Usanii juu ya usanii; JK kukutana na vyama vyote

wamegundua kuwa cdm wana hoja ya msingi na kuna uwezekano wakashinda sasa hili isionekana kuwa mabadiliko yametokana na influence ya cdm badala yake wanataka michango ya vyama vingine ambayo hatutegemei kuwa na mpya zaidi ya kile walichokisema bungeni ili baadaye waseme ilikuwa mawazo ya vyama vyote.

Magamba wanataka wamtumie mke wao cuf ili akavuruge mazungumzo ndiyo maana wanataka vyama vingine vishirikishwe. Huu ni ujanja. Ni vizuri cdm wawe na msimamo kwamba wao kama cdm wameomba kukutana na raisi hawajaomba kukutanishwa na vyama vingine. Kwanza kuna chama kingine cha upinzani zaidi ya cdm?? Hivyo vinavyosemwa ni vya upinzani ni vya kitapeli tu na vimepandikizwa na hao hao magamba. cdm wasikubali ujinga huo
 
Hii ya CCM ni sawa na kumuona jamaa anaelekea Ubungo ukamfuata wakati wewe ulikuwa huna mpango wa kwenda huko. Chadema ina sababu zake wanapinga mswada kusainiwa sasa CCM au CUF watakwenda na hoja gani, kama hoja yao ni kupinga sawa waunganishe hoja waende pamoja lakini kama wana hoja tofauti na Chadema waombe siku nyingine wakutane na rais hawakatazwi. Hii ni sawa na fujo za kisiasa, halafu toka lini CCM akawa msemaji wa vyama vingine?
 
ccm na tasisi zake zinakurupuka hawajui wanachotaka, cdm wameshaainisha nini wanakwenda kumwereza rais.
Hii inch ni imefikia hapa sababu watu wanopomaanisha ccm wanafanya mzahaa nasema itawaghalimu we acha wajaribu kuchezea huo mchakato nasema hasirani hawataeleweka.

Ikiwa wlipitisha mswada kwa maelekezo sasa wanataka tena kuharibu mchakato inje ya bunge? huku hatukubari.

Najua cdm inawatu makini wenye kufanya maamuzi ya hekima na kuwaacha ccm bila kujua la kufanya.hata katika hili sina wasiwasi.
Magamba wala wasijidanganye kuwa wanaweza kuchakachua nia ya cdm.
kama walivyoshangaa msimamo wa kuwafukuza madiwani arusha, hata hili hawakulijua.

cdm ina Mjembe ya ukweli ccm wana magamba ya ukweli.
 
Unajua bunge letu linanishangaza sana na ushabiki wa vyama. Nakumbuka Chadema waliposhinda uchaguzi na kuwa chama rasmi cha Upinzani waligeuza sheria za bunge papo kwa hapo kwa kupiga kura ati kamati za Upinzani zihusishe vyama vyote, kama kwamba siasa zetu zinashindana vyama na sio itikadi na sera. Zikapigwa kura haraka haraka za kubadilisha kipengele hicho ili mradi wawakomeshe Chadema kwa kutoshirikiana na CUF au NCCR - Mageuzi..

Kwa hiyo sintoshangaa kuona vyama vyote vikialikwa kuupinga muswada ikiwa kweli ni wapinzani au pengine kila upande uwakilishe mawazo yake kwa nini wanapinga..Kama wataalikwa wote mimi ningependa sana kuona mjadala huu ukisimamiwa na rais mwenyewe kwenye luninga (TV), yaani tuwasikie hao wabunge wakipinga ama kuunga mkono kwa hoja ambazo ni pinzani na za hao wajumbe wa Chadema...Au kukutana na rais nako kuna Posho za kikao?

Inasikitisha sana kuona hata nafasi ya mjumbe kuwakilisha mawazo ya kupinga muswada vyama vinataka kugombania halafu hili sio swala la CCM hata kidogo.. wao hawapingi muswada na ushahidi wao upo ktk muswada wenyewe kinachowaweka roho juu kipi?

Hao wabunge wa vyama vingine wanaopendekezwa kushirikishwa katika mazungumzo watakuwa na hoja gani mpya zaidi ya ile walioitoa kule bungeni na kuwezesha kupitishwa kwa muswada wenyewe?? Hivyo vyama vingine vinavyoitwa vya upinzani viko kwa ajili ya kupinzana na cdm na ndiyo maana waliridhia kukaa ndani ya bunge na kupitisha huo muswada. Sasa wakishirikishwa katika mazungumzo ya rais na cdm watakuwa na jipya gani zaidi ya kuwapinga cdm?? wengine wana na ndoa kabisa na magamba nao eti washirikishwe. Hata hao magamba wanakaa na kuchekacheka tu utafikiri ni mazuzu.

Huwezi kuelewa wao wanauchukuliaje huu muswada wa kutunga katiba, katiba ambayo inawahusu hata wao wenyewe, watoto wao, wajukuu na vitukuu lakini wanashabikia mambo ambayo wanajua kabisa yatakuja kuwaumiza wao wenyewe na koo zao.

