Usaliti wa CUF ni sawa na usaliti wa Mangi Sina, watatumiwa na kisha kuachwa solemba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usaliti wa CUF ni sawa na usaliti wa Mangi Sina, watatumiwa na kisha kuachwa solemba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Godfrey GODI, Nov 20, 2011.

 1. G

  Godfrey GODI Member

  #1
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi sio mwanahistoria mzuri lakini ninaweza kukumbuka vitu vya kihistoria katika nchi yetu hususani wakati wa ukoloni. Wanahistoria watakubaliana nami kuwa Tanganyika ilitawaliwa na wakoloni wa kijerumani. Kabla ya ukoloni, jamii zetu za kitanzania zilikuwa tayari zimejipanga katika suala la uongozi wa makabila.Wajerumani walipoingia nchini Tanganyika walipambana na upinzania mkali kutoka kwa wananchi waliokuwa wanaongozwa na viongozi wao. Mara nyingi wajerumani pekee walishindwa vibaya katika mapambano hayo.Wajerumani walibuni mbinu ya ulaghai. Waliweza kulaghai viongozi wa kabila moja ili waungane na kabila hilo kuwapiga kabila lingine katika Tanganyika. Kwa mfano, wajerumani waliungana na Mangi Sina wa Kibosho na kumpiga Mangi Meli wa Marangu. Watanganyika wakapigana wao kwa wao. Baadaye ujerumani ilimrudi Sina na kumshambulia na kumwagusha. Hila za kikoloni.Ndugu zangu, mtakubaliana nami kuwa hila hizo za mkoloni zinatumika hadi leo katika nchi yetu. Na kwa hiyo zinatumika katika siasa yetu. Kwa hali ilivyo sasa, umasikini wa mtanzania na raslimali za Tanzania ni vitu viwili tofauti. Imekuwa laana kwa mtanzania kuzaliwa katika Tanzania yenye raslimali kibao. Kupitia raslimali hizo si tu kwamba hazimnufaisha mtanzania lakini pia zimepelekea kuongezeka kwa vitendo vya uporwaji wa haki zao.Wakati hayo yanaendelea na kufanywa na serikali ya CCM, na baada ya watanzania kuanza kuhoji namna raslimali zao zilivyogeuzwa laana. CCM inatumia hila ya kikoloni, inaungana na CUF kuishambulia CHADEMA, ambacho ndicho chama kinachowatetea wananchi. CUF zaidi ya CCM ndicho kimekuwa mstari wa mbele katika kukipiga vita CHADEMA na kukifanyia hila za hapa na pale kama alivyotumiwa Sina kumpiga Meli. Cuf, historia hujirudia. Huyo bwana uliyempata ipo siku atakutariki baada ya kukutumia vya kutosha, kama iliyokuwa kwa Mangi SINA. CUF bara take care. Yetu macho na nia yetu kamwe haitabadilika. TUNATAKA UKOMBOZI WA NCHI YETU, UKOMBOZI WA RASLIMALI ZETU NA UKOMBOZI WA RAIA WETU.Nawasilisha……..
   
 2. T

  Topical JF-Expert Member

  #2
  Nov 20, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hujasikia Tundu alipewa pesa kupitia kwa Mbatia wa NCCR mageuzi kufanya yale maujinga??

  Hujasikia Mbowe kapewa pesa na CCM asiwashirikishe wapinzani kwenye bunge..ili muendelee kugawanyika

  Chadema ni agent wa kugawa upinzani tanzania ..endelea kusubiri utaona..ukweli

  hizo ni habari za ndani..
   
