyesha mzaha katika kuendeleza amani ya nchi.

Alisema hoja hiyo ya wananchi kuamua hatima ya mpasuko wa kisiasa Zanzibar kwa kutumia kura ya maoni, haikuwa sehemu ya mambo waliyokubaliana katika kikao cha kamati ya pamoja cha mazungumzo yao yaliyochukua muda wa miezi 14.

Alieleza kushangazwa na madai kwamba hoja hiyo ya kutaka kura ya maoni iamue hatima ya suala la Zanzibar ilitolewa na kamati ya mazungumzo ya pamoja na si Halmashauri Kuu ya CCM, hatua aliyoielezea kuwa ni njama yenye ajenda moja tu aliyoielezea kuwa na nia ya ‘kuipiku CUF katika ubunifu wa kujenga’.

“Kitendo cha kamati ya CCM kuwasilisha kitu kipya nje ya makubaliano yaliyofikiwa ni upotoshaji mkubwa wenye lengo la kulifanyia usanii wa kisiasa suala kubwa kama hili linalogusa masilahi ya taifa na watu wake moja kwa moja”, alisema Maalim.

CUF katika tamko lake hilo ilisema pendekezo zima la kutaka kura ya maoni ifanyike limezongwa na vikwazo vingi vikiwamo kujua ni chombo gani kitakachoisimamia kura hiyo na orodha itakayotumika katika kuendesha zoezi hilo.

Chama hicho kilitoa dukuduku hilo kutokana na kuwapo kwa ukweli kwamba, hadi hivi sasa kumekuwa na mabishano kati ya vyama hivyo viwili kuhusu Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na Daftari la Kudumu la Wapigakura lililopo sasa.

“Hoja nyingine ni kwamba kura ya maoni hiyo itaendeshwa na chombo kipi na kwa utaratibu upi, hasa ikitiliwa maanani tayari CCM na CUF wamekubaliana kuwa, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na Daftari la Kudumu la Wapiga kura vina matatizo ya msingi ambayo yanahitaji kurekebishwa?” inasema CUF katika tamko lake hilo.

Kutokana na hali hiyo, CUF ilisema maamuzi hayo ya NEC yamesababisha wao wavunjwe moyo na kukatishwa tamaa mno na Rais Jakaya Kikwete ambaye aliahidi kuupatia suluhisho la kudumu mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar.

“CUF imevunjwa moyo sana na Mheshimiwa Jakaya Kikwete akiwa kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, imani tuliyokuwa nayo kwake kama kiongozi wa wananchi na ambayo tulibaki nayo hadi CCM inaelekea katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa, imetetereka sana.

“Kitendo cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM chini ya uenyekiti wake kukataa kupitisha makubaliano yaliyofikiwa na kamati ya mazungumzo ya CCM na CUF na badala yake kuja na hoja mpya za ajabu ajabu zenye lengo la “kuipiku CUF”, kisiasa kinamwonyesha Rais kikwete ama hakuwa mkweli na mwaminifu tokea mwanzo na kwamba alikuwa akifanya usanii wa kisiasa wakati alipotangaza kuwa anasononeshwa sana na mpasuko wa kisiasa Zanzibar au ni kiongozi dhaifu asiye na udhibiti wa chama anachokiongoza. Yote mawili hayampi sifa ya kiongozi ambaye nchi inamhitaji inapopita katika vipindi vigumu,” alisema Maalim Seif.

Katibu mkuu huyo aliendelea kusema, CUF imeshangazwa na kushindwa huko kwa Kikwete ambaye ndiye huyo huyo anayetajwa kuwa alifanikisha kufikiwa kwa suluhu ya kisiasa katika nchi jirani ya Kenya, kati ya vyama vya ODM na PNU.

“Inasikitisha zaidi kwa Rais Kikwete kuwatangazia Watanzania na ulimwengu kuwa, amefanikiwa kuwakutanisha Rais Mwai Kibaki na Mheshimiwa Raila Odinga wa Kenya na kufanikisha kufikiwa kwa makubaliano kati ya ODM na PNU nchini humo, lakini ameshindwa kulifanikisha hilo nchini mwake ndani ya chama anachokiongoza mwenyewe kati ya CCM na CUF,” alisema Maalim Seif.

Kutokana na hilo, CUF imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuingilia kati mgogoro huo kabla mambo hayajaharibika kama ilivyotokea katika nchi nyingine za Afrika.

Wakati huo huo wanasiasa na wasomi mbalimbali walioulizwa maoni yao juu ya mvutano wa CCM na CUF, wameunga mkono msimamo wa CUF, na kuwatahadharisha viongozi wa serikali na CCM kuwa wanachezea amani na utulivu wa taifa.

