Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

Status
Not open for further replies.
hata hao waliotoa hzo fedha kwa ajili ya kupata kazi nao ni wahalifu,kwa muono wng hakuna kesi hapo kwani hawatakuwa na ujasiri wa kutoa ushahidi mahakamani
 
Kigogo,mke wa kigogo,mtoto wa kigogo ndio nini.?? Ina maana hata mahakamani watapelekwa kwa majina hayohayo.!!

...ASANTE. Hapo ndipo ninapoamini kuwa baadhi ya Magazeti ni Dugu Moja na Mafisadi! Wanaona Tatizo gani kutaja majina ya Hao Wahusika wengine?? Mbona jina la huyo Baraka wanalitaja haraka haraka? Huyo Mtoto na Mama yake Mbona Hawawataji kwa Majina? Kwa sababu wana Connection na Vigogo?? Kweli Bongo Hakuna Vyombo Vya Habari wala Waandishi wa Habari! Wote ni Waganga Njaa Tu!
:angry::A S angry:
 
Tanzania kila kitu kinawezekana nchi haina mwenyewe, pamoja na wengi kusoma taarifa hii, mwingine kesho aanzishe utapeli wa ajira katika taasisi kama BOT, TRA n.k watu watatoa tu pesa. Kwa hiyo wajinga ndio waliwao.
 
MBONA KIGOGO HUYO WA POLISI ANAJULIKANA NI CHAGONJA NA MKEWE NDIYE MTUHUMIWA. KUNA UZI ULISHATOLEWA HAPA KWAMBA MKEWE HUYU NI RAIA WA RWANDA NA AMEINGIZA RAIA WENGI WA RWANDA KWENYE JESHI LA POLISI. MMOJAWAPO YUPO KWENYE BAND YA CHUO CHA POLISI MOSHI ANAITWA VERONIKA, WENGINE WAKO MIKOANI WANAFANYA KAZI ZA POLISI TANZANIA. HUYO MWANAMKE NI TAPELI KWELIKWELI HATA POLISI WENYEWE WAMEMGWAYA. KIONGOZI WAO HUYO CHAGOJA AMELIAIBISHA JESHI LA POLISI NA AMEONYESHA NI JINSI GANI HAO ASKARI WALIVYO. KITENDO CHAKE CHA KUDAI KUWA MKEWE NAYE ALITAPELIWA NA AKAKAA KIMYA HADI TUHUMA HIZO ZILIPOIBULIWA NA WENGINE KINAONYESHA NI JINSI GANI ALIVYO NA UPEO MDOGO WA KUFIKIRI HATA KUTOA WASIWASI WA JINSI AMBAVYO ALIPEWA HIYO NAFASI. NIMEAMINI KUWA SERIKALI YETU HII NI DHAIFU. KWA UPANDE MWINGINE NI KUWA KUSEMA KUWA MKEWE PIA KATAPELIWA NI KUTAKA KUMFANYA MKEWE NAYE AWE SHAHID KATIKA HILO SAKATA BADALA YA KUWA MTUHUMIWA HALISI HUO NAONA NI UTOTO NA UFINYU WA KUFIKIRI WA KIGOGO HUYU. UTAKUMBUKA HATA KAULI YAKE SIKU MWANDISHI ALIPOUWAWA KULE IRINGA YEYE AKAKIMBILIA KUTOA TAMKO KUWA ALIRUSHIWA KITU KUTOKA KWENYE KUNDI LA WANANCHI NA ALIKIMBILIA KWA POLISI KOMBA MSAADA. KAULI HIYO NA NYINGINE NYINGI PAMOJA NA HII YA KWAMBA MKEWE KATAPELIWA NI USHAHIDI TOSHA KUWA KIONGOZI HUYU NI DHAIFU NA NDIYE AMBAYE NAHISI ANALIFANYA JESHI LA POLISI LIWA PIA DHAIFU.:flypig::flypig:[/QUOT]

