Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Uchaguzi Mkuu umemalizika na majeraha yaliyosababishwa na uchaguzi huo yameshapona na makovu yake yameanza kufutika. Hii ni baada ya walioshindwa kukubali kushindwa na kutoa ushirikiano kwa mshindi. Napenda kukiri kwa dhati ya moyo kwamba, haijapatapo kutokea Mshindi wa Uchaguzi wa Rais Tanzania kuungwa mkono na Upinzani kwa kiasi kikubwa tofauti na ilivyotokea mwaka huu. Haikuwa Rahisi kwa Mrema chini ya NCCR Mageuzi kumkubali Mkapa. Ilitokea pia mwaka 2010 ambapo Dr Slaa alikuwa mgumu kukubali ushindi wa Jakaya Kikwete.
Sote tunajua kuwa wapinzani walikula yamini kuwa hawatakubali ushindi ikiwa uchaguzi hautakuwa huru na haki. Pia tunajua kuwa baada ya Uchaguzi, Mgombea wa UKAWA, Edward Lowasa amenukuliwa akilalama kuwa ameshinda uchaguzi huo kwa asilimia 62 isipokuwa CCM wamebadilisha matokeo. Kwa hali hiyo, aliwataka viongozi wenzake wa UKAWA kutotambua ushindi wa Dr Magufuli.
Hata hivyo, kadri siku zinavyoenda, ile yamini waliyokula wapinzani imeanza kupotea. Alianza Maalim Seif Sharif Hamad ambapo alimtembelea Rais Magufuli Ikulu na kufanyanaye Mazungumzo. Baada ya Mazungumzo, Maalim Seif amenukuliwa akisema kuwa ana imani na Rais Magufuli na kwamba ndiye mtu pekee ambaye anaweza kuleta suluhu ya mgogoro wa Zanzibar. Maalim Seif alirejea tena kauli yake wakati alipoongea na Waandishi wa Habari na kumuomba Rais Magufuli aingilie kati kwa vile imani aliyonayo kwake ni kubwa.
Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye alikuwa bega kwa bega na Lowasa kuhakikisha kuwa Magufuli hawi Rais. Baada ya uchaguzi, kulikuwa na kimya kingi juu yake wengi wakitaka kufahamu nini msimamo wa Sumaye baada ya Magufuli kushinda. Kitendawili hicho kimeteguliwa juzi baada ya Rais Magufuli kumtembelea Sumaye Muhimbili ambako amelazwa kwa matatizo ya moyo. Sumaye alionekana mwenye furaha kutembelewa na Rais na akasema kuwa amefarijika kuona kuwa Rais ana mtembelea na kwamba ana upendo kwa watu wake.
Taarifa rasmi ninazowapa ni kwamba Freeman Mbowe na James Francis Mbatia ijapokuwa hawajaonana ana kwa ana lakini wameshampigia simu Dr Magufuli na kumpongeza kwa ushindi. Taarifa hizo ambazo JF imekuwa ya kwanza kufahamu zinasema kuwa Mbowe na Mbatia wameahidi kumpa ushirikiano wa kutosha Rais Magufuli kwa vile wanaamini kuwa ataifikisha mbali Tanzania.
Kwa hali hiyo, mpaka sasa, mtu pekee ambaye hajabainika kuubali ushindi wa Dr Magufuli ni Edward Lowasa pekee. Taarifa zinasema kuwa Lowasa analalama kitendo cha wenzake kubatilisha msimamo wao hali ambayo inaonekana kuwa wanampalia Mkaa kwa jamii. Kwamba, kitendo cha Lowasa kuendelea kutomuunga mkono Magufuli huku viongozi wote wa upinzani wakifanya hivyo kinapokelewa kwa hisia tofauti miongoni mwa wana jamii. Kwa hali hiyo, Lowasa hana namna nyingine ya kufanya zaidi ya kuungana na wenzake kumpa ushirikiano Dr Magufuli ili tujenge kwa pamoja Mama Tanzania.
Nimalizie kwa kusema kuwa Mchezo wa Siasa una matokeo mawili tu. Ama kusninda ukafurahia ushindi wako au Kushindwa ukakubali kushindwa. Lowasa anayo kazi moja tu ya kufanya mbele yake. Kukubali kushindwa na kumpa ushirikiano aliyeshinda.