Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 19, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Tuesday, 18 September 2012 19:54[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]


  [​IMG]


  Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa,Othman Rashid

  NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI, MKURUGENZI AMTAKA IGP KUCHUKUA HATUA, MTUHUMIWA AJITETEA

  Waandishi Wetu

  SAKATA la mke wa kigogo wa polisi kudaiwa kuwatapeli vijana 120 kwa kuwachangisha zaidi ya Sh100 milioni ili awatafutie kazi Idara ya Usalama wa Taifa na Takukuru limechukua sura mpya, baada ya Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Othman Rashid kuwataka polisi wamkamate na kumchukulia hatua za kisheria mwanamke huyo.
  Utapeli huo wa aina yake, unadaiwa kufanywa na mama huyo kwa kushirikiana na mwanaye (majina tunayo). Pia yumo kijana anayejulikana zaidi kwa jina moja la Baraka ambaye kwenye mpango huo, anajitambulisha kuwa anafanya kazi Ikulu.

  Akizungumza na mwandishi wetu Dar es Salaam juzi, Rashid alisema tayari amewasiliana na Mkuu wa Polisi, IGP Said Mwema kuhusu tuhuma hizo ili kujua hatua zilizochukuliwa dhidi yake.

  "Nimewasiliana na IGP Mwema ili aweze kunipa ufafanuzi kuhusu mke wa kigogo huyo, lakini nashukuru amenipa ushirikiano na kuniambia kuwa suala hilo wanalishughulikia kisheria zaidi. Watanipa taarifa pindi watakapokuwa wamekamilisha," alisema Rashid.

  Alisema huo ni mfano tu wa baadhi ya watu wanaotumia jina la Usalama wa Taifa kufanya utapeli na kwamba tabia hiyo tayari imewaingiza baadhi ya watu matatani baada ya kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria na wengine bado wanatafutwa.

  Alisema sheria ni msumeno, hivyo ikibainika mwanamke huyo alijihusisha kutapeli kwa kutimia jina la Usalama wa Taifa, hatua kali zitachukuliwa dhidi yake ili iwe fundisho kwa wengine ambao wanatumia majina ya waume zao kutapeli watu.

  Rashid alisema bado ana imani kwamba polisi itamchukulia hatua za kisheria mwanamke huyo ikiwa itathibitika kwamba amejihusisha na utapeli kwa kuwa jeshi hilo lipo kulinda usalama wa raia na mali zao.

  Azungumzia tuhuma
  Akizungumzia madai hayo jana kigogo huyo wa polisi ambaye mkewe ndiye anayetuhumiwa (jina tunalihifadhi), alisema tangu mwanzo
  alielewa kwamba anayezungumziwa ni mkewe, lakini akakanusha kuhusika katika utapeli huo.

  Alisema kutokana na taarifa ambazo zimekuwa zikiandikwa katika gazeti hili na kumtaja Baraka, vijana wengi waliotapeliwa kutoka mikoa mbalimbali walifunguka akili zao na kubaini kuwa aliyetajwa katika habari ndiye aliyekuwa akichukua fedha kwao.

  "Jambo linalonisikitisha ni kwamba, aliyewaletea taarifa hizo za uongo zinazomhusisha mke wangu na utapeli huu ndiye tapeli aliyekuwa akizunguka mikoa mingi nchini kutapeli watu. Hata mke wangu ni mmoja wa waliotapeliwa. Alikusudia kuwapeleka wanafamilia watatu akiwemo mtoto wake, mke wa kaka yake na wifi yake ambaye tunamlea," alisema.

  Alisema mkewe alitoa fedha taslimu zisizopungua Sh1.5 milioni, mbali na gharama za kununua bidhaa na vifaa mbalimbali ambavyo wanafamilia hao wangetakiwa kwenda navyo mafunzoni.

  Alisema walishtuka kuwapo dalili za utapeli baada ya watu waliokuwa wakidai kushughulikia ‘mipango' hiyo kuanza kutoa ahadi zisizotekelezwa, huku wakati mwingine simu zao zikipatikana kwa nadra.

  Alipotakiwa kuwataja kwa majina waliokuwa wakishughulikia mipango, ambao walichukua fedha kutoka kwa mkewe kigogo huyo alisema hakumbuki vizuri majina yao. Hata hivyo, alisema mmoja wao anaitwa Baraka.

  Mke wa kigogo huyo alikataa kuzungumzia tuhuma hizo akisema: "Hayo yote yapo kwa wakubwa, mimi siwezi kuongelea kitu kilicho ngazi za juu yangu."