 3. j

  jigoku JF-Expert Member

  #3
  Nov 20, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Wewe ni topical au Tropical?maana kwa hoja zako ni kama user name yako hueleweki
   
 4. F

  Falconer JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Unayosema ni maoni yako nyinyi muna yenu na CUF wana yao. Mulipoulizwa kwanini mumetoka bungeni hamukuwa na lakujibu. Kama kuna wasaliti ni nyinyi munaojifanya mdomo juu. Wakati wa Mkapa alipotuuwa zanzibar mbona hatukusikia sauti zenu?. Upinzani tanzania wenye kutumiwa ni nyinyi chadema maana mpaka leo mumeshindwa kutambua zanzibar kama ni moja katika nchi mbili zilizoungana. Mpaka leo chadema wanahisi zanzibar i mkoa ndio maana wazaznibari hawawezi kabisa kuwapa kura chadema. Chadema hawapati kitu kutokana na sera zake za kuwadhalilisha wazanzibari. CCM wanatambuwa kasoro ziliopo za muungano na sisi tunaangalia maslahi ya nchi sio maslahi ya chama. Usalama wa nchi uko juu kuliko sera ya vyama.Kiliopo kutokana na vurumai munazozileta, wazanzibari wanadai referndum juu ya muungano kwasabau wapinzani wengine hamuaminiki. Chadema wakishika wadhifa, Zanzibar imekufa na hiyo ni vita kubwa sana itatokea tanzania. CUF ndio chama pekee kinachoweza kuzungumza masuala ya demokrasia tanzania. wenzetu mupomupo tu.
   
 5. m

  maselef JF-Expert Member

  #5
  Nov 21, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  "Zanzibar si nchi" rejea Pinda
   
 6. gimmy's

  gimmy's JF-Expert Member

  #6
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 2,362
  Likes Received: 1,145
  Trophy Points: 280
  Unajua wa2 wengi huwa wanajidanganya eti chadema ni chama cha ukombozi!
  Tatizo kubwa ni uchu wa madaraka hizi nyingine ni ulaghai 2 kwa watanzania,yani hua najiuliza maswali yasio na majibu,
  kamwe hua hainingii akilini eti mfanya biasha kama mbowe siku akipewa madaraka atawatendea haki watanzania ukweli hizi ni propaganda za kisiasa!CDM wamejaliwa maneno matamu sana tena yenye ma2maini makubwa,sasa angalia mpambanaji kama Lisu mtu anaeoneka kua mstari wa mbele kujifanya anapigania haki za wa tz yeye ndio kinara wakujaza ndugu ndani ya CDM,ila naitamani sana siku watanzania watakapo kipa ridhaa CDM yakuongoza nchi ili tutambue udhaifu na unafiki walioanza kuuonesha mapema,
  CDM ni chama kidogo sana ila kimesha anza kuonesha ubinafsi mkubwa,wa2 wenye influence kubwa ndani ya CDM wamekua wakipeana ulaji ndani ya chama,viti maalumu vimejaa undugu mkubwa,
  Zaidi ya ulaghai kwa watanzamia bado sijaona watakacho kuja tufanyia sisi kama watanzania
   
 7. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #7
  Nov 21, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Watu wa CCM wakiona hizi hoja dhaifu wanakomalia kweli, lakini zikija hoja muhimu hapa huwa wanafyata mkia na kukimbia. Wanasubiri upuuzi kama huu wanavyochangia sio mchezo ukija hoja juu ya matatizo ya umeme, kina jairo, nk huwaoni wanajificha. Mnyidanganye kuwa CDM ni chama kidogo na muendelee kubweteka na kuchangisha pesa ili bajeti zenu zipite kirahisi. Saa yaja mtalia na kusaga meno.
   
 8. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #8
  Nov 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ujinga wa kudhani kwamba kila wanachopigania Chadema ni sahihi na kwamba wanafanya hivyo kwa niaba ya au kwa maslahi ya wananchi ni danganya toto ambayo hatuwezi kuikubali. Hawa jamaa ni wapotoshaji ambao ni watu makini tu wanaweza kuwashtukia. Cuf kama chama kina haki ya kuwa na maamuzi yao ambayo kwa utashi wao yanawakilisha maslahi ya wapiga kura wao. Ieleweke wazi kwamba Cuf siyo tawi la Chadema, kama ambavyo siyo tawi la CCM. Wana haki ya kusimamia katika wanachokiamini na hakuna wa kuwalazimisha kufuata njia ambayo wao hawaiamini.Watu waache kudhani kwamba Chadema ni kiranja wa vyama vingine. Cuf hawawezi kutishwa na mob justice inayoendeshwa na Chadema na hizo populist approaches ambazo haziwezi kutupatia matunda ya kweli ya mchakato huu. Wao wanataka kuhodhi mjadala na mchakato huu ili waonekane ni mashujaa na waanzilishi wa mchakato. Wakiona kwamba wanaporwa hoja wanakuja juu na kuleta upotoshaji. Haikubaliki!
   
 9. j

  jumalesso Member

  #9
  Nov 21, 2011
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kila jambo Chadema wanapenda kulikuza naona mara hii wamechemka wanatakiwa waache kukurupuka na kujiona wao ndio wanaweza kusimamia mambo. Kwanini watoke Bungeni na wasisimame kupangua hoja ndani ya Bunge? ni bora ile Chadema ya wakati ule uliyokuwa na wabunge kina marehemu Chacha kuliko hawa ambao wingi wao Bungeni umeshaanza kuwatia kiburi. Huu usanii wa kila jambo makelele tuu na kuwalaumu CUF ambao nao walikuwa makelele siku za nyuma wakaona hayana tija vile vile wakajifunza ustaarabu someni kwao
   
 10. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #10
  Nov 21, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,078
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  cuf inawanyima usingizi cdm,

  cuf ni chama makini sio cha kuburuzwa buruzwa ... mwataka cdm wakisema jambo basi cuf iitikie tu ...
   
 11. m

  marembo JF-Expert Member

  #11
  Nov 21, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Topical kadata anahitaji msaada wa wana JF. Hata kama umetumwa au ni mamluki kuna namna ya kutumika. Tuepuke kuwa marobot.
   
 12. Mwangaza

  Mwangaza Senior Member

  #12
  Nov 21, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33

  CUF ina nini cha kuinyima usingizi CHADEM ??

  CHADEMA inapigania haki za watz, ambazo CCM imewapola miaka yote. ktk mpamnabo huu CUF inaingiaje??

  CuF ndio inalinda ndoa yake na ccm, haichi kupiaga piga kilele (kama ipo mwezini) kila mume wake anaposumbuliwa.

  mfano hai tu angalia: hakuna shutuma wanayotoa CHADEMA kwende cuf, bali zipo za kutoka CHADEMA kwenda ccm na serikali yake lkn badala ya kujibiwa na ccm ,mke wake (cuf) anaanza kulopoka lopoka haraka haraka!! ...wanawake wa uswahilini bwana!
   
 13. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #13
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Uko sawa kabisa.CUF chama makini aisee!Umakini wake hata sisi tuliuona kule IGUNGA.
   
 14. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #14
  Nov 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Maneno yako tu yanaonyesha kwamba wewe ni mtoto aliyelelewa katika mazingira magumu. Chadema wanaweweseka baada ya kuona kwamba hoja waliyodhani ni hoja sasa haipati uungwaji mkono na sasa watu wameanza kuwaona wajinga. Wenzenu CUF waliligundua mapema hilo kwa sababu wao walikuwa ni watu wa kususa kule zanzibar mpaka wakafukuzwa na kupoteza uwakilishi. Wamejifunza kwamba katika mijadala kama hii, ni lazima mtu uelewe kwamba minority should have their say as the majority have their way. Uchanga wa elimu ya demokrasia na udikteta wao wa kudhani kwamba wao ni viranja wa upinzani sasa umeshtukiwa na ndiyo maana wanakasirika kuona kwamba watu hawawafuati blindly!
   
Loading...