Mkuu kwenye rangi umeongea kiume. Cha kuongezea tu, Hivi hakuna shughuli za kijasusi kati ya Rwanda na Tanzania? Huyu mwanamke hawewezi kutumiwa katika shughuli hiyo na huko anakotoka kwani kipindi cha Cold War mabosi wengi wa kimarekani walikuwa wananasa au kukaribia kunasa kwa majasusi warembo wa Urusi kwa njia ya kimahusiano. Huku ni kuhatarisha taifa jamani. Wapenzi na wake wa hawa wanoitwa vigogo sijui magogo wawe wanachunguzwa sana na serikali mapema na kutahadahrishwa wahusika kwani wakiaachwa tu, mapenzi ni upofu bila kujali umri, cheo, rangi n.k na hii hupelekea shida kukabiliana nao na wake zao katika hatua hizi. Mtu asipokuwa makini, mapenzi hupunguza hata ufanisi katika kazi ikiwemo kumtetea mke/mpenzi wako kwa lolote ikiwa ni utekelezaji wa ahadi motomoto wanazopeana chumbani. Kwa ujumla, hii ndo kazi ya UWT.
 
Kwa hiyo huyo mheshimiwa sana Kamanda wa Polisi alijua mchezo mzima wa hao kina Baraka,ikiwamo kuomba rushwa wafanikishe vijana kuajiriwa,lakini bado alitoa ruhusa kwa mkewe kuendelea na huo mpango?

Kama ni hivyo basi nchi hii itazinduliwa na kiama! Kamanda wa Polisi anashiriki kutoa rushwa,Kamanda wa Polisi haamini katika haki bali pesa mbele,Kamanda wa Polisi hajiongezi na kutaka kufatilia kwa nini ajira kwa pesa,kamanda wa Polisi anakaa kimya ili watu wake wafaidike, kamanda wa Polisi.
Kumbe ndio mchezo unaofanywa na hao vigogo: wanapeana kazi tu, huo kigogo ana akili kweli!!! mpaka ana diriki kusema alishaandaa 1.5milioni ili mke wa mdogo wake sijui mwanae pamoja na wifi yake wote wajiunge na Usalama wa Taifa!!! Aisee; hivi ni kwanini hizi nafasi huwa azitangazwi kama ilivyo ada kwenye kada nyinginezo?????
 
Mi mwenyewe nilipigwa 20000/=tu nyingine niliwaambia kwamba mpaka nione wamefikia wapi ikawa sanaa na mimi hela ya kuunga unga mpaka leo naona sanaa tu kumbe tuko wengi tuanzishe chama cha waliotapeliwa

Tutajie basi, ni genge gani hilo lililokutapeli?
 
usalama wa taifa! mali za watanzania kutoroshwa/kuibwa na wajanja wachache haiusu usalama wa taifa? mauaji yanayoendelea ktk mikutano ya siasa hayahusu usalama wa taifa? vizuri wamehamushwa usingizini!
 
Kwa mambo yanavyoendeshwa hapa bongo nchi zingine wana doubt hivi watanzania ni timamu au tumerogwa..hayavumiliki kwa mtu aliyetimamu
 
sasa hao vijana nao duh... hawakuchukua hata muda kidogo kujifunza ajira za usalama wa taifa zinapatikana vipi? kadizooo!!!

mkuu Mzee MwnKJ si kila siku tunaambiana kuwa wapo watu wanakula shavu kwa staili hizi?nao ndio wakajua kuwa itakuwa hivyohivyo.The issue katk deal haramu hakuna njia sahihi ya ku verify dealer.Na dealer wa leo kesho anaweza kuwa link yake imekatika kesho.

Kuna shule Mhaya mmoja aliwahi wapanga wahaya kibao akachukua hela zao za ada na rushwa akawaambia wakija ni kuingia shule tuu.Siku ya shule mhaya akawa amekula kona na hela zote.Kumbe jamaa alikuwa na moto enzi zile Moto haukuwa na matumaini ya kuua wengine kama leo,so alipiga issue ya kumtohs kusumia siku kipindi kigumu kikikaribia.
 