Akizungumza kwa njia ya simu, Mhadhiri Mwandamizi wa Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mwesiga Baregu, alisema uamuzi wa CCM wa kuingiza jambo jipya katika suala la muafaka kinyume na makubaliano kati yao na CUF, kuwa ni ufisadi wa kisiasa na kuonya kuwa hatua hiyo ni ya hatari kwa amani ya taifa.

“Huu ni ufisadi wa kisiasa. Hatua hii si nzuri kwa amani ya taifa letu, kwani ni kinyume na matumaini ya wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Hali hii itawafanya wananchi wapoteze imani kwa viongozi wao wa serikali na kuwalazimisha kujichukulia sheria mkononi. Suala hili likiachwa bila kupatiwa ufumbuzi linaweza kuifikisha nchi yetu ilipokuwa imefika Kenya”, alionya Profesa Baregu.

Naye Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, aliuelezea uamuzi huo wa CCM kuwa ni kielelezo cha wazi cha kupwaya kiuongozi kwa Rais Kikwete na chama hicho tawala.

“Uamuzi wa CCM kuhusu muafaka ni hatari kwa taifa na ni ishara ya kufilisika kiuongozi. CCM imejenga msingi mbaya. Ni ishara kuwa Rais Kikwete ameshindwa kukidhibiti chama chake. Taifa linaelekea pabaya. Tunahitaji uongozi,” alisema Zitto.
Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 28 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
CUF mmechoka hamna mwelekeo ndio mana hata matamko yenu mnayatoa yanachapishwa siku ya wajinga duniani.dhambi yenu ya ubaguzi hiyo inamiandama, mpaka mtakapokubali kuwa muafaka uhusishe vyama vyote vya siasa ndio itakuwa salama yenu vingenevyo mtaendelea kupigwa changa la macho mpaka mwisho.kama mnafikiri kuna mtu mwenye huruma nanyie mnajisumbua,hao wakimataifa wafadhili na mataifa makubwa hawanahaja nanyi,wanashindwa kumiambia wazi tu wanatumia diplomasia mana na wao hawamitaki ila wanashindwa kumifutilia mbali tu kwakuwa wanajua uwepo wenu zanzibar ni kutengeneza ngome ya magaidi.usitegemee marekani atakubali wazembe nyie mchukue kisiwa kile mzalishe ******** wanaosumbua kwakujilipua watu wakila maisha duniani.nyie itisheni mikutano yenu ,toeni matamko lakini ngoma imelala hiyo, tusubiri 2010 muibiwe tena mana mnajifanya machizi nyie kila uchaguzi mnaibiwa tu lakini ukiitishwa tena mnaenda.akili zenu matope nyie.mkiambiwa akili ni nywele msifikiri ni za kidevuni au za kwapa mkazifuga ziwe ndefu...ni nywele za kichwani.

na faki, kigusatundu-mchambawima, - 2.04.08 @ 03:20 | #4536

Kibanda waambie CUF tumechoka na matamko ya kila wakati, tuafurahi mkichukua hatua kali na ya kudumu, hizi hadithi wakati mwingine mnataka hela za CCM mkipewa mkae kimya.

CHUKENI HATUA, JUMUIYA YA KIMATAIFA HAITAKUJA WALA KUWASAIDIA MPAKA JAMABO FULANI LIFANYIKE, ANZISHENI MAANDAMANO MFULULIZO MUWE TAYARI KUFA, KAMA ALIVYOFANYA ODINGA, WEWE SEIF SAFARI HII SIYO UNAKIMBIA NJE YA NCHI. PIGANA HATA KAMA HAUNA SILAHA, MAJIMAJI MPAKA LEO TUNASOMA USHUJAA WAO HATA KAMA WALISHINDWA , DUNIA HII YA GLOBALIZATION WATU WATASHTUKA,KIKWETE HATA KAA KWA AMANI.

KUNA NCHI KIBAO AMBAYO SERIKALI ILIANGUKA KWA MAANDAMANO.

AU FANYENI PEMBA KUWA NCHI HURU ITANGAZENI KAMA WALIVYOFANYA CHECHINIA NA KWINGINEKO.

AMA SIVYO KWA HALI YA HAPA NCHINI MTATOA MATANGAZO MPAKA MWENDE KABURINI CCM HAWATASIKIA NG'O , WAKIITWA NA HIZO JUMUIYA ZA KIMATAIFA WANATOA MANENO MAZURI SANA NA KUTIA MOYO.MTABAKI HIVYO HIVYO NA UJINGA WENU.

CHUKUA HATUA SASA.

WALA SIJASOMA TAMKO LENU NAONA NIKUPOTEZA MUDA WANGU.

WEWE HAPO JUU MIMI SIYO MZANZIBAR LAKINI MAISHA YAO NAWAJUA, CCM NI MADIKTETA ZANZIBAR.

