Usanii juu ya usanii; JK kukutana na vyama vyote

wamegundua kuwa cdm wana hoja ya msingi na kuna uwezekano wakashinda sasa hili isionekana kuwa mabadiliko yametokana na influence ya cdm badala yake wanataka michango ya vyama vingine ambayo hatutegemei kuwa na mpya zaidi ya kile walichokisema bungeni ili baadaye waseme ilikuwa mawazo ya vyama vyote.

ktk hivyo vyama na CUF wamo? maana matusi waliyoporomosha wakati wa uchangiaji wa hiyo sheria yao, sipati picha wataongea nini. Ni heri ya nccr kuliko cuf, jamaa wanapumulia mashine
 
Hapa pana changanya kidogo,hiyo kamati ya CC inamtaka raisi akutane na vyama vyote kwa pamoja au kwa wakati tofauti?Na kwa nini hii kamati ya CC ivisemee vyama vingine?Pana nini kimejificha hapa nyuma ya hili tamko la CC?
kuna watu walisema, kumpa rais rungu la katiba ni kuipa nec rungu.

and id didnt even take a week kuona hayo

kukutana na rais si sawa na kukutana na mwenyekiti wa chama
 
Ni wazo la busara sana hongera CC ya CCM,kumbukeni mkutano wa Pinda na CDM walivyogeuza maneno tofauti na mazungumzo na Pinda,bora wawepo na vyama vingine

Acha ushabiki wa kishamba wewe, wenye hoja ndo wameomba kukutana na Muheshimiwa raisi, wengine waliona hawana jipya ndo maana walikaa kimya. Sasa waende kuonana na raisi kwa lipi? Wakae ofisini watimize majukumu mengine, sio kusindikiza mkutano usiowahusu waende kupasha viti moto!!. Anayemba ndo hupewa, asiyeomba inamaana anavyo navinamtosheleza
 
Ni wazo la busara sana hongera CC ya CCM,kumbukeni mkutano wa Pinda na CDM walivyogeuza maneno tofauti na mazungumzo na Pinda,bora wawepo na vyama vingine

Kweli wewe ni Liberal, unakubaliana na lolote mradi kasema Pinda au JK, uwezo wako wa kupambanua uko wapi?
CDM pekee wameomba kuonana na Rais na ndo maana hawakushiriki mjadala wala kupitisha muswada wa Katiba mpya Bungeni. Vyama vingine vilikubali mapendekezo ya Serikali, sasa vyama vingine vina jipya lipi?
 
Very strange. CCM ni ujinga mtupu au uzee umewazidi. CDM wmeomba kuonana na Rais kwa sababu wanazojua wao. CCM wanataka nao kumona Rais kumweleza nini wakati wao hawana malalamiko? Ina maana wanataka kumlazimsha Rais asaini haraka au vipi?
Hivi Rais ikikubaliana na CDM wao wataandamana au wataingia mitaani kama sisi tunavyosubiri ? Ujinga mtupu. Wakitaka waombe kivyao na sio waombewe.
 
My good Lord! CC ni zero kabisa! Sasa vyama vingine si vilishirikiana na magamba na kuukubali na kuridhia muswada kama ulivyokuwa? Leo hii wanalazimishwa wakaonane na rais? How come!
 
Nape has a point in his suggestion inthat the process of constitution composition must be done under consideration of equal representation. Chadema should not attempt to appropriate the president's move to revive the constitution and assume for themselves but rather should allow for other groups have their contributions listened. We should not forget that Tanzania observes rule of law with one of provisions requiring that everyone has the right to air their opinions provided they do not contravene the law itself.

Nape has a point only if he thinks the president should invite other political parties and other groups to discuss on the matter BUT it is pointless to advice the president to invite other groups to be included in CHADEMA representatives-President discussion. The CHADEMA request is to meet the president and have a discussion, how then bring in other people who had not put any request to the president for similar purpose? It is very unwelcoming if I request to meet you, you accept but later you invite other people whom I had no reason to meet. This is a CHADEMA request. If the president plans to have a meeting with all political parties, it is fine but for sure it will be another meeting and I hope CHADEMA will also be invited.
 