Hawaelewi kwamba huu mchakato ukikosewa tu katika hatua za mwanzo za uundaji wa katiba maana yake ni kwamba hata katiba yenyewe itakuwa mbovu na huwezi kutegemea kuja kuuondoa kwa kura ya maoni kwa sababu kwa vyovyote vile matokeo ya kura ya maoni yatachakachuliwa na magamba kama walivyozoea kwa kuwatumia usalama wa taifa na polisi.

Cha ajabu unaona wale wale wanaoumizwa kwa kununua sukari kilo shs zaidi ya elfu mbili, mafuta ya taa bei ya kuruka isiyo na sababu eti kwa sababu ya kulinganisha bei na petrol ili wafanyabiashara wasichakachue petrol, sababu za kipumbavu tu za kumuumiza mtu wa hali ya chini lakini ndiyo hao hao wanaoshabikia upumbavu huu wa magamba kuchakachua mchakato wa kuandikwa katiba mpya. Watanzania sio bure kuna kasoro mahali fulani sijui nani katulaani.
 
Kwa mujibu wa TBC1; Nape ametoa taarifa kuwa CCM imemwomba JK akutane na vyama vyote vya siasa vyenye uwakilishi Bungeni.

Red Quote: Ni wazi CCM wanawajua washirika wao na wangependa itambulike hivyo rasmi!

Lakini nina swali dogo, Kwani hao CCM wametumia vigezo gani kufikia uamuzi huo wa kutaka vyama vilivyo na wabunge ndio vishiriki? Napenda kujua.
Kwa nini isiwe, kwa mfano, vyama vyote vya siasa vilivyosajiliwa?


 
Sikupenda niliposikia kwa mara ya kwanza kuwa cdm wanaomba kukutana na raisi. Kwa nini?

Moja: hiyo pekee imetoa fursa adhimu kwa ccm na raisi kwa msingi huo kuendelea kuuhodhi na kuudhibiti mchakato wa kuelekea kupata katiba mpya.

Mbili: imewapa ma-pro status quo fursa ya kumanipulate mchakato wa katiba kwa pace na style watakayotaka.

Tatu: hili litatumika kama turufu ya ma pro status quo kuwanyamazisha political forces zingine (mbali ya vyama vya siasa) ambao hawajaridhishwa na namna mchakato wa kuelekea kupata katiba mpya unavyopelekwa. Hawatakua na namna nyingine ya kuonesha kutorishwa na mchakato kwa kisingizio cha jamani mlango wa majadiliano bado upo wazi, si mmeona raisi yupo tayari kujadiliana juu ya hili kama alivyoongea na cdm? Nahisi hii turufu ndio iliyotumika kuwazima jukwaa la katiba kusitisha maandamano yao ya tarehe 26 november.

Nne: kuomba kukutana na raisi kunathibitisha nguvu (kubwa) ya raisi ile ile ambayo wao wanaipinga katika mchakato wa kuelekea kupata katiba mpya. Sasa kama wako tayari kukutana na raisi katika hatua hii wajiandae tena kukutana na raisi kwa mara nyingine pale kamati ya katiba itakayoundwa na raisi itakapomaliza kazi yake na ikatokea draft ya katiba kutowaridhisha cdm.
 
Nape has a point in his suggestion inthat the process of constitution composition must be done under consideration of equal representation. Chadema should not attempt to appropriate the president's move to revive the constitution and assume for themselves but rather should allow for other groups have their contributions listened. We should not forget that Tanzania observes rule of law with one of provisions requiring that everyone has the right to air their opinions provided they do not contravene the law itself.

Wrong! Since this meeting was not proposed by the president, but rather by CHADEMA, then it is natural that the agenda will be set by CHADEMA; so what will the other parties bring to the table if not a deliberate move to disrupt CHADEMA's agenda.
 
Sijakuelewa..naomba fafanue kidogo. CDM wameshinda uchaguzi upi? Unajcichanganya zaidi unaposema na wakafanikiwa kuunda kambi ya upinzani.

Unamaanisha hivyo viti 23 ndio ushindi au hiyo serikali kivuli ndio serikali...Kaazi kweli keli. Amakweli JF imevamiwa.
Kiswahili ndicho kinakupiga chenga... Mshindi ni yeyote anayeshika nafasi za ushindi zilizowekwa. Kwa mfano ktk mbio za 100 mshindi wa kwanza - Kikwebo alichukua medali ya dhahabu, Mshindi wa pili ni JK - medali ya fedha na Mshindi wa tatu Mkandara medali ya shaba..Sasa nikisema JK alikuwa mshindi na ndio maana alipata medali ya fedha unataka ushindi huo upimwe kwa dakika alizokimbia ndio uitwe ushindi au ushindi ni lazima uwe mtu wa kwanza tu, huyo wa pili haitwi mshindi?...

Mkuu wangu Msitumie sana ushabiki wa vyama, CDM ndio wameomba kukutana na JK mnaweza hata nyie kuomba haijakatazwa na mkakutana na JK baada ya CDM au hata kabla ya CDM mkipewa nafasi hiyo, hakuna mtu anayepinga wala kuwazuia ni haki yenu kuwasilisha mawazo ya wale mlopata mchango wao. CDM wameomba kukutana na JK na yawezekana kabisa ktk orodha ya wajumbe watakao kwenda kumwona JK watakuwepo wawakilishi wa Kamati ya Katiba, NCCR - Mageuzi, Chuo Kikuu na pengine hata Taasisi za haki za kimataifa.. na JK hatakuwa pekee atakuwa na watu wake ambao wataiwakilisha Ifisi yake kwa niaba ya chama..Wasiwasi yenu nini hasa?

Halafu kwa nini tunavutana leo hii ktk swala hili?... ni kwa sababu hakuna baina yenu iwe CCM CDM wala NCCR mwenye mchango na mawazo ya wananchi kuhusu uratibu na mchakato mzima wa katiba, nyote mnataka kwenda kumwona rais kwa kufikiria, kukisia na hisia pengine sisi tunataka nini na hakika CDM na NCCR Mageuzi wako karibu sana na jinsi tunavyotaka mwanzo wa mchakato wa katiba mpya... Sisi wananchi ndio tuloomba katiba mpya - JK, CCM, CUF, CDM na NCCR wote hawa mnawakilisha tu ombi letu bila kujua Upya huo utatokana na nini.
 
..hivi ni vichekesho sasa.

..CDM ndiyo wameomba kukutana na Raisi na ombi lao limekubaliwa.

..sasa hawa kina Nape wanamshauri Raisi aombe kukutana na vyama ambavyo tangu awali havikuwa na nia ya kufanya hivyo.

..mimi nadhani wapiga debe wakubwa wa CDM ni viongozi wa CCM aina ya Nape.
 
CCM mambo yote ni MDORORO mtindo mmoja kutokana na makosa mazito kiufundi waliofanya hapa katikati. Tatizo letu wengine huwa hatuamini mambo mpaka tuje tukayaone kwa macho na kuyagusa kwa mikono yetu.

Narudia hapa na tuelewane; ndani ya CCM mambo hivi sasa ni MDORORO MTINDO MMOJA na kwamba wala hamna wa kukiokoa kwa ukaidi na uhiayana wake kwa mambo nyeti ajabu kitaifa
 
Kiswahili ndicho kinakupiga chenga... Mshindi ni yeyote anayeshika nafasi za ushindi zilizowekwa. Kwa mfano ktk mbio za 100 mshindi wa kwanza - Kikwebo alichukua medali ya dhahabu, Mshindi wa pili ni JK - medali ya fedha na Mshindi wa tatu Mkandara medali ya shaba..Sasa nikisema JK alikuwa mshindi na ndio maana alipata medali ya fedha unataka ushindi huo upimwe kwa dakika alizokimbia ndio uitwe ushindi au ushindi ni lazima uwe mtu wa kwanza tu, huyo wa pili haitwi mshindi?...

Mkuu wangu Msitumie sana ushabiki wa vyama, CDM ndio wameomba kukutana na JK mnaweza hata nyie kuomba haijakatazwa na mkakutana na JK baada ya CDM au hata kabla ya CDM mkipewa nafasi hiyo, hakuna mtu anayepinga wala kuwazuia ni haki yenu kuwasilisha mawazo ya wale mlopata mchango wao. CDM wameomba kukutana na JK na yawezekana kabisa ktk orodha ya wajumbe watakao kwenda kumwona JK watakuwepo wawakilishi wa Kamati ya Katiba, NCCR - Mageuzi, Chuo Kikuu na pengine hata Taasisi za haki za kimataifa.. na JK hatakuwa pekee atakuwa na watu wake ambao wataiwakilisha Ifisi yake kwa niaba ya chama..Wasiwasi yenu nini hasa?

Halafu kwa nini tunavutana leo hii ktk swala hili?... ni kwa sababu hakuna baina yenu iwe CCM CDM wala NCCR mwenye mchango na mawazo ya wananchi kuhusu uratibu na mchakato mzima wa katiba, nyote mnataka kwenda kumwona rais kwa kufikiria, kukisia na hisia pengine sisi tunataka nini na hakika CDM na NCCR Mageuzi wako karibu sana na jinsi tunavyotaka mwanzo wa mchakato wa katiba mpya... Sisi wananchi ndio tuloomba katiba mpya - JK, CCM, CUF, CDM na NCCR wote hawa mnawakilisha tu ombi letu bila kujua Upya huo utatokana na nini.

Ili kuondoa kila chama kuomba kukutana na Rais baada ya kukutana na cdm, then ili kupunguza muda utumike kwa shughuli zingine ni vema rais akutane na vyama vyote vyenye hoja kwani hakuna siri kwenye hoja ya katiba .
 
Back
Top Bottom