Usalama wa Taifa wamshukuru Zitto

Status
Not open for further replies.

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Kwa mara ya kwanza baadhi ya maafisa wa Usalama wa Taifa wamepokea kwa furaha hotuba ya Mhe. Zitto kuhusu idara hiyo wakiamini kuwa hatimaye na wenyewe wamepata msemaji Bungeni. Vyanzo vya kuaminika vinasema kuwa watumishi wa idara hiyo ambao walikuwa wanafuatilia kwa ukaribu atakachosema Zitto wamepata ahueni kuwa hotuba ya Zitto ililenga kuboresha idara hiyo na hivyo baadhi yao wakasikika wakisema wamepata mtu wa "kuwasemea".

Nakala ambayo Zitto ameiweka hapa imeanza kusambazwa miongoni mwa watumishi mbalimbali wa idara za usalama. Sasa hivi wanasubiri majibu ya serikali kuhusu maangalizi ya Zitto kuhusu Idara hiyo na kama serikali itatambua uzito wa suala hili na kulifanyia kazi.
 
Kama Wanaweza Kuona Na Kuanza Kutoa Pongezi Basi Wajue Kuwa Kazi Yao Ni Kulinda Nchi Na Sio Yeyote Kwani Hii Ni Chanagamoto Kwao Kuwa Wanatakiwa Wawalinde Watanzania Na Hata Kukuza Uchumi Wa Nchi.

Naona Huenda Pakawa Na Mabadiliko Kwani Baadhi Yao Kila Ukikutana Nao Wanakuwa Wanalalamika Kuwa Sheria Yao Wanayofanyia Kazi Imepitwa Na Wakati ,huu Ni Wakati Wa Kubadilisha Sheria Ili Waeze Kupambana Na Mafisadi Moja Kwa Moja .
 
Ili kutuonyesha (waTanzania) kwamba walikuwa wanapiga mzigo kweli kweli basi watueleze Richmond ni nani!!
 
Kama ni kweli wamepongezwa wafanye kazi kweli na siyo 'Kubalali' na 'kuwakolimba' watu.Wasijifanye trained assassins eliminating people.Washiriki kwenye ujenzi wa taifa hili kwa kuumbua machafu yote yanayokazaniwa kufichwa na viongozi wachafu siyo kila siku kujiongezea bajeti wakati wanalofanya hatulijui wala kulifahamu.
 
Kwa mara ya kwanza baadhi ya maafisa wa Usalama wa Taifa wamepokea kwa furaha hotuba ya Mhe. Zitto kuhusu idara hiyo wakiamini kuwa hatimaye na wenyewe wamepata msemaji Bungeni. Vyanzo vya kuaminika vinasema kuwa watumishi wa idara hiyo ambao walikuwa wanafuatilia kwa ukaribu atakachosema Zitto wamepata ahueni kuwa hotuba ya Zitto ililenga kuboresha idara hiyo na hivyo baadhi yao wakasikika wakisema wamepata mtu wa "kuwasemea".

Nakala ambayo Zitto ameiweka hapa imeanza kusambazwa miongoni mwa watumishi mbalimbali wa idara za usalama. Sasa hivi wanasubiri majibu ya serikali kuhusu maangalizi ya Zitto kuhusu Idara hiyo na kama serikali itatambua uzito wa suala hili na kulifanyia kazi.

Mkuu ningependa kuiona hotuba ya Zitto, iko sehemu gani?
 
Ni hatua nzuri.
Hao wanausalama wazalendo wakamate wale ambao ni wanausalama MAFISADI ili ku cut off the infected part..HEAL THE NATION...AND MOVE FORWARD.
 
Ni hatua nzuri.
Hao wanausalama wazalendo wakamate wale ambao ni wanausalama MAFISADI ili ku cut off the infected part..HEAL THE NATION...AND MOVE FORWARD.

Lol....inategemea hao mafisadi wamejikita vipi na wapi...Ndio maana tunataka overhaul kuanzia chini hadi juu, kubadilisha sheria na vitu kama hivyo.
 
True...Kauli TATA SANA.

WANAUSALAMA HAWATAKI SIRI ZA UASALAMA ZIJADILIWE BUNGENI...and then sasa...WANAUSALAMA WAMSHUKURU ZITTO KWA KUWASEMEA BUNGENI.

TUNATAKA....WANANCHI WAMSHUKURU ZITTO BUNGENI NA OFCOURSE WANAUSALAMA WASIOKUWA MAFISADI NAO PIA WAMSHUKURU ZITTO.

Kwa sababu ya hayo hapo juu...Na conclude hivi...Kuwa WANAUSALAMA WAMEGAWANYIKA.

WALE WANAUSALAMA WANAOTAKA TUJUE UKWELI VS WALE WANAODAI KUWA NI SIRI YA JESHI KAMA KAYAANZA MIZWENGWE MPINDA HAKI.

WE WANT THE THRUTH.

WE WANT THE PATRIOTS TO BE VICTORIOUS.

AND YES WE WILL!

"WE"....."WE THE PEOPLE!"

WE WILL BE VICTORIOUS....GOD WILLING!
 
Mmkjj Ni kweli? labda? maana wengi wa hawa wana usalama mbona ni marafiki na watoto wa hao hao wana usalama? ajira wanazipata vipi? hiyo recruitment yao si ya kifisadi? sasa wanaweza kufurahia mabadiliko hayo?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom