Usalama wa Watanzania sasa uko hatarini!

asha ngedere

Member
Nov 6, 2009
92
11
Wadau hebu naomba tuchangie hoja hii. Hivi ni kweli usalama wetu uko hatarini kiasi hiki?

Usalama wa Watanzania sasa uko hatarini!

Na Daniel Mbega

YAMEANDIKWA mambo mengi katika siku za karibuni kumhusu Zitto Kabwe Zuberi, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia chama hicho.

Yanayoendelea kuandikwa na kuzungumzwa kila kona ni kuhusiana na mgogoro au tofauti zilizopo kati yake na viongozi wenzake ndani ya Chadema, hasa kutokana na msimamo wake wa kuwa tofauti na maamuzi ya vikao vingi vya chama hicho baada ya uchaguzi mkuu wa 2010.

Katika kile kinachoonyesha bayana kwamba hali haiko shwari ndani ya Chadema, ni mambo ambayo yamefululizwa kuandikwa katika wiki takriban tatu sasa yakimhusisha Zitto Kabwe na watu wa nje ya chama, na mbaya zaidi kuhusishwa kwake na Idara ya Usalama wa Taifa pamoja na mfanyabiashara Rostam Aziz, ambaye ni Mbunge wa Igunga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kusema kweli taarifa zinazoenea zinaleta taswira mbaya miongoni mwa Watanzania ambao sasa wanaona wazi kwamba usalama wao uko hatarini kwa kuwa taarifa zao, tena hata zile za faragha, zinafahamika na wengi kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano na Sheria za Nchi.

Jumatano iliyopita gazeti la MwanaHALISI liliripoti kwa mapana kuhusiana na maongezi ya simu ya mkononi ya mara kwa mara baina ya Rostam Aziz na Zitto Kabwe, bila kuweka bayana kile wawili hao walichokuwa wakikizungumza zaidi ya kuweka muda tu wa maongezi hayo.

Katika ripoti yake, gazeti hilo limetoa mfano wa mazungumzo hayo ambapo limesema Zitto akitumia simu namba+255756809535 na Rostam simu namba +255754555555 walifanya mawasiliano Agosti 11, 2010 saa 7:08:35, saa 22:09:02, saa 22:28:39, saa 22:44:37, saa 22:45:09, na saa 22:49:54, na kwamba wakati mawasiliano hayo ya simu yanafanyika simu ya Zitto ilisomeka kuwa yuko Uzunguni, Dodoma huku simu ya Rostam ikisomeka kuwa yuko Area D, Dodoma.

Ikaelezwa kuwa mawasiliano mengine kati ya Zitto na Rostam yalifanyika Novemba 30, 2010 yakionyesha kuwa Zitto yuko Ohio, Dar es Salaam, ambapo yalifanyika saa 14:58:42, saa 15:38:00, saa 16:09:56, saa 16:41:58, na saa 17:48:35, na mawasiliano mengine yalifanyika Desemba 7, 2010 ikiwa ni siku mbili kabla ya kikao cha wabunge wa Chadema kilichofanyika Bagamoyo, yaliyofanyika saa 07:57:27, saa 09:44:36, saa 14:07:07, na saa 14:32:08.

Machapisho ya mazungumzo haya, kwa mujibu wa gazeti hilo, ni mwendelezo wa machapisho ya wiki iliyotangulia kuhusiana na maongezi ya mara kwa mara kati ya Zitto na Jack Zoka, Naibu Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa.

Katika toleo lililotangulia, gazeti hilo lilieleza kwamba vigogo wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) wanaingilia Chadema na kwamba wana mahusiano ya karibu na Zitto Kabwe, huku wakimtaja moja kwa moja Naibu Mkurugenzi wa TISS, Jack Zoka.

Ikaelezwa kwamba, Zitto na Zoka walifanya mawasiliano mara tisa Agosti 8, 2010 huku Zitto akitumia simu namba +255756809535 na Zoka akitumia simu namba +255754787550 na wakati mawasiliano hayo yakifanyika Zitto alikuwa katika maeneo tofauti kwani wakati mwingine ilisomeka akiwa Mtambani, Kinondoni jijini Dar es Salaam, Kigoma Mjini, Kigoma Vijijini, Mtwara, Uwanja wa Ndege-Ilala, Oysterbay, Ukonga, Upanga na katikati ya jiji la Dar es Salaam!

Gazeti hilo halikuweza kugundua nini walichokuwa wakizungumza, lakini kinachowashangaza wengi ni namna mawasiliano hayo, kwa mujibu wa gazeti hilo, yalivyofanyika kwa nyakati tofauti – siku moja – katika mikoa mitatu tofauti: Dar es Salaam, Kigoma, Mtwara, kisha Dar es Salaam.

