lete rimoti
Senior Member
- Aug 24, 2021
- 152
- 192
Mwanao anasoma shule yenye school bus?. Huwa unaangalia gari hiyo inakuwa na idadi ya wanafunzi wangapi? tukemee huu upuuzi tusije wapoteza watoto wetu
Well said mkuu. Naimani wamekusikiaKwa harakaharaka abiria wa hiyo school bus wankaribia 50!!! Baadhi ya watoa huduma ya school buses wanatamaa saana sana. Wanawapanga watoto kama mizigo ili wao wapate pesa zaidi
Serikali ingewawekea masharti ya idadi ya watoto wanaoruhusiwa kupanda kwa wakati mmoja kama ambavyo jiji la Dar lilivyowahi kuwawekea sheria ya kupaka rangi ya njano
Na hili wala sio kusubiri Rais au PM au Waziri wa Elimu au TAMISEMI walitolee tamko bali hata maofisa elimu wilaya kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya ndani wanaweza kulisimamia vizuri
Naungana na mleta uzi kutoa wito kwa wazazi na walezi wafuatilie kujua namna watoto wao wanavyosafirishwa kila asubuhi na jioni kwenda na kurudi shule na waikatar hali hii ya utesaji wa watoto
Kweli kabisa yaani kuna umuhimu kabla hawajaingia kwenye gari Mzazi ujiridhishe lasivyo bora utafute njia nyingine za usafiriMimi watoto wangu bora nipate shida ya kuwapeleka na kuwachukua kuliko kuwatia kwenye school bus, wanajazwa kama mifugo