Usalama Wa Taifa Z'bar Ndiyo Mawakala Wa Tume Ya Uchaguzi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usalama Wa Taifa Z'bar Ndiyo Mawakala Wa Tume Ya Uchaguzi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Junius, Jul 17, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Taarifa kwa vyombo vya habari 14 Julai, 2009
  Chama cha Wananchi (CUF) kimefadhaishwa sana na taarifa kwamba maafisa wa Usalama wa Taifa wilaya ya Micheweni, wamekuwa wakiingilia utendaji wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kwa kuwafukuza wananchi wanaokwenda kujiandikisha katika vituo vya kupiga kura, kama ilivyoripotiwa kwenye magazeti ya leo ya Mwananchi na Nipashe.
  Tukio hili sio tu kwamba linathibitisha ile kauli ya muda mrefu ya CUF kwamba ZEC inaendesha uchaguzi kwa kufuata maagizo ya Idara ya Usalama wa Taifa, bali pia linapigilia misumari mingine kwenye jeneza la kuizikia demokrasia Zanzibar. Kila mara tumekuwa tukisema kwamba vyombo vya dola ndivyo hasa vinavyosimamia na kuendesha uchaguzi wowote unaofanyika Zanzibar, huku ZEC ikiwa kama ni alama tu ya kuwepo kwa chombo huru kinachoendesha shughuli za uchaguzi. Taarifa zilizokusanywa na waandishi katika vituo vya Wingwi Mapofu, Mgogoni na Kinyasini, zinaonesha kwamba vyombo hivyo vya dola vimekuwa vikishiriki kikamilifu katika kutoa maelekezo ya nini kifanyike katika vituo vya uandikishaji wapiga kura ikiwemo hata kuwazuia masheha wasiongee na waandishi wa habari ambao huwa wanataka kujua usahihi wa madai yanayotolewa dhidi yao.
  Itakumbukwa kwamba Usalama wa Taifa ni miongoni mwa mambo ya Muungano na, kwa hivyo, ni idara inayosimamiwa moja kwa moja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Kwa mantiki hiyo, hakuna namna yoyote ambayo Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wanaweza kujivua na lawama za kuchafuliwa kwa uchaguzi wa Zanzibar, maana inaonesha wazi kwamba ama wanaridhia utendaji wa vyombo vilivyo chini ya mamlaka yao Zanzibar au hawajali kile kinachofanywa na vyombo hivyo. Lolote kati ya hayo mawili linamaanisha kwamba wao ndio wanaopaswa kubeba dhamana na lawama za hali ya juu katika jambo hili.
  Sisi, CUF, tunachukua fursa hii tena na tena kuwakumbusha viongozi wetu hawa wawili kwamba wao ndio wenye jukumu la kulinda usalama na haki zote za kikatiba za wananchi wa Tanzania. Kisingizio kwamba Zanzibar ina sheria zake za uchaguzi hakitoshi kuviachia vyombo vilivyo chini ya mamlaka yao kuvunja haki za wananchi wa nchi hii. Hakitoshi pia kudharau ukweli kwamba uchaguzi wa Zanzibar unavurugwa na vyombo vile vile ambavyo vilitarajiwa kuusimamia. Hili la kuwanyima wananchi haki ya kuandikishwa na kuweka vyombo vya dola kuhakikisha kuwa haki hiyo haipatikani ni katika mifano halisi.
  Wakati tunathamini nafasi ya vyombo vya dola, ikiwemo Idara ya Usalama wa Taifa, katika kuifanya nchi yetu iwe katika amani, umoja na mshikamano, hatukubaliani kabisa na dhana kwamba jukumu la Idara hiyo ni kuhakikisha kuwa wananchi wenye mawazo tafauti ya kisiasa na watawala hawana haki katika nchi yao na kwamba lazima wadhibitiwe kwa namna yoyote ile, ikiwemo hii ya kuwafukuza kwenye vituo vya kujiandikisha kupiga kura.

  Pamoja na salamu za Chama.

  Imetolewa na:
  Salim Bimani,
  Mkurugenzi wa Uenezi na Mahusiano na Umma,
  CUF
  Simu: +255 777 414 112
  E-mail: cufhabari@yahoo.co.uk
  Weblog: Haki Sawa kwa Wote
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Muda mrefu imekuwa ikisemwa na sasa nazidi kusadiki kuwa SMT katka msaada mkubwa inayoipatia Zanzibar ni kuhujumu mustakabali wa maendeleo yake ikiwemo ya demokarasia ya uchaguzi. Sioni sababu ya Idara ya Usalama wa Taifa ijiingize moja kwa moja katka zoezi la uandikishaji na kuwazuia watendaji kufanya majukumu yao kwa uhuru, wala sioni kwanini nisipate mashaka na wasiwasi wa uadilifu wa serikali ya Muungano kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani, kutumia vyombo vyake kukandamiza demokrsia zanzibar. Sasa nikiunganisha nukta napata mstari kamili wa nini kinafanyika katika zoezi hilo la uandikishaji kupitia usalama wa taifa na nini kitafanyika katka uchaguzi mkuu wa 2010 kwa mamia ya askari wanaotarajiwa kupelekwa huko.
   