Yawezekana alikuwa na helikopta na ndege ya kukodi, hilo siyo la msingi sana, na ambacho gazeti hilo – ambalo linatajwa kuwa na uhusiano wa karibu na Chadema – lilihoji ni uswahiba gani uliopo baina ya Zoka na Zitto, kwani wanaeleza kwamba mawasiliano baina ya wawili hao yalianza kupamba moto tangu Agosti 6, 2010, siku moja baada ya Chadema kuzindua kampeni zake za urais.

Inaelezwa kwamba, kuanzia hapo hadi sasa, Zitto na Zoka wamekuwa na mawasilino ya mara kwa mara, na karibu kila siku huzungumza kwa simu. Mawasiliano mengine ya mara kwa mara yalifanyika tarehe Agosti 7, 2010, siku mbili tangu hotuba kali ya Jangwani na yalianza saa 10:17 na kuendelea tena saa 10:50, saa 10:51:31, saa 11:46:13, saa 12: 14:46, saa 12:26:48 na saa 13:50: 21.

Makala haya hayana haja ya kutaka kujua undani wa mazungumzo baina ya Zitto Kabwe na Rostam au Zitto na Zoka, na inaeleweka kwamba gazeti hilo limekuwa likifichua mambo mengi yanayoendelea kuhusiana na kiongozi huyo wa Chadema anayedaiwa kutaka kukisaliti chama.

Gazeti la MwanaHALISI halikuishia kufichua mawasiliano baina ya Zitto na Rostam na Zoka kwa njia ya simu tu, lakini pia limeweza kuchapisha mawasiliano ya Zitto kwa Rais Jakaya Kikwete na pia mawasiliano ya barua-pepe ya Zitto na watu wengine.

Kwa mfano, gazeti hilo lilichapisha mawasiliano ya Zitto kwenda kwa Rais Kikwete Aprili 25, 2009 akisema: “…ninaleta kwako ushauri ufuatao ili kumaliza suala hili kabisa bila ya kuathiri sura (image) ya nchi katika uwekezaji duniani na pia kuongeza ufanisi wa bandari. Kwanza, Serikali ikubaliane na TICTS kuondoa kipengele cha exclusivity (hodhi ya biashara) katika mkataba wake ili kuruhusu ushindani na hivyo kuongeza ufanisi; na zabuni ya kuendesha kitengo kingine cha makontena katika Berths 13 & 14 itangazwe kwa kufuata sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2004. Pili, Serikali itangaze rasmi kuwa nyongeza ya mkataba na TICTS itaendelea kwa sababu uwekezaji katika miundombinu ya bandari ni ya muda mrefu na hivyo mkataba wa mwanzo wa miaka 10 haukuwa na mantiki kiuwekezaji.”

Inaelezwa kwamba, mapendekezo ya Zitto ya kutaka serikali isivunje mkataba, yanafanana na yale ambayo serikali ilitekeleza, pamoja na zogo kubwa kuibuka ndani na nje ya Bunge, na katika mawasiliano hayo, anaeleza kuwa kilichoandikwa ni siri kati yake na serikali na rais, lakini siku tatu baadaye, Zitto alipeleka nakala ya barua aliyompelekea rais, kwa mtendaji mkuu wa kampuni ya Vertex International Securities, Peter Machunde, Aprili 28, 2009 saa 3:45 asubuhi ikiwa na maneno, “This is for me and you only (Hii ni kwa ajili yako na mimi tu) ambayo nimepeleka kwa mkuu wa nchi.”

Mbali na mawasiliano na baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi, Zitto amedaiwa kuwa na tabia ya kuwasiliana na baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari na kujiandikia habari huku wao wakitakiwa “kuzichapa kama zilivyo.”

Kwa mujibu wa gazeti hilo, Zitto anatuhumiwa pia kuwa na mawasiliano ya karibu ya kikazi na binafsi, na Maria Kejo, mtumishi wa serikali katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), anayetuhumiwa na Chadema katika kashfa kadhaa nchini ikiwemo kutoa ushauri uliowezesha kufikiwa kwa makubaliano yaliyozaa mkataba wa kufua umeme wa Independent Power Tanzania Limited (IPTL).

Katika mawasiliano yake ya barua-pepe na Kejo ya Aprili 23, 2009, Zitto anamtumia Kejo mapendekezo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC) kuhusu mkataba kati ya serikali na IPTL, akisema: “…Pitia kisha ushauri katika mambo ya IPTL na Benki Kuu. Pia pengine popote utakapoona inafaa kushauri. Tunaisoma Jumatano na ni draft (rasimu) bado, but strictly confidential. Can come to your office (lakini hii ni siri kubwa, naweza kuja ofisini kwako kuzungumza)… Halafu sina hela mpenzi…”

Kwa hali ya kawaida tunaweza kulipongeza gazeti hili na waandishi wake kwamba wamefanya kazi kubwa ya uandishi wa kijasusi (investigative journalism), lakini ukichungulia kwa upande wa pili ambao ni mkubwa zaidi unaweza kubaini kwamba kuna walakini mahali fulani.