KUHUSU OMBI LA CHADEMA KUKUTANA NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA JUU YA UTATA MZIMA WA 'MUSWADA WA MAKINDA': CCM KINATOA MAELEKEZO YA MKUTANO KWA JAKAYA MRISHO KIKWETE YUPI TUELEWESHANE??

Ndugu Wa-Tanzania,
ombi la CHADEMA kupata maridhiano kwa njia ya mazungumzo juu ya swala nyeti kitaifa la KATIBA MPYA nchini sasa yaelekea kutuumbua sote kama taifa juu ya mapungufu mkubwa ya KI-UFUNDI NA KIKATIBA ya 'Muswada wa Makinda' na kutokujulikana hadi sasa kwamba wadau hawa muhimu wa katiba watakutana na nani hasa.

Wakatini ni takriban chini ya wiki moja tu tangu muswada huo upitishwe kiubabe na mbwembwe nyingi toka kwa chama tawala CCM mjini Dodoma, ni ajabu na kweli kwamba ombi hilo la chama mahiri cha upinzani nchini (CHADEMA) sasa limeibua jambo zito nyuma ya pazia linaloumana moja kwa moja na mojawapo tahadhari tisa nilizowahi kutoa humu baada ya hotuba ya Rais Kikwete kwa Wazee wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam.

Utata wote huu unaojitokeza hata kabla ya muswada wenyewe haujapata baraka za kutiliwa sahihi na kuwa sheria kamili ya nchi licha ya pingamizi lukuki na hasira zilizotanda kwa sehemu kubwa ya wadau wa katiba kote nchini kimsingi hadi tunaingia mtamboni ni dhahiri shahiri kwamba unatokana na ukweli kwamba bado haija umepata tafsiri kinzani kama ambavyo wadadisi wa mambo walivyokua wakitarajia kutoa.

Wakati ambapo CHADEMA kimeripotiwa kutuma maombi kutaka mkutano na taasisi ya urais ambao kwa nchini mwetu unaongozwa na mwenzetu aitwaye Rais Jakaya Mrisho Kikwete juu ya swala hili nyeti na ambalo wao wanaupinga tangu kupitishwa kwake bungeni, wenzao wa Chama Cha Mapinduzi hadi sasa wametuma ishara za kuonyesha ya kwmba mahasimu wao hawa huenda wameomba kukutana na Mwenyekiti wao wa CCM taifa hivyo kutangaza kumpa maelekezo yatokanayo na maazimio ya kichama juu ya jambo gani akalizungumzo na akina nani na wakati gani.

Hakika jambo hili tayari limezua gumzo na hata kuharibu kabisa sura inayoonekana kulazimiswa na huo muswada kumpa kepteni wa timu ya CCM fursa ya kuwa mchezaji mkuu wa timu yake na vile vile kuweza kupigiwa hodi na timu pinzani hata akawasikiliza na kuwatolea maamuzi maridhawa kama refarii mahiri na mwaminifu kwa dakika hizo, kulingana na sheria tarajiwa inavyomtaka akafanye na vile vile kuendelea tu kucheza pindi amalizapo jukumu hilo ndogo tu, kwa furaha, demokrasia halisi, utawala wa sheria na burudani kwa wachezaji wote washiriki huku tukiendelea kudumisha tunu letu la taifa - amani!! Na hiyo ndio demokrasia ya tawala zetu za Ki-Afrika anyway.

