Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,399
- 39,550
Kwa mara ya kwanza baadhi ya maafisa wa Usalama wa Taifa wamepokea kwa furaha hotuba ya Mhe. Zitto kuhusu idara hiyo wakiamini kuwa hatimaye na wenyewe wamepata msemaji Bungeni. Vyanzo vya kuaminika vinasema kuwa watumishi wa idara hiyo ambao walikuwa wanafuatilia kwa ukaribu atakachosema Zitto wamepata ahueni kuwa hotuba ya Zitto ililenga kuboresha idara hiyo na hivyo baadhi yao wakasikika wakisema wamepata mtu wa "kuwasemea".
Nakala ambayo Zitto ameiweka hapa imeanza kusambazwa miongoni mwa watumishi mbalimbali wa idara za usalama. Sasa hivi wanasubiri majibu ya serikali kuhusu maangalizi ya Zitto kuhusu Idara hiyo na kama serikali itatambua uzito wa suala hili na kulifanyia kazi.