Kama nilivyosema hapo awali, hatuhitaji kujua walichozungumza Zitto na Rostam au Zoka, lakini kinachotisha ni hali hii ya mawasiliano ya faragha kuweza kuibuliwa na gazeti ambalo limeamua kufanya kazi ya ujasusi zaidi ya upashaji habari.

Nafahamu kwamba walikuwa wanajivunia Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Ibara ya 18(b) na Sheria ya Uhuru wa Maoni ya mwaka 1984 Na.15 ib. 6 na Sheria ya 2005 Na. 1 ib. 5, lakini ibara hiyo ya 18(c) inaonya kwamba kila mtu anao uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake.

Pia Sura ya Kwanza, Sehemu ya Tatu, Ibara ya 16(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, kuhusu Haki ya faragha na usalama wa mtu, kwa kuzingatia Sheria ya mwaka 1984 Na. 15 ib. 6, inaeleza bayana kwamba uhuru na faragha ya mtu haipaswi kuingiliwa.

Yawezekana mawasiliano baina ya Zitto na Rostam yalikuwa ya binafsi kabisa, na hata mawasiliano yake na Zoka yalikuwa ya binafsi pia, kwa sababu katika hali ya kawaida mtu yeyote anayo haki ya kuchagua rafiki amtakaye, siyo kuchaguliwa.

Ikumbukwe pia kwamba, pamoja na Zoka kuwa mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, bado ni binadamu wa kawaida aliye na uhuru wa kuwasiliana na watu wengine kwa masuala ambayo siyo ya kikazi, hivyo kumhukumu moja kwa moja na kuituhumu Idara hiyo kuwa inaihujumu Chadema tunaweza kuwa tunakosea.

Itakumbukwa kwamba, Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Willibrod Slaa alitajwa kwamba alikuwa akiwasiliana na maofisa wa TISS ambao inaelezwa ndio wanaompatia taarifa nyingi za ndani kiasi ch kushikwa na ‘kiburi’ na kutamka bayana kwamba ataendelea kupokea taarifa kutoka huko na idara nyingine za serikali pamoja na Zoka kukaririwa akisema hao ni maofisa feki.

Taarifa hizo zinaelezwa ndizo zilizomfanya Dk. Slaa akatangaza kwamba TISS ilihusika na uchakachuaji wa matokeo ya kura. Sijasikia hata mara moja hili likitajwa kwa mapana kama Zitto kuwasiliana na Rais, maofisa wa serikali, TISS na Rostam. Au kwa vile taarifa alizopewa Dk. Slaa zilikuwa zinainufaisha Chadema?

Bado narudia kusema kuwa, silituhumu gazeti hili wala waandishi wake kwa kilichoripotiwa, lakini nahoji, ikiwa mawasiliano baina ya mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa yameweza kunaswa kirahisi kiasi hiki, hivi hali ya usalama wa Watanzania ikoje?

Kilichoandikwa ni kile kinachomhusu Zitto Kabwe na Chadema, lakini je, ni mambo mangapi ambayo gazeti hilo, waandishi wake ama wapasha habari wao wameyanasa yakiwa ni mazungumzo baina ya Zoka na watu wengine, hasa ikizingatiwa kwamba Zoka anafanya mawasiliano na watu wengi sana – ya kikazi na ya faragha?

Kama hata mawasiliano ya barua-pepe pia yameweza kunaswa, hivi tuseme nchi yetu iko salama kiasi gani ama Watanzania waendelee kuamini kwamba utandawazi umeboresha mawasiliano yanayowavua nguo hadharani?

Kwa tunavyoelewa, kilichofanywa na gazeti hili ni kuichunguza Idara ya Usalama wa Taifa na jinsi inavyowasiliana na watu mbalimbali, jambo ambalo nachelea kuliita kama ni uchochezi, jinai ama uhaini, kwa sababu ni mbinu za hatari za kijasusi tu zinazoweza kuchunguza idara nyingine, kitu ambacho, kama gazeti, halina mamlaka ya kisheria wala kikatiba kukifanya.

Wale wataalamu wa masuala ya kijasusi (espionage) wanaweza kulieleza hili kama ni counter-intelligence, yaani ujasusi wa kuwachunguza majasusi!

Vinginevyo, inafahamika kisheria kwamba, chombo chenye dhamana ya kupekua mawasiliano ya simu baina ya mtu na mtu, au kikundi ama kampuni ni Jeshi la Polisi hasa pale kunapokuwepo na kesi ya jinai, tena kwa kibali maalum.

Najaribu kuhoji, Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeridhia mtu yeyote kufanya ujasusi wa aina hii au ndiyo mwanzo mpya wa uhuru wa habari uliopitiliza? Kama leo hii Idara ya Usalama inaweza kuchunguzwa na watu wan je, na nyaraka za Rais zinaweza kunaswa na yeyote mahali popote, hivi tuamini kwamba usalama wetu uko imara?

Nadhani hapa kuna kitu ambacho kinahitaji majibu, tena ya haraka, vinginevyo wananchi wataendelea kutokuwa na imani na serikali ikiwa usalama wao uko mashakani kama hivi.

Ikiwa kuna matundu ndani ya Idara hiyo yanayovujisha siri hizi, ni vyema yakazibwa, kwa sababu mwelekeo wake ni mbaya kwa taifa. Yeyote anayefanya hivyo asidhani anamkomoa mwenzake au wenzake, bali atambue kwamba anautoboa mtumbwi ambao yeye pia yumo ndani yake, ukizama hakuna atakayebaki salama.

Nawasilisha.

CHANZO: DIRA YA MTANZANIA DESEMBA 20, 2010.
 
Mwanahalisi wana kazi moja tu nayo ni kutuhabarisha.wanachotakiwa ni kueleza habari za kweli tu na sio uzushi,haijalishi wanazipata vipi iwe kupitia UWT(kundi la wazalendo) au kwa kumwagiwa Tindikali.
Kwa maoni yangu usalama wa watz utahatarishwa zaidi pasipokuwa na leakage ya information kama hizi.hivi ni kweli hatuoni uhuru wetu kuingiliwa na magazeti ya udaku(watu wanapigwa picha gesti) mbona hapa tuko kimya!
Mi naona poa tu uhuru wangu wa privacy ukiingiliwa kwa manufaa ya taifa.
 
Mbona hata huko kwenye FBI siri zinavuja sembuse UWT wanaotumia radio call za kichina?
 
Jamaa jinga kweli, Wikileaks, Abu Girebu jela ya Irak, watergate scandal during Nixon era,monica Lewisky, na kashfa nyinginezo nyingi za CIA,zilizovuja sembuse Zito na Jk,au na Zoka. Kuna usalama wa Taifa Bongo? ni ajira za kupeana kusaidiana maisha .
 
Usalama Wa Taifa,walishindwa kujua EPA ,kagoda na Richmond na madudu mengine mengi tu. Halafu Today unatueleza nini? au na wewe nae ni Nyoka? uko under cover JF? kwani tunawajua kila mwisho wa mwezi mna cheki Zenu toka TISS .
 
Hakuna siri ambayo ni siri kwa 100%. Ukitumia email ni lazima ujue wamiliki wa saver unayotumia wana uwezo wa kuona kila kitu lakini pia wapo wajanja wa Teknohama ambao japo hawamiliki saver lakini wana uwezo wa kunasa mawasiliano ambayo wewe unaweza hata kuwa umeyapiga chapa ya, 'TOP SECRET', ndiyo gharama ya teknolojia.

Mwanahalisi kwa kutumia mbinu zao wameweza kutafuta vithibitisho vyao kwa nini wanamtilia mashaka Zito, ni lazima wapongezwe sana kwa kutafuta sababu za kuipa hoja yao ya kumtilia shaka Zito uzito.

Mwasiliano ovu mengi hutendeka katika siri, ili kuweza kuyagundua mawasiliano yoyote ya uovu ni lazima mbinu kama hizi zifanyike.

Kama mawasiliano yake na watu hao waliotajwa hayakuwa kwa nia ambayo mwandishi anahisi, njia pekee kwa Zito ni kutoka na vielelezo na kuueleza umma mawasiliano yake na watu hao yamekuwa yakihusu nini, na labda kuwa hao watu wote ni marafiki zake. Lakini nahisi kuna ukweli ambao Zito ameshindwa kuukataa ndiyo maana mpaka leo hakuna kauli yoyote kutoka kwake.

Hiyo ndiyo gharama ya kuwa kiongozi. Kama haki hiyo unayoiongelea mleta hoja ingekuwa inazingatiwa kikamilifu, basi maovu mengi yasingeweza kujulikana.
 
Huyu jamaa nadhani katumwa, usifanye watu mbumbu kiasi hiki katika karne hii, unapozungumzia usalama wa taifa ni pamoja na usalama wa miundo mbinu inayolifanya taifa hili kuwepo (to exist) kama miundombinu hii inachukuliwa kiujanjaujanja afu usalama huu uko kimya ati wanaogopa kumkasirisha bwana mkubwa JK, basi hautufai, ndomana mwanahalisi wameamua kufanya kazi iliyowashinda usalama wa taifa. Ninawaunga mkono mwanahalisi kwasababu kazi yao inakubalika kwa uma wa watanzania.
Mr. Kubenea endelea na mapambano tuko nyuma yenu.
 