Hata hivyo kwa kadri ilivyonakiliwa katika vyombo mbali mbali vya hapa nchini na vya kimataifa majuzi ni CHADEMA ndicho kilichomtaka mkutano Rais Kikwete juu ya kukubaliana kukubaliana kwamba mchakato mzima wa kuandikwa upya katiba mpya si shughuli ya kiserikali bali ni haki ya msingi ya umma wa Tanzania kwa mujibu wa katiba ya sasa ya taifa letu. Pengine kw furaha tu au kwa kutokutambua uharibifu mkubwa aliojiletea juu ya muswada huu muswada ambao unaendelea kuongezeka upinzani toka kwa wadau wa katiba nchini kadiri siku zinavyoongezeka, Rais Kikwete alinukuliwa kupenyeza kwenye mkutano wa kichama kilichokua kikiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho Ndg Jakaya Mrisho Kikwete pengine kwa kutaka kuchangamsha hadhara kwamba kuna matumaini ya serikali yake kuzuia kujikinga na tishio la maandano makubwa nchini kwa kufungua mazungumzo na CHADEMA kisha chama kudandia furaha hizo na kuzitolea msimamo kulingana na matakwa ya maslahi binafsi kichama juu ya swala hilo zito lenye vuta nikuvute kitaifa.

Ndio, Mkurugenzi wa mawasiliano ikulu amenukuliwa akikiri kupokea barua ya CDM na kwamba kwa furaha kubwa kaelekeza pango ufanyike mara moja kwa ajili ya mkutano huo. Lakini kwa mikanganyiko ya ajabu ni kwamba wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akionyesha utaya na mkuta huo huku akipongeza hatua ya kutafuta suluhu kwa CDMkwa njia ya mazungumzo, furaha hizo sasa ni wazi kuingia dosari kubwa kwa kuwa kuna taarifa kwamba am Rais huyo huyo au Mwenyekiti wa CCM kwa upande mwingine naye aonekana kuwa na mpango wa kuvitaka mkutano mwengine vyama vya siasa na asasi za kiraia nchini lakini kwa tarehe na dhumuni ambalo bado kuwekwa wazi hadi sasa.

Mpaka hapo bado haijajulikana kama CHADEMA nao wataalikwa kwenye huo mkutano wa pili au la. Lakini kumbu kumbu zote zinaonyesha kwamba ktika mawasiliano kati ya wadau wa katiba na ikulu yetu, hakuna barua nyingine ya kuomba na au kuombwa mkutano uliokwishapita zaidi tu ya yale kati ya CHADEMA na taasisi ya urais ikulu hivyo nafasi hiyo ya mkutano ni vema kupangiwa siku yake kipeke yake.

Mbali na hapo, tunayo taarifa kwamba kuna chama cha kisisasa (CCM) ambacho chini ya uenyekiti wa bwana mmoja aitwae Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete wao tayari walishapata fursa ya kuhudhurisha kwenye mkutano wao binafsi kule Dodoma Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Amiri Jeshi Mkuu Refarii mahiri asiyekua na upande katika mchakato mzima kuundwa kwa 'katiba mpya' ya Tanzania.

Sasa madai haya na Nape kutoka kwenye chama chake KUTOA MAELEKEZO yaliotokana na kikao chao binafsi kichama kilichongozwa na Mwenyekiti wao, Ndg Jakaya Mrisho Kikwete, kwenda kwa ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ndiye anayependekezwa na muswada hatarishi unaolalamikiwa hivi sasa ndiye muundaji mkuu wa katiba yenyewe na mwamuzi wa hatua zote muhimu kwa faida ya vyama vyote vikiwemo CHADEMA, CUF, CCM, NCCR-Mageuzi na asasi zote kiraia knchini, yote haya ni utata mtupu kikatiba na kwa mantiki ya dhana zima ya utawala bora!!