Kumbe ndio mchezo unaofanywa na hao vigogo: wanapeana kazi tu, huo kigogo ana akili kweli!!! mpaka ana diriki kusema alishaandaa 1.5milioni ili mke wa mdogo wake sijui mwanae pamoja na wifi yake wote wajiunge na Usalama wa Taifa!!! Aisee; hivi ni kwanini hizi nafasi huwa azitangazwi kama ilivyo ada kwenye kada nyinginezo?????

Yet tutegemee kweli kuwa salama chini ya watu wa jinsi hiyo? Juzi niliwasifia sijui walionisaidia ni wale wachache wa zamani ambapo kweli tulijisikia salama? Ndiyo maana walipojifanya wezi nyumbani kwangu hata ku-act as thieves walishindwa mpaka mm ambaye siyo jasusi nikaweza kugundua walinitembelea..Lord have mercy on us!
 
bot_tabimg.gif

Tuesday, 18 September 2012 19:54


othuman-usalama.jpg



Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa,Othman Rashid

NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI, MKURUGENZI AMTAKA IGP KUCHUKUA HATUA, MTUHUMIWA AJITETEA

Waandishi Wetu

SAKATA la mke wa kigogo wa polisi kudaiwa kuwatapeli vijana 120 kwa kuwachangisha zaidi ya Sh100 milioni ili awatafutie kazi Idara ya Usalama wa Taifa na Takukuru limechukua sura mpya, baada ya Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Othman Rashid kuwataka polisi wamkamate na kumchukulia hatua za kisheria mwanamke huyo.
Utapeli huo wa aina yake, unadaiwa kufanywa na mama huyo kwa kushirikiana na mwanaye (majina tunayo). Pia yumo kijana anayejulikana zaidi kwa jina moja la Baraka ambaye kwenye mpango huo, anajitambulisha kuwa anafanya kazi Ikulu.

Akizungumza na mwandishi wetu Dar es Salaam juzi, Rashid alisema tayari amewasiliana na Mkuu wa Polisi, IGP Said Mwema kuhusu tuhuma hizo ili kujua hatua zilizochukuliwa dhidi yake.

“Nimewasiliana na IGP Mwema ili aweze kunipa ufafanuzi kuhusu mke wa kigogo huyo, lakini nashukuru amenipa ushirikiano na kuniambia kuwa suala hilo wanalishughulikia kisheria zaidi. Watanipa taarifa pindi watakapokuwa wamekamilisha,” alisema Rashid.

Alisema huo ni mfano tu wa baadhi ya watu wanaotumia jina la Usalama wa Taifa kufanya utapeli na kwamba tabia hiyo tayari imewaingiza baadhi ya watu matatani baada ya kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria na wengine bado wanatafutwa.

Alisema sheria ni msumeno, hivyo ikibainika mwanamke huyo alijihusisha kutapeli kwa kutimia jina la Usalama wa Taifa, hatua kali zitachukuliwa dhidi yake ili iwe fundisho kwa wengine ambao wanatumia majina ya waume zao kutapeli watu.

Rashid alisema bado ana imani kwamba polisi itamchukulia hatua za kisheria mwanamke huyo ikiwa itathibitika kwamba amejihusisha na utapeli kwa kuwa jeshi hilo lipo kulinda usalama wa raia na mali zao.

Azungumzia tuhuma
Akizungumzia madai hayo jana kigogo huyo wa polisi ambaye mkewe ndiye anayetuhumiwa (jina tunalihifadhi), alisema tangu mwanzo
alielewa kwamba anayezungumziwa ni mkewe, lakini akakanusha kuhusika katika utapeli huo.

Alisema kutokana na taarifa ambazo zimekuwa zikiandikwa katika gazeti hili na kumtaja Baraka, vijana wengi waliotapeliwa kutoka mikoa mbalimbali walifunguka akili zao na kubaini kuwa aliyetajwa katika habari ndiye aliyekuwa akichukua fedha kwao.

“Jambo linalonisikitisha ni kwamba, aliyewaletea taarifa hizo za uongo zinazomhusisha mke wangu na utapeli huu ndiye tapeli aliyekuwa akizunguka mikoa mingi nchini kutapeli watu. Hata mke wangu ni mmoja wa waliotapeliwa. Alikusudia kuwapeleka wanafamilia watatu akiwemo mtoto wake, mke wa kaka yake na wifi yake ambaye tunamlea,” alisema.