  Alipoambiwa kuwa mwandishi wetu amezungumza na mumewe ambaye ameeleza kuwa mama huyo naye ni miongoni mwa waathirika katika utapeli huo, hivyo atoe ufafanuzi alikataa pia kuzungumzia hilo na kukata simu.

  Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah alipotakiwa kuzungumzia tuhuma hizo alisema: "Kwa sasa niko huku Maputo (Msumbiji), siwezi kuzungumzia suala hilo lakini nikirudi nitafutane nitatoa ufafanuzi."

  Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai wa Polisi (DCI), Robert Manumba hakutaka kuzungumzia tuhuma hizo akielekeza atafutwe msemaji wa polisi ambaye simu yake haikupatikana kutwa nzima jana.

  Ilivyokuwa
  Wiki iliyopita gazeti hili liliripoti habari kuhusu mke wa kigogo kuwatapeli vijana 120 kwa ahadi ya kuwapa ajira katika Idara ya Usalama wa Taifa na Takukuru.

  Kati ya Agosti 5 na 7, mwaka huu vijana hao 120 kwa nyakati tofauti walipata taarifa kwamba kuna nafasi za kazi Idara ya Usalama wa Taifa na Takukuru na kwamba nafasi hizo zinapatikana kupitia kwa vigogo wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini.

  Kwa kupitia kwa mtoto wa mwanamke huyo na kupewa taarifa na rafiki zao, inadaiwa kwamba watu hao ambao wengi wao ni wenye elimu ya chuo kikuu walielezwa kwamba ili kupata kazi hizo ni lazima watoe fedha kati ya Sh700,000 hadi Sh1 milioni.

  Walielezwa kuwa mafunzo ya kazi hizo yatatolewa kwa miezi minne katika vyuo vya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), vilivyopo eneo la Mbweni (Dar es Salaam), Zanzibar na Monduli (Arusha).

  Siku ya kwanza ambayo waliambiwa kukutana katika viwanja vinavyozunguka uwanja wa zamani wa Taifa, karibu na Ofisi za Baraza la Michezo Tanzania (BMT), ili wapelekwe Mbweni kwa ajili ya kupangiwa vituo vyao vya kazi walielezwa kwamba baadhi yao majina yao yalikuwa hayajaingizwa katika mfumo. Baada ya wiki moja walitakiwa kukutana tena eneo hilo ili kupelekwa, lakini walielezwa kuwa wangepelekwa Septemba 2, mwaka huu kwa kuwa baadhi yao hawakuwa na namba.

  Ilipofika Septemba 2, vijana hao wakati wakielekea Mbweni, walielezwa kuwa muda umekwenda na hawataweza kupokewa katika kambi hiyo hivyo kupangishiwa nyumba za kulala wageni zilizopo Tegeta.

  Hadi walipofika katika Ofisi za Mwananchi, Ijumaa wiki iliyopita, bado baadhi yao walikuwa wanaishi katika nyumba hizo na wengine kupewa nauli ili warudi katika mikoa waliyotoka kwa maelezo kuwa nafasi zitatangazwa gazetini Oktoba 3, mwaka huu.

  Habari zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa polisi imefungua jalada kuhusu tuhuma hizo na tayari limewahoji watu kadhaa Dar es Salaam na mikoani, lakini mke wa kigogo huyo hajahojiwa.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]   
 2. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,534
  Likes Received: 10,451
  Trophy Points: 280
  Kigogo,mke wa kigogo,mtoto wa kigogo ndio nini.?? Ina maana hata mahakamani watapelekwa kwa majina hayohayo.!!
   
 3. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2012
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 160
  Duh! Kaaz kweli kweli
   
 4. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Hivi ni mke wa nani huyo kigogo??
   
 5. kande kavu

  kande kavu JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2012
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 235
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo huyo mheshimiwa sana Kamanda wa Polisi alijua mchezo mzima wa hao kina Baraka,ikiwamo kuomba rushwa wafanikishe vijana kuajiriwa,lakini bado alitoa ruhusa kwa mkewe kuendelea na huo mpango?

