Usalama wa Walaji wa Kuku wanaokuzwa kwa WIKI 3 tumemkabidhi nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usalama wa Walaji wa Kuku wanaokuzwa kwa WIKI 3 tumemkabidhi nani?

Discussion in 'JF Doctor' started by kichwat, Oct 3, 2011.

 1. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Ndugu wana JF.

  Nimebahatika kuongea na wafugaji watatu wa kuku wa nyama wa kisasa (broilers) hivi karibuni. Nimegundua kuwa siku hizi kuku wa nyama wanakuzwa kwa wiki tatu (3) hadi (4) tu. Madai yao ni kwamba wanafanya hivyo ili kupunguza gharama na kuweza kushindana sokoni.
  Mbinu zinazotumika ni kutumia MADAWA mbalimbali mbayo hayakutengenezwa kwa kusudi hilo.

  Tatito langu ni moja tu: Kama kwa upande wa nyama ya ng'ombe kuna mabwana nyama wanaokagua nyama kule machinjioni, je hawa VIFARANGA WA MADAWA ni jukumu la nani? manake ni vigumu kukagua chipsi-kuku.

  Na ndio maana tatizo la hormone imbalance kwa watoto limeongezeka. Wanaotakiwa kuwa na testosterone (male) wanaibuka na oestrogen (female) & vice versa. Achilia mbali kansa na balaa nyingine.

  Nionanvyo kuna JANGA linatunyemelea kama Watanzania tukiendelea na IGNORANCE YA KUTISHA katika kila jambo. Kiukweli tunauana wenyewe kwa wenyewe sababu ya fedha. Lakini naamini tunaweza kuepuka.

  Nawasilisha.
   
 2. Jeji

  Jeji JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  ndio maana siku hizi maradhi ni mengi sana.
   
 3. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,331
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  hata wazungu hula vyakula artificial kama hivi.
   
 4. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  kwa hiyo tule sababu wazungu wanakula?
   
 5. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  ..kwamba eti hata wazungu wanakula kama sisi nakataa. Wenzetu wako makini na viwango vya ubora. hakuna kiunachoingia sokoni bila TFDA zao kuchunguza sampuli. Halafu mfumo wao ni wa supermarkets na masoko/maduka maalum (kama machinjioni au ferry za hapa kwetu). Hakuna masoko ya mtu mmoja mmoja.
   
 6. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #6
  Oct 3, 2011
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Mara zote binadamu wanauwa binadamu wenzao ama kwa kujuwa au kwa kutokujuwa, lakini chanzo cha yote ni FEDHA. Mpaka hapo binadamu atakapothaminiwa zaidi kuliko fedha ndiyo itakuwa mwisho wa binadamu kuuguwa. lakini hao wenyewe wanaoangamia kwa kukosa maarifa ni wabishi!. Siyo kuku tu, tunalishwa sumu katika vyakula na vinywaji vingi tutumiavyo siku hizi kwa sababu tu ya fedha mwanahalamu. Tukitaka tunaweza. Ubinadamu kwanza: Utangulizi | maajabu ya maji
   
 7. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #7
  Oct 3, 2011
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  chakula chao, malazi yao, usafiri wao, kazi zao, hospitali zao na maisha yao tu kwa ujumla ni tofauti sana na sisi. hata hivyo wapo wazungu wengi tu wanatamani maisha ya asili kama ambavyo bado kidogo yanapatikana afrika hasa kwa upande wa vyakula, mi nimepika hotelini nalijuwa hilo vizuri.
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Oct 3, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hili kweli ni janga.....wiki 3 si kifaranga hicho?
   
 9. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #9
  Oct 4, 2011
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Nilishawahi kusikia kuwa siku hizi vinakuzwa kwa madawa mbalimbali yakkeiwemo ARV's.
   
 10. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #10
  Oct 4, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  very true. pamoja na vidonge vya NYOTA YA KIJANI na VIAGRA.
   
 11. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,331
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  au mkuu tuwe wanaharakati wa afya na tuanzie hapa JF kuwaelimisha watu na zaidi tuanzisha ka NGO ketu ili tuombe fedha za kuendeshea semina elekezi kwa kada mbalimbali hasa walezi?
   
 12. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,331
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  kumbe ulisikia, peleleza mkuu ili uwe na uhakika na hiyo taarifa. maana kuna hatari nawewe ukaendelea kuwaambia watu wengine habari usiyo na uhakika
   
 13. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2011
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  uhakika sina kwa sababu mimi si mfugaji wa hao kuku. Ila taarifa hii ya kuwa hao kuku wanalishwa hizo dawa sio ngeni ni kitu kilichoripotiwa hata kwenye vyombo vya habari nafikiri kama kumbukumbu iko vyema tukio hilii lililipotiwa kutokea huko mbea kati ya mwaka jana fatilia.

  Pendeleeni kujifugia wenyewe kuku wa kienyeji au kula kuku wa kienyeji. hivi vitu vinavyoitwa vya kisasa ni bora kuviogopa kama sio taratibu basi kwa haraka maana vingi ni pirate siku hizi ubinadamu nyuma pesa mbele mtu hajali afya ya mwingine na wala hawamwogopi Mungu. mtu anafanya kwa makusudi mazima akijua mimi sili ila nawalisha wengine mimi nipate pesa yatakayojiri baada ya kula watajiju. Hiyo ndio dunia ya sasa.
   
Loading...