CUF NDIO WANANGUVU ZANZIBAR ANAYETAKA VYAMA VYOTE NI MJINGA KUNA VYAMA HAVINA HATA SERA WALA WANACHAMA KUMI.

UPINZANI WA CUF KWA CCM ZANZIBAR NDIO AINA YA UPINZANI AMBAO NI WORLDWIDE RECOGNIZED, MAREKANI TUNAZUNGUMZA DEMOCRATIC NA REPUBLICAN.

TANZANIA MTASEMA NANI NA NANI, KUNA VYAMA VINA MAJINA MPAKAA WAKE ZAO!!!

na imani, usa, - 2.04.08 @ 04:51 | #4537

Tumechoka na matamko chukueni hatua wajinga nyie wewe SEIF HUNA LOLOTE MWOGA TU, MTU WA CCM WEWE!!

na Lowelo - 2.04.08 @ 04:52 | #4538

Du kama kuna mafanikio ambayo CCM wameyapata katika kipindi chake cha uongozi ni kuweka rehani mawazo ya Watanzania walio wengi kama huyu mgosi mwenzangu mwenye jina la Kipemba. Tatizo la Zanzibar si la CUF kama mheshimiwa huyu anavyoliona. Ni tatizo la kutetea haki. Ikiwa majeshi ya Tanzania sasa yako Comoro kutetea haki ya Wangazija usiniambie kwamba damu yao ina thamani kuliko ya sisi raia wake wa Tanzania.
CCM ni madhalimu na kushabikia CCM ni kudumisha udhalimu nchini Tanzania. Leo twacheka kwa kuwa twaona ni ya Wapemba lakini juzi tu kilio kilikua kwa watu wa Kiteto. Hao kina Kolimba, Kighoma Malima, Gibons Mwaikambo, Moringe Sokoine, Abdallah Kassim Hanga,nk. hawakuwa Wapemba na wote wanasadikiwa kuathirika na ufisadi wa Viongozi wa CCM. Kama wananchi wa Tanzania kukicha wanakuwa masikini zaidi katika nchi iliokithiri kwa utajiri wa kila aina, basi ni dhahiri kwamba tatizo ni la uongozi. Kwa bahati mbaya uopngozi huu hautaki kuwapisha watu wenye uwezo waikomboe Tanzania. Wanafanya hivyo si kwa masilahi ya nchi bali kwa masilahi yao binafsi na hofu ya kuwajibishwa kwa madhambi yao. Lakini yafaa ukumbuke kwamba katika historia, siku zote udhalimu umeshindwa na uetezi wa HAKI. Na iwe miaka mia, lakini iko siku tu ufisadi wa CCM utafikia kikomo.

na Al Assad, Sungai Pusu, - 2.04.08 @ 04:53 | #4539

kwanza nawapa hongera cuf kwa utulivu kwa muda wote huo wanaopigwa kalenda ila km mimi tu mtu wa nje ya siasa nilijua hakuna lolote la mana litakalofanikiwa ktk muafaka itakua mtu km maalim seif na chama chake ambao naamini ni wakongwe wa siasa hili swala kweli linachukuliwa kisanii km ccm walijua mwishoe utakua ni wananchi kwa nn wasingefanya ivyo mwanzo kuliko kudanganya na kupotezea watu muda wao halafu wanakuja na usanii km huu,kikwete ni mtu wa masihala mwanzo mwisho,anachojua yeye ni kuchekacheka na wanawake zake anaowapa ukamishna na vyeo lukuki kila kukicha,ila inapofikia kukaa na vidume wenzake kusuluhisha mambo ya msingi anashindwa,juzi juzi hapa wakenya walipofanikisha mambo yao walikua wanasema haloo kikwete katusaidia sana,nikasema huko ni kuwanyima heshima wale waliokua pale toka mwanzo ila kikwete kaja maji ya jioni baada ya kuona mambo yatakua poa halafu anapewa sifa zote,sasa niliwaambia ya kua km kweli kikwete mtu wa mana mtaona km atafanikisha swala km hili tz na ameshindwa,narudia tena wkt wa theory umeisha sasa cuf wafanye practical ndio hao watu wa kimataifa watakuja ila hawawezi kuja hivihivi wkt ndio huu na tumeona nani alikua mnafiki sababu mnayo na watu wengi tutakua nyuma yenu kwa lolote lile.

na mstari wa mbele, calif/usa, - 2.04.08 @ 07:38 | #4542

mstari wa mbele calif/usa tuko pamoja kaka.