Alisema mkewe alitoa fedha taslimu zisizopungua Sh1.5 milioni, mbali na gharama za kununua bidhaa na vifaa mbalimbali ambavyo wanafamilia hao wangetakiwa kwenda navyo mafunzoni.

Alisema walishtuka kuwapo dalili za utapeli baada ya watu waliokuwa wakidai kushughulikia ‘mipango’ hiyo kuanza kutoa ahadi zisizotekelezwa, huku wakati mwingine simu zao zikipatikana kwa nadra.

Alipotakiwa kuwataja kwa majina waliokuwa wakishughulikia mipango, ambao walichukua fedha kutoka kwa mkewe kigogo huyo alisema hakumbuki vizuri majina yao. Hata hivyo, alisema mmoja wao anaitwa Baraka.

Mke wa kigogo huyo alikataa kuzungumzia tuhuma hizo akisema: “Hayo yote yapo kwa wakubwa, mimi siwezi kuongelea kitu kilicho ngazi za juu yangu.”

Alipoambiwa kuwa mwandishi wetu amezungumza na mumewe ambaye ameeleza kuwa mama huyo naye ni miongoni mwa waathirika katika utapeli huo, hivyo atoe ufafanuzi alikataa pia kuzungumzia hilo na kukata simu.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah alipotakiwa kuzungumzia tuhuma hizo alisema: “Kwa sasa niko huku Maputo (Msumbiji), siwezi kuzungumzia suala hilo lakini nikirudi nitafutane nitatoa ufafanuzi.”

Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai wa Polisi (DCI), Robert Manumba hakutaka kuzungumzia tuhuma hizo akielekeza atafutwe msemaji wa polisi ambaye simu yake haikupatikana kutwa nzima jana.

Ilivyokuwa
Wiki iliyopita gazeti hili liliripoti habari kuhusu mke wa kigogo kuwatapeli vijana 120 kwa ahadi ya kuwapa ajira katika Idara ya Usalama wa Taifa na Takukuru.

Kati ya Agosti 5 na 7, mwaka huu vijana hao 120 kwa nyakati tofauti walipata taarifa kwamba kuna nafasi za kazi Idara ya Usalama wa Taifa na Takukuru na kwamba nafasi hizo zinapatikana kupitia kwa vigogo wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini.

Kwa kupitia kwa mtoto wa mwanamke huyo na kupewa taarifa na rafiki zao, inadaiwa kwamba watu hao ambao wengi wao ni wenye elimu ya chuo kikuu walielezwa kwamba ili kupata kazi hizo ni lazima watoe fedha kati ya Sh700,000 hadi Sh1 milioni.

Walielezwa kuwa mafunzo ya kazi hizo yatatolewa kwa miezi minne katika vyuo vya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), vilivyopo eneo la Mbweni (Dar es Salaam), Zanzibar na Monduli (Arusha).

Siku ya kwanza ambayo waliambiwa kukutana katika viwanja vinavyozunguka uwanja wa zamani wa Taifa, karibu na Ofisi za Baraza la Michezo Tanzania (BMT), ili wapelekwe Mbweni kwa ajili ya kupangiwa vituo vyao vya kazi walielezwa kwamba baadhi yao majina yao yalikuwa hayajaingizwa katika mfumo. Baada ya wiki moja walitakiwa kukutana tena eneo hilo ili kupelekwa, lakini walielezwa kuwa wangepelekwa Septemba 2, mwaka huu kwa kuwa baadhi yao hawakuwa na namba.

Ilipofika Septemba 2, vijana hao wakati wakielekea Mbweni, walielezwa kuwa muda umekwenda na hawataweza kupokewa katika kambi hiyo hivyo kupangishiwa nyumba za kulala wageni zilizopo Tegeta.