Sasa pale tunaposikia kwamba eti maazimio ya kikao cha kichama kilichoongozwa na Mwenyekiti wa chama kimojawapo cha sisasa nchini CCM chini ya mtu aitwaye
Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete asikika kwenye vyombo vya habari kumpa MAELEKEZO ama kwa Mwenyekiti wao wa CCM taifa au Rais wa Jamhuri wa Tanzania kwamba naye kwa upande wake aone haja na sababu ya kuitisha ama mkutano au mikutano na vyama vingine vya siasa nchini, ambavyo hata hivyo vyama hivyo hadi sasa havijaripotiwa kuomba mkutano wowote na hiyo TAASISI YA URAIS nchini, tunatumainia kwamba endapo CHADEMA nacho kitapata taarifa rasmi za kutakwa mkutano kwa huo mpangilio wa pili na pia kufahamishwa malengo ya mkutano wenyewe basi maamuzi yatatoka kulingana hali itakavyokua juu ya hilo.

Kwa kutahadhari zaidi hapa, ni kwamba mbali na mikanganyiko ambayo tayari yamekwishajitokeza hapo juu, kuna kila dalili ya huu muswada wa makinda kutuhatarishia ulama wetu kama taifa endapo itatiliwa sahihi kwa sura yake ya sasa bila ya kurudishwa kwa wadau na hatimaye bungeni kwa kuwa hadi sasa na vyombo vya kisheria Zanzibar navyo vitakua vimeingizwa kushughulikia maswla ya Jamhuri yetu ya Muungano wa Tanzania kinyume kabisa na mkataba asili unavyoelekeza juu ya eneo zima hilo licha ya muingiliano mkubwa kichama cha CCM katika jambo hilo zito kitaifa.
.

Kwa mujibu wa TBC1; Nape ametoa taarifa kuwa CCM imemwomba JK akutane na vyama vyote vya siasa vyenye uwakilishi Bungeni.

CCM kwa tikitaka ni komesha. Kugeuza-geuza mambo muhimu kwa manufaa yake haijambo.

Nawashauri CHADEMA wasikubali kuchanganywa na vyama vingine katika Mkutano walioomba kukutana na JK.
 
The now rather reckless and most profoundly thoughtless Offers and counter-offers of a discussion over controversial law-in-the-making in the country not only paints the state house both black and blunk over their true commitmet to this all-sensitive national endeavour with grave public interest to accomplish from a driver position but more so signals a false start of the whole spectrum of events on costitution and constitutionalisation only best destined none other than a sure STILLBIRTH Constitution with no flavour to the citizenry the least!
 
halafu nilivyomsikia nape anasema CDM wanakutana na mwenyekiti wa CCM, alirudiarudia sana hayo maneno wakati anaongea na clouds redio kwa simu, sijui kwanini anapotosha wananchi? CDM walisema wanakutana na Rais wa jamhuri na sio mwenyekiti wa CCM.
 
wamegundua kuwa cdm wana hoja ya msingi na kuna uwezekano wakashinda sasa hili isionekana kuwa mabadiliko yametokana na influence ya cdm badala yake wanataka michango ya vyama vingine ambayo hatutegemei kuwa na mpya zaidi ya kile walichokisema bungeni ili baadaye waseme ilikuwa mawazo ya vyama vyote.
Kwani wao si walisha pitisha mswada huo bungeni, sasa wanataka nini maana hawana la kupoteza siwalishapata walilolitaka???????????Waambie waache kubabaika!!!!!!!!

 
The now rather reckless and most profoundly thoughtless Offers and counter-offers of a discussion over controversial law-in-the-making in the country not only paints the state house both black and blunk over their true commitmet to this all-sensitive national endeavour with grave public interest to accomplish from a driver position but more so signals a false start of the whole spectrum of events on costitution and constitutionalisation only best destined none other than a sure STILLBIRTH Constitution with no flavour to the citizenry the least!
Mkuu uwezo tunao please be explicit for the benefit of the entire public with no exception, so to digest the intended massage!!!!!!!!!
 
DOES OUR STATE HOUSE REALY HAVE ANY IDEA OF 'THE NEXT-BEST THING TO DO' TO MAINSTREAM THE KEY STAKEHOLDERS OF THE CONSTITUTIONAL-MAKING FROM A DRIVER'S SEAT?