CUF FANYENI JAMBO MSIPOFANYA KAENI KIMYA.

na imani, usa, - 2.04.08 @ 07:57 | #4544

Tatizo kubwa la ccm sio kushirikiana na vyama vya upinzani jamani! CCM wanaogopa madhambi na dhuluma wanazotufanyia sisi Watanzania zitafichuka.Kwa sasa ccm inakimbia kivuli chake yenyewe hivyo nachoweza kuwashauri viongozi wa vyama vya upinzani kama ccm wasipotekeleza makubaliano yaliyofikiwa baina yake na CUF wasikubali tena kufanya uchaguzi wowote ule hadi katiba irekebishe na tume ya uchaguzi ivunjwe iunde nyingine maana hivyo ndivyo ccm inategemea.Kwa udhaifu unaooneshwa na vyama vya upinzani hakuna hata siku moja ccm itaheshimu Watanzania.Tume iliyofikia maamuzi juzi imetumia hela za walipa kodi alafu ccm kwa kukosa hayana huruma kwa watanzania kwa makusudi inavuruga kile walichokubaliana. Sasa hivi kilichopo ni kwa CUF kuungana na vyama vingine ili kuhakikisha mikakati yao inakuwa moja tu.Kama wasiposusia uchaguzi wowote hadi matakwa yao yapatiwe ufumbuzi wajue wanatwanga maji.
Kama viongozi wa ccm wangekuwa waadilifu basi hayo yote yasingekuwa na tatizo kwani lengo ni kujenga Taifa kwa kila chama kinachotaka madaraka.
Ukitaka kuja hili nalosema rejea ufisadi uliopo na jinsi ccm inapata kigugumizi kilishughulikia.
Mkisema mumlaumu Kikwete nadhani itakuwa kazi bure kwani yeye kama mwenyekiti wa ccm hana udhu wa kumkemea mjumbe yeyote ndani ya NEC ufisadi uliofanywa BOT unadaiwa kuihusisha ccm moja kwa moja na hilo tu tayari ni doa kwake.Cha msingi badala ya kumtafuta mchawi vyama vya upinzani wakubali kwanza ndivyo wachawi wa maendeleo ya kidemokrasia kwani wao kukubali kujiingiza ktk uchaguzi wowote ule wakati wakijua kuwa haki haitatendeka maana vyombo vya kusimamia chaguzi hizo ni vya ccm.
Tumeshuhudia chaguzi zote tangu mfumo huu uanze ccm inatumia tume ya uchaguzi kujinyakulia majimo hata yale ambayo wananchi wake walionyesha wazi wazi kutomkubali mgombea wa ccm. Mfano mzuri ni jimbo la ubungo KILICHOFANYIKA UFI NADHANI WENGI WALIJUA! Na wapinzani kwa kukubali huko kushiriki chaguzi ambazo wenyewe wanajua wazi haki haitotendeka ni kuwanyima haki watanzania kwa ujumla. KULALAMIKA TU KILA MARA BAADA YA UCHAGUZI NA MATOKEO KUTANGAZWA haisaidii kitu dawa ni KUGOMA KUSHIRIKI UCHAGUZI HADI KATIBA NA TUME YA UCHAGUZI VIREKEBISHWE! Pengine labda watuambie uchaguzi huo utaandaliwa na utasimamiwa na umoja wa
mataifa.

na kimalando, tz, - 2.04.08 @ 08:17 | #4547

Wewe mchangiaji wa kwanza na wa pili mnaudhi na kukera kweli kweli. Mmeandika upuuzi. Mungu awahurumie. Lugha ya matusi ni matokeo ya uvivu wa kufikiri na kuchuja hoja. Cuf tupo nanyi, anzisheni maandamano makubwa yatakomesha ubabaishaji

na Sapi kawawa, Tanganyika, - 2.04.08 @ 08:20 | #4548

Inasemekana Seif Sharifu Hamad alisoma na Kikwete chuo kikuu, mimi sijui, ni hadithi za mtaani.
Kama ni kweli basi inashangaza kwa muda wote huo anaomjua Kikwete hakuwahi kuijua rangi halisi ya mtu huyu asiye serious na kila anachofanya na kusema.
ALipoingia madarakani akaitaka Tanesco ishushe bei ya umeme, matokeo wote tunayajua.
Aliahidi maisha bora kwa kila mtanzania, sina haja ya kujadili hilo.
Rais anayecheza ngoma hadharani baada ya kumsindikiza rasi wa Marekani si makini huyo.
Rais anayewatoa hofu mafisadi kwenye NEC si wa kutumainiwa huyo.
Rais aliyewang'ang'ania Lowasa na Karamagi hadi kamati ya Mwakyembe ilipowalazimisha wajiuzulu hutegemei kitu kwake.
Rais anayeshindwa hadi leo kuwachukulia hatua Mwanyika na Hosea wakati kamati ya Bunge, iliyotumia fedha zetu imewaona kuwa na hatia, hupaswi kumuani.
Ilikuwaje Hamad na CUF wakashindwa kuona yote hayo?
Au na nyie mlitegemea peremende ya kuingizwa Serikalini mkafumbia macho mambo ya wazi hivyo?
Ndio maana hata Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni juzijuzi alitetea kitendo cha wanajeshi kutumwa Komoro bila idhini ya Bunge kwa matarajio angeingia kwenye serikali ya mseto?
Wote CUF na CCM ni mafisadi na majahili wa kisiasa.
Matamko yenu ni uchungu wa kunyimwa peremende ya kuwa kwenye serikali ya mseto.