Hadi walipofika katika Ofisi za Mwananchi, Ijumaa wiki iliyopita, bado baadhi yao walikuwa wanaishi katika nyumba hizo na wengine kupewa nauli ili warudi katika mikoa waliyotoka kwa maelezo kuwa nafasi zitatangazwa gazetini Oktoba 3, mwaka huu.

Habari zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa polisi imefungua jalada kuhusu tuhuma hizo na tayari limewahoji watu kadhaa Dar es Salaam na mikoani, lakini mke wa kigogo huyo hajahojiwa.



PAMBAF what is the credibility of TISS to hold anyone accountable! Where is RAMA IGHONDU by the way! We want to see actions! otherwise they are just other crooks!!
 
Mkuu ni mke wa kamishina Chagonja anafanya kazi pale NBC, UDSM Branch, ni mpepe sana huyu mama,
muongeaji kupitiliza na anapenda kutishia sana....

Duh, tapeli anafanya kazi benki (NBC) mbona hatari hii. Hajasimamishwa kazi bado? Kingine ninachoona hapa ni usanii wa hali ya juu. Hii intelijensia tunayosikia kila siku mbona haikushtukia hili dili kabla halijafika mbali? Kama mchangiaji mwingine alivyosema ;huu ni mgao umeharibika mahali- watu wakachomeana. Na huyu Othman Rashid naye usanii mtupu. Usikute alienda kuzungumza na Mwema jinsi yakuimaliza hii kitu chini kwa chini. Hawa watu kwakweli ni aibu tupu. Hao waliotoa hela usikute ndio hao kila siku wanapiga kelele ya kutaka Tanzania mpya alafu wao wenyewe sio mfano. Ni Tanzania mpya ipi utakayoiona without hard work? Naona sasa mtajifunza uzuri wakupenda short cuts in life.
 
Kama mmefuatilia habari ya mwananchi jana ni kuwa mke wa kigogo wa polisi naye alidai kuwa katapeliwa lakini inadaiwa kuwa yeye ndie kiongozi wa matapeli. sasa kesi imefikishwa mahakamani na mke wa Chagonja anadai nae katapeliwa. Soma habari ifuatayo


Na Tausi Ally, Mwananchi | Sept 20, 2012

WATU wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, kujibu mashtaka 12, likiwamo kujipatia zaidi ya Sh102.8 milioni baada ya kuwadanganya watu akiwamo anayedaiwa kuwa mke wa Kamishna wa Operesheni wa Polisi, Paul Chagonja, Happyphania kuwa watawasajili kujiunga na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Idara ya Usalama wa Taifa.

Kosa jingine linalowakabili watuhumiwa hao ni kujaribu kutenda uhalifu wa kusafirisha binadamu.
Wakili wa Serikali, Sakina Sinda aliwataja washtakiwa hao kuwa ni mkazi wa Magomeni Mapipa, Baraka Mkufunzi (28), maarufu kama Rajabu Mbwana au Msati au Ernest na mkazi wa Mtoni Kijichi, George Enos (45), maarufu kama Ernest Salehe.

Sinda alidai kuwa washtakiwa hao walitenda makosa hayo, kinyume na Kifungu cha 380 na 381 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Alidai kuwa kati ya Aprili, Mosi na Septemba 8, mwaka huu, katika Wilaya ya Ilala, washtakiwa hao kwa pamoja walijaribu kutenda uhalifu wa kusafirisha binadamu kinyume na Kifungu cha 4 (1) (4) cha Sheria ya Kusafirisha Binadamu Sura ya 6 ya mwaka 2008.

Aliendelea kudai kuwa, katika kipindi hicho, washtakiwa hao walijipatia Sh5 milioni kinyume na Kifungu cha Sheria cha 302 cha Kanuni ya Adhabu Sura ya 6, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Ilidaiwa kuwa fedha hizo walizipata kutoka kwa Happyphania baada ya kumdanganya kuwa ni malipo ya kumwezesha kujisajili kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Polisi, Kitengo cha Takukuru au Usalama wa Taifa.