 3. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Wasipowahusisha ''vijana wa kazi'' sisiemu itakuwa haishindi bwana!

  NB:JInius am counting three posts to reach 1000+!am waiting men!i will post a special conngrats post for you!
   
 4. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi unataka kueleza nini? Ndugu yangu!!!!. Watu wasilindwe? Huitaki amani wewe? sasa kama kunaonekana dalili za kuvunjika kwa amani na kufanywa fujo na vitimbakwiri kwanini watu wenye dhamana ya kulinda amani yetu wasitekeleze wajibu wao? Acha ushabiki huo !!! Amani ni muhimu kwako wewe na jamaa zako- kule.
   
 5. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Pakacha :umejiuba au Umeubwa ?kuna wale ambao walifika wakajita wao ni waungu,endelea hivyo hivyo sio wewe ni uwezo wa aliyekupa nguvu za kupumuwa .
   
 6. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Pakacha huenda akafa kibudu ,maana ana macho lakini haoni,ana akili lakini hafahamu ,ana masikio lakini hasikii ,anajifanya kipofu,ana jifanya too mucha know ,anajifanya kiziwi ,ni mtu ambae stage aliyofikia ni ile ya jambo la kweli akalifanya la uongo na la uongo akalifanya la kweli ,sasa hapa hatumwambii aseme ukweli ila tunamzindua tu, kama anayafanya hayo kwa kuwafurahisha wachache na kuudhalilisha umma wa WaPemba ,aendelee wala hakuna wa kumzuia .labda wa kumtanabahisha tu ,maana katika dini yangu na yetu kwa wengine tumeambiwa tukumbushane kwani ukumbusho una faida yake.
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  Jul 18, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Pakacha uko kazini ama ? Maana hii si statement ya mtu mwenye akili zake , mzalendo na anapenda Tanzania
   
 8. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #8
  Jul 18, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kwani kulikuwa kuna fujo au hali yoyote ya uvunjifu wa amani? Kwanini Usalama wa taifa wawe mbele kuwapa maelekezo watendaji wa tume as if hawana muongozo wwote? kwanini wawazuie kuzungumza na waandishi wa habari na kwanini wawafukuze watu wanaokwenda kujiandikisha? kama hawana vitambulisho vya ukaazi hilo si jukumu la tume ya uchaguzi kuwaelekeza pa kuvipata kwa kuwa ni sehemu ya utaratibu wao. hapa wanalinda nini na nani kwa maslahi yepi?
  Pakacha,mbinu hizi za usalama wa taifa ni za kitoto na wanachoitafutia Zanzibar hawawezi ku-imagine kwa saivi lakini mti na macho!!!
   
 9. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #9
  Jul 18, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Na ulinzi huo ufanywe na maofisa wa usalama wa taifa?

  Na polisi na FFU kazi yao itakuwa nini?

  Na kwanini amani ivunjike kama watu watapewa haki yao bila ya mizengwe?

  Omarilyas
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Jul 18, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Bila shaka wewe umetumwa.
  Kama hujatumwa basi unatekeleza majukumu yako ya payroll za watu flani flani ambao wanaona kuruhusu demokrasia ni kuruhusu machafuko nchini unanifanya na kunilazimisha niamini hivyo.
   
 11. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #11
  Jul 18, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  CUF, hasa huko PBA wana tabia ya kuiba kura, hivyo kuwepo kwa UWT ni vizuri ili kuzuia wizi wa kura 2010
   
 12. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #12
  Jul 18, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kibunango,
  CUF hawahitaji hata kufanya mkutano mmoja wa kampeni kuwashawishi wapemba wawachaguwe. Lakini CCM na wafanye mikutano 1000 huko, hakuna mwenye haja nayo. Sasa CUF wanahaja gani kuiba kura eneo ambalo mtoto akizaliwa baada ya kuadhiniwa tu anasomewe manifesto ya CUF? Wanaoiba kura ndo hao wanaojaza usalama wa taifa na vikosi vya askari chungu nzima.
   
 13. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #13
  Jul 18, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Safari hii twende na Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi. Wale shemegi zenu wa kisukuma na kidigo hawatakwenda tena Chanja-njawiri kupiga kura. Tuone Wapemba wale wakaazi wa Chanja -njawiri hawaipi CCM?
   
 14. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #14
  Jul 18, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Pakacha, SMZ watawapumbaza wengine siyo akina sisi tuliozaliwa huko tukaasi, kuna mpango kabambe unafanywa na SMZ&CCM wa kuwagawia mamluki vitambulisho vya ukaazi ili waandikishwe katika daftari, hii inakwenda sambamba na kuwanyima wale wote wanahisiwa tu kuwa ni wafuasi wa vyama vya upinzani hasa CUF. Kwa hiyo, bado mambo ni yale yale kama chaguzi zilizopita CCM haipo tayari kushindwa kwa kura. Lakini mara hii...hadithi itakuwa nyengine...tusubiri tuone.
   
Loading...