na Danny - 2.04.08 @ 08:42 | #4551

Kamati ya muafaka ya CCM inakasoro


Nachukua fursa hii kutoa maoni yangu kuhusu kusua sua kwa upatikanaji wa muafaka visiwani Zanzibar. Mimi binafsi imani yangu muafaka huu haupatikani hata miaka 20 ijayo kama wajumbe wa kamati ya muafaka wa CCM kubadilishwa na kuingizwa wale wanaojulikana kama wahafidhina.hii itasaidia hata huo muafaka ukipatikana kweli utakua muafaka utaokubaliwa na wahafidhina hao.
sasa kumeibuka kufanyika kura ya maoni visiwani baada ya wahafidhina kupinga kwa nguvu zote kuhusu muafaka huo, naamini itakuja hata kura maono badala ya maoni na itakuja kura ya maongezi na pia itakuja kura ya malalamiko lakini ufumbuzi bado utazidi kuwa mgumu kama kamati iliopo kwa sasa ya CCM haitavunjwa na kuundwa upya chini ya wahafidhina kutoka Zanzibar. Kama utaangalia kamati iliopo hivi sasa kutoka ccm ni dhahiri ni kamati inajumuisha wajumbe kutoka bara na mmoja tu ndugu Ali ameir ndio Mzanzibar. Licha ya yeye kuwa Mzanzibar lakini pia kwa sasa ni kiongozi dhahiri asienguvu kisiasa jambo ni vigumu mambo yake yakakubaliwa na wahafidhina hao. Lakini kwa uapnde wa CUF wao ni dhahiri wajumbe wa kamati hiyo imeundwa na wazanziabr na wanaojua hasa Siasa za Zanzibar kinyume na CCM. Jee Cuf hawakushtuka hali hii kamati ya muafaka inayohusu Zanzibar kuuundwa zaidi na watu wa ccm kutoka bara walitegemea nini?maalim seif hakupima alam aza nyakati? Hazijui siasa za Zanzibar? Sio msomi aliehitimu chuo kikuu? Sio mwanasaisa yule tunaemjua? Sio black killer kama anavyojiita au sio mwanamapinduzi wa kweli ? amezaliwa upya? au tuseme ndio yule seif tunaepata minongono kwamba tayari amenunuliwa na CCM
Ni wazi maalim seif na tume yake kufahamu kasoro hii vyenginevyo porojo kutoka CCM itaendelea hata miaka 20 ijayo huku ufumbuzi wa mpasuko wa kisiasa Zanzibar kuwa mgumu
Ni mimi
Wanafunzi wa elimu ya juu
Dar Es Salaamna kk, tz, - 2.04.08 @ 08:58 | #4555

sapi kawawa usingizi haujakutoka bado nini, mbona maoni yako na mtu wa pili yanafanana kabisa?? mtu wa kwanza ndo kaharibu

na msuluhishi, a, - 2.04.08 @ 09:13 | #4558

Danny tuko pamoja, kanyaga twende wajinga waliwao.SEIF HANA LOLOTE.

na imani - 2.04.08 @ 09:16 | #4559

SIF MTU WA CCM, HANA LOLOTE,LIANZISHE HUKO,STORI HIZI ZIPO TANGU 1995,ULIKIMBIA WEWE WAKATI WATU WAKO WANA KUFA ,SASA TAMKO LAKO HILI NDIO UMESEMA NINI?? CHUKUA HATUA ,JUMUIYA ZA KIMATAIFA ZITAKUJA ZENYEWE,LIANZISHENI ANDAMANENI,TANGAZENI PEMBA KUWA HURU,HATA MKIFA NDIO UHURU UNAVYOPATIKNA HAMNA UHURU NYIE WAPEMBA.STORI HIZI TUMEZICHOKANAUNGA MKONO MAWAZO YA MTU WA PILI,

na KANYAU - 2.04.08 @ 09:29 | #4560

CUF ni chama cha watu wabinafsi,hivi kwa nini wanataka mawazo yao na ya CCM ndio yatuamulie mamabo ambayo hayapo hata kwenye katiba? nilitegemea wangekubaliana kuwaa mambo haya yapelekwe kwa raia ndio wananchi waamue,hiyo ndio demokrasi,sio Seif na Makamba wanakubaliana then tupindishe hata katiba. Nilikuwa nawatetea sana CUF lakini kwa hili naungana na watu waliokuwa wanasema CUF ni chama cha kisultani,maamuzi ya Seif ndio msimamo wa chama.