Mbali na kumtapeli Happyphania Paul Chagonja pia washtakiwa hao wanadaiwa kumtapeli Issa Mohamed Chikundi Sh22,250,000, Issa Hussein Rutemba Sh13,450,000, Daud Mgonja Sh3,700,000, Calota Philemon Ngowi Sh2,342,000 na Emmanuel Chagonja Sh11, 400,000.

Pia wapo, Dunstan Eliapenda Mkwizu Sh1,420,000, Yudas Simon Mkelane Sh2,200,000, Ibrahim Hashim Sh10,500,000 na Lauriana Joseph Sh29,200, 000 na kufanya jumla ya fedha hizo kufikia Sh102,862,000.

Washtakiwa hao walikana mashtaka yote yanayowakabili na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Hakimu Mkazi, Augustina Mmbando aliamuru washtakiwa hao wapelekwe rumande hadi Oktoba 2, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa baada ya kushindwa kukamilisha masharti ya dhamana.

Walitakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao kila mmoja angesaini bondi ya Sh25 milioni na mmoja wao kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika mahakamani yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

Kukamatwa hadi kufikishwa mahakamani kwa watu hao kumekuja baada ya wiki iliyopita gazeti hili kuripoti kashfa hiyo.

Kati ya Agosti 5 na 7, mwaka huu vijana hao 120 kwa nyakati tofauti wanadaiwa kwamba walipata taarifa kwamba kuna nafasi za kazi Idara ya Usalama wa Taifa na Takukuru na kwamba nafasi hizo zinapatikana kupitia kwa vigogo wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini.
 
Sasa maadui wa taifa, maadui wa uchumi wa taifa, maadui wa usalama wa taifa, maadui wa uchumi, ustawi na usalama wa mtu binafsi ni wale waliopewa dhamana ya kulinda na kutunza uchumi na usalama wa taifa na mali zao. Sote tumeona yanayofanywa na baadhi ya watoto wa rais, waziri mkuu m(wa)staaf, vigogo wa polisi, wake wa viongozi walioko madrkani etc. Hii ni ishara ya anguko kuu la dora.freedom is coming tommorow!!!!!!.
 
Hii sio kazi ya polisi ni ya investigative Journalism, na ndio hapo waandishi sijui na jukwaa la wakina chakubanga waliposhindwa kabisa, hivi unaongea nini na Jeshi la polisi kwenye hili? aibu badala yake waandishi wameanzisha saccos ya kuchangiwa na Rais JK shilingi 100,000,000/ hela za serikali, halafu wanataka kuwa huru waandishi wa dizaini za wakina Kibanda na Neville Meena, wanataka kifo cha Mwangosi kilaaniwe, na nani? hawana uwezo wa kunyooshea kidogo muuaji, wanakasirika kwa nini mwanahalisi imeandika habari za muuaji eti uandishi ule ni kinyume cha maandishi, mtanzania anapoponea tundu la sindano kuuawa, swala la kumtaja muuaji lina kinyume cha ethics,'shit' hawa ndio wanataka tuwakabidhi taifa letu eti wao ni mhimili wa nne' wanakataa ukweli kwamba wao ni ma cheer leaders, kwamba wanakalishwa vikao na kuagizwa vya kufanya, kituko cha kufa ni kile cha wahariri kumualika waziri Nchimbi, eti rafiki yao, bila kuwashirikisha wenzao, wakati wanajulikana kabisa kwamba nchimbi kawatuma wafanya hivyo ili apate point ya kisiasa, wamemtengenezea namna rafiki yao, halafu wanasema ka winni kisiasa, hao ndio wanaotaka tuwaamini kwamba ni waandishi kioja, ndio maana wako hivyo hadi leo, kama watanzania hatutalipigania mwanahalisi na kuwa wakweli kuhusu maisha yetu, tumelikwa, hawana moral authority hawa, wanaishi kwa bakshishi zao, wako kwenye payrole zao, maskingi Mwangosi amekwenda akiwa victim wa wahahari na waandishi wenyewe, tangulia mwangosi, hata wao watakwenda kwa njia hiyo hiyo, sema walau watoto wao watakua wamesogea kidogo sio kama wako, matapeli na wabinafsi wakubwa hawa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom