Usalama wa safari zetu wakati wa likizo

Buswelu

JF-Expert Member
Aug 16, 2007
1,998
352
Shalom ndugu zangu, kama unasafiri usiku kuja moshi ukifika maeneo ya lembeni uwe makini jamaa wanapanga mawe na wana Gari na pia bodaboda.

Gari wanaitumia kuhakikisha unapishana nao eneo lenye mawe ili ubane upande wa mawe usiweze kukwepa.

Jana tumekutana nayo wamepanga km manne, hivyo hatukuwa na option nyingine tukayaingia nikapasua tairi ya mbele hapo hapo Mungu amesaidia haikupinduka.

Tukaanza kutafuta pa kusimama ili tuweze kubadili ghafla tukaona Bodaboda inaanza kutufuata spidi ikabidi tuondoke hivyo hivyo, walivyoona tunaondoka wakazima taa wakaingia msituni, tukaendelea kwa muda Bahati tukaingia mji unaofuata.

Tukakuta watu pale wakatuambia mna Bahati sana maana haipiti siku mbili wanatega mawe na kuiba hata juzi wameiba hivyo hivyo na wanawapiga mapanga.

Cha kushangaza eneo hilohilo tumeambiwa polisi walikuwepo muda si mrefu. Ila tumekuja kuwakuta huku mbele wakatuambia ngoja waende huko

Nashauri unaposafiri hakikisha unamuomba Mungu awalinde dhidi ya wasio haki kwani sisi tulikuwa na Zaburi ya 17.

Shetani anatumia watu wasio haki kama hawa. Pia mfahamu kuna watu shetani amewabadili kuwa wauaji, wezi na waharibifu ila ukiwa na Roho wa Mungu utakuwa salama tu.

Ni hayo niliyokutana hivyo muwe makini na haya, mchana tochi, usiku mawe!!!! Sasa hiyo ni bufee chagua mwenyewe.

Mosha

Nimeona kuna haja ya kushauriana kupeana updates namna ya kukwepa kadhia hii wakati huu...
 
Roho yangu imezimika, siku zangu zimekoma
Kaburi i tayari kunipokea.
Ni kweli wako kwangu wenye kufanya dhihaka,
Jicho langu hukaa katika kunifanyia uchungu kwao........
(zab 17)
 
Back
Top Bottom