na Wether u like or not!, TZ, - 2.04.08 @ 09:46 | #4567

naomba usitumie jina la mh.kwa matusi fikiri kabla ya kutype maana utaishia kutype jirekebishe wewe mchangiaji fikiri maisha achana na siasa 'its a game'kuwa makini sana ktk maneno yako.

na busara, tanzania, - 2.04.08 @ 10:01 | #4579

CUF MUWE WAPOLE KUTOKANA NA UOGA WENU. TOKA 1995 MNALALAMIKIA KUIBIWA KURA!! HUKU SEIF AKIPETA KWA RUZUKU NA MARUPURUPU KEDEKEDE TOKA CCM, BADO TU HAMSHTUKI? KAMWE HATA KAMA NI WEWE HUWEZI KUKUBALI KUUNDA SERIKALI YA MSETO BAADA YA MIAKA MITATU YA UTULIVU KUPITA. NAISHANGAA TANZANIA YA LEO!! ETI KILA KIONGOZI ANAPOTOKA MADARAKANI HUACHA KISIMA CHAKE CHA MAFUTA PALE SERIKALINI NDO MAANA WALENGWA WA UFISADI WAMESAMEHEWA KULE BUTIAMA!! JK USINIPE MTIHANI MGUMU WA MAAMUZI BADO NAKUPENDA. JITAHIDI NCHI IWE NA HESHIMA.

na RichmondEPA, Tanzaniabara, - 2.04.08 @ 10:08 | #4583

MAALIMU NA WENZAKE WALIKUWA KIMYA WAKATI WOTE WA VIKAO KWA SABABU YA NJAA ZAO HIVYO COMMISSION KIDOGO WALIYOKUWA WANAPATA IKAWAFANYA WAKAE KIMYA SAA VIKAO VYA USULUHISHI VIMEISHA NA CCM KAONYESHA WAZI KUWA HATAKI KUWAONA CUF KWENYE SERIKALI ETI NDIO MR MIDEVU ANASHTUKA NA KUTOA TAMKO TOOOO LATE BROTHER HAKUNA CHA KUFANYA SASA NI KUSUBIRI 2010 MUINGIE TENA KWENYE UCHAGUZI KAMA KAWAIDA YENU MACHO JUU MUIBIWE KURA TENA MUANZE KUOMBA VIKAO VYA USULUHISHI NA KUHAKIKISHIA KUWA HAKUNA MZANZIBAR WALA MTANZANIA ALIYETAYARI KUANDAMANA WALA KUGOMA KWA AJILI YA CUF HAKUNA NA MIMI NAMBA MOJA CUF NI WAJINGA WANAWASHA MOTO HALAFU WAO WANAENDA ULAYA TERM HII HAMPATI MTU MTAANDAMANA WENYEWE NA WAKE ZENU

na Richard, Tanzania, - 2.04.08 @ 10:25 | #4587

Toka mwanzo kwa sisi tunaojua kusoma alama za nyakati tuliyaona haya haiwezekani kwa watu wanaojitangaza kuwa wanakerwa na MPASUKO wa ZANZIBAR wakayachulia mambo ki mzahamzaha kiasi hiki na tunashindwa kujua wanaishi DUNIA gani leo kila palipotokea mauaji ni Viongozi kuzarau maoni ya watu sasa wewe KIKWETE na watu wako mjue leo Watu hawaishi kwa PROPAGANDA za kina kingunge ni kwa kauli thabiti na zilizo pimwa na watu makini wenye kuyaona mambo kwa mapana yake MUNGU IBARIKI TANZANIA IONDOKANE NA VIONGOZI LEGELEGE WACHOVU WA MAAMUZI MAKINI

na kiondo, tz, - 2.04.08 @ 10:31 | #4590

Nawashukuru Tanzania Daima kwa kutupa nafasi hii ya kutoa maini kwa njia hii. Lakini nawaomba mtafute namna ya kudhibiti kama mtaweza wasomaji wasiwe wanatumia lugha chafu. Naona maoni kadhaa yaliyotolewa kwa habari hii ya tamko la CUF yamejaa jazba na hata matusi, jambo ambalo tusingependa kulisoma sisi wasomaji wa maoni haya. Tunafungua mtandao kwa matarajio ya kusoma hoja, na inatuuma tunapokuta badala ya kusoma hoja tunasoma matusi.