Wadau hebu naomba tuchangie hoja hii. Hivi ni kweli usalama wetu uko hatarini kiasi hiki?

Usalama wa Watanzania sasa uko hatarini!

Na Daniel Mbega

YAMEANDIKWA mambo mengi katika siku za karibuni kumhusu Zitto Kabwe Zuberi, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia chama hicho.

Yanayoendelea kuandikwa na kuzungumzwa kila kona ni kuhusiana na mgogoro au tofauti zilizopo kati yake na viongozi wenzake ndani ya Chadema, hasa kutokana na msimamo wake wa kuwa tofauti na maamuzi ya vikao vingi vya chama hicho baada ya uchaguzi mkuu wa 2010.

Katika kile kinachoonyesha bayana kwamba hali haiko shwari ndani ya Chadema, ni mambo ambayo yamefululizwa kuandikwa katika wiki takriban tatu sasa yakimhusisha Zitto Kabwe na watu wa nje ya chama, na mbaya zaidi kuhusishwa kwake na Idara ya Usalama wa Taifa pamoja na mfanyabiashara Rostam Aziz, ambaye ni Mbunge wa Igunga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kusema kweli taarifa zinazoenea zinaleta taswira mbaya miongoni mwa Watanzania ambao sasa wanaona wazi kwamba usalama wao uko hatarini kwa kuwa taarifa zao, tena hata zile za faragha, zinafahamika na wengi kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano na Sheria za Nchi.

Jumatano iliyopita gazeti la MwanaHALISI liliripoti kwa mapana kuhusiana na maongezi ya simu ya mkononi ya mara kwa mara baina ya Rostam Aziz na Zitto Kabwe, bila kuweka bayana kile wawili hao walichokuwa wakikizungumza zaidi ya kuweka muda tu wa maongezi hayo.

Katika ripoti yake, gazeti hilo limetoa mfano wa mazungumzo hayo ambapo limesema Zitto akitumia simu namba+255756809535 na Rostam simu namba +255754555555 walifanya mawasiliano Agosti 11, 2010 saa 7:08:35, saa 22:09:02, saa 22:28:39, saa 22:44:37, saa 22:45:09, na saa 22:49:54, na kwamba wakati mawasiliano hayo ya simu yanafanyika simu ya Zitto ilisomeka kuwa yuko Uzunguni, Dodoma huku simu ya Rostam ikisomeka kuwa yuko Area D, Dodoma.

Ikaelezwa kuwa mawasiliano mengine kati ya Zitto na Rostam yalifanyika Novemba 30, 2010 yakionyesha kuwa Zitto yuko Ohio, Dar es Salaam, ambapo yalifanyika saa 14:58:42, saa 15:38:00, saa 16:09:56, saa 16:41:58, na saa 17:48:35, na mawasiliano mengine yalifanyika Desemba 7, 2010 ikiwa ni siku mbili kabla ya kikao cha wabunge wa Chadema kilichofanyika Bagamoyo, yaliyofanyika saa 07:57:27, saa 09:44:36, saa 14:07:07, na saa 14:32:08.

Machapisho ya mazungumzo haya, kwa mujibu wa gazeti hilo, ni mwendelezo wa machapisho ya wiki iliyotangulia kuhusiana na maongezi ya mara kwa mara kati ya Zitto na Jack Zoka, Naibu Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa.

Katika toleo lililotangulia, gazeti hilo lilieleza kwamba vigogo wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) wanaingilia Chadema na kwamba wana mahusiano ya karibu na Zitto Kabwe, huku wakimtaja moja kwa moja Naibu Mkurugenzi wa TISS, Jack Zoka.

Ikaelezwa kwamba, Zitto na Zoka walifanya mawasiliano mara tisa Agosti 8, 2010 huku Zitto akitumia simu namba +255756809535 na Zoka akitumia simu namba +255754787550 na wakati mawasiliano hayo yakifanyika Zitto alikuwa katika maeneo tofauti kwani wakati mwingine ilisomeka akiwa Mtambani, Kinondoni jijini Dar es Salaam, Kigoma Mjini, Kigoma Vijijini, Mtwara, Uwanja wa Ndege-Ilala, Oysterbay, Ukonga, Upanga na katikati ya jiji la Dar es Salaam!

Gazeti hilo halikuweza kugundua nini walichokuwa wakizungumza, lakini kinachowashangaza wengi ni namna mawasiliano hayo, kwa mujibu wa gazeti hilo, yalivyofanyika kwa nyakati tofauti – siku moja – katika mikoa mitatu tofauti: Dar es Salaam, Kigoma, Mtwara, kisha Dar es Salaam.

