Usanii JWTZ: waathirika wa mabomu ya gongolamboto bado wapo kwenye mahema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usanii JWTZ: waathirika wa mabomu ya gongolamboto bado wapo kwenye mahema

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lukolo, Aug 6, 2011.

 1. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Inasikitisha, inakera, inaudhi na inaboa kweli kweli pale unapoona kwamba tangu mwezi wa pili hadi leo watanzania wenzetu walioathirika kwa mabomu huko gongo la mboto bado wanakaa kwenye mahema. Hawa watu hawakuingia mkataba na JWTZ kwamba ifanyie majaribio ya mabomu yake kwao, ni kiherehere cha serikali ya Kikwete na jeshi lake kuamua kuwashambulia wananchi wasio na hatia, sasa iweje watu hawa waendelee kutaabika kwenye mahema na mvua hizi zinazoendelea Dar? Jamani kama kuna asiyejua namna ambavyo hawa watu wanataabika, ajaribu japo kupita maeneo ya Majohe, kitunda, Moshi bar na maeneo ya jirani ajionee jinsi watanzania wenzetu wanavyotaabika na familia kwa kuishi kwenye mahema ambayo mengi yake yameoza na yanavuja.

  Juzi nimepita mahali nikaona mama anavyohangaika na watoto kutokana na maji kuingia ndani ya hema, nikasikia uchungu sana. Huyu mtu alikuwa na nyumba yake na maisha yake leo hii anageuka kuwa mtumwa na ombaomba kwa kuwa tu jeshi lilikosa mahali pa kujaribishia mabomu yake. Sitaona shida kuingia msituni kupambana na hii serikali ya kibazazi iwapo nitatakiwa kufanya hivyo. I have nothing to loose if I die. Sioni faida ya mimi kuendelea kuishi wakati watanzania wengine wakiendelea kulia na kuomboleza kutokana na uhuni wa serikali hii ya kiuaji.
   
 2. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Tulishaambiwa kuwa Tukiwa na Serikalia ya Fisadi Papa Kikwete ni Janga la Taifa sasa tutegeme nini? ni Kweli Kikwete ni Janga la Taifa
   
 3. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #3
  Aug 6, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Nimeamini, kweli Kikwete ni Janga la Kitaifa (JK). Hajali kabisa maisha ya watanzania huyu bwana, that is why hata pale wanajeshi walipoua raia wasio na hatia huko Mbagala na Gongo la mboto, aliishia kuwapa pole waliokufa bila kuchukua hatua yoyote ya kuwawajibisha wahusika. Ni hatari sana kwa nchi kuongozwa na viongozi wa aina ya Kikwete.
   
 4. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Madhara ya kujagua Bogus ndio hao sasa
   
Loading...