Usambazaji wa arv feki:serikali inahusika 100% -dk charles lyimo mkuu wa idara ya dawa za ukimwi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usambazaji wa arv feki:serikali inahusika 100% -dk charles lyimo mkuu wa idara ya dawa za ukimwi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Sep 25, 2012.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,485
  Likes Received: 5,721
  Trophy Points: 280
  Kama kuna siku niliosikia kizungu zungu nikiendesha gari ni jana ....kwa waliosikia kipindi cha clouds fm jahazi amtowiwa kuamini hii serikali yetu ni ya wauwaji watupu...sipendi kumumunya mdomo wala kupepesa macho kwa ajili ya wapumbavu wachache wanaoua ndugu zetu kwa tamaa zao binafsi

  kama amkusikia basi nitaomba kipindi kile kirudiwe tena kwa maslahi ya taifa ingawa msemaji alianza kupigiwa simu za kutishiwa kuacha kuongelea habari hizo ..kwa kweli ni huzuni kubwa na leo hii dk charles lyimo mchaga aliesoma na kujiamini na mku wa idara ya dawa za ukimwi kitengo cha amana ameweka wazi akuna haja ya kupepesa macho wala kutafuta mchawi huo ujinga uko wizarani ...siyo rahisi kujua hii ni dawa halisi ama bandia lakini tuna uhakika na dawa zinazoagizwa na serikali pekee na akuna mtu binafsi aliepewa tenda ya kuzileta dawa za arv jamani sasa mwenye akili anaweza kujiuliza msambazaji wa hizi dawa ni nani??

  Awali dawa hizo zilikuwa zikiagizwa toka marekani akachaguliwa waziri mmoja akaenda india akarudi na mfumo wake dawa za arv ziagizwe toka india serikali inapelka oda kiwandani na ndie muagizaji mkuu na kuzisambaza kupitia bohari kuu msd lakini dawa hizi hzi zinatengenezwa na kiwanda cha nchini kiko arusha na kina kibali ncha serikali...

  Kama kuna dawa bandia basi serikali ijihoji yenyewe na kuacha kujibu majibu yaiyofaa wakati wakijua chanzo cha ke ni nani//nikisiaga mambo kama haya nacheka kweli kweli kwasababu tangu sakata hilo lianze ni siku nyingi na wengine tumeshaitwa kuandika mawazo yetu tatizo liko wapi unapofwatilia kwa nini bado yanaendelea wizara inajogonga gonga yenyewe

  alipoulizwa tofauti ya dawa za arv india na tanzania alisema unajua sawa na panadol na aspirin ..zote zinatuliza maumivu lakini kuna wanaoumwa tumbo awawezi kunyw aaspirin so wanakunywa panadol...
   
 2. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Habari hii siyo ya ajabu sana hapa Tanzania. Miezi kadhaa iliyopita, tuliambiwa kuwa MSD wameagiza vifaa vya kupimia UKIMWI "Fake" ambavyo vilipigwa marufuku kutumika hapa duniani na WHO. Kama hiyo haitoshi, tulielezwa pia MSD wamehifadhi dawa za kupunguza makali ya UKIMWI ambazo zimepita muda wake zenye thamani ya mabilioni ya talanta. Hii ya sasa ni mwendelezo huo huo wa kutaka kutumia njia za mkato za kukatisha haraka uhai kwa wale wanaotumia dawa hizo! Wakati tukiambiwa tuchangie fedha za kununulia dawa hizo za ARV kwa njia ya muda wa maongezi ("air time") kwavile wahisani wameacha kuchangia( mapendekezo ya TACAIDS), jamaa wengine wanataka kuwaangamiza kabisa wagonjwa kwa dawa feki!
   
 3. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kama kawaida ya serikali yetu TUKUFU, na sikivu,
  Watamshughulikia msemaji (Dkt), na sio kilichosemwa.
   
Loading...