Yawezekana alikuwa na helikopta na ndege ya kukodi, hilo siyo la msingi sana, na ambacho gazeti hilo – ambalo linatajwa kuwa na uhusiano wa karibu na Chadema – lilihoji ni uswahiba gani uliopo baina ya Zoka na Zitto, kwani wanaeleza kwamba mawasiliano baina ya wawili hao yalianza kupamba moto tangu Agosti 6, 2010, siku moja baada ya Chadema kuzindua kampeni zake za urais.

Inaelezwa kwamba, kuanzia hapo hadi sasa, Zitto na Zoka wamekuwa na mawasilino ya mara kwa mara, na karibu kila siku huzungumza kwa simu. Mawasiliano mengine ya mara kwa mara yalifanyika tarehe Agosti 7, 2010, siku mbili tangu hotuba kali ya Jangwani na yalianza saa 10:17 na kuendelea tena saa 10:50, saa 10:51:31, saa 11:46:13, saa 12: 14:46, saa 12:26:48 na saa 13:50: 21.

Makala haya hayana haja ya kutaka kujua undani wa mazungumzo baina ya Zitto Kabwe na Rostam au Zitto na Zoka, na inaeleweka kwamba gazeti hilo limekuwa likifichua mambo mengi yanayoendelea kuhusiana na kiongozi huyo wa Chadema anayedaiwa kutaka kukisaliti chama.

Gazeti la MwanaHALISI halikuishia kufichua mawasiliano baina ya Zitto na Rostam na Zoka kwa njia ya simu tu, lakini pia limeweza kuchapisha mawasiliano ya Zitto kwa Rais Jakaya Kikwete na pia mawasiliano ya barua-pepe ya Zitto na watu wengine.

Kwa mfano, gazeti hilo lilichapisha mawasiliano ya Zitto kwenda kwa Rais Kikwete Aprili 25, 2009 akisema: "…ninaleta kwako ushauri ufuatao ili kumaliza suala hili kabisa bila ya kuathiri sura (image) ya nchi katika uwekezaji duniani na pia kuongeza ufanisi wa bandari. Kwanza, Serikali ikubaliane na TICTS kuondoa kipengele cha exclusivity (hodhi ya biashara) katika mkataba wake ili kuruhusu ushindani na hivyo kuongeza ufanisi; na zabuni ya kuendesha kitengo kingine cha makontena katika Berths 13 & 14 itangazwe kwa kufuata sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2004. Pili, Serikali itangaze rasmi kuwa nyongeza ya mkataba na TICTS itaendelea kwa sababu uwekezaji katika miundombinu ya bandari ni ya muda mrefu na hivyo mkataba wa mwanzo wa miaka 10 haukuwa na mantiki kiuwekezaji."

Inaelezwa kwamba, mapendekezo ya Zitto ya kutaka serikali isivunje mkataba, yanafanana na yale ambayo serikali ilitekeleza, pamoja na zogo kubwa kuibuka ndani na nje ya Bunge, na katika mawasiliano hayo, anaeleza kuwa kilichoandikwa ni siri kati yake na serikali na rais, lakini siku tatu baadaye, Zitto alipeleka nakala ya barua aliyompelekea rais, kwa mtendaji mkuu wa kampuni ya Vertex International Securities, Peter Machunde, Aprili 28, 2009 saa 3:45 asubuhi ikiwa na maneno, "This is for me and you only (Hii ni kwa ajili yako na mimi tu) ambayo nimepeleka kwa mkuu wa nchi."

Mbali na mawasiliano na baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi, Zitto amedaiwa kuwa na tabia ya kuwasiliana na baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari na kujiandikia habari huku wao wakitakiwa "kuzichapa kama zilivyo."

Kwa mujibu wa gazeti hilo, Zitto anatuhumiwa pia kuwa na mawasiliano ya karibu ya kikazi na binafsi, na Maria Kejo, mtumishi wa serikali katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), anayetuhumiwa na Chadema katika kashfa kadhaa nchini ikiwemo kutoa ushauri uliowezesha kufikiwa kwa makubaliano yaliyozaa mkataba wa kufua umeme wa Independent Power Tanzania Limited (IPTL).

Katika mawasiliano yake ya barua-pepe na Kejo ya Aprili 23, 2009, Zitto anamtumia Kejo mapendekezo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC) kuhusu mkataba kati ya serikali na IPTL, akisema: "…Pitia kisha ushauri katika mambo ya IPTL na Benki Kuu. Pia pengine popote utakapoona inafaa kushauri. Tunaisoma Jumatano na ni draft (rasimu) bado, but strictly confidential. Can come to your office (lakini hii ni siri kubwa, naweza kuja ofisini kwako kuzungumza)… Halafu sina hela mpenzi…"

Kwa hali ya kawaida tunaweza kulipongeza gazeti hili na waandishi wake kwamba wamefanya kazi kubwa ya uandishi wa kijasusi (investigative journalism), lakini ukichungulia kwa upande wa pili ambao ni mkubwa zaidi unaweza kubaini kwamba kuna walakini mahali fulani.