Nashukuru.

na Bernard Mukasa, Sumbawanga, - 2.04.08 @ 10:31 | #4591

HAPA WATU TUNATAKIWA KUTOA MAONI YETU NA TUNATAKIWA KUJUA KUWA HAPA NDIPO TUNAPO PIMWA. SIO SEHEMU YA KUTOA MATUSI NA LUGHA MBAYA KAMA HUNA CHA KUSEMA KAA KIMYA WWAACHE WENZAKO WASEME

na MKATAMBUGA, DAR, - 2.04.08 @ 10:32 | #4593

CCM wanafanya mchezo wa kuigiza kama ni kura ya maoni wananchi walishaamua walipopiga kura na matokeo kuwa hayakupishana sana kati ya vyama hivyo viwili - lilohitajika ni viongozi makini kutafsiri maana ya kura hizo na kutunga katiba kutokana na matokeo hayo - watu wanaoitakia mema Tanzania walishasema serikali ya Umoja wa kitaifa ndio suluhsho sasa wao wanaitakia nini nchi hii.

Ushauri kwa CUF na wao waitishe kura ya maoni ya kuwauliza Wapemba wanataka kuwamo kaika serikali ya Znz au wanataka wajigawe? matokeo yatajulikana na kama CCM ni wakuheshimu maoni ya wananchi watayaheshimu.

na Zakaria, Kigoma, - 2.04.08 @ 10:45 | #4599

CUF haina sera zaidi ya kutaka kuigawa
Nchi.Wananchi angalieni Jaja ya CCM ni
kwamba,ili msahau swala la Ufisadi ambalo ni nyeti kwa Uchumi na Ustawi wa
Nchi yetu inawaletea huu Upuuzi wa Mwafaka.WATANZANIA NI VEMA KUDHALAU HILI LA MUAFAKA tunataka Mutakasbali wa
Ufisadi unatufanya tuwe MASKINI ndani ya Nchi Tajiri.

na Komba Kasoma, Germany, - 2.04.08 @ 08:15 | #4606

kiKWete full msanII NANi AlIkuwa HajuHI?mtabaki kusema anazungukwa kUmBe TWAZUNGUKWA SIE.UDumu Rais bOya wa kuKenua

na kiMune - 2.04.08 @ 08:32 | #4610

Mazungumzo ya muafaka yameshakuwa ajira ya watu.
CCM na CUF wote wanapenda yaendelee milele. Muafaka ni idara ya serikali- hivyo mazungumzo haya hayatakuwa na mwisho. Ni, cost centre ya serikali.
Kwa hali ilivyo, hakuna makubaliano ambayo yatafikiwa kwa style hii ya mazungumzo. Na, hakuna mtu anayetaka yafikiwe kwa sababu ni mazungumzo haya ni ajira ya watu fulani.


na john, arusha, - 2.04.08 @ 08:32 | #4611

Tatizo la siasa za Tanzania ni ubabaishaji na njaa:
Hivi tangu mwaka 1995 kumeshakuwepo na mazungumzo ya muafaka mara ngapi?? Na ni mara ngapi wameshasaini makubaliano?
Ni kitu gani kilifanya hayo makubaliano yaliyosainiwa yavunjwe kama si njaa. Watu wote wanaoshiriki katika mazungumzo haya toka CUF na CCM ni wahujumu uchumi- wafunguliwe mashtaka. Wanawafanya watanzania watoto wadogo ambao hawana uwezo wa kufikiri.

Makamba anasema shida ni " Huyu Seif kwenda kutangaza kwa wananchi matokeo ya mazungumzo kabla hawajakubaliana" Hivi huyu mzee ana akili kweli? kwani wananchi wakitangaziwa kuna shida gani?

na eva, mwanza, - 2.04.08 @ 08:46 | #4616

kwa jinsi walivyoamua ccm,kwangu mimi binafsi naona wako sahihi.hao viongozi wa CUF wakae chini na wafikilie kwa undani zaidi siyo kufikilia kwa juu juu,na kutoa uamuzi wa kusema wameonewa.

na kapande Noni, Bunda, - 2.04.08 @ 09:21 | #4622

Naomba ukiingia humu utoe mawazo yako sio kulaumu lugha za wenzio waliotoa mawazo...usilazimishe watu wote kufikiri utakavyo wewe.sisi wote humu sio CUF tunaofikiriwa na kuamuliwa mambo na mtu mmoja ambaye akisema yeye ndio waCUF wote wanafuata.humu ni free mawazo na wala hulazimishwi kusoma hoja za wenzio,soma habari kuu toa maoni yako tambaa.sio lazima usome maoni ya wengine kama unajua unamtazamo wa kikafukafu.
kwakifupi sasa CUF wameingia pale CCM walipokuwa wanapataka.walijua tu kuwa kwa ufinyu wa kufikiri wa CUF na uroho wakuingia ktk mseto, kitakachofuata baada ya tamko la CCM ni wao kujitoa.hilo ndio lililokuwa linatakiwa na CCM kwakuwa kwakujitoa kwenu sasa siku zinazidi kusogea na mtalijua jiji 2010 tena mtakapojipendekeza uchaguzini ambako kila siku mdai mnaibiwa sijui hamna macho?na kwanini mnashiriki tena kama wa jana mliibiwa?sheria zilizokuibia jana zimebadilishwa kiasi gani hadi leo upate hamu tena ya kushiriki uchaguzii?jibu ni uroho wa madaraka na kufikiri leo tutashinda.hamtakaa mshinde nyie kwa kura hata mkipewa muhesabu nyie wao watangaze tu. mana hamna akili.hakuna mtu kutoka nje atamisaidia mana nyie mnajulikana kwa agenda za siri kisiwani humo.CUF ni mazalio mazuri ya magaidi kwahiyo hakuna watu wa kimataifa watakaomisapoti labda waarabu ambao hawana akili na ushawishi wowote katika dunia hii zaidi ya kutumiwa kama sehemu ya kujaribia siraha na kuibiwa mafuta.
CUF mgomee hivyohivyo kuendelea na mazungumzo mana lengo la CCM linatimia.mjiulize mlivyogomea kuingia kwenye baraza la wawakirishi miaka ya nyuma kilimisaidia nini?bado kuna mianya mingi tu kwa CCM kuchelewesha muafaka hata kama mtakubali kura ya maoni mana nyie mnaangalia vyeo na ubinafsi wenu bila kujua kuwa wenzenu wanakuja full nondo.hivi hukujistukia muafaka unajadili na watu wa bara na sio wazanzibar wenzio?nyie kweli mmechelewa.unategemea wabara wakusaidie nini?inatuhusu nini sisi?mmelianzisha wenyewe mtalimaliza wenyewe hakuna mbara atashughulikana watu ambao badala ya kuhangaikia maendeleo kazi kuhangaikia siasa.nyie mnashindwa kutumia akili kanchi hata dar kubwa lakini kanamishinda kukaletea mandeleo kazi misiasa ya chuki tu.kwanza sijui kwanini wanakazania muungano.bora mtupiliwe mbali mmalizane wenyewe huko.

na nukita, dar, - 2.04.08 @ 09:55 | #4630

Wahenga walisema "kinyosi hajinyoi". Hayo ndiyo ya JK. Kama tulidanganyika kuwa tumepata raisi shupavu tumeula wa chuya. Jambo kama hili lingeangukia mikononi mwa Mwalimu basi hao wahafidhina ambao JK anawagwaya wasingeyumbisha mambo haya.Ni maamuzi ya kikomavu yanahitajika kutunza amani hii ambayo CCM inaiweka rehani.

Kwa kweli inachukiza mwenendo mzima wa nchi inavyoendeshwa kiholela ili mradi tu waanaridhishana wenyewe.Ufasidi juu ya ufisadi hakuna hatua za dhati kukabili mauzauza hayo. Wa TZ. kwa usukule wetu tumekwisha tungojee mwisho wa dunia. Alamsik.

na Kipanga Ngusii, Dsm Tanzania, - 2.04.08 @ 10:07 | #4634
 
Nafikiri kama Kikwete Raisi wa Tanzania basi aitishe Uchaguzi wa haki na huru huko Zanzibar ili kukata mzizi wa fitna ndani ya mwaka huu.
Aitishe kama raisi wa Tanzania na sio Mwanachama au Mwenyekiti wa CCM.Ijulikane kuwa amri inatoka kwa Raisi wa Tanzania.iwe hakuna cha muawafaka wala maoni ,maana wakianza na hili la maoni basi ajue likimalizika tu litazuka la kura ya maoni ya Muungano ,mnautaka au hawautaki na hili litakuwa halina mjadala.
 
Nafikiri kama Kikwete Raisi wa Tanzania basi aitishe Uchaguzi wa haki na huru huko Zanzibar ili kukata mzizi wa fitna ndani ya mwaka huu.
Aitishe kama raisi wa Tanzania na sio Mwanachama au Mwenyekiti wa CCM.Ijulikane kuwa amri inatoka kwa Raisi wa Tanzania.iwe hakuna cha muawafaka wala maoni ,maana wakianza na hili la maoni basi ajue likimalizika tu litazuka la kura ya maoni ya Muungano ,mnautaka au hawautaki na hili litakuwa halina mjadala.

Katiba inaruhusu?
 
Back
Top Bottom