  Kama ni hivyo basi nchi hii itazinduliwa na kiama! Kamanda wa Polisi anashiriki kutoa rushwa,Kamanda wa Polisi haamini katika haki bali pesa mbele,Kamanda wa Polisi hajiongezi na kutaka kufatilia kwa nini ajira kwa pesa,kamanda wa Polisi anakaa kimya ili watu wake wafaidike, kamanda wa Polisi.
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  NDIO USIRI WA SERIKALI YETU... atakayekwenda Mahakamani atakuwa ni kigogo Mshona VIATU na sio KIGOGO MKE WA TAPELI.

  Tunaficha Majina ya WEZI!
   
 7. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ukiona tapeli anatapeliwa basi ujue kumekucha. Mwizi haibwi kirahisi. Ina maana tecknologia imezidi kimo. Watachekana tu kuzidiana kete halafu yanaisha.
   
 8. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #8
  Sep 19, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Kwanza hao vijana wote inabidi washitakiwe pia kawa kutoa hongo!
   
 9. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #9
  Sep 19, 2012
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,437
  Likes Received: 1,017
  Trophy Points: 280
  Polisi wakati mwingine wanaoa wahalifu, yote tisa kumi kuna mcharuko mwingine huo nouma keshatapeli sana mjini kupitia polisi na mpaka polisi wenyewe anawatia ndimu na kupitia jina la mumewe kuwa kigogo polisi na ikulu. Anaishi kwa kuhama hama mjini na kubadili namba simu.

  Mie siamini kama hao usalama au polisi wanaubavu huo wengi waalifu.
   
 10. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #10
  Sep 19, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  hii nchi ina serikali inayotoa mafunza! imeoza! haifai kuitwa serikali, ni pango la majambazi! mwisho wao unakaribia.
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Sep 19, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  sasa hao vijana nao duh... hawakuchukua hata muda kidogo kujifunza ajira za usalama wa taifa zinapatikana vipi? kadizooo!!!
   
 12. akohi

  akohi JF-Expert Member

  #12
  Sep 19, 2012
  Joined: Jul 13, 2012
  Messages: 761
  Likes Received: 173
  Trophy Points: 60
  Majina tafadhari
   
 13. harakat

  harakat JF-Expert Member

  #13
  Sep 19, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Mi mwenyewe nilipigwa 20000/=tu nyingine niliwaambia kwamba mpaka nione wamefikia wapi ikawa sanaa na mimi hela ya kuunga unga mpaka leo naona sanaa tu kumbe tuko wengi tuanzishe chama cha waliotapeliwa
   
 14. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #14
  Sep 19, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kila siku nawaona humu jf, wakidanganyana watapata vipi hizo ajira ... Usijekuta mambo haya yanaanzia kwenye PM, kwan utapeli wa namna hii unahitaji kuwakuta watu wenye nia na kazi hizo na wako desperate pia
   
 15. mwaxxxx

  mwaxxxx JF-Expert Member

  #15
  Sep 19, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 846
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  yale yale tu, nchi hii kila idara imeoza. Anayebana na anayebanwa wote kundi moja
   
 16. L

  La Voz Member

  #16
  Sep 19, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama kuna mwana jf ni muhanga atutajie majina plz, then kuanzia hapo tuanze kutiririka
   
 17. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #17
  Sep 19, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Halafu mbaya zaidi ni vijana wenye elimu ya vyuo vikuu vyetu!
   
 18. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #18
  Sep 19, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  strong point...unatisha kamanda hizi naomba ni PM zina mchango mkubwa kwenye hili na miongoni mwa wahanga wa utapeli huu bila shaka ni wana jf na great thinker wetu
   
 19. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #19
  Sep 19, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu MMJ,

  Sio watanzania wote wanaojua ni jinsi gani ajira za usalama wa taifa zinapatikana, lakini ninashangaa ilikuwaje huyo kigogo wa Polisi alimuacha mke wake akatoa Tshs. 1.5 ili ndugu zake wapate ajira. Ina maana yeye hajui ni jinsi gani ajira za UWT zinapatikana vipi? Nafikiri kuna ukweli kwamba huyo mke wa kigogo alikuwa anahusika kwenye huo utapeli na sasa wanatafuta jinsi ya kujinasua.

  By the way, anayejua jina la huyo kigogo wa polisi ni nani amwage jina lake hapa. Hatuwezi kuendelea kuzungumza kwa mafumbo na hapa JF ni sehemu tunayosema "where we dare to talk openly"

  Leta majina hapa!!!!!!!! Kwa nini jina la Baraka litajwe na mengine yafichwe?

  Tiba
   
 20. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #20
  Sep 19, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tena ni wahitimu wa chuo kikuu...kaazi kweli kweli!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...