Kama nilivyosema hapo awali, hatuhitaji kujua walichozungumza Zitto na Rostam au Zoka, lakini kinachotisha ni hali hii ya mawasiliano ya faragha kuweza kuibuliwa na gazeti ambalo limeamua kufanya kazi ya ujasusi zaidi ya upashaji habari.

Nafahamu kwamba walikuwa wanajivunia Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Ibara ya 18(b) na Sheria ya Uhuru wa Maoni ya mwaka 1984 Na.15 ib. 6 na Sheria ya 2005 Na. 1 ib. 5, lakini ibara hiyo ya 18(c) inaonya kwamba kila mtu anao uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake.

Pia Sura ya Kwanza, Sehemu ya Tatu, Ibara ya 16(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, kuhusu Haki ya faragha na usalama wa mtu, kwa kuzingatia Sheria ya mwaka 1984 Na. 15 ib. 6, inaeleza bayana kwamba uhuru na faragha ya mtu haipaswi kuingiliwa.

Yawezekana mawasiliano baina ya Zitto na Rostam yalikuwa ya binafsi kabisa, na hata mawasiliano yake na Zoka yalikuwa ya binafsi pia, kwa sababu katika hali ya kawaida mtu yeyote anayo haki ya kuchagua rafiki amtakaye, siyo kuchaguliwa.

Ikumbukwe pia kwamba, pamoja na Zoka kuwa mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, bado ni binadamu wa kawaida aliye na uhuru wa kuwasiliana na watu wengine kwa masuala ambayo siyo ya kikazi, hivyo kumhukumu moja kwa moja na kuituhumu Idara hiyo kuwa inaihujumu Chadema tunaweza kuwa tunakosea.

Itakumbukwa kwamba, Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Willibrod Slaa alitajwa kwamba alikuwa akiwasiliana na maofisa wa TISS ambao inaelezwa ndio wanaompatia taarifa nyingi za ndani kiasi ch kushikwa na ‘kiburi' na kutamka bayana kwamba ataendelea kupokea taarifa kutoka huko na idara nyingine za serikali pamoja na Zoka kukaririwa akisema hao ni maofisa feki.

Taarifa hizo zinaelezwa ndizo zilizomfanya Dk. Slaa akatangaza kwamba TISS ilihusika na uchakachuaji wa matokeo ya kura. Sijasikia hata mara moja hili likitajwa kwa mapana kama Zitto kuwasiliana na Rais, maofisa wa serikali, TISS na Rostam. Au kwa vile taarifa alizopewa Dk. Slaa zilikuwa zinainufaisha Chadema?

Bado narudia kusema kuwa, silituhumu gazeti hili wala waandishi wake kwa kilichoripotiwa, lakini nahoji, ikiwa mawasiliano baina ya mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa yameweza kunaswa kirahisi kiasi hiki, hivi hali ya usalama wa Watanzania ikoje?

Kilichoandikwa ni kile kinachomhusu Zitto Kabwe na Chadema, lakini je, ni mambo mangapi ambayo gazeti hilo, waandishi wake ama wapasha habari wao wameyanasa yakiwa ni mazungumzo baina ya Zoka na watu wengine, hasa ikizingatiwa kwamba Zoka anafanya mawasiliano na watu wengi sana – ya kikazi na ya faragha?

Kama hata mawasiliano ya barua-pepe pia yameweza kunaswa, hivi tuseme nchi yetu iko salama kiasi gani ama Watanzania waendelee kuamini kwamba utandawazi umeboresha mawasiliano yanayowavua nguo hadharani?

Kwa tunavyoelewa, kilichofanywa na gazeti hili ni kuichunguza Idara ya Usalama wa Taifa na jinsi inavyowasiliana na watu mbalimbali, jambo ambalo nachelea kuliita kama ni uchochezi, jinai ama uhaini, kwa sababu ni mbinu za hatari za kijasusi tu zinazoweza kuchunguza idara nyingine, kitu ambacho, kama gazeti, halina mamlaka ya kisheria wala kikatiba kukifanya.

Wale wataalamu wa masuala ya kijasusi (espionage) wanaweza kulieleza hili kama ni counter-intelligence, yaani ujasusi wa kuwachunguza majasusi!