It is rather become more apparent now than ever that a man's easy-dive on to an idea that he never owned from the start nor believed in t any point in time can sometimes be such an uphill task to pursue success and connected thinking as the twists and bents so embedded there shall always seek to remain a distant star from the east him.

To such persons with SUDDEN LOVE another person's noble idea but with a detached link with the base, theirs would always remain an endless guess onto the yawning blue skies with a bleak future and very minimal promise since none of the new advent forks would ever seem to be sure of the NEXT-STEP to confidently take a particular instance.

However, in order to keep safe from the keen mind of this kind of apparent weakness such soul would ofte that resort to a temporary refuge in unreasonable conservatism of some sorts. Let's prepare for this on muswada wa makinda sooner than later here.

In this kind of scenario, everything else sporadic, chaotic and often hundled with signs of unconnected moves full rumbles and gambles. And that kind of pre-occupation shall remain a riskier business a personal touch and factual conceptualisation of the whole idea only anchors of IDEAL SITUATIONS and factual scenarios seeks to take a backroom in it all.

Yes, the now rather reckless and most profoundly thoughtless
Offers and counter-offers of a discussion over controversial law-in-the-making in the country not only paints the state house both black and blunk over their true commitment to this all-sensitive national endeavour with grave public interest to accomplish as all cries out for more anwers in every other inch than not.

It is in records to-date that it is ONLY the ruling party on the lines, CHADEMA, has since boldly stepped out of the parks and crowds to hold the monster be the horns by calling for tet-a-tet meeting with the state over the infamous 'Muswada wa Makinda'. This way one deeply fails to configure how Chama Cha Mapinduzi would be fighting tooth-and-nail seeking to further clean its other dirty linens in public but a cruel disregard for a most dangerously dangling party backlog of unaccoplished business of seeking redress with itself of numerous instances mega-corruption within its top ranks that has since melted away drive for economic growth and sustainability of sorts in our country. Bure kabisa; hakuna kitu hapo kutarajiwa kutoka Dodoma zaidi ya gumzo za kuwaida na kuuziana chai kule Chimwaga.

Indeed, the idea here is definitly very simple that we immediately stop the poorly mastered games on constitution making and instead embrace a working national spirit to embark on the new constitution making with franklinees, brotherliness, utmost good faith, trust and openness within our best deserving constitutional jurisdictions as we couragously restrain ourselves from the weaknesses of sheer human greed, superiposition of parochial notions to a national endeavuor in order that we minimise bloodletting in this so noble an undertaking called-for and rightfull to the common citizenry from a driving seat point of view.

Just as much as Tanzania has been a house for the run of the most desparate souls from failing nations on the sides over ages, it is crucially important to remember that the same streak of blends of human greed to monopolises everything to own advantage even where none is on rightful call set those communities apart that we are never insulated enough from similar shocks without a well-checked ego and partisan politics over a common-interest weighty national issue to the like of a constitution.

Finally, how would one help not saying a return back to the drawing boards is but our only sure next move to register as we most genuinely seek to return the thunders to its best deserved place that mos decisively puts common mwananchi development to the driver's position on constitution making lest of which signals of a false start to the whole spectrum of events on constitution and constitutionalisation can never easily be unhooked from the express
destiny for a sure STILLBIRTH Constitution with no flavour to the citizenry the least!
 
Sidhani kama Cdm watakubali,kwa sababu Cuf,Tlp na baadhi wa Nccr walishatoa mawazo bungeni,ila kama ule msemo wa kwenye msafara wa mamba......Nepi yupo sawa kabisa.
 
Chama cha upinzani hapo ni CDM tu CUf ni mke wa CCM waliobabi ni vidumu wa CCM sasa hapo tusitegemee huyo mke na mahawala wa CCM kuiunga mkono CDM,watamuunga mkono bwana yao ambaye ni CCM.
 
Back
Top Bottom