Vinginevyo, inafahamika kisheria kwamba, chombo chenye dhamana ya kupekua mawasiliano ya simu baina ya mtu na mtu, au kikundi ama kampuni ni Jeshi la Polisi hasa pale kunapokuwepo na kesi ya jinai, tena kwa kibali maalum.

Najaribu kuhoji, Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeridhia mtu yeyote kufanya ujasusi wa aina hii au ndiyo mwanzo mpya wa uhuru wa habari uliopitiliza? Kama leo hii Idara ya Usalama inaweza kuchunguzwa na watu wan je, na nyaraka za Rais zinaweza kunaswa na yeyote mahali popote, hivi tuamini kwamba usalama wetu uko imara?

Nadhani hapa kuna kitu ambacho kinahitaji majibu, tena ya haraka, vinginevyo wananchi wataendelea kutokuwa na imani na serikali ikiwa usalama wao uko mashakani kama hivi.

Ikiwa kuna matundu ndani ya Idara hiyo yanayovujisha siri hizi, ni vyema yakazibwa, kwa sababu mwelekeo wake ni mbaya kwa taifa. Yeyote anayefanya hivyo asidhani anamkomoa mwenzake au wenzake, bali atambue kwamba anautoboa mtumbwi ambao yeye pia yumo ndani yake, ukizama hakuna atakayebaki salama.

Nawasilisha.

CHANZO: DIRA YA MTANZANIA DESEMBA 20, 2010.

LETS EXPeRIENCE THIS LABDA VIONGOZI WETU WATASOMA UPEPO
 
Ukiwa kiongozi lazima uwe mwadilifu kuanzia nyumbani mpaka kazini.

Mi hawa watekaji wa mawasiliano siku za karibuni walini nyanyasa kweli kweli kila ninachofanya anatumiwa wife...kila mawasiliano yasiyo ya kikazi lazima yaforwadiwe kwa wife....ANYWAY NILICHOKIFANYA NI KUBADILI TABIA.
Therefore na wao wabadili tabia.

USALAMA WA TAIFA NI DHANA PANA HATA KUBENEA ANAWEZAKUA USALAMA VILE VILE SO TAKE CARE.
 
kwenye mawasiliano usalama wa taifa hapa bongo bado mdogo watu wanapeana kazi kindugu zaidi wengi hawana upeo, wa technologia hata walishindwa kujua ghalani ambaye yupo guatemala aliwasilianaje mpaka anatekeleza ujuma zidi ya marekani lakini marekani haikukuwa muda kuwapata. EPA Wizi wa makonteiner bandarini, upitishaji wa magari ya Bei juu kama Q7, BMW, Rang Sport kama marobota ya mitumba, madawa ya kulevya kuwa kituo kikuu tanzania, alafu utawakuta pale Breakpoint wanatanua mkinyanganyana madem wanakutolea bastola eti nyamaza wewe sie usalama wa taifa, Je usalama wa Taifa anasemaga, nchi nyingine ukisema kazi hii wanakuua kabisa
 
Asante sana kaka....Usalama wa taifa now uko hoi...vijana wadogo wasiojua hata sheria ya uanzishwaji wa usalama wa taifa ikoje....just coz we baba yako ni fulani njoo huku upige hela. nyambaaaaa.....fu
 
kwenye mawasiliano usalama wa taifa hapa bongo bado mdogo watu wanapeana kazi kindugu zaidi wengi hawana upeo, wa technologia hata walishindwa kujua ghalani ambaye yupo guatemala aliwasilianaje mpaka anatekeleza ujuma zidi ya marekani lakini marekani haikukuwa muda kuwapata. EPA Wizi wa makonteiner bandarini, upitishaji wa magari ya Bei juu kama Q7, BMW, Rang Sport kama marobota ya mitumba, madawa ya kulevya kuwa kituo kikuu tanzania, alafu utawakuta pale Breakpoint wanatanua mkinyanganyana madem wanakutolea bastola eti nyamaza wewe sie usalama wa taifa, Je usalama wa Taifa anasemaga, nchi nyingine ukisema kazi hii wanakuua kabisa
Unayosema ni kweli kabisa, zamani ilikuwa ni vigumu hata mke kujua kama Mume ni afisa usalama wa Taifa, lakini sikuhizi vijana wanaona ni ujiko kufahamika. Sijui kama wanapewa orientation hata japo kwa wiki moja kwa kweli. It is such a shame
 
kUNA LIJAMAA TULIKUWA TUNAKULA NALO BIA SINZA HONGERA BAA, LINATUAMBIA HALAFU LINAONESHA NA LIKITAMBILISHO LAKE JEKUNDU.
YAANI NI UPUPU MTUPU.
 
utakufa masikini na ukada(utumwa) wako kwa ccm huku mabosi wako wakizidi kutajirika kifisadi. umbeya tu...thread iko kinafiki zaidi
 
Back
Top Bottom